FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Kigarama,
Sijakataa kueleza kwa nini Nyerere alipewa kadi na. 1. Wewe hujanijua? Sipigiwi nacheza leo mganda unaniletea uwanjani kwangu si itakuwa hatari ingawa salama!:
"Ally Sykes ndiye aliyechora kadi ya TANUna kuchagua rangi na nembo yake. Rangi alizochagua zilikuwa, nyeusi kuwakilishataifa la Kiafrika na kijani ardhi ya Tanganyika. Mfano wa kadi ya TANUulitokana na kadi yake ya Tanganyika Legion. Baada ya kumaliza kuichora ilekadi, aliwaendea Tanganyika Standard Newspapers ili wamchapishie. Kutokamfukoni mwake mwenyewe alichapisha kadi 1000 za kwanza na akitumia fedha zaTAGSA alichapisha kadi nyingine 2000. Kadi nambari 1 ilitolewa na Ally Sykeskwa rais wa TANU, Julius Kambarage Nyerere na Ally aliweka sahihi yake kamaafisa aliyeitoa. Ilipendekezwa kwamba kadi chache za mwanzo lazima zipigwemnada na fedha zitakazokusanywa zitiwe kwenye hazina ya chama. Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz, Rupia na wenginewalipanda dau kununua kadi hizo. Ally alimshinda kaka yake Abdulwahid kwa beiakapata kadi ya TANU nambari 2; Abdulwahid alipewa kadi nambari 3; Dossa Azizkadi nambari 4; Phombeah kadi nambari 5; Dome Okochi, mmoja wa wale wazalendokutoka Kenya katika TANU alipata kadi nambari 6 na Rupia kadi nambari 7. BibiTiti kadi nambari 16; Iddi Tosiri kadi nambari 25."
Mimi nikijuana na Dome Okochi Budohi. Katika kitabu kuna picha yangu na yeye tumepiga nyumbani kwake Nairobi, Ruiru mwaka 1972. Huyu kasi yake ni na 6. Nimepata mengi sana kuhusu siku za awali za TANU. Yeye alikamatwa baada ya "Operation Anvil" iliyowakumba Wakenya wote Afrika Mashariki waliotuhumiwa kuwa na Mau Mau na akarudishwa Kenya akafungwa Lamu. Baada ya uhuru alitolewa na akafanya kazi katika gazeti la Argus Uganda. Kwa masikitiko sana anasema alijitahidi sana kukuonana na Nyerere kila akija Nairobi kwa kumtumia ujumbe na kuomba wakutane. Kumbuka hawa wote walikuwa wanachama wa mwanzo wa TANU, wanaharakati lakini Nyerere alikataa kuonananae. Hivi ni katika vitu vilivyokuwa vikinishangaza wakati naandika kitabu cha Nyerere kujiweka mbali na watu alioanzanao harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.
Yako mengi taratibu tutaeleweshana Insha Allah.
Mohamed
Jee nikipigiwa? hiyo ya "Khatar lakin salama" umenikumbusha wangu Sheikh Nurdin. WaLlahi Unanfurahisha.





