Historia ya kweli ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda

Nasubiria kwa hamu sehem inayofuata

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwa kulitambua hili nadhani kagame Yuko much aware na amefaulu kwa kias fulani kudhibiti mifumo mingi ya kiusalama nchini mwake na nje ya mipaka.time will Tell anyways
iyo in kweli maana ukiangalia kwasasa yeye ndio mental wa East Africa na kila state inapenda kuwin influence toka kwake
 
ENDELEA KUPATA UHONDO KATIKA HISTORIA YA KWELI YA MAUAJI YA KIMBARI YA RWANDA

Sehemu ya saba

Katika sehemu ya sita nilieleza namna ambavyo RPF iliundwa na jinsi ambavyo jaribio la kwanza la kupindua serikali ya Rwanda likiongozwa na Fred Rwigyema lilikuwa na mafanikio makubwa katika siku ya kwanza tu lakini Fred aliuwawa katika mazingira ya kutatanisha sana kwenye siku ya pili tu ya jaribip hilo la mapinduzi huku tayari wakiwa wamedhibiti mji Kigali kutoka kwa majeshi ya serikali ya Kihutu.

Tuendelee…

KAGAME ANASHIKA USUKANI

Kifo cha Fred Rwigyema kilimshitua kila mtu na hasa hasa Rais Yoweri Museveni. Pasipo kuchelewa alipiga simu nyumbani Uganda (alikuwa bado hajarejea kutoka kwenye mkutano wa UN nchini Marekani) na akamuagiza mtu anayemuamini kwenye jeshi, kaka yake Salim Salehe kwenda Rwanda haraka kuchunguza tukio hili.

Nchini Rwanda mpaka leo hii moja ya mijadala ambayo ni 'mwiko' kuizungumza ni kifo cha Fred Rwigyema. Kama wewe ni mwandishi na ukajitoa ufahamu kuandika 'mawazo' yako kuhusu kifo cha Fred Rwigyema basi ndani ya siku chache jiandae kutembelewa na 'watu wasiojulikana'.
Hii ni kwasababu Fred Rwigyema mpaka leo hii anahesabika kama moja ya mashujaa wa nchi hiyo na anaheshimika zaidi na Watusi kama shujaa ambaye ana mchango mkubwa katika kufanikisha kuwatoa watusi kwenye mateso na manyanyaso ya Wahutu. Kwa hiyo hoja yoyote yenye mlengo wa kumbebesha lawama hizo mtu fulani aliye hai kwamba alihusika na kifo hicho zinazimwa ili kuepuka mtu huyo kuchukiwa na watusi wenzake.

Suala la kuuwawa kwa Fred Rwigyema limezua nadharia nyingi sana. Mwanzoni ilianza kuenezwa propaganda kwamba Fred Rwigyema ameuwawa na risasi ambayo ilipigwa kwenda kwingine lakini ikagonga mahala fulani na kubadili uelekeo na kwenda kumpata Rwigyema Kichwani. Nadharia hii imepigiwa upatu kwa muda mrefu sana na serikali ya Kagame. Lakini mwanzoni mwa miaka ya 2000s kuna ukweli ambao ulibainika na kufanya nadharia hii kugeuzwa tena.

Nimesema kwamba Rais Yoweri Museveni alimtuma kaka yake Salim Salehe ili kwenda kuchunguza tukio la kuuwawa kwa Fred Rwigyema. Mwanzoni mwa miaka ya 2000s iligundulika kwamba Salim Salehe na kikosi chake alipofika Rwanda aliondoka na makamanda wawili wa RPF ambao baadae waliuwawa walipofika mpakani mwa Rwanda na Uganda. Makamanda hawa walikuwa ni Peter Bayingana na Chris Bunyezi. Hawa walikuwa ni makamanda wasaidizi wa Fred Rwigyema.

Baada ya taarifa hii kuvuja mwanzoni mwa miaka ya 2000s serikali ya Rwanda ikaja na nadharia/propaganda kwamba Fred Rwigyema alipigwa risasi na mojawapo wa makamda hao baada ya kutokea mabishano wakiwa kambini. Kwamba Fred Rwigyema alitaka waweke mkakati wa kijeshi ambao utawafanya kusonga mbele taratibu lakini kwa hakika na hatimaye kuidhibiti Kigali yote sawa sawa na kuwadhibiti wapiganaji wa Kihutu. Lakini Bayingana na Bunyezi wao walitaka wasonge mbele kwa haraka na kwa nguvu kubwa ya kijeshi.
Serikali ya Rwanda inasema kwamba baada ya mabishano makali Bayingana alipandwa na hasira na kumtolea bastola Rwigyema na kumtandika risasi ya kichwa.

Huu ndio msimamo wa serikali ya Rwanda mpaka leo hii juu ya kifo cha Fred Rigyema.

Maelezo haya yana ukakasi katika viwango kadhaa.

Kwanza kabisa, heshima ambayo Fred Rwigyema alikuwa nayo kwa wapiganaji wa RPF si jambo rahisi kwa mwanajeshi yeyote kuthubutu kumnyooshea bunduli Fred Rwigyema.
Lakini pia Bayingana si mtu mwenye haiba ya hasira za haraka na paniki mpaka kufikia hatua ya kumuua ghafla kwa hasira kamanda wake katika uwanja wa vita.

Ukakasi zaidi unaletwa na ushahidi wa afisa mwingine wa ngazi za juu wa RPF ambaye alishuhudia Rwigyema akipigwa risasi, afisa huyu anaitwa Stephen Nduguta. Nduguta anasema kwamba hakumbuki wala hakushuhudia watu hao watatu wakibishana, kitu ambacho anakumbuka ni kwamba Bayingana ghafla tu alichomoa bastola kutoka kiunoni na kumfuata Rwigyema pale ambapo alikuwa amekaa na kumtandika risasi kichwani. Hii inaonyesha dalili kabisa kwamba alikuwa na dhamira ya kumuua… kana kwamba alipewa maagizo kutoka kwa mtu wa juu zaidi kufanya hivyo.

Maagizo hayo yalitoka kwa nani?? Kagame? Najaribu tu kufikiro kwa sauti…

Hii ni moja ya mijadala ambayo mpaka leo inahitaji uchunguzi zaidi na tafakuri ya kina. Ni bahati mbaya vile ambavyo serikali ya Rwanda inazuia kabisa mjadala huru juu ya kifo cha Fred Rwigyema.
[16/01, 02:40] The Bold: Baada ya taarifa hii ya kifo cha Fred Rwigyema kumfikia Kagame kule nchini Marekani kwenye chuo cha kijeshi cha Fort Leavenworth, Kansas, mara moja alitoa taarifa kwenye uongozi wa chuo kwamba anahitaji kuondoka mara moja kurejea Africa. Uongozi wa chuo ulimkubalia ombi lake hilo na pia kumruhusu kuondoka na vitabu kadhaa ambavyo huko baadae Paul Kagame alivitumia sana kupanga mikakati ya kijeshi.

Kagame aliruka kwa ndege mpaka London, na kisha Addis Ababa, na hatimaye kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe ambako alipokelewa na watu wa 'Usalama wa Taifa' wa Uganda na walimsafirisha mpaka mpakani na Rwanda.
Kagame alivuka mpaka na kuingia Rwanda siku ya tarehe 15 Octoba, 1990.
Kagame aliwakuta wapiganaji wa RPF wakiwa kwenye hali mbaya kweli kweli kinidhamu na morali. Kagame anaeleza kwamba kipindi hiki cha kwanza cha kuchukua mikoba kuiongoza RPF ni moja ya nyakati zake mbaya zaidi kwenye maisha yake. Wanajeshi hawakuwa na nidhamu na hawakuwa na kiwango cha kuridhisha cha morali. Kwa hiyo ilikuwa inamlazimu Kagame aanze kuwajenga upya wanajeshi wake kisaikolojia na kisha awajenge kwa uwezo wa kijeshi/kivita.

Jambo la kwanza kabisa ambalo Kagame alilifanya ni uamuzi wa kurudisha majeshi ya RPF nyuma. Hakuona busara au akili yoyote kuendelea kupeleka majeshi mbele vitani kwa hali mbaya ambayo aliwakuta nayo.
Kwa hiyo kwa wiki kadhaa baada ya kuchukua mikoba ya kuiongoza RPF Kagame pamoja na viongozi wengine wa juu wa RPF waliitumia muda huo kukusanya Intelijensia. Pia waliondoa vikosi vyao kutoka eneo la kaskazini mashariki mwa Uganda na kwenda kuweka makazi mapya kwenye eneo la milima ya Virunga. Nyuma waliacha wapiganaji wachache tu ambao walikuwa wanafanya mashambulizi madogo madogo ya kushitukiza dhidi ya vikosi vya serikali ambavyo walikuwa hawajui kwamba RPF wamehamishia makazi yao kwenye milima ya Virunga.

Kagame alichagua eneo hili la milima ya Virunga kutokana na ugumu wake wa kufikika. Kama ikitokea vikosi vya serikali wakigundua kuwa RPF wanajificha hapo kwa sasa itakuwa ni ngumu kuwavamia au kwafanyianshambulio la kusbitukiza. Kwa mfano ili kufika kileleni ambako wao walikuwa wameweka kambi ilikuwa ni safari ya wiki nzima kutoka vikosi vya serikali vilipo.
Lakini pia wakiteremka na milima hiyo kwa upande wa magharibi walikuwa wanashuka moja kwa moja na kuingia Uganda bila usumbufu wowote kutokana na ruhusa ya Rais Museveni.

Japokuwa milima ya Virunga ilikuwa ni sehemu mujaribu kabisa kuweka kambi kutokana na kuwapa faida ya kujilinda na kujihami lakini hali ya hewa ya eneo hili haikuwa rafiki. Milima ya Virunga iko mita 5,000 kutoka usawa wa bahari. Hakukuwa na vyakula wala miti ya matunda au mazao asili.
Mwanzoni wanajeshi wengi walikufa kwa baridi katika eneo hili. Lakini baada ya wiki kadhaa waliweza kuimudu sehemu hii na kuishi vyema.

Kagame alitumia miezi kadhaa akilijenga upya jeshi lake pasipo kuanzisha mashambulizi yeyote yale dhidi ya serikali ya Rwanda.

Paul Kagame ni 'born-tactician' na mtu mwenye akili nyingi sana. Na ni katika kipindi hiki ambacho sifa yake hii ilijidhihirisha kwa kiwango kikubwa zaidi.

Kuna bwana mmoja anaitwa Alexis Kanyarengwe. Huyu alikuwa ni mhutu na Kanali kwenye jeshi la Rwanda na mtu wa karibu sana na Rais Juvenile Habyarimana. Ilifika kipindi alitofautiana sana na Rais Habyarimana na ikabidi akimbie nchi ya Rwanda.
Kagame alimtafuta Alexis Kanyarengwe na kumshawishi ajiunge na RPF.
Kagame alifanya hivi makusudi ili kitendo hiki cha mhutu wa hadhi na kaliba ya Kanyarengwe kujiunga na RPF kutoa picha kwamba RPF ilikiwa 'inclusive', yaani ni kikundi chenye kujumuisha watu wa namna zote (Watusi na Wahutu) japokuwa uhalisia ni kwamba RPF ilikuwa ni kikundi cha watusi tena watusi waliozaliwa au kukulia Uganda.

Eneo la Milima ya Virunga

Ili kuonyesha zaidi 'nia yake njema' Kagame alimteua Kanyarengwe kuwa mwenyekiti wa kamati ya uratibu wa jeshi la RPF.

Kagame alianzisha ratiba kali ya mazoezi kwa wanajeshi wake kila siku. Na pia aliweka sheria kali ambazo wanajeshi wake walipaswa kuzifuata na kuziheshimu. Kwa mfano alitaka wanajeshi RPF wakienda kwenye vijiji vya karibu wanunue kile ambacho wanahitaji badala ya kuchukua kwa mabavu kama ambavyo imezoeleka kwa vikundi vya wapiganaji wa msituni. Pia wanajeshi wote wa RPF walipigwa marufuku kutumia pombe au dawa za kulevya na pia walitakiwa kuhakikisha wanakuwa watu wa mfano wa kuigwa wakiwa kwenye jamii za vijiji vya jirani.

Wanajeshi ambao walifanya makosa kama vile kuua, kubaka au kuasi RPF waliadhibiwa kwa kifo cha kupigwa risasi.

Hali hii ya nidhamu ya hali ya juu ya wanajeshi wa RPF iliwajengea sifa njema ambayo ilivuma kila mahala. Ghafla kulitokea idadi kubwa ya vijana hasa vijana wa kitusi kutoka Burundi, Zaire, Tanzania na Uganda ambao walijitolea kujiunga na RPF.

Kagame pia akaanzisha ofisi jijini Kampala ambayo ilikuwa na jukumu la kukusanya michango kutoka kwa watusi wenzao duniani kote ambao walikuwa tayari kuichangia RPF. Aloisia Inyumba ndiye alikuwa kamishna wa fedha kwenye ofisi hii ya Kampala.
Michango ilitolewa kutoka kwenye kila pembe ya dunia na hata kutoka ndani ya Rwanda kwa wafamyabiashara ambao walikuwa wamechoshwa na utawala wa kimabavu wa Rais Habyarimana.

Sifa njema ya RPF ambayo Kagame alifanikiwa kuijenga ndani ya muda mfupi ilifanya RPF nje ya medani ya vita, huko mitaani ionekane kama harakati fulani hivi za 'kibinadamu' ambazo zilikuwa zinapswa kuungwa mkono kwa nguvu zote.

Japokuwa fedha za michango walizopokea hazikuwa nyingi sana, lakini Kagame alikuwa ametengeneza utaratibu wa kuishi kwa kujinyima sana. Inajulikana namna ambavyo wanajeshi wa vikundi vya waasi na wapiganaji wa msituni namna ambavyo wanapenda kuishi maisha ya anasa iliyopindukia, starehe kila usiku na wakilala na kundi la makahaba au watumwa wa ngono. Lakini hii ilikuwa tofauti kabisa kwa Kagame yeye mwenyewe aliishi kwa mfano kabisa kwa kujinyima mno japo alikuwa ndiye kiongozi wao mkuu. Wapiganaji wake wote nao walifuata mfano huu. Waliishi maisha ya kujibana na kuepuka gharama ambazo hazikuwa na lazima. Kwa hiyo walifanikiwa kuokoa fedha nyingi ambazo walizitumia kununulia silaha.

Ikumbukwe kwamba katika kipindi hiki ndicho kipindi ambacho pia vita baridi kati ya Marekani na washirika wake na Urusi na washirika wake iliisha. Kwa hiyo kwenye soko la duniani kulikuwa kumefurika silaha ambazo zilikuwa zinauzwa kwa bei chee kabisa. Kwa hiyo Kagame alitumia vyema fursa hii kununua silaha za kisasa kabisa kwa kutumia kiasi kidogo cha fedha ambazo walikuwa wanafanikiwa kukipata kutoka kwenye michango wanayopokea.
Lakini pia jeshi la Uganda walikuwa wanapenyeza kwa siri kubwa silaha mpakani kwenda kwa RPF.

Ilipita karibia miezi mitatu tangu Kagame achukue uongozi mkuu wa RPF bila kufanya shambulio lolote au tukio lolote la kijeshi. Muda wote huu alikuwa analijenga upya jeshi lake na kwa hakika alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.

Kwa hiyo baada ya miezi hiyo mitatu alihisi kwamba ulikuwa umefika wakati sahihi kwa wao kuanza tena mashambulizi ya kijeshi dhidi ya majeshi ya serikali ya Rwanda.
Na kwa makusudi kabisa alichagua jiji la Ruhengeri kama sehemu ya kwanza ambayo wanapaswa kuzindua oparesheni zao za kijeshi.

Mji wa Ruhengeri... tazama milima Virunga kule nyuma kwenye 'background'

Huko nyuma kwenye shehemu zulizopita nilieleza kwamba Kagame ni gwiji wa 'psychological warfare'.
Hii inadhihirishwa na sababu ya kuuchagua mji huu lakini pia na namna ambavyo walikuwa wanaushambulia.

Tuanze na sababu za uchaguzi wa mji huu.

Sababu ya kwanza ya kuchagua mji huu ilikuwa ni kutaka ushindi wa haraka na kuingiza hofu kwa vikosi vya serikali. Kwa namna gani au kwa nini?

Katika kipindi cha miezi mitatu ambayo RPF walikuwa kimya, serikali ya Rwanda walikuwa wamejiaminisha na kuamisha ulimwengu kwamba wamewashinda RPF. Kwa hiyo kama RPF walikuwa wanarejea tena kwenye uwanja wa vita walihitaji wafanye kitu ambacho watawadhalilisha serikali kwa kujipatia ushindi wa haraka. Lakini pia ushindi huo wa haraka utatoa taswira ya ufanisi wa hali ya juu ya vikosi vya RPF na hivyo kuanza kujenga hofu ndani ya wanajeshi wa serikali.

Kwa hiyo ili kujihakikishia ushindi mkubwa na wa haraka walihitaji sehemu ambayo wanaweza kuishmbulia kwa kushitukiza. Sasa mji huu wa Ruhengeri uko kusini mwa milima ya Virunga. Yaani kwamba ukishuka milima ya Virunga haraka sana unakutana na mji huu. Kwa hiyo hii ilikuwa ni sehemi mujarabu kabisa kwa 'ambush'.

Lakini hii haikuwa sababu pekee… kulikuwa na sababu nyingine kubwa zaidi na ya kisaikolojia zaidi.

Rais Habyarimana pamoja na mkewe na familia yote ya mkewe ambayo ilikuwa na ushawishi mkubwa kama ambavyo nilieleza huko nyuma wanatokea eneo hili na ukanda huu. Kwa hiyo Wanyarwanda wengi kipindi hicho waliona eneo hili na ukanda huo kama ni 'moyo' wa nchi.
Ni kama vile ingekuwa hapa Tanzania tuseme kikundi chenye malengo hayo washambulie Chato na kanda ya ziwa, au miaka miwili nyuma tuseme wangeshambulia Msoga na eneo lote la Chalinze.

Kwa hiyo lengo lake kuu hapa lilikuwa ni moja kutoa ujumbe kwamba RPF ipo na iko na nguvu lakini pia pili ilikuwa ni kuleta taharuki ndani ya serikali.

Lakini pia kulikuwa na sababu nyingine ya tatu ya kwa nini walichagua mji huu. Na sababu hii ya tatu ilikuwa ni Gereza kuu la Ruhengeri. Nitaeleza sababu hii muda si mrefu.

Upande wa pili nimesema ni namna ambavyo walikuwa wanafanya mashambulizi.

Usiku wa January 22, 1991 wanajeshi mia saba wa RPF waliteremka kutoka kwenye milima ya Virunga mpaka chini kabisa karibu na mji na kujificha. Walisubiri mpaka asubuhi ya tarehe 23 January na kuuvamia mji.

Vikosi vya jeshi vya serikali vilichakazwa kama watoto wadogo. Auheni yao kidogo waliipata baada ya serikali ya Ufaranasa kwa haraka kupeleka wanajeshi wao pia kuongeza nguvu. Mwanzoni asubuhi hiyo waliwatunishia misuli RPF lakini mpaka kufika mchana tu, vikosi vya serikali ya Rwanda pamoja na wanajeshi wa Ufaranasa walikuwa wamepigwa kwa aibu kabisa.

Kwa hiyo mpaka kufikia mchana, RPF walikuwa wameuweka mji mzima wa Ruhengeri kwenye kiganja chao. Na ndipo hapa ambapo Kagame alianza kuitesa serikali kwa 'mind games' na kuonyesha ugwiji wake.

Nimeeleza kwamba sababubya tatu ya RPF kuchagua mji huu ilikuwa ni Gereza kuu la Ruhengeri.
Sasa baada ya mji mzima wa Ruhengeri kuwekwa chini ya RPF, Charles Uwihoreye Mkuu wa Gereza hili baada ya kufahamu kabisa kwamba hakukuwa na tumaini lolote la kulinda gereza lake dhidi ya wapiganaji wa RPF, alipiga simu Kigali makao makuu ya serikali ili kuomba maelekezo ni nini anatakiwa kufanya.

Serikali pasipo kusita au kufikiria mara mbili mbili walimuamuru ashirikiane na askari wenzake magereza wawapige risasi wafungwa wote.

Ikumbukwe kwamba gereza hili pia lilikuwa linamshikilia Bw. Théoneste Lizinde, ambaye zamani alikuwa swahiba mkubwa wa Rais Juvenile Habyarimana lakini baadae alifanya jaribio la kumpindua swahiba wake Rais Habyarimana.

Kagame alikuwa anamtaka mtu huyu akiwa hai. Lakini Mkuu wa Gereza alipewa amri awapige risasi wafungwa wote.

Itaendelea...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ENDELEA KUPATA UHONDO KATIKA HISTORIA YA KWELI YA MAUAJI YA KIMBARI YA RWANDA. Sehemu ya saba. Katika sehemu ya sita nilieleza namna ambavyo RPF iliundwa na jinsi ambavyo jaribio la kwanza la kupindua serikali ya Rwanda likiongozwa na Fred Rwigyema lilikuwa na mafanikio makubwa katika siku ya kwanza tu lakini Fred aliuwawa katika mazingira ya kutatanisha sana kwenye siku ya pili tu ya jaribip hilo la mapinduzi huku tayari wakiwa wamedhibiti mji Kigali kutoka kwa majeshi ya serikali ya Kihutu. Tuendelee… KAGAME ANASHIKA USUKANI Kifo cha Fred Rwigyema kilimshitua kila mtu na hasa hasa Rais Yoweri Museveni. Pasipo kuchelewa alipiga simu nyumbani Uganda (alikuwa bado hajarejea kutoka kwenye mkutano wa UN nchini Marekani) na akamuagiza mtu anayemuamini kwenye jeshi, kaka yake Salim Salehe kwenda Rwanda haraka kuchunguza tukio hili. Nchini Rwanda mpaka leo hii moja ya mijadala ambayo ni 'mwiko' kuizungumza ni kifo cha Fred Rwigyema. Kama wewe ni mwandishi na ukajitoa ufahamu kuandika 'mawazo' yako kuhusu kifo cha Fred Rwigyema basi ndani ya siku chache jiandae kutembelewa na 'watu wasiojulikana'. Hii ni kwasababu Fred Rwigyema mpaka leo hii anahesabika kama moja ya mashujaa wa nchi hiyo na anaheshimika zaidi na Watusi kama shujaa ambaye ana mchango mkubwa katika kufanikisha kuwatoa watusi kwenye mateso na manyanyaso ya Wahutu. Kwa hiyo hoja yoyote yenye mlengo wa kumbebesha lawama hizo mtu fulani aliye hai kwamba alihusika na kifo hicho zinazimwa ili kuepuka mtu huyo kuchukiwa na watusi wenzake. Suala la kuuwawa kwa Fred Rwigyema limezua nadharia nyingi sana. Mwanzoni ilianza kuenezwa propaganda kwamba Fred Rwigyema ameuwawa na risasi ambayo ilipigwa kwenda kwingine lakini ikagonga mahala fulani na kubadili uelekeo na kwenda kumpata Rwigyema Kichwani. Nadharia hii imepigiwa upatu kwa muda mrefu sana na serikali ya Kagame. Lakini mwanzoni mwa miaka ya 2000s kuna ukweli ambao ulibainika na kufanya nadharia hii kugeuzwa tena. Nimesema kwamba Rais Yoweri Museveni alimtuma kaka yake Salim Salehe ili kwenda kuchunguza tukio la kuuwawa kwa Fred Rwigyema. Mwanzoni mwa miaka ya 2000s iligundulika kwamba Salim Salehe na kikosi chake alipofika Rwanda aliondoka na makamanda wawili wa RPF ambao baadae waliuwawa walipofika mpakani mwa Rwanda na Uganda. Makamanda hawa walikuwa ni Peter Bayingana na Chris Bunyezi. Hawa walikuwa ni makamanda wasaidizi wa Fred Rwigyema. Baada ya taarifa hii kuvuja mwanzoni mwa miaka ya 2000s serikali ya Rwanda ikaja na nadharia/propaganda kwamba Fred Rwigyema alipigwa risasi na mojawapo wa makamda hao baada ya kutokea mabishano wakiwa kambini. Kwamba Fred Rwigyema alitaka waweke mkakati wa kijeshi ambao utawafanya kusonga mbele taratibu lakini kwa hakika na hatimaye kuidhibiti Kigali yote sawa sawa na kuwadhibiti wapiganaji wa Kihutu. Lakini Bayingana na Bunyezi wao walitaka wasonge mbele kwa haraka na kwa nguvu kubwa ya kijeshi. Serikali ya Rwanda inasema kwamba baada ya mabishano makali Bayingana alipandwa na hasira na kumtolea bastola Rwigyema na kumtandika risasi ya kichwa. Huu ndio msimamo wa serikali ya Rwanda mpaka leo hii juu ya kifo cha Fred Rigyema. Maelezo haya yana ukakasi katika viwango kadhaa. Kwanza kabisa, heshima ambayo Fred Rwigyema alikuwa nayo kwa wapiganaji wa RPF si jambo rahisi kwa mwanajeshi yeyote kuthubutu kumnyooshea bunduli Fred Rwigyema. Lakini pia Bayingana si mtu mwenye haiba ya hasira za haraka na paniki mpaka kufikia hatua ya kumuua ghafla kwa hasira kamanda wake katika uwanja wa vita. Ukakasi zaidi unaletwa na ushahidi wa afisa mwingine wa ngazi za juu wa RPF ambaye alishuhudia Rwigyema akipigwa risasi, afisa huyu anaitwa Stephen Nduguta. Nduguta anasema kwamba hakumbuki wala hakushuhudia watu hao watatu wakibishana, kitu ambacho anakumbuka ni kwamba Bayingana ghafla tu alichomoa bastola kutoka kiunoni na kumfuata Rwigyema pale ambapo alikuwa amekaa na kumtandika risasi kichwani. Hii inaonyesha dalili kabisa kwamba alikuwa na dhamira ya kumuua… kana kwamba alipewa maagizo kutoka kwa mtu wa juu zaidi kufanya hivyo. Maagizo hayo yalitoka kwa nani?? Kagame? Najaribu tu kufikiro kwa sauti… Hii ni moja ya mijadala ambayo mpaka leo inahitaji uchunguzi zaidi na tafakuri ya kina. Ni bahati mbaya vile ambavyo serikali ya Rwanda inazuia kabisa mjadala huru juu ya kifo cha Fred Rwigyema. [16/01, 02:40] The Bold: Baada ya taarifa hii ya kifo cha Fred Rwigyema kumfikia Kagame kule nchini Marekani kwenye chuo cha kijeshi cha Fort Leavenworth, Kansas, mara moja alitoa taarifa kwenye uongozi wa chuo kwamba anahitaji kuondoka mara moja kurejea Africa. Uongozi wa chuo ulimkubalia ombi lake hilo na pia kumruhusu kuondoka na vitabu kadhaa ambavyo huko baadae Paul Kagame alivitumia sana kupanga mikakati ya kijeshi. Kagame aliruka kwa ndege mpaka London, na kisha Addis Ababa, na hatimaye kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe ambako alipokelewa na watu wa 'Usalama wa Taifa' wa Uganda na walimsafirisha mpaka mpakani na Rwanda. Kagame alivuka mpaka na kuingia Rwanda siku ya tarehe 15 Octoba, 1990. Kagame aliwakuta wapiganaji wa RPF wakiwa kwenye hali mbaya kweli kweli kinidhamu na morali. Kagame anaeleza kwamba kipindi hiki cha kwanza cha kuchukua mikoba kuiongoza RPF ni moja ya nyakati zake mbaya zaidi kwenye maisha yake. Wanajeshi hawakuwa na nidhamu na hawakuwa na kiwango cha kuridhisha cha morali. Kwa hiyo ilikuwa inamlazimu Kagame aanze kuwajenga upya wanajeshi wake kisaikolojia na kisha awajenge kwa uwezo wa kijeshi/kivita. Jambo la kwanza kabisa ambalo Kagame alilifanya ni uamuzi wa kurudisha majeshi ya RPF nyuma. Hakuona busara au akili yoyote kuendelea kupeleka majeshi mbele vitani kwa hali mbaya ambayo aliwakuta nayo. Kwa hiyo kwa wiki kadhaa baada ya kuchukua mikoba ya kuiongoza RPF Kagame pamoja na viongozi wengine wa juu wa RPF waliitumia muda huo kukusanya Intelijensia. Pia waliondoa vikosi vyao kutoka eneo la kaskazini mashariki mwa Uganda na kwenda kuweka makazi mapya kwenye eneo la milima ya Virunga. Nyuma waliacha wapiganaji wachache tu ambao walikuwa wanafanya mashambulizi madogo madogo ya kushitukiza dhidi ya vikosi vya serikali ambavyo walikuwa hawajui kwamba RPF wamehamishia makazi yao kwenye milima ya Virunga. Kagame alichagua eneo hili la milima ya Virunga kutokana na ugumu wake wa kufikika. Kama ikitokea vikosi vya serikali wakigundua kuwa RPF wanajificha hapo kwa sasa itakuwa ni ngumu kuwavamia au kwafanyianshambulio la kusbitukiza. Kwa mfano ili kufika kileleni ambako wao walikuwa wameweka kambi ilikuwa ni safari ya wiki nzima kutoka vikosi vya serikali vilipo. Lakini pia wakiteremka na milima hiyo kwa upande wa magharibi walikuwa wanashuka moja kwa moja na kuingia Uganda bila usumbufu wowote kutokana na ruhusa ya Rais Museveni. Japokuwa milima ya Virunga ilikuwa ni sehemu mujaribu kabisa kuweka kambi kutokana na kuwapa faida ya kujilinda na kujihami lakini hali ya hewa ya eneo hili haikuwa rafiki. Milima ya Virunga iko mita 5,000 kutoka usawa wa bahari. Hakukuwa na vyakula wala miti ya matunda au mazao asili. Mwanzoni wanajeshi wengi walikufa kwa baridi katika eneo hili. Lakini baada ya wiki kadhaa waliweza kuimudu sehemu hii na kuishi vyema. Kagame alitumia miezi kadhaa akilijenga upya jeshi lake pasipo kuanzisha mashambulizi yeyote yale dhidi ya serikali ya Rwanda. Paul Kagame ni 'born-tactician' na mtu mwenye akili nyingi sana. Na ni katika kipindi hiki ambacho sifa yake hii ilijidhihirisha kwa kiwango kikubwa zaidi. Kuna bwana mmoja anaitwa Alexis Kanyarengwe. Huyu alikuwa ni mhutu na Kanali kwenye jeshi la Rwanda na mtu wa karibu sana na Rais Juvenile Habyarimana. Ilifika kipindi alitofautiana sana na Rais Habyarimana na ikabidi akimbie nchi ya Rwanda. Kagame alimtafuta Alexis Kanyarengwe na kumshawishi ajiunge na RPF. Kagame alifanya hivi makusudi ili kitendo hiki cha mhutu wa hadhi na kaliba ya Kanyarengwe kujiunga na RPF kutoa picha kwamba RPF ilikiwa 'inclusive', yaani ni kikundi chenye kujumuisha watu wa namna zote (Watusi na Wahutu) japokuwa uhalisia ni kwamba RPF ilikuwa ni kikundi cha watusi tena watusi waliozaliwa au kukulia Uganda. Eneo la Milima ya Virunga Ili kuonyesha zaidi 'nia yake njema' Kagame alimteua Kanyarengwe kuwa mwenyekiti wa kamati ya uratibu wa jeshi la RPF. Kagame alianzisha ratiba kali ya mazoezi kwa wanajeshi wake kila siku. Na pia aliweka sheria kali ambazo wanajeshi wake walipaswa kuzifuata na kuziheshimu. Kwa mfano alitaka wanajeshi RPF wakienda kwenye vijiji vya karibu wanunue kile ambacho wanahitaji badala ya kuchukua kwa mabavu kama ambavyo imezoeleka kwa vikundi vya wapiganaji wa msituni. Pia wanajeshi wote wa RPF walipigwa marufuku kutumia pombe au dawa za kulevya na pia walitakiwa kuhakikisha wanakuwa watu wa mfano wa kuigwa wakiwa kwenye jamii za vijiji vya jirani. Wanajeshi ambao walifanya makosa kama vile kuua, kubaka au kuasi RPF waliadhibiwa kwa kifo cha kupigwa risasi. Hali hii ya nidhamu ya hali ya juu ya wanajeshi wa RPF iliwajengea sifa njema ambayo ilivuma kila mahala. Ghafla kulitokea idadi kubwa ya vijana hasa vijana wa kitusi kutoka Burundi, Zaire, Tanzania na Uganda ambao walijitolea kujiunga na RPF. Kagame pia akaanzisha ofisi jijini Kampala ambayo ilikuwa na jukumu la kukusanya michango kutoka kwa watusi wenzao duniani kote ambao walikuwa tayari kuichangia RPF. Aloisia Inyumba ndiye alikuwa kamishna wa fedha kwenye ofisi hii ya Kampala. Michango ilitolewa kutoka kwenye kila pembe ya dunia na hata kutoka ndani ya Rwanda kwa wafamyabiashara ambao walikuwa wamechoshwa na utawala wa kimabavu wa Rais Habyarimana. Sifa njema ya RPF ambayo Kagame alifanikiwa kuijenga ndani ya muda mfupi ilifanya RPF nje ya medani ya vita, huko mitaani ionekane kama harakati fulani hivi za 'kibinadamu' ambazo zilikuwa zinapswa kuungwa mkono kwa nguvu zote. Japokuwa fedha za michango walizopokea hazikuwa nyingi sana, lakini Kagame alikuwa ametengeneza utaratibu wa kuishi kwa kujinyima sana. Inajulikana namna ambavyo wanajeshi wa vikundi vya waasi na wapiganaji wa msituni namna ambavyo wanapenda kuishi maisha ya anasa iliyopindukia, starehe kila usiku na wakilala na kundi la makahaba au watumwa wa ngono. Lakini hii ilikuwa tofauti kabisa kwa Kagame yeye mwenyewe aliishi kwa mfano kabisa kwa kujinyima mno japo alikuwa ndiye kiongozi wao mkuu. Wapiganaji wake wote nao walifuata mfano huu. Waliishi maisha ya kujibana na kuepuka gharama ambazo hazikuwa na lazima. Kwa hiyo walifanikiwa kuokoa fedha nyingi ambazo walizitumia kununulia silaha. Ikumbukwe kwamba katika kipindi hiki ndicho kipindi ambacho pia vita baridi kati ya Marekani na washirika wake na Urusi na washirika wake iliisha. Kwa hiyo kwenye soko la duniani kulikuwa kumefurika silaha ambazo zilikuwa zinauzwa kwa bei chee kabisa. Kwa hiyo Kagame alitumia vyema fursa hii kununua silaha za kisasa kabisa kwa kutumia kiasi kidogo cha fedha ambazo walikuwa wanafanikiwa kukipata kutoka kwenye michango wanayopokea. Lakini pia jeshi la Uganda walikuwa wanapenyeza kwa siri kubwa silaha mpakani kwenda kwa RPF. Ilipita karibia miezi mitatu tangu Kagame achukue uongozi mkuu wa RPF bila kufanya shambulio lolote au tukio lolote la kijeshi. Muda wote huu alikuwa analijenga upya jeshi lake na kwa hakika alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana. Kwa hiyo baada ya miezi hiyo mitatu alihisi kwamba ulikuwa umefika wakati sahihi kwa wao kuanza tena mashambulizi ya kijeshi dhidi ya majeshi ya serikali ya Rwanda. Na kwa makusudi kabisa alichagua jiji la Ruhengeri kama sehemu ya kwanza ambayo wanapaswa kuzindua oparesheni zao za kijeshi. Mji wa Ruhengeri... tazama milima Virunga kule nyuma kwenye 'background' Huko nyuma kwenye shehemu zulizopita nilieleza kwamba Kagame ni gwiji wa 'psychological warfare'. Hii inadhihirishwa na sababu ya kuuchagua mji huu lakini pia na namna ambavyo walikuwa wanaushambulia. Tuanze na sababu za uchaguzi wa mji huu. Sababu ya kwanza ya kuchagua mji huu ilikuwa ni kutaka ushindi wa haraka na kuingiza hofu kwa vikosi vya serikali. Kwa namna gani au kwa nini? Katika kipindi cha miezi mitatu ambayo RPF walikuwa kimya, serikali ya Rwanda walikuwa wamejiaminisha na kuamisha ulimwengu kwamba wamewashinda RPF. Kwa hiyo kama RPF walikuwa wanarejea tena kwenye uwanja wa vita walihitaji wafanye kitu ambacho watawadhalilisha serikali kwa kujipatia ushindi wa haraka. Lakini pia ushindi huo wa haraka utatoa taswira ya ufanisi wa hali ya juu ya vikosi vya RPF na hivyo kuanza kujenga hofu ndani ya wanajeshi wa serikali. Kwa hiyo ili kujihakikishia ushindi mkubwa na wa haraka walihitaji sehemu ambayo wanaweza kuishmbulia kwa kushitukiza. Sasa mji huu wa Ruhengeri uko kusini mwa milima ya Virunga. Yaani kwamba ukishuka milima ya Virunga haraka sana unakutana na mji huu. Kwa hiyo hii ilikuwa ni sehemi mujarabu kabisa kwa 'ambush'. Lakini hii haikuwa sababu pekee… kulikuwa na sababu nyingine kubwa zaidi na ya kisaikolojia zaidi. Rais Habyarimana pamoja na mkewe na familia yote ya mkewe ambayo ilikuwa na ushawishi mkubwa kama ambavyo nilieleza huko nyuma wanatokea eneo hili na ukanda huu. Kwa hiyo Wanyarwanda wengi kipindi hicho waliona eneo hili na ukanda huo kama ni 'moyo' wa nchi. Ni kama vile ingekuwa hapa Tanzania tuseme kikundi chenye malengo hayo washambulie Chato na kanda ya ziwa, au miaka miwili nyuma tuseme wangeshambulia Msoga na eneo lote la Chalinze. Kwa hiyo lengo lake kuu hapa lilikuwa ni moja kutoa ujumbe kwamba RPF ipo na iko na nguvu lakini pia pili ilikuwa ni kuleta taharuki ndani ya serikali. Lakini pia kulikuwa na sababu nyingine ya tatu ya kwa nini walichagua mji huu. Na sababu hii ya tatu ilikuwa ni Gereza kuu la Ruhengeri. Nitaeleza sababu hii muda si mrefu. Upande wa pili nimesema ni namna ambavyo walikuwa wanafanya mashambulizi. Usiku wa January 22, 1991 wanajeshi mia saba wa RPF waliteremka kutoka kwenye milima ya Virunga mpaka chini kabisa karibu na mji na kujificha. Walisubiri mpaka asubuhi ya tarehe 23 January na kuuvamia mji. Vikosi vya jeshi vya serikali vilichakazwa kama watoto wadogo. Auheni yao kidogo waliipata baada ya serikali ya Ufaranasa kwa haraka kupeleka wanajeshi wao pia kuongeza nguvu. Mwanzoni asubuhi hiyo waliwatunishia misuli RPF lakini mpaka kufika mchana tu, vikosi vya serikali ya Rwanda pamoja na wanajeshi wa Ufaranasa walikuwa wamepigwa kwa aibu kabisa. Kwa hiyo mpaka kufikia mchana, RPF walikuwa wameuweka mji mzima wa Ruhengeri kwenye kiganja chao. Na ndipo hapa ambapo Kagame alianza kuitesa serikali kwa 'mind games' na kuonyesha ugwiji wake. Nimeeleza kwamba sababubya tatu ya RPF kuchagua mji huu ilikuwa ni Gereza kuu la Ruhengeri. Sasa baada ya mji mzima wa Ruhengeri kuwekwa chini ya RPF, Charles Uwihoreye Mkuu wa Gereza hili baada ya kufahamu kabisa kwamba hakukuwa na tumaini lolote la kulinda gereza lake dhidi ya wapiganaji wa RPF, alipiga simu Kigali makao makuu ya serikali ili kuomba maelekezo ni nini anatakiwa kufanya. Serikali pasipo kusita au kufikiria mara mbili mbili walimuamuru ashirikiane na askari wenzake magereza wawapige risasi wafungwa wote. Ikumbukwe kwamba gereza hili pia lilikuwa linamshikilia Bw. Théoneste Lizinde, ambaye zamani alikuwa swahiba mkubwa wa Rais Juvenile Habyarimana lakini baadae alifanya jaribio la kumpindua swahiba wake Rais Habyarimana. Kagame alikuwa anamtaka mtu huyu akiwa hai. Lakini Mkuu wa Gereza alipewa amri awapige risasi wafungwa wote. Itaendelea. Sent using Jamii Forums mobile app

ASEE HUYU JAMAA NI KWELI ANAIBA KAZI YA THE BOLD... LEO NIMEAMINI

kwenye post yake #65 Kuna Sehemu Amesahau Kutoa Muda Na Jina AliCopy Yanii The Bold...

Mkuu Sio Vizuriii Kuiba Kazi Za Watu... Basi Hata Ungekuwa Una Acknowledge

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
ASEE HUYU JAMAA NI KWELI ANAIBA KAZI YA THE BOLD... LEO NIMEAMINI

kwenye post yake #65 Kuna Sehemu Amesahau Kutoa Muda Na Jina AliCopy Yanii The Bold...

Mkuu Sio Vizuriii Kuiba Kazi Za Watu... Basi Hata Ungekuwa Una Acknowledge

Sent from my iPhone using JamiiForums
Lakini anajitahidi kazi yake nzuri
 
Mibongo mijuaji sana,the bold kwani hayupo humu?haoni?na je utajuaje kama kamuomba behnd the scene??the bold huyo huyo akileta mada kama hizi mnaanza kumponda mara anajisikia mara nae story zake zipo google anacopy na kupaste!!yani kuna watu hapa dunian na nahisi Tanzania wapo weng ambao wamezaliwa kukatisha tamaa wenzao kwenye kila kitu,kila kitu...kacopy kacopy copy na wewe basi!!!PATHETIC

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natamani wanaoponda eti amekopi na kupesti nao wafanye hivyo kwa story za kusisimua kama hii badala ya kuishia kulalama kwa wivu huku wanasoma kichinichini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo hii story ilishawahi letwa zamani sana na the bild,naye aliitafsiri tu iko mahali imeandikwa yoote ingawa the bold anavyoitafsiri ni km anabase kwa Kagame wakati kwenye maandiko sahihi wameelezea kinagaubaga unyama uliofanyika miaka hiyo kwa pande zote mbili.
Niliisoma deep sana.
Anyway sioni kosa lolote kwa huyu jamaa kuileta tena watu wasomi,maana member wengi sidhani km walikuwepo jf.
 
ENDELEA NA HISTORIA YA KWELI YA MAUAJI YA KIMBARI YA RWANDA.

Sehemu ya nane.

Kama ambavyo nilieleza kwenye sehemu iliyopita kwamba Kagame alichagua mji wa Ruhengeri kuwa mji wa kwanza kuushambulia kutokana na sababu tatu… kwanza ulikuwa ni mji wa Ukanda ambao anatoka Rais Habyarimana na mkewe, pili mji ulikuwa chini ya milima ya Virunga ambayo RPF walikuwa wameweka kambi kwa kipindi cha miezi mitatu lakini pia walichagua mji huu kutokana na uwepo wa Gereza kuu la Ruhengeri ambalo ndilo lilikuwa gereza kubwa kushinda magereza yote nchini Rwanda.

Mkuu wa Gereza mara ya kwanza alipiga simu Kigali na kuongea na Kanali Elie Sagatwa ambaye alikuwa ni moja ya wale 'akazu' ambao niliwaongolea huko nyuma (inner circle ya Rais Habyarimana ambayo ilijengwa na ndugu wa mkewe na familia yake).
Kanali Sagatwa alimuamurj kwamba ashirikiane na askari wenzake awapige risasi wafungwa wote.

Mkuu wa gereza Bw. Charles Uwihoreye kwa kiasi fulani kuna chembe za busara zilimjia kichwani… mji wote wa Ruhengeri ulikuwa chini ya RPF kwa hiyo hakukuwa na uwezekano wa wao kutoka mahala hapo na kukimbia salama. Kwa hiyo kama anahitaji kuishi ni vyema awe na kitu fulani cha kuwafurahissha RPF.

Uwihoreye alikataa kutekeleza agizo hilo la kanali Sagatwa la kuua wafungwa wote.
Ilibidi Sagatwa awasiliane na Rais Habyarimana kumueleza kuhusu kinachoendelea gereza la Ruhengeri. Rais Habyarimana akatoa ruhusa kwamba wafungwa wote wapigwe risasi.
Kanali Sagatwa akapiga simu tena kwenda kwa mkuu wa gereza Ruhengeri kumtaka atekeleze agizo hilo na kumsisitiza kwamba agizo limethibitishwa na amri kutoka kwa Rais.

Kwa mara nyingine tena Mkuu wa gereza alikataa katakata kutekeleza agizo hilo.
Dakika chache baadae wapiganaji wa RPF walivamia gereza la Ruhengeri na kuliweka mikononi mwao. Kutokana na kitendo cha mkuu wa gereza kuweka msimamo na kukataa kutekeleza agizo la Rais Habyarimana na kanali Sagatwa kuua wafungwa wote, RPF walimsamehe mkuu wa gereza na kumuacha aishi japokuwa isingekuwa hivyo ni lazima wangempiga risasi kutokana na mafungamano yake na Rais Habyarimana.

Wafungwa wote wa gereza la Ruhengeri waliachiwa huru huku Bw. Théoneste Lizinde ambaye alikuwa ni moja wa wafungwa kwenye gereza hilo na rafiki mkubwa wa zamani wa Rais Habayarimana kabla ya kumsaliti na kutaka kumpindua, alishawishiwa na kujiunga na RPF kutoka na taarifa adhimu ambazo alikuwa nazo kuhusu serikali nzima na Habyarimana mwenyewe binafsi.

Wapiganaji wa RPF waliushikilia mji mpaka mida ya alasiri kabla ya kuondoka na kurejea msituni kwenye milima ya Virunga. Tayari walikuwa wamefanikiwa kutuma ujumbe waliotaka kwamba, RPF bado iko na iko imara na pia walikuwa wamemdhalilisha Rais Habyarimana na kuonyesha udhaifu wa jeshi lake.

Ilipita siku moja nyinginendipo serikali ilitangaza hali ya hatari nchi nzima na kutuma vikosi vingine vya jeshi kwenda mji wa Ruhengeri.

Wapiganaji wa RPF waliendelea kuuvamia mji wa Ruhengeri kila siku usiku na kupambana na vikosi vya serikali. RPF hawakuwa na ya kuushikilia huu mji. Walikuwa wanafanya hivi (kuvamia usiku na kuondoka) ili kuwachosha tu vikosi vya serikali. Hii ni moja ya mbinu adhimu ya kisaikolojia ambayo kagame aliitumia sana kwenye vita. Kumchosha kwanza adui vya kutosha na kisha kufanta shambulio kubwa madhubuti.

Kwa hiyo hatimaye nchi ya Rwanda ikarejea vitani tena baada ya kutulia kwa karibia miezi minne.

Vita iliendelea kupamba moto. Majeshi ya serikali yalizunguka sehemu zote muhimu za milima ya Virunga. Ubaya ni kwamba RPF ndio ambao walikuwa wako sehemu ya kimkakati (juu ya milima) kwa hiyo vikosi vya serikali walikuwa hawawezi kufanya "all out assault" kwenda juu mlimani.

Kagame aliendelea kuwaongoza wapiganaji wa RPF kufanya mashambulizi makali na kisha kurudi kujificha milimani. Walikuwa wanafanya hivi mara kwa mara na kwa umahiri mkubwa.
Kuna wakati kagame alikuwa anawaongoza wapiganaji wake kushambulia maeneo kumi tofauti kwa pamoja ili kuwachanganya vikosi vya serikali wasijue ni wapi hasa ambako walipaswa kuelekeza nguvu zao.

Mashambulizi ya namna hii yaliendelea kwa miezi kadhaa huku taratibu RPF wakipata kile ambacho walikuwa wanakitaka. Walifanikiwa kuwachosha vikosi vya serikali na hatimaye kuanza kuweka maeneo muhimu kwenye himaya yao. Moja ya maeneo ya kimkakati kabisa ambayo RPF walifanikiwa kuyaweka chini yao ilikuwa ni mji wa Gatuna ulioko mpakani.
Mji huu ndipo ambapo mizigo yote kutoka bandari ya Mombasa inapitia hapa na kuingia ndani ya Rwanda.
Hii iliifa ya serikali ya Rwanda kubadili route na kuanza kutumia bandari ya Dar es Salaam kwa kiwango kikubwa ambapo route hii gharama yake ni kubwa mno kulinganisha na gharama ya kutoka bandari ya Mombasa kuingilia mji wa Gatuna.

Kutokea hapa kwenye mji huu taratibu vikosi vya RPF vilianza kusonga mbele. Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 1991 vikosi vya RPF vilikuwa vimeweka chini ya himaya yao karibia 5% ya nchi ya Rwanda.

Wakahamisha makao makuu yao kutoka kwenye milima ya Virunga mpaka jimbo la Byumba karibu na mji wa Mukindi ambako kulikuwa na kiwanda cha chai kilichotelekezwa kutokana na vita hiyo na wakafanya hizi kama ofisi zao na makao makuu yao.

Katika kipindi hiki ndipo ambapo Wahutu nao labda kwa kiasi fulani waliweza kuhisi yale maumivu ambayo Watusi waligapitia kwa miongo kadhaa ya kuishi kama wakimbizi. Miji mingi hii ambayo RPF waliiteka ilikuwa na idadi kubwa ya wakazi wa kabila la Kihutu. Kwa hiyo baada ya miji kutekwa na RPF ilibidi wakimbie miji hiyo, lakini hawakuweza kukimbilia Uganda kwa kuwa RPF walikuwa wanamiliki eneo kubwa la mpakani. Hivyo kwenye kipindi hiki Rwanda ilishuhudiwa ikiwa na idadi kubwa zaidi ya wakimbizi wa ndani (internally displaced).

Japokuwa kuibuka tena huku kwa vita kulikuwa na manufaa makubwa kwa RPF ambao walionekana kuchanja mbuga siku baada ya siku lakini kulikuwa na athari kubwa kwa watusi ambao walikuwa ndani ya Rwanda. Mateso yalianza tena upya kwa kiwango cha juj zaidi.

Kwanza yalianza kama tukio dogo tu... ambapo wafugaji wapatao 60 wa Kitusi katika wao pamoja na mifugo yao walikatwakatwa mapanga kwenye eneo la Kinigi. Baadae mauaji haya dhidi ya Watusi yalianza kuenea kuelekea mikoa ya kusini mpaka maeneo ya Ruhengeri na Gisenyi.
Ndani ya muda mchache tu Rwanda ilishuhudia mauajibya zaidi ya Watusi 1000. Mwezi June, 1991 vikosi vya RPF na vikosi vya serikali viliweka makubaliano kwamba pande zote mbili ziruhusu waathiriwa wa vita hiyo kukimbia na kwenda kujificha sehemu salama. Kwa kiasi fulani ilipunguza kasi ya raia wasio na hatia kuuwawa. Lakini rohonu bado kila pande ilikiwa imejawa na vihoro wakitaka kutimiza lengo ambalo walikuwa nalo mioyoni mwao.

Agathe Habyarimana

Kwenye sehemu zilizopita huko nyuma nilieleza kidogo juu ya uwepo wa 'Akazu' mara baada ya Rais Juvenile Habyarimana kushika madaraka.
Nilieleza pia kuwa moja ya vitu muhimu ambavyo vilimsaidia Habyarimana kubaki madarakani ilikuwa ni ushawishi na nguvu ya familia ya mkewe Agathe Habyarimana. Sasa basi hawa 'Akazu' walikuwa ni ndugu wa Agthe Habyarimana pamoja na ndugu wachache wa Habyarinama mwenyewe na watu wake wa karibu. Watu hawa walikuwa wamejipa jikumu la kuamua hatma ya nchi ya Rwanda, kwamba hawataki uwepo wa Watusi kwenye 'nchi yao'.
Hivyo basi kikundi hiki ambacho kilikuwa na nguvu kubwa mno, kilikuwa kinaratibu matukio mengi ovu dhidi ya watusi.

Jina lingine ambalo walijipachika lilikuwa ni "Zero Network" wakimaamisha kwamba lengo lao kuu lilikuwa ni kuwa na Rwanda yenye idadi sifuri ya Watusi.

Akazu ndio ambao walichochea kuibuka kwa itikadi ya "Hutu Power". Itikadi ya msimamo mkali dhidi ya Watusi na hata Wahutu wenye kuwakumbatia Watusi. Akazu walikuwa na kikundi chao cha wapiganaji kilichoitwa 'Impuzamugambi' na miezi michache baadae walichangia pia kuratibu kuibuka kwa kikundi cha 'intarahamwe' ambavyo tutavijadili zaidi hapo mbele kidogo.

Akazu walianzisha propaganda ya hali ya juu dhidi ya Watusi. Walifika mbali mpaka kufungua vituo vya redio na kuchapisha majarida kueneza ujunbe wao wa propaganda.
Ujumbe wao ulikuwa ni mmoja tu, kwamba Watusi si Wanyarwanda na hawana haki ya kuwepo hapo.

Propaganda hizi zilienda mbali zaidi na kufikia hatua ya wanachama wa Akazu wenye nguzu wakiongozwa na mwanahabari nguli n mmiliki wa gazeti maarufu kipindi hicho lililoitwa 'Kangura' kukaa chini na kuyengeneza "AMRI KUMI ZA WAHUTU" ambazo walizichapa kwenye gazeti la Kangura na majarida yote yanayoendeshwa na Akazu.

Amri hizi kumi ulikuwa ni muongozo ambao Wahutu wote walikuwa wanapaswa kuufuata kuanzia muda huo katika maisha yao.

Amri zenyewe ni hizi;

1. Kila mhutu anapaswa kujua kwamba kila mwanamke wa Kitusi, haijalishi ni nani, anatetea maslahi ya Watusi wenzake.
Hivyo basi Mhutu yeyote atakayefanya yafuatayi tutamuhesabu ni msaliti:
- anaye muoa mwanamke wa Kitusi
- anafanaye urafiki na mwanamke wa Kitusi
- anayemuajiri mwanamke wa kitusi kama sekretari au muhudumu wa ndani

2. Kila Muhutu anapaswa kujua kwamba mabinti zetu wa Kihutu wanafaa zaidi na wenye kuwajibika kama wanawake, wake na mama wa familia. Je sio wazuri, kufaa kuwa masekretari na waaminifu zaidi?

3. Wanawake wa Kihutu muwe hodari, washaurini waume zenu na watoto wenu wa kiume wajielewe.

4. Kila Muhutu anapaswa kujua kwamba Watusi wote sio waaminifu kwenye biashara. Malengo yao pekee ni yeye na kabila lao kutawala. Hivyo basi Muhuti ambaye atafanya chochote kati ya hivi atahesabika ni msaliti;
- atakayefanya ubia wa kibiashara na Mtusi.
- atakayewekeza fedha zake au za serikali kwenye kampuni ya Mtusi.
- kukopa au kumkopesha Mtusi
- atakayefanya fadhila ya kibiashara kwa Mtusi (kupata kibali cha kuagiza bidhaa nje, mkopo wa benki, ujenzi, masoko ya umma n.k.)

5. Nyadhifa zote za kimkakati za kisiasa, kiutawala, kiuchumi, kijeshi na kiusalama zinapaswa kuaminiwa kwa Wahutu pekee.

6. Sekta ya elimu (wanafunzi na walimu) inatakiwa kujazwa na Watusi kwa idadi kubwa zaidi.

7. Wanajeshi wote wa Rwandan Armed Forces wanapaswa kuwa Wahutu. Vita ya mwaka 1990 imetupa somo. Na hakuna mwanajeshi ambaye anaruhusiwa kuoa Mtusi.

8. Wahutu wanatakiwa kuacha kuwaburumja Watusi.

9. Wahutu, popte walipo, wanatakiwa kuungana na kushikamana na kutafakari hatma ya ndugu zao wahutu
- Wahutu walio ndani na nje ya Rwanda lazima muda wote wawatunze ndugu zao wahutu.
- wanapaswa kupinga propaganda za Watusi bila woga.
- wahutu lazima wawe shupavu na wakali dhidi ya adui yetu Watusi.

10. Mapinduzi ya mwaka 1959, Mabadiliko ya katiba ya mwaka 1961 na itikadi ya Kihutu inapaswa kufundishwa kwa Wahutu wote katika ngazi zote.
Itikadi hii pia inapaswa kusambazwa kwa kasi na Muhutu popte ulipo. Mhutu yeyote mwenye kumkataza au kumsema Muhutu mwenzake kwa kusambaza itikadi hii atahesabika ni msaliti.

Amri hizi kumi zilisomwa kwenye vituo vya redio, kuchapwa kwenye magazeti na majarida na kusambazwa kwenye vipeperushi mitaani.
Itikadi ilienea kwa kasi kama moto wa kifuu.

Kagame kwa kuona hatari iliyo mbele naye alifungua kituo cha redio jijini kampala kilichoitwa Radio Muhabura kwa ajili ya kueneza propaganda za kupinga itikadi ya "Hutu power" na amri kumi.. lakini haikufua dafu.
Bundi alikuwa ametua mlangoni na hakukuwa na wakumfanya aruke kwenda mtini.

Harufu ya damu zaidi ilinukia.

Kurasa ya mbele ya gazeti la Kangura tolea la November 1991... hayo maandishi makubwa ya kichwa cha habari tafsiri yake ni "Watusi: Wana wa Mungu"
Tamaza hayo maandishi pembeni ya picha ya Panga... maana yake "Silaga gani tutumie kuwaua hawa mende?"
Alafu pembeni hiyo picha kubwa ni Rais wa zamani Gregoire Kayibanda aliyeongoza mapinduzi na umwagaji damu wa mwaka 1959 na kuwafanya Wahutu kabila tawala.

Itaendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo hii story ilishawahi letwa zamani sana na the bild,naye aliitafsiri tu iko mahali imeandikwa yoote ingawa the bold anavyoitafsiri ni km anabase kwa Kagame wakati kwenye maandiko sahihi wameelezea kinagaubaga unyama uliofanyika miaka hiyo kwa pande zote mbili.
Niliisoma deep sana.
Anyway sioni kosa lolote kwa huyu jamaa kuileta tena watu wasomi,maana member wengi sidhani km walikuwepo jf.
Story zote za kusisimua Zilizoletwa zamani hapa jf ziletwe upya mimi nilikua bado kuzaliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika, watu wanapiga mayowe stori imo humu imo humu.... wengine tumezaliwa juzi humu hivyo basi walioisoma kokote watulie au washiriki kutuletea nasi tusome.
Tena wasitutingishea,Akili zetu zote tumezamisha hapa.Muuza kahawa ongeza Kashata.Wahid 1,endelea Baba.Wasiotaka wakajinyonge na Uzi wa Buibui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nazidi kujifunza jinsi 'ukabila' ulivyokuwa mbaya
 
Back
Top Bottom