Historia ya BITCOIN: Uliza chochote nitajitahidi kukujibu

Historia ya BITCOIN: Uliza chochote nitajitahidi kukujibu

Hii pesa ninaweza kuidraw na kuitumia kwa matumizi ya kawaida?
mfano. Nina hela kwenye mpesa, nitaweza kuitoa na kununua kitu chochote ninachotaka.
Je, bitcoin iko hivyo?
 
Mmmmh hiyo currency gani uliyotumia kwa 1 bitcoin!?

Najua zilivyo nashangaa haujaweka.

2.kununua bitcoin na kuuza inapopanda. bitcoin hupanda kila mara na kila mwaka hivyo unaweza kuinunua na kuitunza kwa muda fulani kisha kuiuza kwa sasa 1bcn =2510.27 na hii ni kwa sababu wiki hii imeshuka ilitegemewa kufikia 4000 watalaamu wanasema ifikapo 2019 huenda ikafika 10000 bila shaka ukiitunza kufikia wakati huo utapata faida.
 
Madhumuni yake ilikuwa ni kurahisha utumaji na upokeaji wa pesa pasipo mtu wa kati ikimaanisha pesa inatumwa moja kwa moja kutoka mtumaji hadi mpokeaji tofauti na paypal ilivyo
Hiyo Pesa unaitumia kwenye vitu gani sijawahi kuona kwenye online markets zikifanya transaction kwa kutumia bitcoin
 
Hiyo Pesa unaitumia kwenye vitu gani sijawahi kuona kwenye online markets zikifanya transaction kwa kutumia bitcoin
pesa hiyo ilikuwa ikitumika kulipia huduma huko dark web lakini kwa sasa baadhi wanapokea pesa hiyo ingawa si wengi ndiyo maana hujaiona mahali
 
pesa hiyo ilikuwa ikitumika kulipia huduma huko dark web lakini kwa sasa baadhi wanapokea pesa hiyo ingawa si wengi ndiyo maana hujaiona mahali
Kwa hiyo haina umuhimu wowote Zaidi kwenye illigal business ama taja hizo masoko ya mtandao yanayotumia bitcoin
 
Labda kwa kuongezea.

Kwa nini bitcoin?

Pesa kawaida ina "central authority" yaani sehemu ambayo inacontrol, kawaida ni banks. Mfano pesa ya Tanzania mwenye control kubwa ni Bank of Tanzania.
Bitcoin ilitengenezwa kwa dhumuni kua hakuna central authority, yaani haiwezi kua controlled na institution moja, kwa sababu inarun kwenye mfumo unaoitwa blockchain ambao upo distributed kwa mtu yeyote yule, kwa lugha nyingine controlling institution ni kila mtu, kutokua na sehemu moja inayocontrol hii pesa kuna faida zake :

Kwanza kabisa mtu hawezi kuhack akaiba au kuchange data, kwa kua ili kuhack itabidi uhack computer milioni kadhaa ambazo zipo distributed kila kona, ni kazi sana kumhack kila mtu, bank unaweza hack data points zao ukawaangusha ila sio watu ambao wapo connected kwenye blockchain.

Pili kutuma na kupokea fedha ni rahisi zaidi, kwa kua haipitii bank, ukitaka kutuma bitcoin kutoka Tanzania kwenda Japan mfano, unaandika wallet number ya unayemtumia hapohapo inakua ishafika anaenda anatoa anapotaka, ni bure, labda gharama atakazolipia ni wanaocharge kufanya exchange kutoka bitcoin kwenda currency husika. Ni rahisi, faster na cheaper kuliko hata hizi western union au moneygram services.

Tatu kuna kitu kinaitwa immutability, yaani record ikiwekwa imewekwa haiwezi kubadilishwa, blockchain ndivyo inavyofanya kazi, kila transaction unayofanya ikiwekwa kwenye record ndo inakua imetoka hivyo, huwezi fanya chochote kile, sasa hii si kwa bitcoin tu, inatumika kwenye vitu vingine mfano kutunza medical records, kutunza biometric information kama fingerprint hash ambazo zinaweza kutumika kwenye mambo kibao. Mfano Dubai international airport kufikia 2022 ukienda hupiti getini kuchekiwa passport sijui visa, wanaondoa matumizi ya makaratasi yote, utakua unapita kwenye mlango unaweka kidole, data yako inavutwa kutoka kwenye blockchain, computer ishajua we ni nani inakuruhusu upite kama unaruhusiwa.

Tatizo moja la bitcoin ni kua haitabiriki, leo 1bt ni $2,000+ kitu kinaweza tokea wakati wowote ukashangaa imeshuka hadi kufikia $500, au ikapanda hadi kufikia hata $10,000. Na tatizo jingine si rahisi kupata sehemu wanayotoa huduma ambazo unalipia kwa bitcoin, hasa kama upo Afrika sahau, kuuza na kununua bitcoin kwa Africa ni next to impossible, nje angalau wanajitahidi kuipush. Serikali zisipoleta pingamizi sana kwenye huu mfumo kuna uwezekano bitcoin ikatumika sana miaka ya mbele kuliko mfumo mwingine wowote wa pesa.
 
Madhumuni yake ilikuwa ni kurahisha utumaji na upokeaji wa pesa pasipo mtu wa kati ikimaanisha pesa inatumwa moja kwa moja kutoka mtumaji hadi mpokeaji tofauti na paypal ilivyo
kwa kuongezea

kwa sababu tunatuma na kupokea moja kwa moja (peer to peer) hupunguza gharama za kutuma pesa kwani gharama hazitegemei wingi wa fedha bali memory in bytes mfano unaweza tuma 1milion kwa buku na mwingine akatuma lak5 kwa bukujero.

kingine inawezesha malipo kuwa ya siri kwani naweza nikafanya biashara na wewe na nikakulipa bila ya ww kunijua na serikali kujua japo inahitaji uwe na software maalumu kama unataka usiri hususan zile za kuingilia darkweb mfano tor n.k

Ndio maana darkweb kuna biashara nyingi haram na halali zinafanyika kama vile madawa ya kulevya, hitman(kumwajiri mtu akuulie mtu), hacking(kuna jamaa wana hack kwa malipo iwe vyuoni kubadili matokeo au taasisi yoyote), magaidi vyote hivyo vimewezekana kwa kupitia bitcoin kwani pesa inatumwa bila kujua wahusika ni akinanani(kumbuka kwa kupitia software ndio usiri waweza kufanyika)
 
Hii pesa ninaweza kuidraw na kuitumia kwa matumizi ya kawaida?
mfano. Nina hela kwenye mpesa, nitaweza kuitoa na kununua kitu chochote ninachotaka.
Je, bitcoin iko hivyo?

Ndio unaweza kuibadilisha kwenda ktk fedha yoyote ile hivyo unaweza kuitumia ile uliobadilisha ktk matumizi. Mfano kupitia local bitoin unaweza kununua bitcoin na kuziuza na biashara ni rahisi na salama cha msingi ni kujua inafanyaje kazi

kama unahela kwenye mpesa unaweza inunua hiyo na uka kaanayo baada ya siku kadhaa au kesho tu unaangalia soko likoje(huwa inapanda na kushuka thamini haraka kuliko pesa za kawaida)kisha unaiuza tena mfano tarehe 14/06/2017 ilikuwa 1bitcoin = Tsh 6,3000,000/= Ila leo ni milion5.8 so huwa inapanda na kushuka
 
Hii fursa hapana aseeh
Hii fursa ni nzuri sana ila kama huna uelewa usiwekeze kwani inahitaji uelewa mkubwa kidogo ukilinganisha na fursa nyingine kwasababu zifuatazo

unaweza kupata bitcoin bureee bila kufanya kazi kupitia bitcoin mining (1bitcoin = tsh 6,000,000)

unaweza nunua na kuhifadhi soko likipanda ukauza (soko hubadilika sana kupita maelezo ndani ya siku mbili au tatu tofauti inaweza kuwa mpaka 1milion)

unaweza wekeza kwa kulipia gharama za mitambo na umeme inayofanya kazi ya mining kisha bitcoin zinazopatikana wanagawa kutokana na shea
 
ok
 
Bitcoin ni pesa ya kielektroniki ambayo haimilikiwi na nchi wala serkali yoyote duniani, pesa hii hutegemea mzunguko katika soko kupata nguvu dhidi ya fedha zingine. pesa hii haitabiriki kuanzia utunzaji hadi nguvu yake.

Pesa hii imewahi kushuka thamani mara kadha kwanza kipindi ambacho tovuti iliyokuwa ikiuza dawa za kulevya huko darkweb ilipoharibiwa na FBI pili siku ambayo wadukuzi waliiba fedha hiyo kutoka soko la japan lililokuwa likiuza fedha hiyo.

lakini pia kuna changamoto kuitunza fedha hiyo baada ya kuinunua kutoka soko husika unapoinunua na kuitunza kwenye soko ulilonunua kuna hatari ya wadukuzi kuipitia, lkn unaweza kuitunza kwenye wallet yako kwenye komputa lkn unapaswa kuapdate wallet wakati wote la sivyo inapotea. mtu mmoja huko UK alipoteza hard disk ya pc yake ambamo alikuwa ametunza bitcoin yenye thamani ya $30 millioni hivyo kuwa makini unapoamua kufanya biashara hii

fursa na changamoto zinazopatikana katika fedha hii.
1.Kununua na kuuza bitcoin. kila mtu anauwezo wa kununua na kuuza bitcoin mahali popote duniani lakin biashara hii inahitaji uelewa wa hali ya juu kuhusu biashara hii kwasababu kunawatu wamewekeza fedha nyingi wakisubili wageni katika biashara hii ili wajipatie faida kupitia makosa yao.

2.kununua bitcoin na kuuza inapopanda. bitcoin hupanda kila mara na kila mwaka hivyo unaweza kuinunua na kuitunza kwa muda fulani kisha kuiuza kwa sasa 1bcn =2510.27 na hii ni kwa sababu wiki hii imeshuka ilitegemewa kufikia 4000 watalaamu wanasema ifikapo 2019 huenda ikafika 10000 bila shaka ukiitunza kufikia wakati huo utapata faida.

Thewajibu
ni wajibu wangu
MKUU IVI BITCOIN WALLET NZURI NI IPO
 
Back
Top Bottom