unajua mambo anayoeleza bwana M/S ni sawa na hii kauli ya kumlinganisha Alex Fergie na makocha wengine na kusema wako kwenye mizani moja.Kwanza Nyerere unamsimulia ni mtu ambaye hakutoweka muda mrefu hapa duniani. kama angeishi karne ya 12 hivi kweli watu wangekusadiki.Sikiliza hotuba aliyosema kuhusu udini akisema ni upumbavu kwa Watanzania kuwaza mambo hayo.Sasa wewe unadai alikuwa nao .Aliutumia muda gani ambao sisi wa leo hatuuona.Watu wa sampuli hizi watamsifia Iddi Amini kwa vile ni muisilamu.Unapoteza muda wako ukidhani utaharibu jina lake kumbe, unajiharibu wewe mwenyewe. Ukifanya mazuri watukupenda waisilamu na wengine lakini ukiona kuna kundi la kukushabikia basi kuna kasoro. Lakini endelea kuandika na kufunua yale ya moyoni mwako.
