Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa


Jee nikipigiwa? hiyo ya "Khatar lakin salama" umenikumbusha wangu Sheikh Nurdin. WaLlahi Unanfurahisha.
 

Ahsante sana mkuu kwa observation yako.

Na mimi nilikuwa nimejiuliza swali hilo hilo baada ya kusoma huo utetezi wa mzee mohamed.

Bila shaka mzee mohamed ameamua kwa makusudi kutengeneza historia ya ''ubaya'' wa Nyerere dhidi ya waislamu kiasi kwamba waislamu waliomuunga mkono Nyerere baada ya ''mfarakano'' hapendi kuwazungumzia.

Kama mzee mohamed ataamua kuwazungumzia na hao pia, basi atakuwa ametutendea haki wasomaji wa historia iliyofichika.
 

Heshima kwako Mag3, ebu simama kwenye hoja mkuu.

Mie ni Mkristo, lakini nikiri kuwa Mohamed Said kaeleza vizuri sana historia ya upande wake na sijaona hapa akiongea kwa dhihaka wala dharau, may be nina definition tofauti ya hayo, mambo mengi aliyoongea humu mie binafsi sikuwahi kuyasikia, tumesikiliza sana historia za upande mmoja kumhusu Nyererea na uhuru wa tanganyika, so ni afya pia kuwafahamu wahusika wengine na upande mwingine wa Nyerere, hili ni muhimu kwa kujua kwa usahihi kule tulipotoka.

Mohamed Saidi yeye ka-base kwa wazee wake wa Gerezani, tusimhukumu kwa kufanya hivyo kwa sababu may be ndio aliko na taarifa za kutosha na za uhakika zaidi, hayo ya mashujaa wengine sasa ni wajibu wako sasa kutuhabarisha ushujaa wao tu kistaarabu tu kwa kuonyesha ustahiki wa mchango wao kwa harakati za kisiasa za wakati ule, na pia kuonyesha ni kwa namna gani basi wazee wa Mohamed said hawastahili ushujaa aliowapa.

Naamini huu ni mjadala muhimu sana, jamii yoyote isiyojua ilipotoka ni jamii mfu, so kujua mabaya kwa mazuri yaliyopita ni muhimu sana kwa taifa lolote.
 

Butola,

Ahsante sana.

Mohamed
 

MM,

Tusende kwenye haki ya Nyerere na Saleh Masasi kutatuvuruga.
Namzungumza Nyerere kwa sababu ana mengi ya kueleza.

Saleh Masasi yeye yake ni hiyo BAKWATA na baada ya hapo
hakusikika tena.

Mohamed
 
mag3 anamsoma mohamed said between the lines na katika small print,Butola kiswahili ni lugha pana sana,though its not open,lakini kwa mawazo ya wengi humu MS anaweka tabaka la wao na sisi,yaani wenyeji na wakuja
 
mag3 anamsoma mohamed said between the lines na katika small print,Butola kiswahili ni lugha pana sana,though its not open,lakini kwa mawazo ya wengi humu MS anaweka tabaka la wao na sisi,yaani wenyeji na wakuja

Dhana na hisia reading between the lines...ningekuwa na fikra kama hizo maisha yangu yangekuwa magumu sana. Sisi ni kitu kimoja lau kama mie kwetu ni Dar es Salaam. Nawajua watu kwao bara lakini hakuna amjuae huko, kazaliwa Muhimbili, kakulia Sinza, kasoma Bunge, Chuo Kikuu Dar es Salaam...hata accent ya kibara hana anazungumza kama mtu wa Dar es Salaam. Utampeleka wapi mtu kama huyu?

Mohamed
 
mag3 anamsoma mohamed said between the lines na katika small print,Butola kiswahili ni lugha pana sana,though its not open,lakini kwa mawazo ya wengi humu MS anaweka tabaka la wao na sisi,yaani wenyeji na wakuja

Wala hakuna "between the lines" yenye maslahi kwa taifa katika hili.

Ebu tuepuke hii mentality ya "wao" na "sisi", tukipenda kuyasikia tu yale yanayotupendeza nafsini mwetu hatutaweza kujifunza, ebu tuwe huru tu kujua kwa uhalisia historia ya nchi yetu na yatokanayo bila kuweka limitations, ni afya kwa nchi.
 
NONDO anazomwaga MS,sio mchezo,tunaweza ku connect dots nyingi tu-tatizo linakuja pale anapotaka kuikamata"audience" kwa ku sacrifice baadhi ya dini na mashujaa ambacho ni kitu hatari sana kwa umoja wa nchi
 
NONDO anazomwaga MS,sio mchezo,tunaweza ku connect dots nyingi tu-tatizo linakuja pale anapotaka kuikamata"audience" kwa ku sacrifice baadhi ya dini na mashujaa ambacho ni kitu hatari sana kwa umoja wa nchi

Huo ni uoga tu unaotokana hasa na sirka ya watu kupenda kuishi kwenye mazoea na kutopenda habari mpya zinazo-challenge yale waliyoyaishi kwa muda mrefu, kama taifa tunapaswa tutoke hapa.

 
NONDO anazomwaga MS,sio mchezo,tunaweza ku connect dots nyingi tu-tatizo linakuja pale anapotaka kuikamata"audience" kwa ku sacrifice baadhi ya dini na mashujaa ambacho ni kitu hatari sana kwa umoja wa nchi

SOA,

Mimi kwa somo hili wala sina wasiwasi tutakesha. Mimi nimeishi ndani ya haya
ninayoandika ingawa nilikuwa mtoto mdogo. Hawa wote mimi nimewaona kwa
macho yangu na wengine wakifika hadi kwetu nyumbani.

Unajua mimi nimeandika habari za wazee wengu na kwa bahati ni Waislam.
Sasa mtu anaposema mbona sikuwataja wazee wake yeye wa Kagera napata shida.
Mimi nitaanzia wapi niwaeleze wazee wa Kagera maana siwajui hata kidogo.

Sasa wewe nawe si andika habari za wazee wako wa Kagera? Kwani umekatazwa?
Namna hiyo ndipo tutakaposonga mbele. Kunitaka mimi niandike habari za wazee wako
ambao mie siwajui ni kunitwisha mzigo nisioweza kuubeba.

Mohamed



Mohamed
 
SOA

Saleh Masasi (Mungu amsamehe) ndiyo waliomsaidia Nyerere kuivunja EAMWS.
Huwa napata tabu sana kuzungumza juu ya hawa watu khasa kwa kuwa wako
mbele ya haki.

Mohamed

Mbona na Nyerere naye yuko mbele ya haki lakini unamzungumza?
 
Mbona na Nyerere naye yuko mbele ya haki lakini unamzungumza?

Hilo swali mbona limeshajibiwa kwenye post #185
MM,

Tusende kwenye haki ya Nyerere na Saleh Masasi kutatuvuruga.
Namzungumza Nyerere kwa sababu ana mengi ya kueleza.

Saleh Masasi yeye yake ni hiyo BAKWATA na baada ya hapo
hakusikika tena.

Mohamed
 
Tatizo lililopo katika historia ya Tanzania ni kwamba, wale ambao tuliwategemea waandike hii historia hawakufanya hivyo matokea yake tumeshindwa kupata historia zuri,sasa sijui walikatazwa au nini walikuwa wanahofia? kwa kweli Napata tabu katika hilo.
Maana historia tunayosoma inaanzia na kuishia kwa Nyerere how come?

Tuchukulie mfano historia ya Yesu katika kitabu kitakatifu cha biblia pamoja na kuwa Yesu ndiye aliye ibuka shujaa wa mwisho, lakini wahusika wote kuanzia Adamu na manabii na mitume wote walitajwa pamoja na michango yao kila mmoja,hata Yuda aliyemsaliti Yesu alitajwa na mwisho wake ulielezewa.

Sasa inakuaje kwa historia ya Tanzania ,Hivi Nyerere kaandika vitabu vingapi?kweli alishindwa kuandika historia ya Tanzania kweli. Au alikuwa anaficha nini?Ni ajabu.

Nazani ni wakati sasa kwa watanzania tuanzishe mjadala huu wa kuandika historia yetu kama ilivyo mjadala wa katiba.
Wandugu nilazima tujuwe mchango wa kila mtu kwani wote hatuwezi play role ya Nyerere lakini tunaweza kuplay role za wengine na kwa play role za wengine tunaweza kutengeneza Nyerere wengine maana nimesikia wengine wakisema mbona Haibuki Nyerere mwingine,tutampataje mwingine wakati waliomtengeneza huwajui ,na njia walizotumia hatuzijui?

Sisi wakristo tunambiwa tuombe kama Paulo na Sila walivyoomba mpaka Milango ya gereza ikafunguka.hivi tungewafahamu vipi wakina Paulo na Sira pamoja mchango wao katika ukombozi wetu sisi wenyewe kama wasingetajwa? pamoja na michango yao?
Na sisi watanzania tunataka tufanye kama vile wale waliokuwa bega kwa bega na Nyerere ili mbinu zile walizotumia tunaweza kuziboresha kwa manufaa ya nchi yetu.

Huyu mtu anayejiita Mohamedi Saidi anastahili pongezi kwa kuonyesha njia,iwe ni starting point kwetu sisi katika mjadala huu.
Ndugu zangu kwa wale wanao fahamu Biblia haikuandikwa na Mtu mmoja imeandikwa na zaidi ya mtu mmoja,kwa maana hiyo basi Mohamed Said ni mojawapo tunaomba wengine wajitikeze ilitupate historia iliyo zuri.

Kwa kumalizia naomba mjadala huu tuujadili kwa upendo na kwa utanzania zaidi tukujua ni kwa manufaa ya nchi yetu na si vingine.

Nawakilisha.
 

Mkuu Butola, kama nilivyosema kutoka mwanzo uwongo ukipewa nafasi ya kurudiwa kurudiwa bila kukemewa kuna hatari kuwa uwongo huo unaweza ukawateka watu wasio makini katika tafakari zao. Na hatari hii ni pale uwongo unaporuhusiwa kugusa hisia za watu na hakuna hisia hatari kama ile inayogusa imani za watu (dini). Ningetaka sana huyu Mohamed Said azingatie hilo lakini kama ilivyo kwa watu wenye hisia kali za kidini ni mara chache wanakuwa tayari kukiri mapungufu yao kirahisi. Mimi nimeambiwa nimemtukana Mohamed Said kwa kumwita mpuuzi lakini ukisoma makala yake nyingi zimejaa kejeli na dhihaka kwa wale wasiokubaliana naye. Hata hivyo tuyaache hayo na tujikite katika hii historia ya taifa letu ambao wapo wanaodai imepotoshwa ili kuwapendelea Wakristo.

The bottom line ni kwamba TANU iliundwa na Raisi wake wa kwanza alikuwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alichaguliwa kwa kura nyingi tu. Mwalimu aliiongoza TANU hadi tunapata uhuru na akawa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika na akaweza kuunda serikali ya kwanza ya Tanganyika huru. Huu hata ukimtukana vipi Mwalimu hauwezi kufutika - Raisi wa kwanza wa nchi hii aliyewaongoza Watanganyika, Waislaam kwa Wakristo na Wapagani, katika mapambano dhidi ya mkoloni ni moja tu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, period.

Kuna vyama vilijitokeza kitaifa kupambana na TANU kabla ya uhuru vikubwa vikiwa viwili:
  • TANC - Tanganyika African National Congress kilichoanzishwa na Zuberi Mtemvu baada ya kutofautiana na Mwalimu kuhusu dira ya baadaye ya taifa la Tanganyika. TANC ambayo ilionyesha tangu awali kabisa kuwa ilianzishwa kwa misingi wa ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa uzawa. Zuberi Mtemvu pamoja na wafuasi aliamini kabisa kwamba TANC ingewateka Waislaam na kukihama chama cha TANU. Hii haikuwezekana na Mohamed Said hili hawezi kulizungumzia kwa sababu inayoeleweka kabisa kuwa Waislaam walio wengi walikuwa bega kwa bega na Mwalimu Nyerere na walimwamini.
  • AMNUT - All Muslim National Union Of Tanganyika kilichoanzishwa na Said Mohamed Chamwenyewe na kama jina linavyosomeka chama hiki kilitawaliwa na ubaguzi wa kidini. AMNUT haikuweza kuitikisa TANU chini ya Mwalimu Nyerere na sana sana ilipata wanachama kutoka TANC ya Zuberi Mtemvu. Hii ya AMNUT ni lingine kati ya mambo ambayo Mohamed Said hawezi kuligusia kabisaa kwa sababu ambazo hata kipofu anaweza kuziona.
Kabla sijaendelea nawaomba wana JF mpitie hivi vipande vifuatavyo, myasome kwa umakini muweze kujua angalau kwa kifupi tu EAMWS East African Moslem Welfare Society anayodai Mohamed Said kwamba ilivunjwa na Mwalimu Nyerere ilikuwa ni nini hasa na ilianzishwa na nani halafu -


Aliyeandika haya anaitwa Ulrich Lohrmann.

- baadaye tutaendelea............
 

Attachments

  • historia1.jpg
    313.2 KB · Views: 69
Yani wewe unatapatapa na historia ya wazee wa gerezani dsm, unafinyangafinyanga tu hata hueleweki.

Wazee wako waliokuwa wakivaa kanzu na misuli walipata wapi ujasiri wa kumfundisha Nyerere kuvaa suruali ambayo wao wenyewe hawaivai?
tena msuli na kanzu bila chupi na hii ni mpaka leo haswa wale wazee wa mabusha pwani!
 

Ukimshutumu mtu kuwa muongo inapaswa utuoneshe ni wapi aliposema ama kuandika uongo, kisha tuendelee kwingine.

Sisi tunakuona wewe ni muongo kwa sababu kwanza hata jina unalotumia hapa ni la uongo na si lako la kupewa na wazee wako. Mohamed Said kaja kama yeye, hutaki hata kutuambia wewe ni nani? umeandika historia ipi? paper ipi? wapi? haya ni maswali ambayo nimekuuliza huko nyuma lakini umeyafumbia macho.

Hakuna ulichotuambia kuwa hiki hapa ndio uongo wenyewe na ukweli ndio huu. Tunaona unakuja na kurukia mara huku mara kule, sijui someni hapa EAMWS imeanzishwa na nani imekuwa vipi. Tueleze kuhusu aliyoyaandika Mohamed Said na uongo wake ni upi? Na utueleze ukweli wako ni upi?

Katika mada anayoibandika Mohamed Said hivi sasa sijaona palipotajwa hiyo EAMWS au wewe unasoma kwingine? kama unasoma kwingine tuoneshe ni wapi ili twende sambamba, sisi tunasoma hiki hapa alichobandika Mohamed Said na mpaka sasa tunaona anawataja wazee wa Dar na "role" walizokuwa nazo na walipoishi, sasa kuna uongo gani hapo? tuelezee huo uongo wacha kupoteza mjadala kwa chuki binafsi, kauli zako zinaonesha umeudhika sana na haya anayoyaandika Mohamed Said na unakuja hapa na kutowa shutuma na kuleta matusi, huo si uungwana wala sio usomi, kama kweli ungalikuwa ni msomi usingejificha na ungejibainisha hapa kinaga ubaga kama alivyofanya Mohamed Said.

Soma hapa tunayoyasoma sisi halafu ujibu: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...50-ya-uhuru-wa-tanganyika-36.html#post2684914
 

Huwezi ukatuambia "TANU iliundwa" halafu ukarukia "na Rais wake".... Tuelezee imeundwa na nani na vipi? TANU ni chama na kama ni chama si mali ya mtu mmoja. Mbona huelezei hao walioamuwa kukiunda chama kinachoitwa TANU kina nani? Tuwekee wewe ujuavyo halafu tutazame na Mohamed Said alivyoelezea halafu sisi tuamuwe nani ni muongo.

Mohamed Said kaanza hivi:

 
Bibie,
Mbona wewe wajiita Faizafoxy? Ama hilo ndilo jina walilokupachika wazazi wako? Umekisoma kitabu cha Mohammed "Life and Times of Abdulwahid Kleist Sykes?" Humo anazungumzia EAMWS Kwa hiyo Mag3 hajaidaka hiyo mada ya EAMWS kutoka hewani. Na kila mara Mohammed anapoulizwa swali ana kutajia usome kitabu chake. Kakisome na wewe pia.
 
Umenena FF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…