Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Hapana mkuu.Hatuhitaji kumbukumbu na biography za watu waliolitia hasara taifa, kumbukumbu zao zibakie kwenye familia zao.
Hata kama wamelitia hasara taifa, tunahitaji historia zao hizo ziandikwe vizuri watu wajifunze mabaya yao, yasirudiwe tena.
Ninapoongelea kuandika historia, siongelei kuandika "hagiography". Hagiography ni historia fulani ya kumtukuza tu mtu, bila kuandika mabaya yake. Ndiyo maana ninesisitiza watu wengi waandike, waandike kwa mitazamo tofauti.
Sasa Mkapa katupiga hela za EPA, halafu kaandika wizi huo kwa rasharasha tu, hajaandika ukweli, hajaandika mambo kwa kina, unataka watu wasiandike vitabu vya jufichua madudu yalivyofanyika na watu walivyoiba mamilioni ya dola?
George Santayana aliandika "Those who cannot remember the past are condemned to repeat it".
Tusipoandika historia yetu, tutarudia mabaya yaleyale tu.