Gwalihenzi
JF-Expert Member
- Oct 21, 2011
- 5,125
- 1,301
profesa alikufa ghafla kwa ugonjwa wa moyo, sasa ndugu zake wataniambia kitu gani cha zaidi?Je profesa alikufa akieneza chuki na uhasama kwa kutumia uislam kama wewe?Gwalihenzi,
Kawaulize ndugu zake.
Prof. Haroub kafa Marxist au kafa Muislam?
Mohamed
Currently...
Previously on this thread...
Need I say more?
Hapo Mgalanjuka mwenzio alitaka ku- twist mjadala kuhalalisha kwamba Mohamed lengo lake ni kuwa enzi wazee wake kama wapigania Uhuru wa Tanganyika na wala si kwa sababu ya udini wakati makala nzima imejaa maneno yenye kuonyesha utengano wa kidini.
Kwa sababu sio ukweli imeshajifuta yenyewe, nakushangaa sana kwa kutumia nguvu kubwa kuielaza na kuwajengea hofu vijana wa kiislam kuwa wanaonewa wakati wenyewe ukweli wanauona. Nimekusikia kwenye clip zako YouTube ukitumia majina ya marehemu akiwemo marehemu Profesa Haroub Othman kuhalalisha chuki yako! Haroub hakuwa mwalimu wako peke yako, wengi tulifundishwa naye, kwa tulie mfahamu msomi yule hakuwa na fikra unazompandikizia wewe, unafanya hivyo kwakuwa unajua kwamba hataweza kuja kujitetea hapa.Waache vijana wa Tanzania wafurahie umoja wao, waache vijana wapambane na umaskini na ufisadi ktk nchi yao kwani matatizo hayo hayawatenganishi kwa imani zao, wote kwa pamoja wanajeruhiwa nayo. Kama kweli Mungu wako anasifa tatu yaani "Omnipotence, Omniscience na Omnipresence" basi nakusihi mwachie yeye atoe hukumu ya haki kwa chuki unayo mpakazi/mzuria mwalimu Nyerere dhidi ya uislam.La sihivyo njoo uuangane na mimi(Atheist) na wala usiusingizie usilamu kujenga sifa na chuki zako binafsi.
Huyo aliniuliza kama najua maana ya "contradictions" hivyo nashangaa mara kawaita watu "wanafik wakubwa" then anawaambia "kazi yao imeota mizizi"
We acha tu! Natamani ningeweza kupata mkalimani awatafsirie wadau wote wa nje ya nchi alikopita MS vilivyomo kwenye hii thread!
Ritz,
Unamchapa farasi aliyekufa.
Ukisoma jibu lake ndiyo utajua mengi zaidi...
Umetoa mifano ya kisomi kabisa anakupa habari za "Cock and Bull."
Hawa hawawezi kuja na historia nyingine.
Waandike nini?
Ndiyo maana waliipiga vita historia ya wazee wetu.
Kuna mradi wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere kuandika maisha yake.
Tuisubiri hiyo Insha Allah.
Mohamed
Gwalihenzi,
Kawaulize ndugu zake.
Prof. Haroub kafa Marxist au kafa Muislam?
Mohamed
Mimi hoja yangu ni kwamba hakuna "Historia kamili" kama kungekuwa na hilo basi dunia nzima labda vitabu vya historia visingezidi mia!!
Hayo aliyoyaandika ndiyo "usomi" wenyewe eeenh!!?? Kweli mfumoKristu ulifanya kazi!!
Sasa hiyo ni "contradiction"? wewe ya Faiza Foxy huyawzi, mambo yako wazi hapa ukumbini tupe nukuu za kusema hii si sawa, sawa hii hapa. Achana na Faiza Foxy kasema nini, mimi nimeandika historia? unanchekesha!
Sasa inanifanya niamini maneno ya Zomba (my cousin) ameni PM na kuniambia hakuna cha Mohamed Said wala Mwanakijiji wote hao ni system na wanawacheza shere
Mkuu, umemshika pabaya FaizaFoxy. Hatoki.....lol.Achana na Faiza kasema nini?? Oh! ilikuwa sio part ya hii thread? Hiki ndo kichekesho haswaa... By the way nani ni mwongo/mnafiki kati ya cousin wako Zomba aliye ku-PM au MS uliyedai anacheza shere? ulisha-apologize kwa mmoja wao?
MM,
......Unadhani haya maswali katika JF itasaidia kitu?
Mohamed
Mr Right,
Usibishane na Jasusi,
Kwa hakika mimi namuelewa sana Jasusi kwa nini fikra zake zinampeleka kutilia shaka kila jambo ambalo kwake analiona hili singeweza kufanya yeyote ila Nyerere.
Bahati mbaya sana na Nyerere akipenda sana watu waamini hivyo.
Akitaka sana kuwa harakati za uhuru zianze na yeye.
Kuna kisa cha kusisimua sana siku Abdulwahid anamfahamisha Nyerere kuhusu baba yake Kleist, kuwa alikuwa anazungumza Kijerumani na Kiingereza, akijua shorthand (hati mkato), akijua kupiga typewriter na akijua kuweka vitabu vya hesabu na ndiye alijenga ile ofisi ya TAA ambayo TANU ilizaliwa.
Abdu akamweleza pia yeye alitokea mwanafunzi wa kwanza Territorial Examination na alikuwa anasubiri kwenda Makerere ndipo alipotiwa jeshini KAR kwenda kupigana Burma.
Hapo wapo katika kuandika historia ya harakati ya kudai uhuru pamoja na Dr Kleruu.
Nyerere alitatazika sana.
Kwa fikra yake alidhani mambo yangeanza na yeye 1954 anakuta historia inarudi nyuma miaka ya 1920.
Bila shaka ilimjia fikra yake mwenyewe. Je yeye ana historia kama ile? Vipi baba yake? Jibu ni kuwa hapana hawana historia kama ile?
Ikabidi historia ile ihujumiwe na ule mswada hadi leo haujulikani ulipo.
Sasa mimi wala simlaumu Jasusi.
Hiki ni kitu kipya sana kwa wengi kwa hiyo kila lile ambalo waliona ni saizi ya Nyerere wakiambiwa hakufanya watalitia kasoro.
Nasema na siishi kusisitiza kuwa ikiwa mie nasema uongo waandike kitabu ukweli ujulikane.
Prof. Haroub alimuonya Nyerere kuwa akiwa kimya katika histroria niloandika itamuharibia sifa yake pakubwa.
Ndiyo sasa tunabishana Nyerere kasoma kitabu cha Mohamed Said au hakusoma...na hiki kitabu changu ndicho kilichosimama tunaingia mwaka wa 14 kuwa ndiyo historia ya kuaminika kuhusu uhuru wa Tanganyika na kinasomeshwa kote duniani.
Toleo la Kiswahili tunaingia chapa ya tatu na kwa kweli kitabu ni maarufu sana watu wakenda dukani wanasema "Nipe kitabu cha Abdu Sykes" na muuzaji anajua ni kitabu kipi.
Sahib wangu mmoja prof wa African History nimemueleza jinsi baadhi ya watu walivyokasirishwa kuona historia rasmi imetolewa manani kanishauri kufuatilia hilo kwa karibu na niandike "paper" Insha Allah watakuwa na kongamano mwaka kesho na angependa nihudhurie na niwasilishe mada hii.
Mohamed
Ndio hulioni. Sasa wewe kama unayajuwa ya huyo unaemtaja si utuletee hapa tufaidike, kwanini umngoje Mohamed Said?
Nguruvi3, Kigarama, Mag3, Mzee Mwanakijiji..
Ebu na nyie jipangeni kama itawezekana muungane kwa pamoja muandike histori ya Uhuru wa Tanganyika..
Tena itakuwa vizuri mpinge yote yale ambayo sio ya kweli kwenye kitabu cha Mohamed Said..
Inawezekana kuna mashujaa wengine nyie mnawajua waliopigania uhuru wetu Mohamed Said, hawakuandika kutokana na udini wake dhidi ya ukirstu..
Na hicho kitabu ndio kitakuwa historia kamili ya uhuru wa Tanganyika sababu kitaandikwa kwa pamoja na magwiji niliowataja..
Tunakisubili kwa hamu...
Siku moja nilimuuliza Mohamed kwamba mbona kwenye masimulizi yake sioni jina la MARTIN KAYAMBA? Mpaka leo Kimyaaa!!
Kigarama,
Nimepata humu ndani kujibu kuhusu Martin Kayamba lakini simkumbuki aloniuliza.
Kayamba alikuwa kibaraka wa Waingereza na akijikomba sana kwao.
Yeye ni "contemporary" wa Kleist Sykes na maisha yao wote yamo katika "Modern Tanzanians" cha John Iliffe.
Chungulia hapo chini Erika Fiah kasema nini kuhusu Kayamba:
"Kalamu ya Fiahilikuwa haina muhali. Katika rambirambi alizotoa za kijeuri na za dharau juu yakifo cha Martin Kayamba,[1]Fiah aliomboleza kwa kusema kwamba Waafrika hawakunufaika kwa elimu ya Kayambawala kwa wadhifa wake kama karani wa kaimu Katibu Mkuu."[1]
Ukipenda unaweza kumsoma Kayamba katika kitabu hiki:
Kayamba, Martin,The Autobiography ofMartin Kayamba, The Story of Martin Kayamba Mdumi, MBE, of the Bondei Tribe MargeryPerham, (ed) Ten Africans, 5-272.
Mwenyewe umeona umeuliza swali gumu sana na shingo unatoa.
Ndiyo maana dada yangu FF husema "usinchekeshe."
Mie mabuku yote hayo nishayanywa miaka mingi ilopita.
Mohamed
Labda ....Zomba(her cousin) alim PM tena FF na kumuambia MS hayupo kwenye system.....ilikuwa ni false alarm tu..!
Yeye atakuambia andika 'paper ' na wewe......ila wale wa mihadhara ya nje ya nchi huwa anawajibu eti kwa sababu hawaulizi maswali kama ya humu ndani! sijawahi kuona 'scholar' aliye bogus kama Mohamed Said. Utaandikaje makala halafu ukashindwa kui defend kwa hoja?Huu ndio ukwepaji wa kujibu maswali......Brother MS jibu swali!
Faiza wewe unapiga makelele wala hujui kujenga hoja, tafadhari acha makelele yako na sifa za kijinga hapa jamvini, mzee Mohamedi Said aliliona bandiko langu akalijibu kabla ya wewe kuweka upupu wako hapa. Rudi usome jibu la mzee wako.Hao wazee unaowaorodhesha hapa na mchango wao hakuna anayeukataa, tunachokikataa hapa ni huo mtazamo finyu wa mzee wako kwamba wao ndio pekee walioleta ukombozi na kwamba Nyerere hakufanya chochote kuwaendeleza waislam.Si ukweli kuwa Nyerere alipokelewa na Abdul Wahid? si ukweli kuwa Nyerere hakuwa muasisi wa TAA? si ukweli kuwa Abdul Wahid ndio alitoa jina la TANU? ni kipi ambacho si ukweli? tuoneshe nukuu ya Mohamed Said ambayo si ukweli halafu wewe tupe iliyokweli, si kuandikia mate na wino upo. "si ukweli" huoneshi hilo "si ukweli" liko wapi, "si ukweli" huoneshi ukweli uko wapi.