Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa


Mag3,

Yote hayo nimeeleza katika kitabu chake.

Yeye alimtaka Chief Kidaha achukue uongozi wa TAA waanzishe TANU na wadai uhuru.
Hii ilikuwa 1950.

Habari zaidi zimo kwenye kitabu.

Mohamed

Ha, ha, ha, haaaa ! mbavu zangu. Bila shaka anayeongelewa hapa ni Mkatoliki Chifu David Kidaha Makwaia wa Sukumaland. Yaani Abdul Sykes alipokuwa anamtaka mtu wa kuongoza chama alichokuwa anapanga kukianzisha, hakuona mtu nje ya Wakatoliki. Oops, samahani labda huo mwaka 1950 Chifu Kidaha alikuwa bado hajapewa jina la David pamoja na kuwa mshikaji mkuu wa Gavana mkoloni. Ehe, halafu baada ya huu mpango kutofanikiwa akatafutwa Mkatoliki mwingine mtoto wa Chifu Wanzagi Nyerere na ilipofika mwaka 1954 naye akapewa TANU chama alichokianzisha Abdul Sykes akiongoze ! Hadithi zingine zahitaji ujasiri wa hali ya juu kuziamini lakini kwa mtoto wa Gerezani hamna taabu. Haya Mwalimu baada ya kupewa Uraisi wa TANU, akakabidhiwa katiba na hotuba iliyokuwa tayari imeandikwa miaka mingi tu huko nyuma akaisome UN. Hayo ndiyo maisha ya Abdulwahid Sykes, the kingmaker wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika !
 
Asante sana Mag3 kwa Nondo zako sisi vijana wa dotcom hatuna cha kuongeza zaidi ya kusoma kwa makini na hakika Pumba na Mahindi zinatengwa. Nashauri Makala za kupinga historia ya MS iandikwe kwenye Magazeti ya Tanzania

Kuna Maswali nyameulizwa lakini yamekosa majibu mpaka sasa Uzi Unalekea Peji ya 110.

1. Nani walijitokeza kugombea Urais wa TANU/TAA
2. Matokeo ya Kura yalikuwaje

Asanteni sana Wazee wangu
 

Siku zote ukweli unasemwa hadharani na uwongo unazungumzwa upenuni.

Nilitaka kukuuliza je kuna mtu yeyote alithubutu au kudiriki kuzijibu hizo makala. zako kwenye magazeti huko Tz?
 
Siku zote ukweli unasemwa hadharani na ukweli unazungumzwa upenuni.

Nilitaka kukuuliza je kuna mtu yeyote alithubutu au kudiriki kuzijibu hizo makala. zako kwenye magazeti huko Tz?

Kuhusu historia ya TANU....au ile ya magerezani mimi binafsi sijawahi kuona watu wakiipinga kwenye magazeti lakini hii ya 'mfumo kristo' watu wamesha ipinga sana.
Soma hapo chini na wewe labda utafuta ujuha wako wa mfumo kristo.

Majeraha ya udini yataangamiza taifa



Na Saed Kubenea -

KONGAMANO la kitaifa la Waislamu juu ya kile kilichoitwa, "Kupambana na mfumo Kikristo" lililofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubelee, jijini Dar es Salaam, 16 Oktoba 2011, limeibua mengi.
Kwanza, limethibitisha madai ya baadhi ya watu, kwamba shutuma, tuhuma na lawama zinazohusu mfumo wa uendeshaji serikali nchini, nyingi hazifanyiwi utafiti wa kutosha.
Kwa mfano, wanazuoni wa kiislamu waliohutubia kongamano hilo la siku moja na kutoa walichoiita, "Waraka mrefu wa utafiti," wametuhumu kitendo cha serikali kutoa misamaha mikubwa ya kodi kwa taasisi za kikristo zinazotoa huduma za jamii nchini, kuliko ilivyofanya kwa madhehebu ya kiislamu.
Aidha, wanazuoni wanasema serikali imekumbatia mfumo kikirsto; inaendeshwa kikirsto na imewageuza waislamu kuwa watu wa daraja la chini.
Pamoja na mambo mengine, wanatuhumu kuwapo wakurugenzi waislamu wawili tu, kati ya tisa katika wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi; mkaguzi mmoja kati ya wakurugenzi wakuu 11 wa kanda; maofisa elimu wa mikoa watano kati ya 21 na maofisa elimu ya msingi 23 kati ya 125.
Ukiangalia kwa haraka madai haya, unaweza kukubaliana nayo. Lakini ukijipa muda, ukapima na kutafakari kilichopo na kinachodaiwa kuwapo, utaweza kubaini kuwa kilichosemwa, ama kimepotoshwa au waliotumwa kufanya utafiti kuna mambo bado hawajaeleza.
Kwa mfano, serikali haiwezi kuwa inatoa fedha za ruzuku au misamaha ya kodi kwa taasisi zinazotoa huduma za kijamii kwa lengo la kubeba ukirsto. Inafanya hivyo kutokana na kuelemewa na mzigo wa uendeshaji serikali; mzigo unatokana na kufikia ukomo wa kufikiri katika kuhudumia wananchi.
Ukiona serikali haina uwezo wa kujenga na kuendesha hospitari zake yenyewe zinazokidhi mahitaji ya wananchi wake; haiwezi kuendesha shule, vyuo vya elimu ya juu wala vyuo vya ufundi vyenye hadhi na viwango vinavyohitajika, basi ujue hapo kuna tatizo.
Matokeo yake, serikali inaamua kujisalimisha ama kwa wahisani wa nje au ndani. Baadhi yao ni madhehebu ya kidini.
Wakati taasisi za kikirsto zinamiliki msululu wa hospitali zikiwamo Bugando Medical Centre, Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) na hospitari za wilaya karibu 28 nchini nzima, madhehebu ya kiislamu hayana hata hospitali moja ya rufaa, wala hospitali yenye hadhi ya kuitwa hospitali kuu ya mkoa au wilaya. Imeishia kwenye vituo vya afya na zahanati.
Kwa upande wa vyuo vikuu, madhehebu ya kikirsto yanamiliki chuo kikuu cha St. Augustine (SAUTI) cheyenye matawi ya Nyegezi, Bugando, Tabora, Iringa, Mtwara, Moshi na Bukoba.
Vyuo vingine ni St. John Dodoma, Mount Meru Arusha, Kisanji Mbeya, Chuo Kikuu cha Arusha na Tumaini chenye matawi Iringa, Moshi, Makumira Arusha, Lushoto Tanga, Dar es Salaam na Mbeya. Hivi sasa, madhehebu hayo yako mbioni kufungua matawi mawili ya Karagwe na Bukoba mjini.
Taasisi za kiislamu zinamiliki chuo kikuu kimoja tu – Morogoro Islamic University (MIU), tena ambacho kiwanja na majengo yake yalitolewa na serikali. Madhehebu ya kiislamu hayamiliki hata taasisi tano zinazojihusisha na elimu ya juu. Nyingi ya taasisi za kiislamu zinaishia kumiliki shule za msingi na sekondari.
Je, katika hili, serikali yaweza kulaumiwa kwa kutoa misamaha kwa madhehebu ya kidini, kwa kisingizio kwamba wanaonufaika zaidi ni madhehebu ya kikirsto?
Kilichopo ni hiki: Serikali imetoa upendeleo kwa madhehebu ya kidini kusaidia katika eneo hilo, hasa afya na elimu. Yule anayefikisha viwango vinavyotakiwa, ndiye anayepewa ruzuku, bila kujali muislamu au mkristo.
Lakini kuna hili pia. Anayetoa msamaha wa kodi kwa mujibu wa sheria ni waziri wa fedha. Kwa sasa, Mustaph Mkullo; ni muislamu. Ndani ya wizara yake, Mkullo anasaidiwa na manaibu waziri wawili – mmoja ni muislamu, Pereira Ame Silima. Yupo pia katibu mkuu, Ramadhan Khijjah; ni muislamu.
Mkullo amekuwa waziri wa fedha tangu mwaka 2008 baada ya Rais Jakaya Kikwete kuunda upya baraza lake la mawaziri kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa aliyetuhumiwa kuingiza nchi kwenye mkataba tata wa Richmond.
Alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Zakia Meghji. Ni muislamu. Sasa waislamu wanataka kusema, Mkullo anawahujumu? Kunahitajika utafiti wa ziada kuthibitisha hili.
Je, ni taasisi ngapi za kiislamu zilizopeleka maombi ya msamaha wa kodi kwake zikakataliwa? Misamaha hiyo iliyoombwa ilikuwa na thamani ya kiasi gani? Nani aliyeoomba? Ni taasisi za kiislamu au watu waliotaka kuzitumia taasisi hizo kujinufaisha binafsi?
Hata kama wakurugenzi katika wizara hiyo, wengi ni kutoka madhehebu ya kikristo, hiyo haiwezi kuhalalisha madai kwamba yanayotendeka ndani ya wizara hiyo yanatokana na shinikizo la kidini; misimamo ya kidini na waislamu wameathirika kwa kiwango kikubwa na jambo hilo.
Hata hoja ya kuwapo wakristo wengi kwenye wizara ya elimu, inaweza kuonekana imetolewa bila utafiti wa kina. Ndani ya wizara ya elimu, pamoja na wakurugenzi, makamishina na watendaji wengine, yupo waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa. Huyu ni muislamu. Anasaidiwa na naibu waziri, Kassim Majaliwa. Naye ni muislamu.
Hivyo basi, kama madai haya yana ukweli, Dk. Kawambwa na Majaliwa watakuwa ndiyo wanatumika kuhujumu waislamu?
Jambo moja ni muhimu. Waislamu wasiendekeze malalamiko. Bali wajipange kama taifa kutafuta njia ya kujikwamua. Watafute mbinu elekezi zinazojenga hoja za kujadili na kuibua utambuzi, badala ya kuibua malalamiko ya "kusalitiwa kwa waislamu katika siasa za Tanzania."
Kwa mfano, Rais Kikwete hakuteuliwa na chama chake kuwa mgombea urais kwa sababu yeye ni muislamu. Alichaguliwa baada ya kuonekana anaweza kushindana na wagombea wengine wa upinzani na kushinda.
Aliposhika nafasi hiyo, akateua wasaidizi kutoka madhehebu mbalimbali, kutokana na jinsi walivyojitokeza kwenye kugombea ubunge na kushinda.
Hivyo basi, kuendeleza madai ya kubaguliwa, kunaweza kuibua madai kutokana madhehebu mengine. Kwamba rais ni muislamu. Makamu wake ni muislamu. Rais wa Zanzibar na makamu wake wawili wote ni waislamu.
Waziri wa fedha, muislamu. Waziri wa ulinzi, naye ni muislamu. Waziri wa utumishi ni muislamu. Waziri wa afya, waziri wa mambo ya ndani na naibu wake, waziri wa uchukuzi na naibu wake, jaji mkuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), mkuu wa usalama wa taifa, wote ni waislamu.
Wengine wanaweza kufika mbali zaidi. Wakasema, ndani ya Benki Kuu (BoT), manaibu gavana wote watatu, ni waislamu. Bodi ya wakurugenzi yenye wajumbe 10, saba ni waislamu. Kwenye mifuko mitatu mikubwa ya hifadhi ya jamii, miwili inaongozwa na waislamu. Orodha ni ndefu.
Jambo muhimu ni iwapo walionufaika na walioshika madaraka, wamenufaika kwa sababu walikuwa na sifa, au ni kutokana na misimamo ya kimadhehebu?
Tuulizane: Ni waislamu wangapi wamenufaika kwa Kikwete kuwa rais? Kama ni wachache, ina maana amewasaliti? Kama amewasaliti, sasa wafanyeje? Mchezo huu ni mauti yetu sote!
 

Mbona hakuna sehemu yoyote hapa ambayo imejibu historia ya Uhuru ya Mohamed Said...

Kwa hiyo hii ndio 'paper' ya kumjibu Mohamed Said?
 
Mbona hakuna sehemu yoyote hapa ambayo imejibu historia ya Uhuru ya Mohamed Said...

Kwa hiyo hii ndio 'paper' ya kumjibu Mohamed Said?
Soma vizuri nilichoandika juu ya kichwa cha habari!
 
Siku zote ukweli unasemwa hadharani na ukweli unazungumzwa upenuni.

Nilitaka kukuuliza je kuna mtu yeyote alithubutu au kudiriki kuzijibu hizo makala. zako kwenye magazeti huko Tz?

Hadharani... then upenuni..??? Kama ulimaanisha vinginevyo rekebisha nikwambie kitu.
 

Nguruvi3,

Umezungumza mengi lakini nitakujibu moja tu.

Mimi sikatai kama hii ni historia ya Gerezani na Kariakoo.
Sasa tatizo liko wapi?

Kuhusu mie kuwa hatari.
Jina langu si hilo hapo mbona sijakamatwa?

Hiyo hatari ni ipi kwa kuandika na kueleza matatizo yanayoikabili nchi yetu?
Narudia tena.

Njia ni kuandika ukaeleza ukweli kama unavyoujua wewe vinginevyo sauti yako itaishia JF.
Mie nimekuja na historia mpya na umeona dunia imeipokeaje.

Hivi sasa naandika paper "Rejection of Realities in History: Stories of Unsung Heroes" nimempa rafiki yangu mmoja outline jibu lake, "Mohamed this is a book call me please I have something for you!"

Njia ni hiyo tu hakuna barabara wala kichochoro cha kukatiza.
Kama nisingeliandika nyie msingelimjua Abdu Sykes, Mshume Kiyate nk na leo tusingekaa hapa jamvini kufanya mnakasha.


Mohamed
 

Mag3,

Kwa hilo la kushangaa hata mie nakuunga mkono tuko pamoja.
Siku nilipokabidhiwa Nyaraka za Sykes ulikuwa mzigo wa mafaili.
Nilikesha.

Sikuweza kuamini macho yangu.
Hivi haya yalitokea kweli?

Nilopoanza mahojiano ndiyo mzigo ulinielemea sana.

Nilipompa "publisher" mswada siku nilipokwenda kumsikiliza kanambia hii ni "gold mine."

Sikupewa shajara za Abdulwahid Sykes kuzisoma.
Nimeambiwa katika mikutano ya mwanzo ya TANU Nyerere akihutubia Abdu alikuwa akionekana nyuma akiandika hotuba zile "verbatim' katika shorthand "hatimkato."

Umezungumza kuhusu hotuba ya Nyerere UNO 1950 hii ni katika kitendawili kikubwa sana.

Nimekwenda Dodoma Maktaba ya CCM jalada ilimokuwa hotuba imenyofolewa "Archivist" pale alikuwa marehemu Said Ngwangwa.

Nimekuja Tanzania National Archives (TNA ) jalada halipo na microfilm vilevile imetoweka.
Ukipenda na wewe unaweza ukafanya utafiti kama nilofanya mie na pindi mwaka uje ukumbini utujuvye.

Hili somo bado lipo wazi sana bado yapo mengi ya kuandika kuhusu kipindi kile.
Vukeni mipaka ya JF mtoke na mfanye utafiti.

Katika mihadhara mingi niliyotoa hivi ndivyo vitu huangaisha sana fikra za wataalamu wa masuala ya Afrika kuwa nyaraka muhimu za historia ya nchi zinapotea bila maelezo na nyingine ziko katika mikono ya watu.

Mohamed

PS: Kuna mtu kanipigia simu anasema, "Mohamed kila unapoulizwa swali na ukatoa jibu unazidi kunichanganya fikra zangu lakini linalonistaajabisha ni kuwa unaowajibu hawahisi kuwa unawapa kitu kipya hakijapata kujilikana kwa wengi. Inanisikitisha kuwa hawa ndugu zangu vichwa vyao haviwezi kupokea kitu kipya." MS
 
 
Hadharani... then upenuni..??? Kama ulimaanisha vinginevyo rekebisha nikwambie kitu.

Nilikusudia kuuliza kwa Ahali yangu Mohamed Said au members mliopo Tz
Siku zote ukweli unasemwa hadharani na uwongo unazungumzwa upenuni.

Nilitaka kukuuliza je kuna mtu yeyote alithubutu au kudiriki kuzijibu hizo makala. zako kwenye magazeti huko Tz?
 

Barubaru,

Dr Mayanja
akijiita Kataroge Mayanja Kiwanuka enzi za Nyerere akificha jina lake la Kiislam . Alipoingia Mwinyi akawa sasa anajinasibu kwa jina lake la Kiislam akijiita Ahmed Mayanja Kiwanuka. Kiwanuka alijaribu kupambana na mimi:
"Katika kuunga mkono kauli ya Nyerere kuhusukuwakumbuka mashujaa wa uhuru wa Tanganyika, na kwa kutaka kuitikia ilechangamoto yake ya kutaka historia ya kweli ya TANU iandikwe kama alivyosemamwaka wa 1984 na 1985, mwandishi wa kitabi hiki alichapisha makala katikaAfrica Events [1]ambayo Abdulwahid na wazalendo wengine wa TANU zilielezwa habari zao. Katikamakala yale mwandishi alifanya jambo ambalo kabla yake lilikuwa halijafanywa namwandishi yeyote. Mwandishi alisema kuwa Waislam ndiyo walikuwa mstari wa mbalekatika kupigania uhuru. Wakati ule ilikuwa mwiko kabisa kunasibisha Uislam auWaislam na harakati za kudai uhuru. Mwandishi alipewa kemeo kali kutoka kwamwanahistoria wa CCM, Dr Mayanja Kiwanuka,[1] kiongozi wa jopolililoandika Historia ya Chama Cha TANU 1954-1977, kitabu kinachoeleza historiarasmi ya Chama. Mwanahistoria wa ChamaCha Mapinduzi alikuwa na haya ya kusema dhidi ya mwandishi: "Makala inadai kuwa ingawa Waislam Tanzaniawalitoa mchango muhimu katika harakati za kudai uhuru, zipo juhudi za makusudiza kufifilisha mchango wao. Kutokana na hayo, makala nzima ina ngano ili kuipanguvu fikra zake, zaidi kwa kutaja majina ya wazalendo wa TANU ambao imetokeakuwa ni Waislam. Ukuu wa TANU, na hasa ukuu wa kiongozi-muasisi wake, MwalimuNyerere, ni kuwa, baada ya muda mfupi tu toka kuasisiwa (TANU), ikawezakuwaunganisha watu katika vuguvugu la utaifa lenye nguvu, lau kama watu haowalikuwa tofauti kwa kabila, utamaduni na dini za. Nia ya Said ni kupandizachuki, kwa bei yoyote ile, ukweli kwake yeye si kitu muhimu."[1]Hizi ndizo fikra zaKiwanuka, ambae aliaminiwa na CCM kusimamia utafiti na uandishi wa historiamahsusi ya TANU. Kilichomkera ni kusema kuwa Waislam ndiyo waliokuwa mstari wambele katika kudai uhuru wa Tanganyika. Kwa ajili ya kuwataja Waislam, makalaya utafiti ikawa sawasawa na "ngano," yaani hadithi. Mwandishi akatuhumiwa kusemauongo. Kiwanuka hakuweza kuuepuka msimamo wa Chama wa kutia mkazo katikakumsifu mtu mmoja, Nyerere peke yake katika kuasisi TANU - "Ukuu wa TANU, nahasa ukuu wa kiongozi-muasisi wake, Mwalimu Nyerere." Wakati akiandika manenohaya Kiwanuka alikuwa Katibu Msaidizi katika Idara ya Propaganda naUhamasishaji Umma katika Chama Cha Mapinduzi. Mwandishi alijibu mashambulizi yaKiwanuka kwa kueleza kuwa yote aliyoyaandika ni matokeo ya utafiti.[1]Kufuatia majibu haya Kiwanuka aliandika fedhuli kwa kumuita mwandishi"mwanahistoria asiye kuwa na kimo" na akamtisha mwandishi kwa kuapa kuwa endapoatajaribu kuibadilisha historia ya Tanzania atamwandama yeye na ndugu zake.[1]Baada ya mjadala huu baina ya mwandishi na Kiwanuka, watu wengi walijitokezakumuunga mkono mwandishi na huo ndiyo ukuwa mwisho wa ubishi. Kingine cha kustaajabisha ni kuwa anaeiwekahistoria kwa kufanya utafiti na kuiandika sawa, ndiyo anayetishwa na walewaliopotosha historia wanaachiwa waendelee kuipotosha historia na kuifanyiafisadi kadri watakavyo. "

Ndugu yangu Barubaru,

Haya usomayo humu ukumbini hayakuanza leo na angalia jinsi lugha zinavyoshahibiana.
Ukimtoa Dr Kiwanuka hakuna mwingine yeyote aliyekuwa na ujasiri wa kutaka kuweka mnakasha na mimi.

Mohamed



 

Umezungumza kuhusu hotuba ya Nyerere UNO 1950 hii ni katika kitendawili kikubwa sana.

Nimekwenda Dodoma Maktaba ya CCM jalada ilimokuwa hotuba imenyofolewa "Archivist" pale alikuwa marehemu Said Ngwangwa.

Nimekuja Tanzania National Archives (TNA ) jalada halipo na microfilm vilevile imetoweka.
Ukipenda na wewe unaweza ukafanya utafiti kama nilofanya mie na pindi mwaka uje ukumbini utujuvye.


Mohamed,
Nina swali moja la ziada. Sasa kama unasema hotuba aliyoitoa Nyerere UN mwaka 1955 ni kitendawili kikubwa sana, uliwezaje kuhitimisha kwamba iliandikwa na Abdulwahid Sykes mwaka 1950? Mimi nilidhani ulifikia hitimisho hilo baada ya kuona original manuscript ya hiyo hotuba kwenye shajara za Abdulwahid na kuilinganisha na hotuba iliyotolewa?
 

Jasusi,

Huko mbona nilishapita na nikaeleza historia nzima toka enzi za Memorandum on Constitutional Development Commitee na TAA Political Sub Committee?

Hii ilikuwa 1950 baada ya Dr Kyaruzi na Abdu Sykes kuchukua uongozi wa TAA na kumtia Sheikh Hassan bin Amir ndani ya kamati kuongeza nguvu.

Hebu soma "Critical Phase in Tanzania" cha Crawford Pratt ingia kwenye faharasha (index) "Memorandum on Constitutional..." hii ni kwa kuanzia upate mwanga kwanza.

Hata hivyo Insha Allah naingia katika maktaba yangu ya vitu vya kale nitakuwekea kitu hapa.

Mohamed
 

Namfahamu sana Dr Kiwanuka.
Watu wa sampuli yake mbona wapo wengi sana huko Tanganyika kama akina Moses Nnauye, Ibrahim Kaduma.

Nakumbuka safari moja nkiwa wizara ya fedha tukiwa safarini kikazi kuelekea geneva tukiwa watu sita miongoni mwao alikuwapo Al marhum Sheikh Aboud maalim na Ibrahim kaduma. Ilikuwa mwezi wa Ramadhani,tukiwa kwenye ndege mimi na Sheikh Aboud maalim tulikuwa tumefunga lakin nilistahajabu kumuona Ibrahim kaduma akiwa anakula tena na kupata pombe. Na hata tulipofika kule mwenzetu aliendelea kula pasi na matatizo yoyote. Na siku moja nilimuuliza alinijibu mie muislam

Baaadae nikasikia kuwa amebadili kabisa dini na kuwa Mkristo na iliandikwa kwenye hata vyombo vya habari vya kanisa. Sina uhakika kama bado yupo huyo mzee alikuwa anaishi maeneo kule ya juu ya UDSM.

Lakini suala langu la msingi kwako Sheikh Mohamed Said hapa. Ni kuwa uliandika makala hii ya Historia a uhuru wa Tanganyika katika gazeti la Mwananchi na wengi walisoma.

Je hakutokea mtu kuandika maka iwe katika gazeti hilo au lingine kupingana na makala zako. Kwani najua kuna magwiji kama Joseph Mihangwa, Padre Privatus karugendo, Generali ulimwengu, Prince Bagenda, na wengine.

Je hakuna aliye andika?
 

Juzi kanpigia simu mtu ananambia angalia Mtanzani hili ni gazeti la kila siku kuna mtu kaandika historia ya TANU.

Yusuf Halimoja kaandika historia ya TANU na kwa ule msisitizo alokuwa akiweka kuhusu Nyerere kuanzisha TANU na kuandika katiba nk nk. mie nikawa nacheka peke yangu.

Katiba haikuandikwa na mtu yoyote. Katiba wamenakili neno kwa neno kutoka katiba ya Convention Peoples Party ya Nkrumah wa Ghana sasa hiyo aloandika Nyerere kaiandikia wapi?

Sasa Nyerere hiyo TANU kaianzishia mji gani na ofisi ipi? Alikuwa na fedha kiasi gani za kuendesha chama?

Nani akimjua nk. nk.

Halimoja karudia yaleyale ya historia rasmi.

Inaandikwa historia ya TANU bila ya wale waliokuwa ndani ya TANU yenyewe...humsomi Abdu, Dossa wala Sheikh Hassan bin Amir wala yeyote yule katika TANU mstari wa mbele...

Hao jamaa ulowataja wananijua vizuri na wananikalia mbali sana...
Nilipata kualikwa kwenye "Hamza Kassongo Hour" kumzungumzia Ali Nabwa.

Kipindi hakikurudiwa na DVD tuliahidiwa kupewa tumekataliwa kupewa.
Nilikuwa mimi, Mohamed Ghassany na Ali Saleh.

Mohamed
 

Mke wangu siku zote anasema si tu Zanzibar bali mpaka Tanzania nzima haijawahi kutokea mwandishi wa habari mahiri kama Ali Nabwa. Na ukitaka kujua mengi kuhusu Huyu basi katika timu yenu wangemwongeza Salim Saleh kwani huyo kidogo anajua chimbuko lake na alisimamia sana maadili ya kiuandishi.

Mola amlaze pema Peponi.
 

MS,

Kuna maswali yamejaa hapa bila majibu sasa huyo mpiga simu anazungumzia majibu yepi? Au tuweke tena list ya maswali yaliyokosa majibu? Haya majivuno yamekuwa mengi mpaka yanatia shaka.
 
MS,

Kuna maswali yamejaa hapa bila majibu sasa huyo mpiga simu anazungumzia majibu yepi? Au tuweke tena list ya maswali yaliyokosa majibu? Haya majivuno yamekuwa mengi mpaka yanatia shaka.

Mgalanjuka,

Mie napenda wewe utawaliwe na shaka kwani shaka hupelekea ukamilifu.
Kupata ukamilifu kuondoa shaka yako si wewe tena kurudi kwangu na maswali.

Ni wewe kufanya uchunguzi na ukanikabili mimi na hicho ulichokiona.

Huyu kijana anasema majibu yangu kila mara yanamuongozea kile alichokuwa hajui.
Anasema kwao kuna picha ya Sheikh Hassan bin Amir lakini hakupata kujua kuwa alikuwa na zawiyya nchi nzima ambazo zikunga mkono TANU wakati wa uhuru.

Mwenyewe anasema ziliipa "tough" TANU.
Sina majisifu ila historia ya TANU naijua kushinda yeyote hapa ukumbini.

Kama hiyo ni majisifu bahati mbaya.

Mohamed
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…