Historia ya Sewa Haji Paroo (1851-1897), Muasisi wa Hospitali ya Muhimbili

Historia nzuri hii nzuri sana,wapo waliojitolea
kujenga Hospital kama Mgiriki aliyeitwa Galanos,Hospital ya Bombo Tanga,Shule ya Secondary Galanos,Shule ya Usagara sekondari(Abdalah Karimjee) nk
 
Kuna siku nilienda Bagamoyo kufanya utalii wa ndani, maelezo kuhusu historia ya Sewa alisema kuwa alikuwa anatoa majengo kwa Serikali ya ukoloni kipindi hicho kama rushwa ili aweze kufanya shughuri zake bila kusumbuliwa na mkoloni.
 


Anaitwa Sewa Haji Paroo Alifika Zanzibar Akitokea Ktk Miji Ya Bhuj Na Kutch Na Mnamo Mwaka 1852 Alifungua Duka La Bidhaa Mbalimbali Huko Zanzibar, Mnamo 1860 Akafungua Duka Lingine Kubwa Bagamoyo Na Kuweka Makazi Yake, Biashara Zake Zikawa Kubwa Na Kuwa Tajiri Mkubwa Sana, Alisaidia Watu Wote Bila Kujali Rangi, Dini Wala Kabila Zao, Alinunua Majengo Mengi Na Kuyafanya Maeneo Ya Watu Wasiojiweza, Alijengaja Mashule Na Hospitali Kadhaa,
Ktk Mji Wa Mzizima
{ Leo Inaitwa Dar es Salaam}. Alijenga Hospitali Akaiita Sewahaji
Hospitali Ikitoa Huduma Bure, Mnamo
February 1897 Sheikhe Sewa Haji Paroo Alifariki Dunia, Ilikuwa Ni Huzuni Na Simanzi
Kwa Wakazi Wa Bagamoyo Na Mzizima Kwa Kuondokewa Na Sheikhe Sewa Haji
Aliependwa Sana, Baada Ya Kufa Kwake
Wakoloni Baadaye Wakabadilisha Jina Kutoka Sewahaji Hospital Na Kuiita Princess Magreth Hospital, Na Mnamo 1963 Iliitwa Muhimbili Hospital, Na Mojawapo Za Wodi Inaitwa SEWA HAJI,
Sheikhe Sewa Haji Alale Mahali Pema

credit @issamichuzi
 

Attachments

  • 19534888_674809022704664_3848932034617540608_n.jpg
    11.9 KB · Views: 106
  • 19534888_674809022704664_3848932034617540608_n.jpg
    11.9 KB · Views: 95
  • 19534888_674809022704664_3848932034617540608_n.jpg
    11.9 KB · Views: 98
  • 19534888_674809022704664_3848932034617540608_n.jpg
    11.9 KB · Views: 99
  • 19534888_674809022704664_3848932034617540608_n.jpg
    11.9 KB · Views: 91
Pongezi sana kwa Sheikh Sewa Haji.

Mungu mlipe malipo mazuri kwa wema alioufanya,
Nilikuwa sijui chimbuko la MNH sasa nimejuwa.

Ahsante sana mkuu kwa kutusogezea hii historia hapa karibu yetu
 
Marehemu mama yangu alikua ananiambia hosotali ilianzia pale station
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…