Historia ya Ali Hassan Mwinyi kama Rais haiko wazi

Umeenda deep sana Mkuu wachache watakuelewa. Ila hizi tafiti na uandishi inahitajika maprofesa wa vyuo vikuu vyetu wajitafakari sana hasa juu ya nini dhima ya elimu na uwepo wao nchini.

Hatuna vitabu vya mambo mengi sana kwa kisingizio cha watanzania hawapendi kusoma vitabu, tuhuma ambazo pia nimekuja kugundua sio za kweli.
 
Ivan...
Nimefungua uzi nia si kubainisha ila kutoa jibu kwa wale ambao wamenisikia na kunisoma nikieleza historia ya Rais Ali Hassan Mwinyi waelewe kuwa nafahamu historia yenyewe lakini sikuona sababu ya kuieleza katika taazia.
Msisahau kueleza na upande wenye ukakasi ili kuitendea haki historia na Mwinyi kama mwanadamu pia.

Loliondo gate
 
Kusoma sasa hivi hata nje ya Tanzania watu wako interested sana. Kuna watu wanataka kuja kuinvest Tanzania, kuishi Tanzania, wanataka kuisoma.

Kuna wanetu wanazaliwa nje ya Tanzania hata hawaijui vizuri, wanataka kuisoma vizuri.

Profesa Timothy Molony wa Edinburgh kaandika kitabu cha miaka ya mwanzo ya Nyerere kinaitwa "Nyerere: The Early Years".

Yani Watanzania tulikuwa hatuna mtu wa kuandika miaka ya mwanzo ya Nyerere mpaka aje Profesa wa Edinburgh?

 
samahani mzee wangu niko nje ya maada yako, hivi unaweza tujuza japo kwa uchache tukio la kifo cha mwandishi wa habari ndg Stan Katabaro enzi za utawala wa Mwinyi?.

Natanguliza shukrani zangu.
K11,
Sina taarifa zake.
 
Swali langu ni kweli Sheikh Thabit Kombo alikuwa akiaminiwa sana na Nyerere, je ni kwa sababu ya urafiki wao? Au kuaminiwa huko kulitokana na nini?

Ni kweli Thabit Kombo ndiye aliyependekeza Mwinyi awe mgombea Urais kutokea Zanzibar?
Mng...
Haya yote kaeleza kitabuni.
Soma kitabu.
 
Hayati Ally Hassan Mwinyi alikuwa;
1) Rais .mswahili
2) Rais Muungwana
3) Rais Mwanadiplomasia
4) Rais aliestaafu Siasa lakini familia yake ikiwa bado kwny Siasa

Mambo yote haya yalimfanya awe makini sana kwny kuandika historia ya maisha yake ya kisiasa kwa kuwa bado hajavua 'Gloves' kwa asilimia mia moja

Huenda kuna mambo Angeandika yangemgombanisha na watu au na Taasisi ambazo asingependa mizozo nazo



Moja ya mambo yaliyoleta changamoto kwny uandishi huu wa Kitabu ni uamuzi wake wa kuwa muangalifu sana kwny hili, Kijana wake wa wakati huo Balozi Ombeni Sefue kapata tabu sana kumkumbusha kumbusha mambo fulani ambayo yangestua na kuleta mvuto sana lakini Mzee alisisitiza kuwa 'kasahau mambo mengi '

Watoto wa Hayati Mzee Mwinyi bado wapo kwny ulingo na asingependa kitabu cha maisha yake kiwe ndio 'taulo ' ambalo wanaweza kurushiwa na refa ili amalize pambano


Hata mie ninayo machache ambayo nilishangaa aliyakwepa kuyaweka

ila kwa maoni yangu naamini hakuna Rais anaeweza kuandika historia ya maisha yake kwa ukamilifu wakati bado ana interest na mwenendo wa Siasa zetu


Mkoa wa Pwani tuna bahati ya kutoa ma Rais wawili wa Muungano na wawili wa Zanzibar ila tuna bahati mbaya sana ya kuwa ma Rais wote hao ni wana diplomasia sana kiasi kwamba hawafunguki

Hayati JPM angepata bahati ya kustaafu na kuandika kitabu tungefaidi sana yale ya kutoka moyoni
 
Swali langu ni kweli Sheikh Thabit Kombo alikuwa akiaminiwa sana na Nyerere, je ni kwa sababu ya urafiki wao? Au kuaminiwa huko kulitokana na nini?

Ni kweli Thabit Kombo ndiye aliyependekeza Mwinyi awe mgombea Urais kutokea Zanzibar?
Rais Mwinyi alirudishwa kutoka Ubalozi 1981 baada ya fitna ya kumtoa Aboud Jumbe kuiva japo mwenyewe wakati huo hajajua kwanini karudishwa

akina Luteni General Abdulrahman Shimbo, Jaji Lubuva, Jakaya Kikwete, kwa nyakati tofauti kuanzia 1977 walishakamilisha uratibu wa kudhibiti Siasa za Zanzibar baada ya kuuawa ASP kwa kile kilichoitwa project ya Harmonisation of TANU and ASP iliyoratibiwa kwa ustadi


bila ya ASP kuvunjwa ilikuwa hakuna namna ya kisiasa ya kumdhibiti Aboud Jumbe zaid ya njia zingine maarufu zaid hapa nchini
 
Mkuu huwa mimi ni fan wako, nakukubali sana
 
Wasiokuelewa watakubeza na kukupinga kwa kujiapiza.
Mimi nimetokea kuwa na fikra mbadala kwa kila unachoandika. Nimegundua kuwa kuna vitu muhimu sana kwa jamii kuvifahamu kuhusiana na hii nchi yetu Tanzania.

Ninarejea na sitoacha kurejea mara kwa mara kukunasihi kwamba uandike miswada ya kutosha (kama hutaki kutoa vitabu) na miswada hiyo basi iweke kwenye wasia wako wa urithi kwa kizazi cha Tanzania.

Mzee Mohamed Saidi jaribu sasa kuishi maisha ya gwiji Saaban Robert ambaye mpaka sasa anaishi kwenye fikra na nyoyo zetu kupitia maandishi yake yaliyobeba mengi chanya kwa maisha ya kila kizazi.

Andika mzee andika
 
1. Kwanini unaziita fitina za kumtoa Jumbe? Je alionewa?

2. 1977 tayari Kikwete alishaaminiwa kiasi hicho?
 
Ni kwanini Augustine lyatonga mrema alijiuzulu wakati wa utawala wa Mzee Mwinyi?
Hili mkuu tunaweza kulijadili, Minister Mrema alikuwa mmoja wa cabinet, na katika cabinet kuna kitu kinaitwa collective decision, jambo likijadiliwa kwenye cabinet na mwafaka ukafikiwa, hata kama huupendi ni lazima uwe sehemu ya makubaliano hayo, issue ya CHAVDA, iliyoibuliwa na mbunge machachari wa makete, na waziri Mrema kulichukua kwa mapana zaidi ya uamuzi wa cabinet ulichangia auache uwaziri, na pia kumbuka waziri Mrema alikamata Vito vingi pale airport vikitoroshwa, Ile nayo naona ni sababu mojawapo maana vile Vito, definitely state house ilihusika navyo, nipo tayari kuwa corrected kwa mawazo haya
 
1. Kwanini unaziita fitina za kumtoa Jumbe? Je alionewa?

2. 1977 tayari Kikwete alishaaminiwa kiasi hicho?
1) Siasa ni fitna na yeye alifitinishwa na ndio sababu hadi leo utasikia tu kuchafuka kwa hali ya Siasa Zanzibar hakuna la ziada

2) Baada ya TANU na ASP kuvunjwa 1977, Katibu Mtendaji wa CCM Mzee Pius Msekwa alielekezwa ampeleke Zanzibar Kijana wa Kazi Jakaya Mrishi Kikwete kwenda ku harmonies na kuratibu kusimikwa kwa CCM Zanzibar na kung'olewa kwa mizizi ya ASP na ASP wote wawe CCM na waache kabisa Siasa za ASP na akalifanikisha kwa kiasi kikubwa akiwa kijana mdogo wa miaka 27 lakini mwenye maarifa ya Siasa makubwa sana
 
Mzee Mwinyi hakuwa mjinga kuacha kuandika hayo,kuruhusu yaandikwe ni kufukua makaburi,Ujue na yeye hakuwa malaika ana mabaya mengi sasa ukitaka wayaandike hapa patakalika kweli
 
Hatuhitaji kumbukumbu na biographies za watu walioliletea hasara taifa kuliko faida, kumbukumbu zao zibakie kwenye familia zao.
 
Mzee Mwinyi hakuwa mjinga kuacha kuandika hayo,kuruhusu yaandikwe ni kufukua makaburi,Ujue na yeye hakuwa malaika ana mabaya mengi sasa ukitaka wayaandike hapa patakalika kweli
Nyerere yeye alikataa kabisa kabisa kuandika kitabu chake japo Taasisi nyingi zilikuwa tayari kufadhili mradi ule

kwa mfano angeandika vipi jinsi alivyofanikiwa kuwa na MoU na Israel kufundisha Intelijensia vijana wetu na ushirikiano kadhaa aliokuwa nao wakati huo huo hataki wawe ubalozi hapa kwetu kutokana na sera zao dhidi ya Wapalestina

aliwezaje kuwa Rafiki wa Marekani, China na Russia kwa wakati mmoja
 

Vipi kuhusu vitabu vya Marais wengine Africa?..umemsoma Andrew Morton kuhusu Daniel Moi...?

Niliona summary na jinsi Moi alivyokuwa openly ana admit kutumika na mataifa ya Ulaya kupinga OAU....kwenye ajenda mbalimbali.. ikiwepo ya kuwepo peace keepers wa OAU.....Hadi akawa anadai helicopter aliyoahidiwa kama zawadi akifanikisha......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…