NI MFULULIZO WA HISTORIA YA KWELI YA MAUAJI YA KIMBARI YA RWANDA
Sehemu ya tano.
Ni jambo la kusikitisha sana kwamba Historia yetu ambayo watoto wetu wanafundishwa mashuleni na kuandikwa kwenye vitabu imechujwa mno kiasi kwamba inakuwa kama ni hadithi tu za kusadikika.
Kwa mfano kama umebahatika kuijui historia ya ukweli kuhusu Vita ya Kagera kisha ukasoma 'version' ambazo zimeandikwa kwenye vitabu na kuaminishwa kwa umma, machozi yanaweza kukutoka.
Ubaya ni kwamba hata wale ambao wamebahatika kujua ukweli halisi wa matukio na vilivyo nyuma ya pazia hawawezi kuthubutu kutia mkono na kuandika kile ambacho wanakijua.
Ndio maana naamini ni busara hata kwangu pia niandike kwa sehemu kile ambacho historia zetu hakivisemi lakini pia ni muhimu kuandika kwa "ustaarabu" kwa faida ya pande zote.
Kutengenezwa kwa Jasusi Paul Kagame
Katika sehemu iliyopita nilieleza kwamba, Paul Kagame mwaka 1977 alitembelea nchi ya Rwanda ambapo hakuwahi kuikanyaga tangu alipokuwa mtoto wa miaka miwili tu. Paul Kagame alifanya safari hii kutokana na kukosa amani ndani ya moyo wake. Alikuwa anatafuta 'kusudi' lake la maisha. Katika kipindi hiki alikuwa amempoteza baba yake mzazi na pia rafiki yake kipenzi Fred Rwigyema alikuwa amepotelea kusikojulikana.
Kwa hiyo Paul Kagame alienda Rwanda kwa ajili ya 'soul searching'. Alikuwa anataka kupata hamasa kwenye roho yake ili aweze kujua kusudi la maisha yake.
Kutokana na historia ya familia yake kuwa na ushawishi kwa kiasi fulani (nilieleza kwamba baba yake ana undugu wa kiukoo na Mfalme Kigeli na mama yake ana undugu wa damu na Malkia wa mwisho wa Rwanda) kwa hiyo hizi safari zake za Rwanda alizifanya kwa siri kubwa pia ukizingatia kwamba serikali ilikuwa makini sana na watusi ambao wako nje ya Rwanda kama wakimbizi kutokana na harakati zao na kiu yao ya kutaka kuipindua serikali mara kwa mara.
Safari hii ilikuwa ya maana sana kwa Kagame na alijenga 'connection' ambazo zilikuja kumsaidia sana miaka ya baadae kwenye harakati zake.
Mwaka 1978 alifanya safari nyingine kwenda Rwanda na safari hii hakupitia mpaka wa Uganda bali aliingia kupitia Zaire (Congo). Kwa wiki kadhaa ambazo alikaa Kigali kwa siri kubwa, alitumia muda huo kuimarisha 'connection' ambazo alikuwa nazo na pia kusoma hali ya kisiasa na uimara wa serikali.
Safari hizi mbili ziliamsha hari kubwa mno katika nafsi ya Paul Kagame. Aliona kwa uhalisia kabisa mateso na manyanyaso ambayo watusi walikuwa wanapitia nchini Rwanda. Akajihisi kabisa kwamba alikuwa ana jukumu la kufanya kitu kuyamaliza mateso hayo.
Aliporejea nchini Uganda Kagame akageuka kama mwanaharakati hivi katika kambi za wakimbizi akihamasisha vijana wenzake kujizatiti na kuweka mipango ya kuikombia Rwanda.
Wakati huo huo, rafiki yake Fred Rwigyema ambaye alipotea bila yeyote kujua ni wapi alikuwa ameelekea… alikuwa nchini Tanzania katika kambi ya FRONASA chini ya uongozi wa Yoweri Musseveni ambao walikuwa wanaweka mikakati ya kumuondoka madarakani Dikteta Idd Amin.
Habari kuhusu kijana mahiri, mwanaharakati Paul Kagame zilimfikia Yoweri Musseveni na alitamani awe sehemu ya 'timu' yake.
Ndipo hapa ambapo Fred Rwigyema ambapo ndio kwanza alikuwa amerejea Tanzania kutoka msumbuji ambako alipelekwa na Musseveni kwenye mafunzo ya pamoja na wapiganaji FRELIMO juu ya vita za msituni…alitumwa kwenda nchini Uganda kwa ajili ya masuala kadhaa lakini mojawapo ilikuwa kumshawishi Paul Kagame kujiunga na wapiganaji wa Yoweri Musseveni walioko nchini Tanzania.
Sasa basi…
Kuna mahala mkoani Morogoro, sitapaja kwa jina au exactly sehemu gani… lakini ni nje ya mji kidogo kuna 'Espionage Farm' ya siri ambayo mwaka 1978 Paul Kagame na maafisa kadhaa wa kikundi cha FRONASA walikuwa recruited na kupata mafunzo ya Ujasusi na masuala ya Intelijensia.
Niseme kwamba Paul Kagame ni moja ya maafisa bora na hodari kabisa kuwahi kuzalishwa na Idara yetu Usalama wa Taifa.
Kagame amewahi kutumia kwenye 'high profile missions' kadhaa lakini kubwa zaidi ni ile ambayo aliongoza kikosi cha Intelijensia ya wapiganaji wa UNLA (Ugandan National Liberation Front) katika vita ya Kagera.
Tofauti na historia ilivyoandikwa kuhusu vita ya Kagera, lakini ukweli na uhalisia ni kwamba wapiganaji wa UNLA ambao walikuwa ni zaidi ya 20,000 walikuwa ni kiungo muhimu sana katika ushindi wa vita ya Kagera. Suala hili tutalizungumzia siku moja kama tukipata wasaa wa kuichambua vita ya Kagera.
Kuna kikao cha siri sana kilifanyika pale Moshi ambacho kinajulikana kana "Moshi Conference" ambacho kiliudhuliwa na watu adhimu kabisa wapatao 28 na mmoja wao alikiwa Paul Kagame.
Katika kipindi hiki, Rais ambaye alikuwa amepinduliwa na Amin na kukimbilia Tanzania, Bw. Milton Obote alikuwa na kikundi chake cha wapiganajia ambacho alikiita kwa jina la Kiswahili "KIKOSI MAALUM" ambacho makamanda wake walikuwa ni Tito Okello na David Oyite Ojok. Hawa nao pamoja na Obote mwenyewe walikuwepo kwenye kikao cha mjini Moshi.
Pia Yoweri Musseveni alikuwepo kuiwakilisha FRONASA. Pia walikuwepi wanaharakati wengine mashuhuri kama vile Akena p'Ojok, William Omaria, Ateka Ejalu, Godfrey Binaisa, Andrew Kayiira, Olara Otunnu pamoja na baadhi ya 'wakubwa' kutoka kwenye vyombo vya ulinzi vya nchi yetu ambao kwa sababu ya 'staha' sitaandika majina. Jumla walikuwa watu ishirini na wanane.
Kikao hiki kilizaa mpango mkakati wa kijeshi ambao ndio ulitumika kwenye vita ya Kagera na kumshinda Amin. Paul Kagame ndiye ambaye alibebeshwa mzigo wa mikakati ya Intelijensia ya kijeshi.
Octoba 1978 tukaingia vitani dhidi ya majeshi ya Amin. Licha ya swahiba wake Kanali Muammar Gaddafi kutuma wapiganaji 2,500 pamoja na silaha nzito za mivita na za kisasa kwa kipindi hichi kama vifaru aina ya T-54, T-55, magari ya kivita ya kisovieti aina ya BTR APC na Grad MRL pamoja na ndege za kivita aina ya MiG 21 na ndege hatari za kivita (supersonic bombers) aina ya Tu-22 kumsaidia Amin… ajabu ni kwamba licha ya majeshi ya amini kuwa imara kiasi hiki kwa maana ya vifaa vya kivita lakini mwanzoni mwa mwezi April 1979 tulimpiga Amin mpaka "Ikulu" na kumlazimu kukimbilia Libya kwa swahiba wake Gaddafi na baadae kukimbilia Saudi Arabia.
Siku moja kabla ya kutangaza kuisha kwa vita ya Kagera, yaani April 10 Tanzania tukamsimika Yusufu Lule kuwa Rais mpya wa Uganda. Yusufu Lule ameishi sana hapa Tanzania hasa baada ya Idd Amin kuingia madarakani.
Pamoja na hilo lakini akina Musseveni nao waliunda chombo chao cha kijeshi ambacho kiliitwa National Consultative Commission (NCC). Hiki kwa kiasi fulani ndio walikifanya kama chombo chenye maamuzi ya mwisho kuhusu nchi.
SILAHA NZITO ZA KIJESHI AMBAZO UGANDA ILIPOKEA KUTOKA KWA KANALI GADDAFI
Gari za kivita aina ya BTR APC
Miezi miwili tu baada ya majeshi ya Tanzania kumsimika Yusufu Lule kuwa Rais, kukaanza kutokea mvutano mkali kati ya NCC ya kina Musseveni na Rais Yusuf Lule. Mvutano huu ulikuwa ni juu ya mamlaka ya Rais ambayo NCC walimuona Lule kama anavuka mipaka yake. Lule naye kwa upande wake alikuwa anaonekana hataki nchi kuingozwa na jeshi (NCC).
Hatimaye tarehe 10 June mwaka huo 1979 NCC kwa ushawishi mkubwa wa Musseveni wakamuondoa madarakani Godfrey Binaisa kuwa Rais mpya wa Uganda.
Kimsingi Binaisa alikuwa kama 'kikaragosi' tu lakini kiuhalisia NCC ndio walikuwa wanaongoza nchi.
Lakini taratibu naye utamu wa madaraka ukaanza kumkolea.
Ikumbukwe kwamba katika kipindi hiki chote Milton Obote bado alikuwa nchini Tanzania hajarejea Uganda.
Kulianza kuzuka taarifa kwamba mnadhimu mkuu wa jeshi Brigedia Jenerali David Oyite Ojok ambaye kipindi cha vita ya Kagera alikuwa kamanda wa jeshhi ka pamoja la Tanzania na UNLA, alikuwa anafanya maandalizi ya kuhakikisha Obote anarejea Uganda.
Jeneralari Ojok anatokea eneo la kaskazini mwa Uganda kama ilivyo kwa Obote. Licha ya Ojok kuanza mikakati ya kumrudisha Uganda Obote lakini pia kwenye jeshi nyadhifa za juu zote alikuwa anahakikisha zinashikiliwa na watu wanaotoka ukanda wa kaskazini mwa nchi.
Harakati zote hizi Binaisi aliziona kama juhudi za kumuondoa madarakani ili kusafisha njia kwa Obote kurejea madarakani.
Mwezi May 1980 Rais Godfrey Binaisa alimuondoa Ojok kwenye cheo cha Mnadhimu mkuu wa jeshi.
Suala hili lilipingwa vikali na NCC na wakafikia hatua ya kumuondoa madarakani Rais Binaisa na kuunda tume maalumu ambayo waliita Presidential Commision ambayo ndiyo ilifanya kazi ya kuongoza nchi badala ya Rais.
Tume hii wanakamati wake walikuwa ni Museveni, Oyite Ojok, Okello na Muwanga.
Muwanga alipewa cheo cha uenyekiti wa tume japokuwa kiuhalisia wenye nguvu za ushawishi kwenye tume walikuwa ni Museveni na Ojok.
Baada ya hapa ndipo ambapo hasa umahiri wa Paul Kagame unaonekana. Ikumbukwe kwamba wakati yote haya yaliendelea Paul Kagame alikuwa na ushawishi mkubwa sana kwenye jeshi la Uganda kutokana na umahiri wake wa masuala ya Intelijensia. Kwa hiyo yeye ndiye ambaye alikuwa anawashauri ni nani anafaa kuwa Rais na nani hafai.
Baada tu ya nchi kuanza kuongozwa na Tume maalumu niliyoitaja hapo juu, Ojok akaanza tena mipango ya kumrejesha Milton Obote ndani ya Uganda. Ilikuwa wazi kwamba Ojok alikuwa anataka Obote ashike madaraka. Lakini watu wengi wa kabila la Baganda/Waganda walikuwa wanampinga Obete kwa kuwa yeye ndiye ambaye alimpindua Mfalme wao wa Baganda miaka kadhaa nyuma na kushika Urais kabla ya yeye pia kupinduliwa na Ids Amin. Kwa hiyo kulikiwa na mvutano kati ya watu wa maeneo ya kaskazini na kusini mwa Uganda.
Ndipo hapa ambapo Paul Kagame akaona fursa. Kwamba 'vita ya panzi, furaha ya kunguru'.
Yoweri Museveni yeye hatokei Kusini wala Kaskazini mwa Uganda… yeye amezaliwa na kukulia eneo la magharibi mwa nchi linalopakana na Rwanda sehemu inaitwa Ntungamo. (Hii ni moja ya sababu ya baadhi ya watu kuamini ana asili ya Kitusi).
Kwa hiyo huu ugomvi wa watu wa kaskazini na wa kusini haukuwa na mslahi nao kabisa. Ndipo hapa kwa kushauriana na Paul Kagame wakaanza michakato ya siri pembeni ya kujitenga na NCC na UNLA japokuwa Museveni alikuwa na ushawishi kwenye vyombo vyote hivyo.
Hatimaye mwaka 1980 Milton Obote alirejea Uganda na kushiriki kwenye uchaguzi mkuu mwaka huo na "kushinda". Matokeo ya uchaguzi yalipingwa vikali na watu wengi akiwemo Yoweri Museveni.
Ndipo hapa ambapo Yoweri Museveni, Pual Kagame na Fred Rwigyema pamoja na Waganda wengine thelathini na saba tu walianzisha kikundi chao cha kijeshi walichokiita National Resistance Army (NRA) lengo kuu likiwa ni kumuondoa madarakani Rais mpya Milton Obote.
Kikundi hiki kiliendesha mapigano ya msituni dhidi ya majesho ya serikali kwa karibia miaka sita.
Licha ya udogo wake kwa idadi ya watu (japo baadae waliongezeka kuzidi watu arobaini wa awali) lakini ufanisi wao kwenye kushambulia kwa uhodar na kulichosha jeshi la serikali ulikuwa wa hali ya juu. Miaka hii sita ya kupambana na majeshi ya serikali yalidhihirisha namna ambavyo Paul Kagame alikuwa ni nguli wa 'psychological warfare' ambayo pia ilikuja kudhihirika kipindi cha mauaji ya kimbari (tutaongelea zaidi tukifika hapo).
Katika kipindi hiki cha vita kwa masuala ya kijeshi Paul Kagame alikuwa mtu muhimu na mwenye kuheshimika zaidi na wapiganaji wa NRA kuzidi hata Museveni mwenyewe. Nyadhifa zao ndani ya NRA zilikuwa karibia kwenye usawa mmoja.
Kwa upande wa jeshi la serikali hali ilianza kuwa tete. Kukaanza kutokea mifarakano ya kikabila kati ya wenyewe kwa wenyewe. Kaskazini mwa Uganda kuna makabila makuu mawili, Walangi (kabila wanalotokea Obote na Ojok) na Waacholi (kabila la Tito Okello ambaye kwa kipindi hicho alikuwa kamanda wa jeshi).
Askari wengi wa miguu walikuwa ni Waacholi na ndio ambao walikuwa wanakufa zaidi kwenye vita hiyo dhidi ya NRA. Walangi wengi walikuwa ni maafisa wa jeshi na 'Special Forces'. Kwa hiyo askari wa miguu wakaanza kushinikiza serikali ifanye mazungumzo na NRA na kumaliza vita.
Yoweri Museveni na wapiganaji wa NRA msituni
Serikali ikafanya shingo ngumu na kukataa.
Wanasema lakuvunda halina ubani, mwezi Desemba 1983 Oyite Ojok alifariki kwa ajali ya ndege ambayo kuna kila dalili ya mkono wa Kagame. Kwa kipindi hicho Ojok ndiye alikiwa mkuu wa jeshi la Uganda. Ilikuwa inategemewa Obote amteue Tito Okello au mwenzake mwingine aliyeitwa Bazilio Olara-Okello (hakuna undugu wa damu kati yao licha ya kufanana ubini japo wanatokea kabila moja la Waacholi) ambaye naye alishiriki vita ya kumuondoa Idd Amin. Lakini ajabu Obote alimteua afisa wa chini kabisa wa jeshi aliyeitwa Smith Apon-Achak ambaye anatoka kabila lake la Walangi kuchukua nafasi ya Oyite Ojok. Hii iliwafanya wanajeshi wenye asili ya kabila la Waacholi kumchukia Obote na serikali yake na hatimaye miaka miwili baadae kumpindua kutoka madarakani.
Baada ya Miltob Obote kupinduliwa na jeshi kutoka madarakani kukaanza mapigano baina ya vikundi vya msituni kila kimoja kikitaka kushika usukani wa kuongoza nchi. Ndipo hapa yalifanyika maongezi ya pamoja baina ya vikundi vyote vya msituni nchini Kenya chini ya Rais Daniel Arap Moi ili kuleta suluhu na kuweka muelekeo mpya wa nchi ya Uganda.
Tarehe 29 January mwaka 1986 Yoweri Kaguta Museveni akaapishwa kuwa Rais mpya wa Uganda.
Paul Kagame akateuliwa na Rais kuwa Chief of Millitary Intelligence.
Swahiba wake Fred Rwigyema akateuliwa kwenye wadhifa wa Waziri wa Ulinzi.
Pia baraza la mawaziri lilikuwa limejaa watusi kibao.
Kwa maneno mengine tunaweza kusema kuwa Paul Kagame alikuwa ameiweka Uganda kwenye kiganja chake cha mkono japo hakuwa Rais. Lakini mtandao wa ushawishi ambao alikuwa ameujenga ndani ya serikali ya Uganda, baraza la mawaziri na kwenye jeshi ulikuwa ni mkubwa na una nguvu zaidi hata ya Yoweri Museveni ambaye aliapishwa kuwa Rais. Uzuri ni kwamba Museveni anafahamu umahiri wa Paul Kagame na hakutaka kutengeneza mvutano wowote naye kwa kuwa alikiwa anajua lengo kuu la Kagame lilikuwa ni lipi. Kagame hakuwa na nia yoyote ile ya kuwa Rais wa Uganda au kuendelea kuliendesha jeshi la Uganda. Ndoto yake ilikuwa ni moja tu, ndoto ambayo aliipata mwaka 1978 alipotembelea kwa siri nchi yake ya Rwanda, kwamba siku moja anataka kuwaokoa ndugu zake watusi kutoka kwenye unyanyasaji, kuuwawa, kudhalilishwa na mateso ambayo walikuwa wanapitia katika nchi yao.
Na sasa alikuwa amekamilika kwa kila kitu. Alikuwa na uzoefu wa kutosha. Alikuwa na weledi wa kutosha, tunaweza kuthubutu kusema kwamba katika kipindi hiki hakuna ambaye alikuwa anaweza kufikia daraja la umahiri wa Kagame katika masuala ya Ujasusi Afika Mashariki yote.
Lakini pia alikiwa na ushawishi katika nchi za kimakakati ambazo zinapakana na Rwanda, kwa maana ya Congo (huku aliwapeleka wapiganaji wa NRA kupata mafunzo ya siri ya Special Forces kipindi cha mapigano ya miaka 6 msituni dhidi ya majeshi ya serikali ya Milton Obote). Lakini pia alikuwa na ushawishi nchini Tanzania (mtoto wetu tuliyemfunza wenyewe ujasusi na alitusaidia sana kwenye vita ya Kagera). Na hakuna haja hata ya kusema kiwango cha ushawishi ambacho alikuwa nacho nchini Uganda.
Mbele yake kulikuwa na jambo moja tu la mwisho ambalo alikuwa anatamani litimie kabla hajaondoka juu ya uso wa dunia. Kuiweka nchi ya Rwanda mkononi mwake.
Itaendelea...
Sent using
Jamii Forums mobile app