Historia ya Ali Hassan Mwinyi kama Rais haiko wazi

Hatuhitaji kumbukumbu na biography za watu waliolitia hasara taifa, kumbukumbu zao zibakie kwenye familia zao.
Hapana mkuu.

Hata kama wamelitia hasara taifa, tunahitaji historia zao hizo ziandikwe vizuri watu wajifunze mabaya yao, yasirudiwe tena.

Ninapoongelea kuandika historia, siongelei kuandika "hagiography". Hagiography ni historia fulani ya kumtukuza tu mtu, bila kuandika mabaya yake. Ndiyo maana ninesisitiza watu wengi waandike, waandike kwa mitazamo tofauti.

Sasa Mkapa katupiga hela za EPA, halafu kaandika wizi huo kwa rasharasha tu, hajaandika ukweli, hajaandika mambo kwa kina, unataka watu wasiandike vitabu vya jufichua madudu yalivyofanyika na watu walivyoiba mamilioni ya dola?

George Santayana aliandika "Those who cannot remember the past are condemned to repeat it".

Tusipoandika historia yetu, tutarudia mabaya yaleyale tu.
 
Mkuu,

Andrew Morton nimesoma kitabu chake cha Princess Diana, cha Moi sijakisoma.

Kenya wamejitahidi kuandika expose, nimemsoma Miguna Miguna katika "Peeling Back The Mask : A Quest For Justice in Kenya" na "Kidneys For The King : De-Forming The Status Quo in Kenya"
 
Ni kweli unachosema lakin Tz hamna wandishi wa kuandika udhaifu wa mtu aliekuwa na nafasi kubwa katika jamii zaidi ya kumsifia na kumtukuza.
 
Lweli?
 
NJe ya mada kidogo, umetaja vyuo vikuu kujitafakari nimeikumbuka hii clip niliona leo pale mjini X


View: https://x.com/EngThomasMinja/status/1764696527509835997?s=20
Elimu yetu sisi tujitafakari upya tokea darasa la kwanza mpaka elimu za juu, maana zimekaa kitapeli tapeli sana.


Nakumbuka kipindi nipo shule practical za physics nilikua sielewi kwanini bado tunafanya yani ukipanga vifaa majibu ni kukimbizana nayo unaona hapa sasa ntakosa maksi unaanza kufoji "kupika data" baadae matokeo safi ila ki uhalisia hakuna cha maana kilichofanyika
 
Lax,
''When he came into office President Ali Hassan Mwinyi maintained the staff which had diligently served his predecessor.

This staff could not conform to the new order and there were reports of disloyalty, split of allegiance and abuse of trust.

Confidential information found their way out of the President's Office into front pages of the private press.''

Mambo mfano wa haya Rais Mwinyi hakuyaeleza katika kitabu chake.
 
Nashukuru mkuu , hasa hii ya dhahabu kukamatwa airport ilikuwa ishu kubwa mzigo ulikuwa wa Nani ??

Style ya mrema ya kufanya kazi ilikuwa inafanana na sokoine .
 
Hii ni kweli kabisa.
 
Reactions: Lax
Nashukuru mkuu , hasa hii ya dhahabu kukamatwa airport ilikuwa ishu kubwa mzigo ulikuwa wa Nani ??

Style ya mrema ya kufanya kazi ilikuwa inafanana na sokoine .
Hiyo ilikuwa ni dhahabu ya Yassir Arafat akiwakilisha Palestine Liberation Organization (PLO).

Kuna mambo yalikuwa yanafanyika kati ya PLO na Tanzania Captain Aziz alikuwa ana facilitate.

Captain Aziz alikuwa anapitisha tu dhahabu za PLO.

Mrema alijiingiza kwa pupa kukamata madili makubwa yaliyohusisha diplomasia kubwa kumshinda yeye.

Mwisho Captain Aziz alipewa msamaha wa rais na Ali Hassan Mwinyi.
 
Lakini jinsi ilivyokuwa alikuwa anatekeleza wajibu wake Kama waziri mwenye kusimamia usalama na mambo ya ndani baada ya waziri wa madini kushindwa kazi.

Inaelekea kipindi hicho dhahabu ilikuwa kama machungwa watu walibeba bila usimamizi na udhibiti ili kulipa mrabaha au kodi
 
Hayo ni mambo ya covert international diplomacy, hakuna habari ya waziri wa madini kushindwa kazi.

Hiyo dhahabu haikuwa inaibiwa, hiyo ilikuwa ni dhahabu ya serikali inapitishwa uwanja wa ndege kwenda kusaidia marafiki wa serikali, Wapalestina, PLO.

Mrema alifanya pupa kuvamia mizigo ya "usalama wa taifa". Angeuliza vizuri angeelezwa tu, tatizo hakutaka kuuliza vizuri.

Ushaelewa?
 
SIdhani kama Mzee Mohamed Said analifahamu hili, au analifahamu ila anajidai kuwa halifahamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…