Nelson Jacob Kagame
JF-Expert Member
- Dec 26, 2022
- 9,576
- 13,545
Mzee wangu leo kwa mara ya kwanza umeongea pointi.Sawa nitakusahiisha mzee wanguNelson,
Nakosoa pale lilipo kosa.
Kama unaona nimefanya sivyo nisahihishe.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mzee wangu leo kwa mara ya kwanza umeongea pointi.Sawa nitakusahiisha mzee wanguNelson,
Nakosoa pale lilipo kosa.
Kama unaona nimefanya sivyo nisahihishe.
City...
Mbona wewe hujanipuuza?
Kimekushinda nini kukaa kimya.
Leo anataka kudanganya watu eti vijana wa UD wamechezea picha, huyu jamaa anawafanya watu humu wakuda eeh?.Mzeee said ana uchungu sababu Nyerere na Kawawa walikataa udini kwenye chama cha Tanu.Maana hapo mwanzoni kuna wazee wa kariakoo walikua wanaleta udini na ukabila mpaka wakafukuzwa uanachama miaka hiyo ya 1950,s.
Nelson,Mm najua unamchukia nyerere kwa kua alimuondoa sultan wa kiarabu madarakani
City...Nimekupuuza.
Today,Leo anataka kudanganya watu eti vijana wa UD wamechezea picha, huyu jamaa anawafanya watu humu wakuda eeh?.
Yaani anadhani kizazi hiki ndicho kile cha "rudi nyumbani nitakuletea pipi" NO!.
Nelson. ...Ngoja nipekue pekue makabrasha nikuletee tukio kamila la wazee waliofukuzwa tanu kwa kuendekeza ubaguzi wa kidini
Toboa mkuu unapaka weseMhina atakuwa wale waliopewa pesa na wakoloni kuharibu history.
Wakoloni waliharibu history kusudi ili waafrika wasije kujaa chuki.
Later on walitumia mawakala wao waliobaki nchini kuharibu history
Sikia chief, week iliyopita nilisafiri kwa ajili ya mkutano na siku ya kwanza alikuja mheshimiwa waziri ili kutufungulia mkutano wetu wa siku nne.Today,
Haya nikuelezayo ni kweli.
Idara ya picha Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam ndiyo waliotia picha ya Kasella Bantu katika picha hiyo ya Waasisi wa TANU.
Kama huamini basi.
Ungefanya kuandika counter TANU history from your perspectiveKitabu hiki nimekuwancho kwa miaka mingi sana.
Lakini kwa kuwa ni kitabu cha picha nilikisoma mara moja tu katika miaka ya 1980 na kikabakia Maktaba.
Sikukigusa tena.
Jana nimeona picha za TANU katika mtandao na haraka nikatambua kuwa picha hizi nimepata kuziona katika kitabu hicho hapo juu.
Ndipo nilipokitafuta kitabu hiki na kuanza kukipitia.
Kwa hakika nilistarehe sana na picha nilizozikuta ndani ya kitabu hiki ikawa kama vile naziona picha zile kwa mara ya kwanza.
Katika moja ya picha ambayo ilinivutia kwa kosa nililoliona katika maelezo ya picha hiyo ni hiyo hapo chini:
Maelezo ya picha hii ya waasisi wa TANU ni kuwa hao ni waanzilishi wa TAA.
Vipi linaweza kufanyika kosa kama hili?
Picha hii ya Waasisi wa TANU mwaka wa 1954 ni maarufu sana.
Hili mosi.
Pili hapajakuwapo na picha ya waasisi wa African Association iliyoanzishwa mwaka wa 1929.
Ingawa nimabahatika kupata picha mbili za waasisi wa chama hicho - picha ya Kleist Sykes na picha ya Mzee bin Sudi.
Tukirejea kwenye picha hiyo ya Waasisi wa TANU kuna kisa kirefu kuhusu picha hiyo iliyowekwa hapo.
Picha hiyo imechezewa kwa kutiwa mkono.
Katika picha yenyewe ya Waasisi wa TANU Ally Sykes, Tewa Said Tewa na Kasella Bantu hawamo.
Hawa walijitoa kwa kjuwa walikuwa ni watumishi wa serikali na sheria ilikuw ainawakataza kujihusisha na siasa.
Ilipokuwa inapigwa picha wao walikaa pembeni.
Angalia picha halisi hapo chini:
Kasella Bantu kapachikwa kati ya Abdul Sykes na Chief Patrick Kunambi.
Kazi hii ilifanywa na Idara ya Picha Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Siku zote kila nikiangalia picha hiyo iliyotiwa mkono hujiuliza kama haja ilikuw akuwaweka waasisi wote wa TANU kwa nini hazikuwekwa pia picha za Ally Sykes na Tewa Said Tewa.
Tuendelee kubakia katika hili suala la picha hii ya Waasisi wa TANU.
Katika kitabu cha maisha ya Julius Nyerere, ''Nyerere Biography,'' kitabu kinaeleza kuwa picha hii ilipigwa na kamera ya Denis Phombeah yeye mwenyewe akiwa mpigaji wa picha hiyo.
Abbas Sykes alikuwapo katika mkutano wa kuasisi TANU lakini hakuwa mjumbe bali kijana mdogo wa kutumwa na kaka yake Abdul Sykes na wajumbe wengine wa mkutano kufanya hiki na kile katika mkutano ule.
Abbas Sykes amenieleza kuwa picha ya Waasisi wa TANU ilipigwa na mpiga picha maarufu Dar es Salaam jina lake Gomez.
Abbas Sykes anaeleza kuwa walimsubiri Gomez ambae studio yake ilikuwa Acacia Avenue kwa muda hakutokea.
Abdul Sykes akamwambia Abbas achukue baiskeli ya TAA amfate wakapishana.
Wakati Abbas Sykes anamfuata Gomez yeye kumbe alikuwa njiani akija New Street kuwapiga picha waasisi wa TANU.
Katika kitabu hiki cha ''Nyerere na Watanzania,'' kuna picha hapo chini ya baiskeli ya kwanza ya TANU.
Bila shaka hii ndiyo baiskeli ya kijana mdogo Abbas Sykes alipanda kumfata mpiga picha Gomez:
View attachment 2576879Ukiangalia picha hii utaona nimeshika kitabu.
Baiskeli ya TANU
View attachment 2576880
Picha niliyopigwa na Gomez 1956
Mwandishi ni huyo kushoto kulia ni ndugu yangu Kapufi Yunge
Mama anasema nilikuwa situlii kwenye kiti ndipo Gomez akanipa kitabu nishike.
Studio ya Gomez ilikuwapo hadi miaka ya 1980.
Kili...Ungefanya kuandika counter TANU history from your perspective
Halafu jambo la kulinganisha pumba na mchele waachie wasomaji
SawaKili...
Nimeandika tayari kitabu cha Abdul Sykes mwaka wa 1998.
Today,Sikia chief, week iliyopita nilisafiri kwa ajili ya mkutano na siku ya kwanza alikuja mheshimiwa waziri ili kutufungulia mkutano wetu wa siku nne.
Sikuwa najua protocol baada ya mheshimiwa kumaliza na kupiga makofi mimi nilitoka nje kidogo (🈲), kumbe huku nyuma wakapiga picha ya pamoja kwa ajili ya ukumbusho.
Nilijua baada ya kuiona ile picha huku mimi simo kwenye ile picha ingali nilikuwepo kwenye tukio, kukata mzizi wa fitina niliomba mtaalam wa graphics anipige picha anipachike popote ili hata ofisini walionituma wanione na wajue nilikiwepo.
◽Asante bana Moud, ngoja niandae ftari.
Kili...Sawa
Nakipata wapi
Mcqu,Nyerere mwenyewe alikuwa muislam jina lake la kwanza ni Ahmed...Sema kuna historia kubwa ilichakachuliwa na kufichwa
Ndio Nyerere alikuwa Muislam asante kwa kukiri hili.Mcqu,
Jina la Ahmed umenikumbusha historia ya Ahmed Adam:
AHMED ADAM – MNUBI ALIYEMKIRIMU NA KUMLAZA MWALIMU JULIUS NYERERE NYUMBANI KWAKE MIKINDANI 1955
Tukio dogo la kiburi cha askari mpumbavu wa mkoloni ndiko kulisababisha watu wa Mikindani wafungue tawi la TANU.
Askari mmoja mpita njia aliingia katika ubishi na kijana mmoja wa pale mjini, akiitwa Hassan Masudi Vuni.
Akitumia mamlaka yake ya kukamata mhalifu, askari huyo alimpiga Vuni kwa kumuonea.
Miongoni mwa watazamaji wa tukio hilo alikuwa Rashid Ali. Rashid Ali alikwenda kusimulia tukio hili kwa Mohamed Ali Abdallah.
Alipokuwa akisimulia mkasa ule, pamoja naye alikuwa Suleiman Hassan Msepele.
Walipokuwa wakijadiliana Msepele alitamka kwamba tukio kama hilo kamwe lisingeweza kutokea Dar es Salaam kwa sababu Mwafrika mmoja jina lake Julius Nyerere alikuwa ameanzisha chama cha siasa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Rashid Ali na Mohamed Ali Abdallah walitamani kujua mengi zaidi kuhusu Mwafrika huyu aliyekuwa akijulikana kwa jina la Nyerere na chama chake cha siasa, lakini Msepele hakuwa na mengi ya kueleza kuhusu Nyerere na hicho chama chake. Kwa hiyo basi, hawa watu watatu waliamua kumtuma mtu Dar es Salaam kupata habari zaidi kuhusu chama hicho.
Mohamed Ali aliandika barua na kumpa Msham Awadh na Ali Muhidin kumpelekea Nyerere Dar es Salaam.
Ndani ya barua hiyo Mohamed Ali alimweleza Nyerere kwamba ukoloni ulikuwa bughudha kubwa katika Jimbo la Kusini, na wangependa kufungua tawi la TANU mjini Mikindani ili kupigania uhuru.
Mwaka 1955 Mohamed Ali alikuwa na umri wa miaka 45.
Alikuwa hana elimu kama elimu inavyojulikana kwa kuwa hakusoma shule yoyote. Alipokuwa kijana mdogo baba yake alimpeleka Zanzibar kusoma elimu ya dini.
Wakati huo Zanzibar ilikuwa ndiyo kitovu cha elimu ya Kiislamu Afrika ya Mashariki na nchi jirani.
Huko Zanzibar kijana Mohamed Ali alisoma kwa Sheikh Mohamed L’Khamus. Kisha aliendelea na masomo yake mjini Dar es Salaam kwa Sheikh Wazir bin Said, mwanafunzi wa Sheikh maarufu sana na aliyekuwa Khalifa wa Tariqa ya Askariyya, Sheikh Idrissa bin Saad. Baada ya kumaliza masomo yake mjini Dar es Salaam alisafiri hadi Belgian Congo na halafu alirudi Ujiji nchini Tanganyika kufanya biashara ndogo ndogo.
Mwaka 1947 Mohamed Ali alirudi Lindi na kutoka hapo alikwenda Mikindani na kuwa fundi cherahani.
Msham Awadh alikuwa akijulikana Lindi nzima na Mikindani kwa sababu ya biashara yake. Mshama Awadh alikuwa alikuwa muuza uzuri, yaani vitu vya urembo kama vile uturi, dalia, marashi, rangi na manukato mengine kwa wanawake wa hii miji miwili.
Alikuwa akiuza bidhaa zake kikapuni akipita nyumba hadi nyumba. Hawa walikuwa ndiyo aina ya watu walioanzisha na kuongoza harakati za kumaliza utawala wa kikoloni.
Hawakuwa wajuzi wa lugha ya Kiingereza wala hawakuwa na ujuzi wa maisha ya ulimwengu wa Kimagharibi kama walivyokuwa baadhi ya Waafrika wengine waliyopata elimu ya Kimagharibi.
Msham Awadh na Ali Muhidin walikwenda hadi Dar es Salaam kukutana na Mwalimu Nyerere, John Rupia, Said Chamwenye, Oscar Kambona na Dossa Aziz katika makao makuu ya TANU, New Street.
Msham Awadh na Ali Muhidin walipewa kadi za TANU na wakaambiwa wafungue tawi Mikindani.
Wakati Msham Awadh na Ali Muhidin wakiwa njiani kwenda Dar es Salaam kukutana na Nyerere, Mohamed Ali alisafiri kwenda Lindi kukutana na Suleiman Masudi Mnonji mmoja wa viongozi wa TANU hapo mjini na kumweleza kuwa Mikindani walikuwa wamekusudia kufungua tawi la TANU.
Mnonji alimpa kadi Mohamed Ali na akawa mwanachama na akamwambia arudi Mikindani na kuanza kufanya kampeni kwa nguvu kwa ajili ya TANU na awafahamishe watu kuwa Nyerere yupo njiani kuja Jimbo la Kusini.
TANU Lindi walikuwa wamemualika Julius Nyerere kuja Lindi na katika ratiba yake alipangiwa kufika Mikindani. Nyerere, Ali Mwinyi Tambwe na Rajabu Diwani waliwasili Mikindani kutoka Lindi siku ya Jumamosi. Kabla ya kuwasili ujumbe huo, kazi kubwa kuliko zote waliyokuwanayo uongozi wa TANU Mikindani ilikuwa kutafuta mahali pa kumlaza Nyerere.
Walimwendea Ahmed Adam, Mnubi mmoja tajiri na mtu wa makamo, aliyemiliki nyumba moja ya fahari.
Nyumba hii ilikuwa ya ghorofa moja na ilijengwa kwa mawe na chokaa.
Ahmed Adam aliombwa awe mwenyeji wa Nyerere na ujumbe wake.
Nyumba hii tayari lilikuwa na kisa chake. Ilijengwa na hayati kaka yake Ahmed Adam baada ya Vita Kuu ya Kwanza.
Kaka yake alikuwa askari wa Kinubi aliyekuwa katika jeshi la Wajerumani.
Huenda alichukuliwa Misri mwishoni mwa mwa karne ya kumi na tisa na Wajerumani kuja Tanganyika kama mamluki katika jeshi la Wajerumani chini ya Kamanda Herman von Wissman.
Baada ya vita alilipwa kiinua mgongo na serikali ya Ujerumani na kwa kutumia fedha hizo alijenga nyumba hiyo.
Katika Vita Kuu ya Kwanza yeye alipigana katika jeshi la Wajerumani dhidi ya Waingereza chini ya Paul von Lettow Vorbeck.
Baada ya vita Wajerumani wakiwa wameshindwa vita, Waingereza waliitikadi nyumba hiyo kama mali ya adui wa himaya ya Kiingereza na kwa hiyo ilibidi itaifishwe.
Hii ilikuwa ndiyo nyumba pekee iliyokuwa nzuri yenye kumilikiwa na Mwafrika na kwa ajili hii haikuweza kukosa kuhusudika.
Utawala wa Waingereza ulikuwa katika taratibu ya kuitaifisha nyumba hiyo wakati ilipofahamika kwamba serikali isingeweza kufanya hivyo kwa sababu ya kifungu cha sheria ambacho kilisema kuwa mali ya Waafrika waliokuwa wakitumika katika majeshi ya watawala wao haiwezi kutaifishwa.
Hii ilinusuru nyumba hiyo na hivyo ilibakia mikononi mwa mwenyewe mpaka alipofariki na nyumba hiyo ikaja kuwa katika miliki ya mdogo wake, Ahmed Adam. Ahmed Adam alikubali kumpokea Nyerere na ugeni wake nyumbani kwake.
Nyumba hiyo ilikuja kuwa tawi la kwanza la TANU Mikindani.
Siku hiyo hiyo ya Jumamosi, usiku Nyerere aliitisha mkutano wa ndani wa wanachama wa TANU na wanachama kama 30 hivi walihudhuria.
Nyerere aliwaeleza kwa ufupi juu ya ile safari yake ya Umoja wa Mataifa na hali ya siasa kwa ujumla kama ilivyo mjini Dar es Salaam.
Nyerere aliwahakikishia wasikilizaji wake kuwa kulikuwa na uwezekano mkubwa sana kuwa Tanganyika itakuwa huru katika uhai wao.
Siku iliyofuatia mkutano wa hadhara ulifanyika mjini Mikindani mahali palipojulikana kama Jangwani, karibu na ufuko wa Bahari ya Hindi.
Mkutano huu uliohudhuriwa na watu wengi na uliendelea bila mushkeli wowote ukitoa kitendo kidogo kilichofanywa na mwalimu mmoja wa shule, Abdulrahman Muhibu aliyekuwa amelewa.
Muhibu alikuwa ametoka kunywa pombe na alipita karibu na uwanja wa mkutano ambapo Nyerere alikuwa akihutubia. Katika hali yake ya ulevi alimpigia kelele Nyerere akamwita muongo.
Huenda Muhibu alikuwa akifahamu vyema ujumbe wa Nyerere, na akiwa vile alivyokuwa, mtumishi wa serikali na mlevi, aliona wazo la mwalimu wa shule Mwafrika kama yeye kuwaongoza watu hadi uhuru upatikane ni jambo lisilowezekana.
Kwa haraka Muhibu alikamatwa na watu na ilikuwa karibu wamtie adabu ndipo Nyerere alipoingilia na hivyo kumnusuru.
Jioni hiyo baada ya mkutano Nyerere na ujumbe wake waliondoka kwenda Newala, kwenye ngome ya Yustino Mponda. Mponda alikuwa mmoja wa wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria waliosafirishwa na Gavana Edward Twining hadi Umoja wa Mataifa, New York, kumpinga Nyerere.
Sasa TANU ilikuwa ikichukua mkokoto wake wa kampeni hadi ndani ya ardhi ya Mponda ambayo yeye alikuwa liwali na mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria.
Nyerere alipomaliza ziara yake ya Jimbo la Kusini, fikra za watu wengi zilibadilika.
Tatizo kubwa kusini mwa Tanganyika kuhusu TANU ilikuwa Kanisa likiwaonya waumini wake kuchukua tahadhari na TANU kwani kanisa likiona harakati zile za kudai uhuru zilikuwa sawa na harakati zilizosababisha Vita Vya Maji Maji na kusababisha majemedari 62 wa vita vile kama Abdulrauf Songea Mbano kunyongwa na kuzikwa katika kaburi la halaiki Songea.
Kuja kwa Nyerere Wakristo waliokuwa wakitishwa na Kanisa hawakuamini tena kuwa TANU ilikuwa harakati za Waislam sawasawa na Vita Vya Maji Maji.
Nyerere, Tambwe na Diwani walipokuwa wanashika njia kurudi Dar es Salaam, matawi ya TANU yalikuwa tayari yamefunguliwa Masasi, Ndanda na Newala ambazo zilikuwa sehemu za Ukristo na ngome kuu ya Kanisa Katoliki katika Tanganyika.
Picha ya kwanza kushoto ni Ali Mwinyi Tambwe baada mapinduzi ya Zanzibar akimbeba Abeid Amani Karume.
Ndio Nyerere alikuwa Muislam asante kwa kukiri hili.