"Its easy to be the expert if you are the only person in the world with any interest." dapper
ukipitia uzi mbali mbali humu utakuta mada tofauti kuhusu bitcoin wengine wamekuwa wakiisifia na wengine wamekuwa wakiikashifu kuwa ni utapeli hii inawafanya watu wasioijua kabisa bitcoin kupata woga na yupi wa kumsikiliza.
Nianze kwa kusema Bitcoin sio kampuni, sio biashara wala sio tovuti au biashara ya kujipatia pesa nk.
Bitcoin ni currency / sarafu kama zilivyo us dollar, Tanzania shillings au pound tofauti ya Bitcoin na currency zingine nii kuwa bitcoin ni online currency.
Bitcoin sio paper money, haiko centralized means hakuna serikali au kampuni inayomiliki. Lakini pia ni currency ambayo ni rahisi kuitumia.
baada ya uvumbuzi wa bitcoin na mgunduzi Satoshi Nakamoto 2009 zimetokea sarafu nyingine nyingi online kama onecoin, ethereum.
kama zilivyo currency zingine pia bitcoin ipo hivyo hivyo inatengenezwa pia lakini utahitahi kuwa na super computer ziitwazo antiminer na vifaa vingine pamoja na softwares zingine ili uweze kutengeneza bitcoin kwa faida utahitaji hizo super computer nyingi ili uweze kutengeneza bitcoin nyingi kwa muda mfupi ambapo itakuwa kama kiwanda kidogo hivi na hizo bitcoin utaweza kuziuza na kutengeneza faida.
Ingawa kwa sasa bitcoin ndio pesa yenye thamani kubwa kuliko zote mpaka muda huu 1 bitcoin ni saw na dola 1100 lakini pia inaweza kupanda thamani au kushuka thamani kama zilivyo currency zingine.
Njia za kujipatia pesa kupitia bitcoin
1. unaweza amua kununua vifaa na software kwa ajili kutengeneza bitcoin kisha ukatengeneza faida kubwa sana, changamoto hapa ni kuwa hiyo mitambo kama antiminer s9 una zaidi ya 1000 watts za umeme means unakula umeme sana kama pasi ya umeme sasa pigia hesabu unaurun for 24 hours so it need a huge investment to make profit with it.
2. kuwa wakala wa bitcoin... just assume bitcoin ni kama pesa iliyopo kwenye account ya mpesa au tigo pesa. means ukiitaka kuinconvert kuwa paper money lazima uende kwa wakala uitoe hivyo wakala atapata faida. same kwenye bitcoin its just like online bureau exchange zipo site trusted ambazo unaweza pata bitcoin kutoka kwa local trusted agents hapa Tanzania.
3. unaweza amua kununua bitcoin na kisha kuitunza tu then ukasuburi ikipanda thamani uje kuuza mfano last year july 1 bitcoin ilikuwa na thamani ya dola 600 lakini hivi leo inathamani ya dola 1100 na pia katika predictions mpaka june this year bitcoin inaweza fika dola 1800 hivyo unaweza tengeneza pesa mingi sana.
Watu wengi wamekuwa wakichanganya bitcoin na kampuni za upatu za online kwasababu tu zinatumia bitcoin. iko hivi hizi kampuni zinatumia Bitcoin just as amode of transaction exchange tu, kama zilivyo other ways kama perfect money, payeer, paypal nk.
So kuna kampuni wanaziita hyip yaani high yield investment program ambazo husema uinvest kiasi fulani cha pesa kisha utatengeneza faida kila siku labda 5% lakini hawa huwa matapeli kampuni husurvive wiki moja mpaka miezi 3 kisha kampuni kukimbia na pesa za watu, kwa sababu njia wanayotumia kulipa ni kupitia bitcoins basi watu hufikiri bitcoin ni scam.
kwa nini huchagua bitcoin as amode of payment???
kama nilivyo eleza Mwanzo bitcoin haiko centralized means mimi naweza fungua online wallet nikatumia tu username then nikatumia hata bitcoin zenye thamani ya billions of money na within a short of time ukaipata bila bank kuu au serikali kujua nani katuma au nani kapokea na imekwenda wapi so ina privacy.
lakini pia bitcoin ni njia rahisi sana kwa ajili ya kufanya malipo online unahitaji account ya online wallet tu kisha unaanza kunua bitcoin kwa urahisi tu hata kwa kwa mpesa kupitia wakala kisha ukaituma popote unapotaka tofauti ungetumia bank ingekuwa process za kupa visa card, kisha ujaze form kwa ajili ya kutumia online nk. ndio manasas online bitcoin ndio inatamba.
Bitcoin pia huweza kushuka thamani kwa sababu nayo ni currency lakini imekuwa ikipanda sana thamani sababu ni nyingi lakini moja ya reason ni kuwa ncho nyingi sasa zimekuwa zikipitisha kuwa official mode of paymeny kwenye nchi zao kama ufilipino na Japan na kufanya kampuni zao kuaddopt hii mfano ni kampuni ya magari beforward.
Hivyo welcome katika uwekezaji wa bitcoin unaweza tengeneza pesa nyingi sana kupitia bitcoin.
next time tutaleta soma la namna ya kununua na kuuza bitcoin.
By , Bitcoin consultant.
Call 0713774746