Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa


Tuoneshe ushahidi wa hilo, mimi nnavyojuwa mfumokristo umeletwa na Nyerere na ndio maana anapigiwa debe kupewa "utakatifu", Utakatifu na wewe Rais uliyeiacha nchi hohehahe "failed economy" utoke wapi?
 
Tuoneshe ushahidi wa hilo, mimi nnavyojuwa mfumokristo umeletwa na Nyerere na ndio maana anapigiwa debe kupewa "utakatifu", Utakatifu na wewe Rais uliyeiacha nchi hohehahe "failed economy" utoke wapi?
Inaonyesha hata husomi anachoandika Mohamed!!
 
Siku moja nilimuuliza Mohamed kwamba mbona kwenye masimulizi yake sioni jina la MARTIN KAYAMBA? Mpaka leo Kimyaaa!!
 
Siku moja nilimuuliza Mohamed kwamba mbona kwenye masimulizi yake sioni jina la MARTIN KAYAMBA? Mpaka leo Kimyaaa!!

Ndio hulioni. Sasa wewe kama unayajuwa ya huyo unaemtaja si utuletee hapa tufaidike, kwanini umngoje Mohamed Said?
 
Nguruvi3, Kigarama, Mag3, Mzee Mwanakijiji..

Ebu na nyie jipangeni kama itawezekana muungane kwa pamoja muandike histori ya Uhuru wa Tanganyika..

Tena itakuwa vizuri mpinge yote yale ambayo sio ya kweli kwenye kitabu cha Mohamed Said..

Inawezekana kuna mashujaa wengine nyie mnawajua waliopigania uhuru wetu Mohamed Said, hawakuandika kutokana na udini wake dhidi ya ukirstu..

Na hicho kitabu ndio kitakuwa historia kamili ya uhuru wa Tanganyika sababu kitaandikwa kwa pamoja na magwiji niliowataja..

Tunakisubili kwa hamu...
 
Nnayasoma sana tena.

Ungeandika "Nnayasoma tena sana" lakini kwa kuandika "Nnayasoma sana tena" sentensi yako yako inakuwa "tasa" kwani inashindwa kuzaa lengo lililokusudiwa.

Ngoja nikwambie kitu, hata sisi ni watu wa pwani kama nyie tofauti yetu ni vizazi. Wenzetu inawezekana mmezaliwa zama za kuzaliana nyumbani, wenzenu tumezaliwa Ocean Road Hospital mita chache kutoka pale kwenye lile jumba jeupe la Magogoni. Na kama anavyosema Khadija Kopa, basi huo nao kwa zama hizi umjini. Usidhani kila mwana JF ambaye yumo humu anayepingana na Mohamed si mtu wa pwani!!
 

Hawawezi, hao ni wapiga porojo wa JF. Wataanzia wapi? wao wangoje kulalamika tu humu. Ritz, kazi ya Mohamed Said imeshaota mizizi na hakuna wakuing'oa, ukweli haufutiki.

"naatamanaaani na kujaribu siweeezi".
 

Ushauri wako ni wa maana sana ingawa natofautiana na wewe kwenye hoja ya "Historia kamili". duniani hakuna Historia Kamili. Kwa mfano mpaka sasa Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad anaamini kwamba mauaji ya Wayahudi ni hadithi za kutunga tu kwani isingewezekana kwa wayahudi zaidi ya milioni 6 kuuawa kirahisi na Manazi wa Ujerumani.

Lakini hata Rwanda watu wanasema Wahutu wenye msimamo mkali waliwaua Watutsi na wahutu wenye msimamo wa wastani (Moderate) lakini hivi hakuna watutsi waliowaua wahutu au watutsi wenzao wenye msimamo wa wastani? Hiyo ndiyo Historia, hakuna iliyo kamili.
 
Hawawezi, hao ni wapiga porojo wa JF. Wataanzia wapi? wao wangoje kulalamika tu humu. Ritz, kazi ya Mohamed Said imeshaota mizizi na hakuna wakuing'oa, ukweli haufutiki.

"naatamanaaani na kujaribu siweeezi".
Kazi ya mzee Mohamed Said imeota mizizi kwenye kikundi kidogo cha 'Wachochezi wa kidini ' kama wewe.
 
Siku moja nilimuuliza Mohamed kwamba mbona kwenye masimulizi yake sioni jina la MARTIN KAYAMBA? Mpaka leo Kimyaaa!!

Kigarama,

Nimepata humu ndani kujibu kuhusu Martin Kayamba lakini simkumbuki aloniuliza.
Kayamba alikuwa kibaraka wa Waingereza na akijikomba sana kwao.

Yeye ni "contemporary" wa Kleist Sykes na maisha yao wote yamo katika "Modern Tanzanians" cha John Iliffe.

Chungulia hapo chini Erika Fiah kasema nini kuhusu Kayamba:

"Kalamu ya Fiahilikuwa haina muhali. Katika rambirambi alizotoa za kijeuri na za dharau juu yakifo cha Martin Kayamba,[1]Fiah aliomboleza kwa kusema kwamba Waafrika hawakunufaika kwa elimu ya Kayambawala kwa wadhifa wake kama karani wa kaimu Katibu Mkuu."[1]
Ukipenda unaweza kumsoma Kayamba katika kitabu hiki:
Kayamba, Martin,The Autobiography ofMartin Kayamba, "The Story of Martin Kayamba Mdumi, MBE, of the Bondei Tribe" MargeryPerham, (ed) Ten Africans, 5-272.
Mwenyewe umeona umeuliza swali gumu sana na shingo unatoa.
Ndiyo maana dada yangu FF husema "usinchekeshe."

Mie mabuku yote hayo nishayanywa miaka mingi ilopita.

Mohamed


 

Kigarama,

Hebu nionyeshe hicho kipande.

Mohamed
 

Nguruvi3,

Tunaridi alif kwa kijiti!

Mohamed
 

Historia huandikwa na Mohamed Said kaandika na nyinyi hamuipendi, kwanini? kila tukiwauliza ni nani aliyetajwa humo hakuwepo au hakufanya kilichoandikwa hakuna, mnakuja ma ra nani kakuambia, mara sijui fulani na fulani kwanini hukuwaandika.

Kwanini hao mnaosema hawajaandikwa msiandike nyinyi. Mohamed Said kawaandika aliowaandika na wa kabla ya Mohamed Said wa Magogoni kule mlishawahi kuwauliza kwanini hawa aliowaandika Mohamed Said nyinyi hamkuwaandika?

Mohamed Said kaona hawakuandikwa, akaanza kuwaandika na sasa MashaAllah, ni miaka inakwenda hakuna kati yenu aliyethubutu kusema huyo hakuwepo au huyo hakuenda na baiskeli rufiji katika harakati za kutafuta madaraka ya Tanganyika au Nyerere hakukaa kwa Sykes alipokuja Dar au Dossa hakumpakia kwenye gari lake au Msume hakumpa chakula au Nyerere hakusahau wadhifa wa Abdul Wahida TAA.

Naona hakuna anaeyapinga yote hayo. Au kuna aneyapinga hayo? Mzee Mwanakijiji alikuja na hoja yake humu, ikasambaratishwa kwa post moja tu, hajairudia tena, tena ikafifirishwa hoja na majibu, haimo tena humu, kama imo nionesheni. Kwanini?
 

Bado nasubiri habari za Musoma...

Mohamed
 
Katika maswali mugumu niyajuayo mimi hilo halimo. Hujajibu swali langu.Pamoja na kwamba kweli Kayamba alilewa "uzungu" na kuwadharau waafrika wenzake. Lakini hana mchango wowote kwenye ukombozi wa nchi hii??
 
Historia huandikwa na Mohamed Said kaandika na nyinyi hamuipendi, kwanini? kila tukiwauliza ni nani aliyetajwa humo hakuwepo au hakufanya kilichoandikwa hakuna. mnakuja ma ra nani kakuambia, mara sijui fulani na fulani kwanini hukuwaandika.

Unafikiri hata Salman Rushdie nukuu alizozitumia kuandikia kitabu chake cha "Satanic Verses" hazikutoka kwenye Quran? Kwa nini waislam walimpinga hadi kumtangazia "Fatwa". Wewe unamuunga mkono Rushdie kwa sababu nukuu zake zilitoka kwenye Quran??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…