Kigarama,
Nimepata humu ndani kujibu kuhusu Martin Kayamba lakini simkumbuki aloniuliza.
Kayamba alikuwa kibaraka wa Waingereza na akijikomba sana kwao.
Yeye ni "contemporary" wa Kleist Sykes na maisha yao wote yamo katika "Modern Tanzanians" cha John Iliffe.
Chungulia hapo chini Erika Fiah kasema nini kuhusu Kayamba:
"Kalamu ya Fiahilikuwa haina muhali. Katika rambirambi alizotoa za kijeuri na za dharau juu yakifo cha Martin Kayamba,[1]Fiah aliomboleza kwa kusema kwamba Waafrika hawakunufaika kwa elimu ya Kayambawala kwa wadhifa wake kama karani wa kaimu Katibu Mkuu."[1]
Ukipenda unaweza kumsoma Kayamba katika kitabu hiki:
Kayamba, Martin,The Autobiography ofMartin Kayamba, The Story of Martin Kayamba Mdumi, MBE, of the Bondei Tribe MargeryPerham, (ed) Ten Africans, 5-272.
Mwenyewe umeona umeuliza swali gumu sana na shingo unatoa.
Ndiyo maana dada yangu FF husema "usinchekeshe."
Mie mabuku yote hayo nishayanywa miaka mingi ilopita.
Mohamed