Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

unajua mambo anayoeleza bwana M/S ni sawa na hii kauli ya kumlinganisha Alex Fergie na makocha wengine na kusema wako kwenye mizani moja.Kwanza Nyerere unamsimulia ni mtu ambaye hakutoweka muda mrefu hapa duniani. kama angeishi karne ya 12 hivi kweli watu wangekusadiki.Sikiliza hotuba aliyosema kuhusu udini akisema ni upumbavu kwa Watanzania kuwaza mambo hayo.Sasa wewe unadai alikuwa nao .Aliutumia muda gani ambao sisi wa leo hatuuona.Watu wa sampuli hizi watamsifia Iddi Amini kwa vile ni muisilamu.Unapoteza muda wako ukidhani utaharibu jina lake kumbe, unajiharibu wewe mwenyewe. Ukifanya mazuri watukupenda waisilamu na wengine lakini ukiona kuna kundi la kukushabikia basi kuna kasoro. Lakini endelea kuandika na kufunua yale ya moyoni mwako.
 
 
 
Huwezi kabisa kutenganisha Waislaam na harakati za kutafuta madaraka. Hilo ukipenda usipende. Wale waliompokea Nyerere Dar. walikuwa dini ipi?

Oh boy! "harakati za kutafuta madaraka"? Sikulijua hili, nilidhani kutafuta uhuru...
 

Zenge,

Huenda unasema haya kwa kuwa hujui yaliyojificha.
Insha Allah endapo yatakudhihirikia ukweli wake huenda ukabadilisha mawazo yako.

Mohamed
 

Sweke34,

Unahudhuria darsa?

Leo niko na Sheikh Hassan bin Amir.
Usipuuze hayo yaliyomo humo wewe huyajuia.

Soma upate faida na uelimike.

Mohamed
 
 

Unaweza kunionesha ni wapi uliyaona hayo niliyoyawekea nyekundu?

Hilo la bluu, Jee, wewe unaweza kutuonesha ni wapi Nyerere kawaendeleza Waislaam wakati tuna 83% vs 17%.
 
Labda ....Zomba(her cousin) alim PM tena FF na kumuambia MS hayupo kwenye system.....ilikuwa ni false alarm tu..!
UNAFIKI huu ni kielelezo cha kwanini baada ya miaka 50 ya uhuru bado kuna watu wanasema kuna mfumo Kristo.

Kila mmoja ana haki ya kusema apendavyo, kama vile wewe unapokuja humu kupinga hata unachokipinga hakijulikani ni nini. Jee, kuna kitu ambacho unakipinga wewe mwenyewe unakijuwa?
 
Mag3, bado tunayangoja ya Mara kama ulivyoahidi na kama Mohamed Said alivyokukumbusha.
 
Unaweza kunionesha ni wapi uliyaona hayo niliyoyawekea nyekundu?

Hilo la bluu, Jee, wewe unaweza kutuonesha ni wapi Nyerere kawaendeleza Waislaam wakati tuna 83% vs 17%.
Kwa chuki na ulimbukeni wa imani yako ya kidini utaonaje juhudi kubwa alizo fanya kuwaendeleza watanzania bila kujali dini, rangi wala kabila zao? Huwezi kuona na hutakaa uone. Utaendele na uchochezi wako bila hekima kwa sababu ya ubinafsi wako wewe na huyo mzee wako. Bahati ukweli ni "inert" utadumu daima na Nyerere ataenziwa daima na watu wa kweli na wapenda amani bila kujali imani zao. Mzee Mohamed Saidi anajua wazi kizazi chake kilifaidi matunda ya utumishi uliotukuka wa mwl Nyerere, hatakubali hilo kwakuwa amejikita katika jitihada za kibaguzi za kidini.
 
 
By Mohamed Said


Gwalihenzi,

Kawaulize ndugu zake.

Prof. Haroub kafa Marxist au kafa Muislam?

Mohamed
Hapa MS bado hatujapata jibu....kuna wakati Prof. Haroub alikuwa siyo muislam? au ulikuwa na maana gani hapo?
 

Huna cha kusema wakati inajulikana kuwa hii nchi Nyerere kang'atuka iko hohehahe. Matunda? matunda yepi hayo? hata dawa za mswaki hakuna wakati wake, hata viberiti kwa foleni, watu taabani unaniambia kutukuka? mimi nilikuwepo toka Nyerere anaichukuwa hii nchi mpaka anakufa. AlhamduliLlah, sijaona cha maana alichoifanyia hii nchi, kipi> vijiji vya ujamaa?
 
Mohamed amefikia mahali pa kujipa wadhifa fulani juu ya hukmu ya waislam wa Tanzania. Siku za awali na katika post moja ya sasa ameeleza kuwa waislam wanaichukulia BAKWATA kama yudas karioti. Hapa keshatoa hukumu kuwa ni makafiri na walifariki wakiwa makafiri mfano ni mwanzuoni na ulamaa Mufti Hemed bin Jumaa.

Mohamed amepitisha hukumu kuwa marehem Haroub Othman(RIP) amefariki Muislam baada ya kuacha umarxist. Tayari keshampangia darja mbele ya mwenyezi mungu.

Si mtume wa mwenyezi mungu wala swahaba au imam yoyote aliyewahi kutoa hukumu dhidi ya mwanadamu mwenzake. Uislam unasema kuwa kila mja atakwenda mbele ya haki na amali zake. Jukumu la waumini ni kuhakikisha wanamtimizia yale yanayojuzu baada ya kufariki.

Sasa Mohamed anapojivika jukumu la kutambua nani mwislam nani kafiri inatia woga na amefikia mahali anavuka mipaka ya kidini.
Jukumu la nani kafariki vipi na ana amali gani ni la mwenyezimungu.

Wewe jibu maswali na hoja ya kitabu chako.
 
Hapa MS bado hatujapata jibu....kuna wakati Prof. Haroub alikuwa siyo muislam? au ulikuwa na maana gani hapo?

Sweke34,

Mafunzo yetu yanatukataza kukumbushana enzi ya ujahilia.
Haifai sasa kuanza kuongea mambo yasopendeza ya marehemu.

Hivi sasa kuna mnakasha mkubwa kuhusu Sayyid Baadawy Quallatein mmoja wa viongozi wa Umma Party.
Amefariki dunia Makka juma lililopita.

Kwenye taazia yake kuna walomwita "comrade."
Wengi hawakupendezewa na hilo kwani wanasema alitubu na akarudi kwa Mola wake.

Nadhani umenifahamu.

Mohamed
 

Nguruvi3,

Prof. Haroub mie ndugu yangu.
Usitake kuleta maneno yasiyokuwa na maana yoyote.

Kuhusu BAKWATA, ukafiri sidhani kama yanakuhusu sana wewe.


Mohamed
 
Bibie,
Sijakusikia unalalamikia umeme unaokatika kwa saa 12 na zaidi kwa zaidi ya mwaka mzima sasa. Nyerere alipoondoka alituachia shirika la ndege Air Tanzania. Leo liko wapi? Umeshupalia tu kuvaa ndara na kukosa dawa ya mswaki. Sisi tulitumia chumvi, angalau maji yalikuwepo na umeme wa uhakika. Nyerere alituachia madini tuje tuchimbe wenyewe M'kwere akawakaribisha mafisadi wenzake sasa wanayamaliza huku Watanzania wakiwa wanazalia kwenye sakafu Temeke. Talk about double standards!
 
Nguruvi3,Prof. Haroub mie ndugu yangu.
Usitake kuleta maneno yasiyokuwa na maana yoyote.Kuhusu BAKWATA, ukafiri sidhani kama yanakuhusu sana wewe.Mohamed
Ni kauli zako usizozipima na za majigambo ndizo zinaleta 'maana'. Hupaswi kusema Marhum Othman alifariki akiwa mwislam na sio marxist, hatukuhitaji habari zote hizo. Tunajua alikuwa na dini na wengi tunamjua alikuwa mwislam.

Hili la BAKWATA nimelitoa katika makala zako(nikunukuu?) kwahiyo huna sababu ya kusema ni la BAKWATA, habari ulizoeleza ni kwa watu wote.
Ndiyo maana nakuuliza kiongozi wa BAKWATA na waumini wao waliokuwa kama Yudas karioti kwa mujibu wa kitabu chako walifariki makafir?

Huwezi kujivua jukumu la wewe kusema huyu ni safi yule ni chafu, hayo yapo ndani ya maandishi yako. Ndiyo matunda ya chuki, baada ya kummaliza Nyerere na soksi ndeefu na vitoweo, dhambi ya chuki inakutuma uwahukumu wengine kwasababu tu wanatofautiana nawe.

Jibu hoja na maswali, unapojieleza ndipo mambo yasio na taaluma kama haya yanajitokeza katika maandiko yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…