punainen-red
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 1,731
- 451
Mzee MS, mimi si mwandishi lkn kuna kitu kinanitatiza, wengi tunasoma tu kila post ktk mjadala huu, ukirudi ktk page ya 123 kuna post umeirudia nadhani mara tano au zaidi!! sijui kiuandishi inamaanisha nini... Lakini nadhani utakuwa umewasaidia wasomaji wengi kama utafuta post ulizorudirudia kama hizo. Asante!
Khaaa! hapa lugha gongana! Kuna mheshimiwa mwingine
Mgalanjuka,
Kwa adabu za kikwetu mtu yeyote mwenye umri sawa na baba yako unamwita "baba" hali kadhalika mwanamke yeyote umri wa mama yako unamwita "mama."
Hakuna jina jingine nje ya hapo.
Na inapokuwa kati ya hao ni rafiki ya baba au mama yako ile heshima ya ubaba na mama huwa juu zaidi.
Huwa hawana jina lingine nje ya hayo.
Utamwita "baba" au "mama."
Hizi ndizo mila, desturi na heshima za watu wa pwani.
Mohamed
Asante mzee, ila nadhani hujanielewa, ukipata mda rudi kwenye hiyo page niliyokupa uone. Ni sawa na hii uliyonijibu sasa hivi ungei-post mfululizo mara tano au zaidi.Punainen,
Huwa nazirudia kwa kuwa maswali yanajirudia.
Hizo post wako wengine hawajaziona hivyo nikizifuta nitakuwa nimewakosesha.
Mohamed
Mohamed,
Hardwood,
Historia yetu imeanza mbali sana na haikuwa kazi nyepesi.
Tulianza kupambana na Nyerere toka miaka ya 1970.
Sasa unatusikia hadhir kwa kuwa Waislam wameamka wanadai haki zao.
Mauaji ya Rwanda tafuta chanzo chake.
Haikuwa kwa serikali kukaa kimya.
Chanzo ni jamii moja kujiona bora.
Serikali hii iko kimya kwa kuwa imepwelewa.
Wanaujua ukweli ila hawana bado ujasiri wa kufanya mazungumzo ya kuondoa dhulma.
Wanategemea labda tatizo hili litajiondosha lenyewe.
Mohamed
Mohamed,
Mauaji ya Rwanda yaliasisiwa na kulelewa na serikali ya Wahutu. Serikali ilikaa kimya kwa sababu yenyewe ndiyo iliyokuwa inatekeleza mauaji dhidi ya Watutsi. Anachosema Hardwood ni kwamba mahubiri yako yanawachochea Waislamu wawaone Wakristo kuwa ndio maadui wao. Waislamu wanakabiliwa na maadui wanaowakabili Watanzani wote kwa ujumla ambao ni ujinga, maradhi, na ufukara.
Tunaweza kuamua kupambana nayo kwa pamoja au tunaweza kuamua kujitenga kila mtu na lake huku kundi moja likinyooshea kidole kundi jingine kuwa ndio adui wao.
Nanren,
Kumwita Nyerere baba wa taifa kama kweli alistahikhi swifa hiyo hakuna shida lakini kama hakustahikhi bali wale aliowafadhili kwa aina moja au nyingine ndio waliopenda aitwe hivyo kwa kuwa wapo kwenyye power ni makosa makubwa sana.
Hata mtu akiwa dikteta lazima kuna watu wake aliwabeba na kuwatazama kwa namna moja au nyingine wakimzunguka na kumsifia katika utawala wake kuwa anafanya mema. Na watu hao hata siku moja hawatathubutu kuona mtawala yule dikteta anaondolewa madarakani na hata kama ataamua kuachia madaraka hao hao watu wake watataka azidi kupewa hishima za kutukuka na kukumbukwa.
Nikirudi kwa Nyerere na uhuru wa tanganyika. Hapa cha msingi ni kuwa Tanganyika walipewa uhuru wao ofisini sio kwa mapambano au kuigania kwa vita kama nchi nyingi nyingine ambapo viongozi majemadari wa vita vile ndio waliokuwa viongozi wa kwanza mara baada kumshinda na kumng'oa mkoloni. Kwa tanganyika hakukuwa na rabsha zozote zile.
Nyerere anajulikana fika alikuwa mwl pale Pugu Secondary tena mwl wa kawaida na mwenye kipato cha kawaida sana. Tunakubaliana wazi kuwa yeye sio muasisi wa vuguvugu la uhuru wa Tanganyika. Tukumbuke kuwa kulikuwa na TAA na vyama vingine vya siasa ambavyo vilikuwapo wakti huo na vyote vilikuwa na maofisi yao.
Sasa tuwaangalie hawa wafadhili wa hivi vyama hata TANU, nani alitoa nyumba yake kuwa ofisi ya Tanu? Nani alitoa nyumba yake kuja kukaa Nyerere pale alipoacha kazi na kuhamia Dar es salaam? Nani alihakikisha anapata fedha na mahitaji yake ya kila siku nyumbani kwake na familia yake? Na alihakikisha wanapata fedha na wale waliojitolea fedha zao kuhakikisha Nyerere anakwenda UNO kudai uhuru?
Kumbuka lazima kulikuwa na watu waliojitolea kwa hali na mali kuhakikisha Nyerere anakwenda kudai uhuru na kuisha salama kabisa mpaka ukapatikana uhuru.
Je watu hao waliojitolea mali zao wamepewa hishma gani? Kwanini hishma apewe pekee mfadhiliwa na mfadhili asipewe hishma hiyo? naomba jibu lako hapo.
Mohamed,
Mauaji ya Rwanda yaliasisiwa na kulelewa na serikali ya Wahutu. Serikali ilikaa kimya kwa sababu yenyewe ndiyo iliyokuwa inatekeleza mauaji dhidi ya Watutsi. Anachosema Hardwood ni kwamba mahubiri yako yanawachochea Waislamu wawaone Wakristo kuwa ndio maadui wao. Waislamu wanakabiliwa na maadui wanaowakabili Watanzani wote kwa ujumla ambao ni ujinga, maradhi, na ufukara.
Tunaweza kuamua kupambana nayo kwa pamoja au tunaweza kuamua kujitenga kila mtu na lake huku kundi moja likinyooshea kidole kundi jingine kuwa ndio adui wao.
Nikuulize kidogo??
Wewe unawachukia waislamu?? je uko tayari kupambana nao??
What makes you think kwamba waislamu wanawachukia wakristo?? na wakristo ni maadui zao???
Waislamu wana tatizo na serikali inatakiwa kutoa majibu???
Matagemeo yetu si wewe jasusi (Mkristo utoe majibu kwa niaba ya serikali) bali ungekuwa muungwana na unawapenda waislamu ungeshirikiana nao kuona ukweli wa mambo na dhulma wanazosema??
[TABLE="class: cke_editor"]Mohamed Said anajaribu kutuambia hivyo. Au wewe humsomi?
Mgalanjuka,
Hebu tupate darsa kidogo:
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="width: 744, bgcolor: transparent"] "Christianity is a relatively a new religion in Tanzania, having been introduced into the country during the eighteenth century by professional missionaries. The Church and the African Christian are a phenomenon of colonialism. Having this common factor the behaviour of the Church in the history of all Africa is that of loyalty and cooperation to the colonising authority. The Church gradually managed to create a special relationship between the colonial government and the educated African Christian whom it had trained in its mission schools. The African Christian therefore became a beneficiary of the colonial system. Muslims suffered as a people whose faith was antagonistic to that of the coloniser. The African Christian on the other hand was loyal to the colonial government in pre-independence Tanganyika and came to control the government in post-independence Tanzania. [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 744, bgcolor: transparent"] Muslims suffered as colonised subjects singled out for discrimination by being denied education opportunities, curtailing any chances for self-advancement. The survival of Muslims as a people and Islam as a religion therefore lay in the total overthrow of the colonial state. The Church maintained its pre-independence position by courting the new government. This alliance between the Church and government, built by Church conformity to the political systems and nurtured by government cooperation, served Christianity well. The Church managed to create for itself an environment conducive to operating without any suspicion or hindrance from the government. From this special relationship, over time the Church devised for itself a powerful base out of the African Christian it had trained in its mission schools. The Church used this special relationship with the colonial and later with independence government to build for itself a domain in which its followers came to control almost all the important positions in the executive, the legislature and the judiciary in free Tanzania. In its mere hundred years, theChurch managed to create its own hierarchy to control and permeate every sector of Tanzanian society. [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 744, bgcolor: transparent"] [h=6]When the British took over Tanganyika (as Tanzania was then known) from the Germans after the First Word War, by then the Germans had done more than their fair share in opening up Tanganyika for Christian influencthrough various Christian establishments. Tanganyika was divided among different Christian organisations originating from various European countries. The Catholic Church, which is the most influential, was already established in Tanganyika. White Fathers were in Tabora, Karema, Kigoma, Mbeya, Mwanza and Bukoba; Holy Ghost Fathers-in Morogoro and Kilimanjaro; Benedictine Fathers in Peramiho and Ndanda; Capuchin Fathers-in Dar es Salaam; Consolata Fathers-in Iringa and in Meru; Passionist Fathers-in Dodoma; Pallotine Fathers-in Mbulu; Maryknoll Fathers-in Musoma; and Rosmillian Fathers-in Iringa.[1] For more than a hundred years the Church concentrated its effort in moulding citizens, most of them African Christians, who would be loyal to both the Church and State. It is through the mission-trained bureaucrats that the Church indirectly controls and influence decisions in the government and ruling party, the CCM, with Muslims and Islam increasingly made irrelevant.[/h] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 744, bgcolor: transparent"] [h=6]By the mid-1960s the Church in Tanzania became a multi-million dollar charity institution with donors and well-wishers from all over the Christian World. It now owns its own hospitals, fleet of small private planes, air strips, printing presses and publishing houses, radio stations and newspapers. The Church was and still is so influential and pervasive, that at times government and party bureaucrats, particularly Christians, are at loss to distinguish where their allegiance and loyalty lies. Is it with the government or with the Church? It is this confusion in loyalty and church-state relations which helped to create mistrust between Muslims and the government soon after independence. The government was perceived by Muslims as a Church institution where Muslims were outsiders and mere spectators. Soon after independence the Church redefined its role vis-à-vis the new state. During colonial rule the Church maintained an image of seeming to respect the line of demarcation between religion and politics. Church-state confrontation was unheard of." [/h] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
https://www.jamiiforums.com/#_ftnref1 [1]See KiongoziNo. 6, June 1950. For more information on missionary penetration in East Africa, see M. Langley& T. Kiggins: A Serving People, Oxford University Press, Nairobi, 1974, p. 19.
Kama serikali inawadhulum kwa nini utaje Ukristo? Acha siasa, unazunguka-zunguka kama pia.
Mohamed Said anajaribu kutuambia hivyo. Au wewe humsomi?
Kama serikali inawadhulum kwa nini utaje Ukristo? Acha siasa, unazunguka-zunguka kama pia.
Ndiyo anastahili, Sifa za huyu mzee ziko wazi, waulize hata watoto wa chekechea watakuambia hilo
As long as Nyerere hakuwa Dikteta, unachosema wewe kinamhusu Idd Amin, Saddam Hussein,Hitler, Mobutu and the alike. Nyerere hana sifa hizo.
Gandhi ni baba wa taifa wa India, unajua jinsi gani alivyoendesha harakati za uhuru...Non-violent
Ndio maana alisisitiza kuitwa mwalimu na si Dr. Dr. By the way, ulitaka awe na billions ngapi na Bungalows ngapi ili umwone muhimu katika harakati za uhuru?
[/FONT]
Unataka tumwite Sabodo baba wa Chadema? Au Rostam Aziz baba wa CCM? hawa hawatoi Nyumba bali mabilioni.
Hata baada ya Uhuru hukuwahi kusikia Nyerere alijengewa Nyumba na JKT? Babu yangu aliuza shamba kuchangia TANU lakini sidhani kama anastahili kupewa "hishma" ya ubaba wa taifa kwa kuuza shamba lake.
Oww! kumbe walikuwa wanapanda ili wavune? Heshima gani unataka apewe mfadhili? Aitwe baba wa Taifa kwa kutoa Nyumba na mali? Mali, mali, mali!! we ni fisadi?
Mohamed,
Mauaji ya Rwanda yaliasisiwa na kulelewa na serikali ya Wahutu. Serikali ilikaa kimya kwa sababu yenyewe ndiyo iliyokuwa inatekeleza mauaji dhidi ya Watutsi. Anachosema Hardwood ni kwamba mahubiri yako yanawachochea Waislamu wawaone Wakristo kuwa ndio maadui wao. Waislamu wanakabiliwa na maadui wanaowakabili Watanzani wote kwa ujumla ambao ni ujinga, maradhi, na ufukara.
Tunaweza kuamua kupambana nayo kwa pamoja au tunaweza kuamua kujitenga kila mtu na lake huku kundi moja likinyooshea kidole kundi jingine kuwa ndio adui wao.
Mhhh...ntarudi baadaye!Jasusi,
Waislamu ndio wanakabiliwa na maadui wa jamii nao ni ujinga, maradhi na ufukara but vile vile wanakabiliwa na mfumo kristo unaowakandamiza kila kukicha.
Mimi namsoma na kumuelewa inawezekana wewe unamsoma lakini hutaki kumuelewa??
Kwanini unataja ukristo?? yes kwasababu viongozi wa kikristo wanaofanya kazi serikalini akiwemo nyerere wanaisaidia kanisa (kwa kutumia nafasi zao) badala ya kusaidia taifa ..hilo ndilo swala ukristo linapokuja kwenye maandishi..
Hakuna anayezunguka kama pia..wewe ndio unaitetea serikali kwasababu inakupendelea wewe mkristo kuna lingine???
Mkuu Mgalanjuka usihangaike na hawa wapuuzi kama Barubaru, huyu alishaikana Tanzania akapata hifadhi hukooo.. walikotoka masultani na bado wana hii ndoto kuwa kuna siku Usultani utarudi. Lengo lao kubwa ni kujaribu kuivunja misingi aliyoijenga Mwalimu, kazi ambayo mimi nimewaapia kuwa hawataiweza kamwe kwani misingi hiyo haikujengwa kwa matope bali kwa zege na chuma. Waacheni watu kama Barubaru waendelee na ndoto zao za mchana.
Kuijenga, kuieneza na kuiendesha TANU kulihitaji hela na hiyo hela ilitokana na michango ya wanachama mbalimbali Tanganyika nzima na walifanya hivyo kutokana na imani yao kwa Raisi wa TANU ambaye hakuwa mwingine bali Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Nikitoa mfano mdogo tu mwaka 1958 kati ya shilingi 1,575,981/= zilizofika makao makuu ya TANU, zaidi ya nusu zilitoka Jimbo la Ziwa (shilingi 590,408/= kati ya hizo zikitoka Sukumaland !)
Hiyo ina maana kuwa nusu iliyobakia ndiyo ilichangwa na majimbo saba yaliyobaki ! Jimbo lililofuatia ni Jimbo la Kaskazini likifuatiwa na jimbo la Nyanda za Juu kusini. Kwenye hii listi Jimbo la Mashariki (Pwani) sidhani hata kama ilishika namba halafu eti leo Wazee wa Gerezani wakumbukwe kwa michango ya kitoweo au kitanda cha kulalia, mbona Mwalimu aliishawapa ahsante ? Kwangu hizi ni soga tu za kuwasimulia wajukuu na hazihitaji kuandikwa kama historia.

Ahh! Hivi kiongozi wa serikali ya Tanzania ni nani vile? makamu wake? Ebo! Sasa si serikali tena bali "viongozi wa kikristo wanaofanya kazi serikalini". Take that slap on your face.
Mgalanjuka said:Ahh! Hivi kiongozi wa serikali ya Tanzania ni nani vile? makamu wake? Ebo! Sasa si serikali tena bali "viongozi wa kikristo wanaofanya kazi serikalini". Take that slap on your face.
Mgalanjuka, mambo yenyewe yako hivi - Wanaotumikia mfumoKristo Tanzania ni hawa;
Na wengine wengi tu............
- Raisi wa Jamhuri ya Tanzania - Al Haj Kanali Dr. Jakaya Mrisho Kikwete
- Makamu Raisi - Dr. Mohamed Gharib Bilal
- Raisi wa Zanzibar - Dr. Ali Mohamed Shein
- Makamu wa kwanza - Maalim Seif Sharif Hamad
- Makamu wa pili - Seif Ali Iddi
- Waziri wa Fedha - Mustafa Mkulo.
- Waziri wa Elimu - Dr. Shukuru Kawambwa
- Waziri wa Ulinzi - Dr. Hussein Mwinyi
- Waziri wa Mambo ya Ndani - Shamsi Vuai Nahidha
- Mkuu wa Polisi (IGP) - Said Mwema
- Mkuu wa Usalama (TISS) - Rashid Othman
- Jaji Mkuu - Mohamed Chande Othman
- Jaji Kiongozi - Fakihi Jundu