Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa


Kigarama.

Sio kweli kuwa historia kamili duniani hakuna, historia kamili zipo tena nyingi tu..

Mfano wa historia kamili dunia zipo wazi..

Histori ya China na Mao ze-Dong ipo wazi toka 1958

Urusi historia ya Jozef Stalin ipo wazi toka 1932.

Germany historia ya Adolf Hitler ipo wazi toka 1939.

Turkey historia ya Ismail Enver ipo wazi toka 1915

Japan historia ya Hideki Tojo ipo wazi toka 1941..

Hizi ni baadhi za historia kamili zipo wazi kwenye mitandao..

Hili kupambana na historia ya uhuru ya Mohamed Saidi na nyie njooni na historia mbadala ya kweli ya uhuru wa Tanganyika..

Kama mtashindwa basi historia ya Mohamed Said bado itakuwa na nguvu na watu wataendelea kuikukubali.

Ritz
 

Mimi nadhani kwamba niliposema "hakuna historia kamili" nilimaanisha kwamba hakuna kitabu au masimulizi yaliyomaliza kila kitu kwenye Historia yoyote ile duniani. Kuna mtu alitoa mfano wa msafiri anayesafiri kutoka Kimara kwenda Kariakoo. Unadhani kwenye maelezo yake ataeleza hadi dereva alipiga honi mara ngapi walipokuwa njiani kuelekea Kariakoo? Jee asipoeleza idadi ya honi zilizopigwa na dereva utasema haijui habari ya safari aliyosafiri toka Kimara hadi Kariakoo?

Hoja kila wakati watu wanakuwa na Mkutadha tofauti kwenye kuangalia mambo na hapo ndipo inapokosekana Historia iliyo kamili. Kwenye Quran na Biblia sijui kama wameandika kama hao Mitume wanaoaminiwa na watu waliwahi kuoga mara ngapi kwenye uhai wao wote!! Hapa hatubishani ni nini kimeandikwa na Mohamed Said, bali tunachambua lengo la maandishi yake.
 
Currently...

Hawawezi, hao ni wapiga porojo wa JF. Wataanzia wapi? wao wangoje kulalamika tu humu. Ritz, kazi ya Mohamed Said imeshaota mizizi na hakuna wakuing'oa, ukweli haufutiki.

"naatamanaaani na kujaribu siweeezi".

Previously on this thread...


Leo mmeshindwa kutetea aya ya Qur'an inayosimamisha Uislaam, mtaweza kuwateteta Umma wa Kiislam. Wanafik wakubwa..

Need I say more?
 
Hapo Mgalanjuka mwenzio alitaka ku- twist mjadala kuhalalisha kwamba Mohamed lengo lake ni kuwa enzi wazee wake kama wapigania Uhuru wa Tanganyika na wala si kwa sababu ya udini wakati makala nzima imejaa maneno yenye kuonyesha utengano wa kidini.
 
MM,

Nami nakuuliza.

Mtafanya nini hii leo kuifuta historia hii niliyoandika?
Ile ya kutia moto magazeti haikusaidia sana.

Unadhani haya maswali katika JF itasaidia kitu?

Mohamed
Kwa sababu sio ukweli imeshajifuta yenyewe, nakushangaa sana kwa kutumia nguvu kubwa kuielaza na kuwajengea hofu vijana wa kiislam kuwa wanaonewa wakati wenyewe ukweli wanauona. Nimekusikia kwenye clip zako YouTube ukitumia majina ya marehemu akiwemo marehemu Profesa Haroub Othman kuhalalisha chuki yako! Haroub hakuwa mwalimu wako peke yako, wengi tulifundishwa naye, kwa tulie mfahamu msomi yule hakuwa na fikra unazompandikizia wewe, unafanya hivyo kwakuwa unajua kwamba hataweza kuja kujitetea hapa.Waache vijana wa Tanzania wafurahie umoja wao, waache vijana wapambane na umaskini na ufisadi ktk nchi yao kwani matatizo hayo hayawatenganishi kwa imani zao, wote kwa pamoja wanajeruhiwa nayo. Kama kweli Mungu wako anasifa tatu yaani "Omnipotence, Omniscience na Omnipresence" basi nakusihi mwachie yeye atoe hukumu ya haki kwa chuki unayo mpakazi/mzuria mwalimu Nyerere dhidi ya uislam.La sihivyo njoo uuangane na mimi(Atheist) na wala usiusingizie usilamu kujenga sifa na chuki zako binafsi.
 
Hapo Mgalanjuka mwenzio alitaka ku- twist mjadala kuhalalisha kwamba Mohamed lengo lake ni kuwa enzi wazee wake kama wapigania Uhuru wa Tanganyika na wala si kwa sababu ya udini wakati makala nzima imejaa maneno yenye kuonyesha utengano wa kidini.

Huyo aliniuliza kama najua maana ya "contradictions" hivyo nashangaa mara kawaita watu "wanafik wakubwa" then anawaambia "kazi yao imeota mizizi"
 
Sweke34,

Hivi niwe mchochezi na miaka yote hiyo niachiwe nisifikishwe mahakamani.

Mohamed
Mzee Mohamed, kama mfumo uliopo madarakani unanufaika na uchochezi wako nani atakufikisha mahakamani? Zaidi sana unapongezwa sana kwani umefanikiwa kuwaondoa vijana wa kiislamu kupambana na adui wao halisia(ujinga, umaskini, maradhi na utawala wa kifisadi) sasa wapo mioyo juu kumfikiria na kumjadili adui wa kufikirika aliyeumbwa na wewe kwa raha zako!
 
Huyo aliniuliza kama najua maana ya "contradictions" hivyo nashangaa mara kawaita watu "wanafik wakubwa" then anawaambia "kazi yao imeota mizizi"
Labda kazi "yao" ya unafiki ndiyo imeota mizizi!!
 

Gwalihenzi,
Ukafiri si sifa ya kujigamba.

Soma kitabu "Haroub Othman Farewell to the Chairman."
Kimehaririwa na Chris Peter Maina na Saida Yahya Othman.

Ndani imegusiwa yeye kuongoza jopo litakaloandika maisha ya Nyerere.
Mimi kwangu ni zaidi ya mwalimu.

Alikuwa ndugu yangu kabisa ukipenda fanya uchunguzi kwa jamaa zake.
Mwisho wa maisha yake alikuwa mwanachama mwenzetu katika Ratib Hadad tukiusoma Msikiti Ngazija kila Alkhamis na alikuwa katibu wa msikiti huo.

Nadhani wewe unamfahamu Horoub Othman Marxist.
Allah alimvua hilo balaa...

Tumekwenda sote Umrah tukenda sote hadi Madina.
Nilizungumzanae sana kuhusu kitabu changu.

Kwa ufupi wa maneno...
Kilimtaabisha sana kiasi alikwenda kwa Ahmed Rashad Ali kutaka kujua mengi kuhusu Abdulwahid Sykes na mchango wake katika TANU.

Najua humjui Ahmed Rashad Ali.
Ukipenda nifahamishe nitakupa darsa kuhusu huyu bwana.

Mohamed
Mie huyu ni mzee wangu.

Mohamed

Mohamed
 

Gwalihenzi,

Nimeandika toka enzi za Nyerere na sijapata kuficha jina langu.

Mohamed
 
wewe sio mwanahistoria, na wala hufahamu filosofia ya historia. Nani kakwambia hisitoria uliyoiolodhesha inakubaliwa na watu wote aslimia 100%? Mwandishi kama mpiga picha huchagua tukio analotaka kuilipiga picha. Nikama mzee wako Mohamedi Said aliyeshupalia wazee wachache wa kiislam kuwa hao ndio walikua "King maker" wa historia ya ukombozi wa Tanganyika.
 
Gwalihenzi,

Nimeandika toka enzi za Nyerere na sijapata kuficha jina langu.

Mohamed
KIUKWELI Mohamed Unamhusudu Mwalimu kiasi kwamba unatamani wewe ungekuwa yeye!! kwa nini waliita "Kiwi' cha macho??
 

Abdul Wahid Sykes alimpokea Nyerere wakati gani? Kabla ya kwenda Edinburg, aliporudi au alipohamia Pugu? Mshume Kiyate alimpa "resheni" kwa vile aliwajibika kama Muislamu kumsaidia asiye na uwezo au kwa mapenzi yake kwa kiongozi wake? Dossa Aziz kweli alitoa gari lililotumiwa na TANU lakini mbona wakina JOHN Rupia nao walitoa pesa nyingi tu? Naam, Hassan Bin Ameir alitumia umaarufu wake kuinyanyua TANU pwani kama walivyofanya wakina John Mwakangale kwa Wanyakyusa, Humplick na dada zake na wengine wengi tu. Hao uliowataja hawakuwa peke yao kama mnavyotaka kutuaminisha.

Hilo la jina la TANU linaelezwa vizuri hapa chini. Walikuwa waki-brainstorm, na watatu walichangia kuboresha jina. Watu watatu wamefunga magoli, itakuwaje udai ni mmoja wao tu ndie aliyeleta ushindi? Hamna hata haya?


Uongo, Goebbels alituambia, ukirudiwa mara nyingi unakuwa ukweli. Porojo za Mohamed Said sasa ziwekuwa historia! Na wavivu wa kufikiri wanameza jumla!

Amandla.....
 
Mzee Mohamed, profesa Haroub kesha fariki, hawezi kuja hapa kuthibisha unayoyasema. Wapi aliandika kuukana umarxist?Wala kuwa ndugu yako haiwi uteteze wa mitizamo yako ya kisiasa na kidini. Bado wengine tunamkumbuka alivyoutetea ukweli bila kujali dini ya mtu. Wewe hufanyi hivyo.
 

Ritz,

Unamchapa farasi aliyekufa.
Ukisoma jibu lake ndiyo utajua mengi zaidi...

Umetoa mifano ya kisomi kabisa anakupa habari za "Cock and Bull."
Hawa hawawezi kuja na historia nyingine.

Waandike nini?
Ndiyo maana waliipiga vita historia ya wazee wetu.

Kuna mradi wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere kuandika maisha yake.
Tuisubiri hiyo Insha Allah.

Mohamed
 

Ama kweli, na hapa mwenyewe ndiyo umeona "umekosowa" maandiko ya Mohamed Said? Unachekesha!
 

Gwalihenzi,

Kawaulize ndugu zake.

Prof. Haroub kafa Marxist au kafa Muislam?

Mohamed
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…