Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Ukisikia kitu kinaitwa inferiority complex ndicho hiki. Wanasaikolojia wanasema dalili za inferiority complex ni mtu kuwa 'too sensitive and reactive'.
Unapokwenda baa wewe musilam unategemea nini?
Nyerere akisema haya '........mumejenga soko kubwa sana, ninachowaomba nguruwe ni marufuku msijenigombanisha na waswahili wangu'.
Sijui hapa anawakejeli au ana waheshimu.
Mbona kila jambo linalohusu majigambo ni la wahaya na wao huwasikii wakisema wanadhalilika hata siku moja. Mbona kuna utani wa wapemba akina nchuzi na nkate na huwasikii wakilalamika. Wala wanapoitwa 'duka la mpemba huwasikii wakisema wamedhalilika, sasa hili la waswahili unalifanyaje kuwa la waislam.
Alichosema mama Makinda ni msemo kama ule ''wewe wa kuja tu' hujui kula chapati n.k. Tena hapo kariakoo utasikia watu wakisema 'hiri ri jitu nitariweka ndani' wakimaanisha wakurya, hatujasikia polisi au wakurya wakisema wanadhalililka.
Unapomwambia mtu bahili kama mpare au mwizi kama mchaga hutasikii wakilalamika. Hawa wa kariakoo si kuwa wanatukanwa ni matokeo ya inferiority complex. Mohamed anajisifia kuwa yeye ni mswahili wa kariakoo( je nivute uzi wa kumnukuu)
? Mama Nkya ni mtu makini sana na nashukuru hakujishugulisha na ujinga kama huo. Tatizo la Watanzania si dini kama mnavyotaka lionekane ni umasikini na kutelekezwa kwa raia, wizi kama wa richmond n.k. Sio hijabu ya mtu kichwani kwasababu anaweza kuwa anayo kichwani kwake lakini je inamsaidiaje yule mtanzania masikini kabisa.
Hawa walio graduate wasikusumbue maana tayari wana taa mkononi, jishughulishe na ile shule ya Kilwa iliyofungwa kwa kukosa wanafunzi halafu angalia Kilwa wakazi ni watu wa aina gani.
Huko walikoendelea si serikali iliyohamasisha ni watu waliohamasika ikiwemo sehemu moja yenye waislam ambao walikuwa nyuma ya miaka 50 tangu ukristo uingie hapo, lakini sasa ngoma droo. Walihamasika hawakushikiwa kiboko au kengele. Jukumu la kuhamasisha ni langu mimi na wewe yule na wale na sisi sote, kwa bahati mbaya wewe umeamua kuunga mkono jitihada za Mohamed kuwadanganya waislam kuwa ufaulu wao unategemea namba za mitihani na kwa vile Malima amefariki basi wao wajikusanye kulalamika, na kwamba hata wafanye nini hawatafanikiwa kwasababu ya mfumokristo.
Njia nyepesi ni kuwahamasisha kushika majambia na si kusimamia fikra na maarifa. Wakati wengine wakijenga vinu vya umeme Mohamed anahimiza chuki na kutunga hadithi kwa kutumia majina ya waislam kana kwamba bila majina uislam hausimami.
Wakati shule na vyuo vikidorora Mohamed yupo bize aksimulia chuo kikuu cha EAMWS miaka 40+ iliyopita. Anasomesha historia ya wazee wake wa Gerezani katika mashule kama anavyodai, si nini cha kufanya kukabliana na Mchina, Mjapan au Mbrazili.
Nguruvi3,
Umeandika mengi nitakujibu moja tu kuhusu EAMWS.
Historia ya uhuru wa Tanganyika na mchango wa Waislam katika vita ile isingeleta maana kamili bila ya kisa cha EAMWS.
Katika mkasa ule ndipo mkono wa Nyerere na Kanisa ulipojititokeza kupiga vita Uislam.
Sasa vitabu vilivyokuja baadae vya Bergen na Sivalon vilikuja kuthibitisha tu.
Umuhimu wa historia hii ni kuwa unaeleza upande wa pili wa Nyerere ulomtoa raha Prof. Haroub Othman na wasomi wengi duniani kwa kuonyesha kile ambacho hawakuwa wakikijua.
Baada ya pale sasa huku kote tunakopita sasa msingi wake ni ile historia ya uhuru na njama dhidi ya Uislam.
Mohamed
