Historia ya Kiwanda cha Tanganyika packers mpaka kuja kuwa Kanisa la maombi

Historia ya Kiwanda cha Tanganyika packers mpaka kuja kuwa Kanisa la maombi

Mada nzuri ila sijaona umuhimu wa kumchomeka Mwamposa!!
Umuhimu upo, to get the mass notified of the current status of Tanganyika parkers! Kwamba badala ya kukifufua kiwanda wanamkodisha/walimpa Mwamposa.
 
Wabongo wote sio serikali tu. Hao serikali wanaonekana sababu wapo kwenye spotlight ila hata kwenye private sector wabongo wanazingua sana.
Inategemea na private ipi kaka kuna zile private ambazo wenye kampuni wako kiwanja hao atleast bizness wanaziwekea mkazo ila kampuni mama imezaliwa hapa hapa mtaimba haleluya
 
Pamoja na maelezo yako yooote!! Dakika za jioooooni nimegundua una chuki binafsi na mwamposa !! Uchungu wako sio kiwanda kufa ni kanisa kuwekwa pale !! Kwa taarifa fupi viwanda vilivyokufa Tanzania vinaweza kufika hata 500! Vyote ni magofu ikiwemo zzk mbeya !! Jambo la pili mwamposa pale ni mpangaji analipa Kodi ya pango isiyopungua milioni 5 Kila wiki !! Hajapewa Bure !! Habari ya mafuta na udongo havihusiani na mada yako !! Hizo ni chuki kwa kanisa la mwamposa na sio kwa serikali iliyoruhusu kiwanda kife kizembe !! Hata kama wasingemkodishia mwamposa Bado kiwanda kisingerudi mjinga mkubwa wewe !
Zombie linapokurupuka kumtetea mfugaji wao .... Hii nchi Ina wajinga wengi sana.... unauziwa udongo wa upako ambao yeye hatumii.... Anakuuzia mafuta ya upako,mara keki ya upako ...aseee wajinga ni wengi sana....
 
Tuliyoambulia kula nyama zile za kwenye kikopo za mwisho mwisho
Hapo tanganyika packers hebu like hapa
Nakumbuka kile kikopo kilikuwa na kama kiufunguo unakinyonga dah

Ova
Afu wakaja wazeee wa mazingaombwe Tanzania ya viwonder tukawa tunachora as if waliua hvyo viwanda ni watu wa mongolia
 
Pamoja na maelezo yako yooote!! Dakika za jioooooni nimegundua una chuki binafsi na mwamposa !! Uchungu wako sio kiwanda kufa ni kanisa kuwekwa pale !! Kwa taarifa fupi viwanda vilivyokufa Tanzania vinaweza kufika hata 500! Vyote ni magofu ikiwemo zzk mbeya !! Jambo la pili mwamposa pale ni mpangaji analipa Kodi ya pango isiyopungua milioni 5 Kila wiki !! Hajapewa Bure !! Habari ya mafuta na udongo havihusiani na mada yako !! Hizo ni chuki kwa kanisa la mwamposa na sio kwa serikali iliyoruhusu kiwanda kife kizembe !! Hata kama wasingemkodishia mwamposa Bado kiwanda kisingerudi mjinga mkubwa wewe !
Kama hilo ndio wazo lake basi pale Mwamposa haondoki leo wala kesho ana watu wengi na serikali inawaheshimu na kuwategemea sana watu wanaoheshimika na jamii.

Mwamposa ana media anafuatiliwa nchi nyingi na Tanzania nzima, halafu hana bifu na serikali na mama Samia huwa anapeleka sadaka yake.
 
Kama hilo ndio wazo lake basi pale Mwamposa haondoki leo wala kesho ana watu wengi na serikali inawaheshimu na kuwategemea sana watu wanaoheshimika na jamii.

Mwamposa ana media anafuatiliwa nchi nyingi na Tanzania nzima, halafu hana bifu na serikali na mama Samia huwa anapeleka sadaka yake.
Waooooh,,
 
Zombie linapokurupuka kumtetea mfugaji wao .... Hii nchi Ina wajinga wengi sana.... unauziwa udongo wa upako ambao yeye hatumii.... Anakuuzia mafuta ya upako,mara keki ya upako ...aseee wajinga ni wengi sana....
Mjinga ni wewe unaepakwa majivu usoni,na kubebeshwa misalaba shingoni na kuzisujudia sanamu za akina maria ,huku mkipewa maji yenu mnayoyaita ya baraka !! Tafuta hela acha wivu WA kimaskini !!
 
(Liebig’s Extract of Meat Corporation) l
Mazungumzo yaanze waitwe, Tukae meza moja, tuone tu nafanyaje!,
°mwekezaji aje na program za kuprocess,
-ngozi
-Kwato
-pembe
-chakula cha mifugo (kuku), kwa damu za ngombe!
-vyakula vya mbwa na paka!
Acha tu, hizo habari za wawekezaji ni rahisi kuziandika mitandaoni. Serikali ikija na mipango hiyo wewe mwenyewe utakuwa wa kwanza kupinga na wengi tu.

Rais Ali H Mwinyi alikuja na mipango hiyo, alipigwa mawe mpaka akaingia mtini. Mashariki ya kati inaagiza nyama toka Ulaya na Brazil ni ghali kwao. Wameomba mara nyingi kuwekeza katika sekta hiyo TZ, lakini kila serikali inayotaka kushughulikia hilo wanakumbana na watanzania vichwa ngumu na mpango unatafuta kaburi.

Tatizo kubwa sio CCM bali watanzania wenyewe wepesi wa kulalamika lakini wagumu wa kukubaliana na ufumbuzi wa matatizo. Fikiria mwenyewe toka tufungue nchi mwaka 1991 mpaka leo katika sekta muhimu kama hiyo, kweli asipatikane mwekezaji hata mmoja makini toka nje kuwekeza katika eneo hilo.

Mpaka watanzania hawajafunguka macho, CCM haiwezi kufanya miujiza yeyote.
 
Mjinga ni wewe unaepakwa majivu usoni,na kubebeshwa misalaba shingoni na kuzisujudia sanamu za akina maria ,huku mkipewa maji yenu mnayoyaita ya baraka !! Tafuta hela acha wivu WA kimaskini !!
Kanunue udongo Mama.... Hivyo vyote tunapewa bure .... Shida ni nyie mnaouziwa mafuta na udongo wa upako.....
 
SERIKALI YA CCM KAMA SIYO KUROGWA NI NINI?

Tanganyika Packers LTD, Kawe, Dar es Salaam 1945-1975. Kilikuwa kiwanda cha kuchakata na kusindika nyama kwa ajili ya kuuza ndani na nje ya nchi.

Eneo lote la Mloganzila (Muhimbili) lilikuwa ni eneo la Tanganyika Packers na ndilo eneo lililokuwa linatumika kuwapokea na kunenepeshea ng’ombe

Walipoletwa kutoka mikoani kwa treni wakiteremshwa stesheni ya Pugu, baada ya mwezi wanaswagwa kupelekwa Kawe kuchinjwa na kuchakatwa.

Kutoka Mloganzila kwenda kilipo kiwanda wakati wa kuswagwa, waingereza waliita COWS WAY (njia ya ng’ombe). Waswahili wakashindwa na kuita “KAWE”

Tanganyika Packers (TPL) kilikuwa kiwanda kikubwa, kikisindika nyama za kusaga kwenye makopo na kusafirisha nje mpaka kwa malkia wa Uingereza,

Kilikuwa kiwanda tanzu cha shirika la LEMCO (Liebig’s Extract of Meat Corporation) linalofadhiliwa na Uingereza, ambalo lilianzia miaka ya 1860 Uruguay.

Liebig ni heshima ya baba wa (Organic Chemistry), Justus von Liebig. Jengo la machinjio la LEMCO lipo kwenye orodha ya Urithi wa Dunia wa UNESCO.

Sehemu kubwa ya nyama kutoka Tanganyika Packers iliuzwa Ulaya hususani katika nchi ya Uingereza. Watanganyika walipata ajira katika kiwanda hicho.

Kiwanda cha Tanganyika Packers kilijengwa na wakoloni kutoka Uingereza 1945 na kilitoa zaidi ya ajira 2,500 ambapo 1,200 zilikuwa ni ajira za kudumu.

Walifanya kazi kwa shift, walichukuliwa kwa mabasi kazini. 1975 serikali ilikitaifisha kutoka kwa waingereza kuingia serikalini kufuatia sera za ujamaa.

Kiwanda cha TPL kilizalisha nyama za mabuchani, mafuta ya kutengeneza sabuni, damu ilikaushwa na mifupa ilisagwa na kuwa chakula cha kuku,

Pembe na kwato za ng’ombe zilichemshwa kwenye boiler zikatoa gundi, kiwanda pia kilisindika nyama na maharage kama ox-tail beans, ngozi nk

Katika vita ya Kagera 1978-1979, kiwanda kilitumika kuwalisha wapiganaji vitani. Chakula cha kusindika kilitoka kiwandani kwenda uwanja wa vita.

Mwaka 1975 Serikali ya Mwl, J.K. Nyerere ilitaifisha kiwanda cha Tanganyika Packers na kukifanya kuwa mali halali ya Serikali ya Tanganyika.

Baada ya Serikaki kutaifisha kiwanda, uzalishaji na ubora wa nyama iliyosindikwa ulipungua kwa kiasi kikubwa sana kwa kukosa utaalam na ufundi.

Serikali walinyimwa leseni ya kusafirisha nyama iliyosindikwa. Walinyimwa (phytosanitary certificate) kuthibitisha ubora wa vyakula vya package

Waingereza wakawanyima cheti cha ubora na usafi wa nyama inayozalishwa. Soko la Ulaya ambako ndiyo walikuwa wanunuzi wakubwa likapotea.

Soko la ndani likawa gumu kiwanda kikaanza kusambaza nyama zake kwenye mabucha ya ndani ya Dar es Salaam na baadae kiwanda kikafariki 1993

Taratibu kiwanda cha Tanganyika Packers kikaanza kufariki. Baadaye kilibinafsishwa kwa mbunge wa Kawe, hata hivyo aliishia kuuza mashine na vipuri.

Mbunge wa Jimbo la Kawe wakati huo alitokana na CCM, aliitwa Zainuddin Adamjee. aliposhindwa Kukiendeleza akaamua kung’oa mitambo na vipuri.

Mapaa, madirisha, milango na vifungashio vilipelekwa Mapambano (veterinary) na kupimwa kama vyuma chakavu na mapaa kuuzwa kama used.

Picha chini, zinaonesha ng’ombe wakiwa Tanganyika Packers kabla kiwanda hakijataifishwa. Video kushoto inaonesha gofu la kiwanda hicho lilivyo leo

Leo pale Tanganyika Packers palipokuwa KIWANDA kilichotoa ajira zaidi 2000, pamefunguliwa KANISA. Watu wanauziwa udongo na mafuta na maji.



Leo pale Tanganyika Packers watu ndiyi wanakondoo na wanajipekeka wenyewe machinjioni. Wananyeshwa maji na kulishwa udongo wakielezwa ni UPAKO.

Kanisa hilo la MWAMPOSA (wao wanamuita MTUME) linawaombea maelfu ya vijana waliomaliza vyuo vikuu wakakosa ajira ili wapate ajira kwa maombi.

Maelfu ya vijana wanakesha na kufunga kwake, wananunua mafuta na maji ya UPAKO wapate KAZI. MWAMPOSA anajenga hoteli kubwa MBEYA.

Aliyewaroga watawala wa CCM na watanzania alikufa zamani na dawa ya kuwasaidia aliitupa katikati ya bahari na haiwezi kupatikana leo au kesho.

Mazombi. MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.

C&P from X by MMM
Hawa wazaramo jau sana isee yaani badala ya cow way wakaita kaww😂😂🤣
 
Badala ya ng'ombe kupelekwa kuchinjwa ni watu wananjichwa kiimani. Ukiowaona watu wanavyotaabika na jua na usafiri ndio machinjo yenyewe. Kuwa na umati mkubwa kiasi hicho ni ",ushirikina " uliokubuhu.
 
Wakenya wametupita sana kwa maamuzi kama hayo ya utaifishaji. Kitu cha kushangaza, "unataifisha unawapa wapigaji". Wapigaji wa enzi hizo ndio matajiri wa leo. Chunguza makampuni ya biashara ya wakati ule, mafisadi walivyokula kilaini.
 
Back
Top Bottom