Labda kwa kuongezea.
Kwa nini bitcoin?
Pesa kawaida ina "central authority" yaani sehemu ambayo inacontrol, kawaida ni banks. Mfano pesa ya Tanzania mwenye control kubwa ni Bank of Tanzania.
Bitcoin ilitengenezwa kwa dhumuni kua hakuna central authority, yaani haiwezi kua controlled na institution moja, kwa sababu inarun kwenye mfumo unaoitwa blockchain ambao upo distributed kwa mtu yeyote yule, kwa lugha nyingine controlling institution ni kila mtu, kutokua na sehemu moja inayocontrol hii pesa kuna faida zake :
Kwanza kabisa mtu hawezi kuhack akaiba au kuchange data, kwa kua ili kuhack itabidi uhack computer milioni kadhaa ambazo zipo distributed kila kona, ni kazi sana kumhack kila mtu, bank unaweza hack data points zao ukawaangusha ila sio watu ambao wapo connected kwenye blockchain.
Pili kutuma na kupokea fedha ni rahisi zaidi, kwa kua haipitii bank, ukitaka kutuma bitcoin kutoka Tanzania kwenda Japan mfano, unaandika wallet number ya unayemtumia hapohapo inakua ishafika anaenda anatoa anapotaka, ni bure, labda gharama atakazolipia ni wanaocharge kufanya exchange kutoka bitcoin kwenda currency husika. Ni rahisi, faster na cheaper kuliko hata hizi western union au moneygram services.
Tatu kuna kitu kinaitwa immutability, yaani record ikiwekwa imewekwa haiwezi kubadilishwa, blockchain ndivyo inavyofanya kazi, kila transaction unayofanya ikiwekwa kwenye record ndo inakua imetoka hivyo, huwezi fanya chochote kile, sasa hii si kwa bitcoin tu, inatumika kwenye vitu vingine mfano kutunza medical records, kutunza biometric information kama fingerprint hash ambazo zinaweza kutumika kwenye mambo kibao. Mfano Dubai international airport kufikia 2022 ukienda hupiti getini kuchekiwa passport sijui visa, wanaondoa matumizi ya makaratasi yote, utakua unapita kwenye mlango unaweka kidole, data yako inavutwa kutoka kwenye blockchain, computer ishajua we ni nani inakuruhusu upite kama unaruhusiwa.
Tatizo moja la bitcoin ni kua haitabiriki, leo 1bt ni $2,000+ kitu kinaweza tokea wakati wowote ukashangaa imeshuka hadi kufikia $500, au ikapanda hadi kufikia hata $10,000. Na tatizo jingine si rahisi kupata sehemu wanayotoa huduma ambazo unalipia kwa bitcoin, hasa kama upo Afrika sahau, kuuza na kununua bitcoin kwa Africa ni next to impossible, nje angalau wanajitahidi kuipush. Serikali zisipoleta pingamizi sana kwenye huu mfumo kuna uwezekano bitcoin ikatumika sana miaka ya mbele kuliko mfumo mwingine wowote wa pesa.