Barubaru,
Nilipoingia humu JF fikra yangu ni mnakasha kama tulivyozoea mnabishana hadi muadhin ndiyo anaamua mnaacha ubishi mnakimbilia msikitini.
Hakunipitikia kama kutakuwa na watu wenye hasira, hamaki na kutukana...
Insha Allah tuendelee na darsa:
"Nyerere alifahamu fika kuwa haitakuwa rahisikwake kumweka Sheikh Hassan bin Amir kizuizini kama alivyofanya kwa Waislamwengine. Sheikh Hassan bin Amir alikuwa ndiyo Mufti wa Tanganyika na Zanzibarna kwa ajili hii alikuwa na hadhi kubwa katika umma wa Waislam. Halikadhalika haikuwarahisi kwa yoyote kumkiuka Sheikh Hassan bin Amir na kuchukua uongozi waWaislam. Mkutano wa Taifa wa Waislam, 1968Hadi kufikia juma la kwanza la mwezi wa Desemba,mikoa mitatu kati ya kumi na saba ilikuwa tayari imeshajitenga kutoka EAMWS.Kile kikundi cha Adam Nasibu kikaunda kamati kwa ushirikiano na Kamati yaMaulidi ya Dar es Salaam, Adam Nasib akiwa katibu na Sheikh Abdallah Chaurembomwenyekiti. Kamati hii ikaitisha mkutano Ukumbi wa Arnatouglo tarehe 3 Desemba,1968 kujadilia ëmgogoroí. Aliyetumiwa kutoa tangazo lile alikuwa katibu waKamati ya Maulidi na Swala ya Iddi, Y. Osman. Kundi la Adam Nasib lilikuwa namchanganyiko wa watu waliokuwa wanaungwa mkono na serikali Adam Nasib akiwakiongozi, halikadhalika kulikuwa na Waislam waliokuwa na nafasi katika TANUkama Sheikh Abdallah Chaurembo na Juma Sued kiongozi wa TANU kutoka Bukoba.Ilikuwa wazi kuwa serikali ilikuwa inamtayarisha Sheikh Abdallah Chaurembokuchukua nafasi ya mwalimu wake na mtu aliyemfikisha pale alipo, Sheikh Hassanbin Amir. Ikawa sasa lazima Sheikh Hassan bin Amir aondolewe na kupelekwaZanzibar ili lile kundi la serikali chini ya Adam Nasibu liweze kuchukuauongozi wa Waislam bila ya kipingamizi chochote.Wakati wa vurugu hizi Kamati Kuu ya TANU ilikuwainafanya kikao chake Tanga. Sheikh Kassim Juma, [1] Adam Nasibu, Omari Muhaji,Sheikh Abdallah Chaurembo na Saleh Masasi [1] walipanda ndege hadi Tangakwenda kushauriana na Kamati Kuu ya TANU jinsi ya kumaliza ëmgogoroí waWaislam. Ujumbe huu ulikwenda Tangakuonana na Nyerere huku ukiwa na orodha ya Waislam ambao kile kikundi cha AdamNasibu walikuwa wanataka serikali wakamatwe na kutiwa kizuizini ili msuguanoupate kumalizika. Dossa Aziz aliona Nyerere akipewa karatasi wakati kikaokikiendelea lakini hakufahamu ujumbe uliokuwamo ndani ya karatasi ile hadi hapobaadae. Alikuja kutambua habari za karatasi ile baada ya majuma mawili kupitawakati alipofatwa na jamaa yake mmoja na kumuomba aingilie kati ili rafiki yakealiyetiwa kizuizini na Nyerere aachiwe kutoka Jela ya Ukonga. Nyererealipofahamishwa habari zile na Dossa, alisema kuwa yeye hakufahamu kuwa rafikiyake Dossa alikuwa katika orodha ile ambayo kwa umuhimu wa jambo lile ilibidialetewe Tanga wakati wa mkutano wa Kamati Kuu. Kwa kejeli Nyerere akamwambiaDossa kuwa yeye huwa hachukuwi tabu ya kusoma majina ya watu anaowawekakizuizini kwa kuwa anawaamini wale wanaofanya kazi ya kumletea majina yale.Inspekta Jenerali wa Polisi, Hamza Aziz, mdogowake Dossa alipopokea amri kutoka kwa rais kupitia Waziri wa Mambo ya Ndanikuwa amkamate Sheikh Hassan bin Amir, hakuweza kuamini masikio yake. Alitakaafahamishwe sababu za kutaka kukamatwa Mufti ñ kiongozi wa juu kabisa katikasafu ya uongozi wa Waislam katika Tanzania. Alipoambiwa kuwa sababu ni kuwaanaihujumu serikali, Hamza Aziz alimwambia Waziri wa Mambo ya Ndani kuwa huendakuna makosa katika amri ile. Alimfahamisha waziri kuwa yeye binafsi alikuwaanamfahamu mzee yule toka yeye Hamza alipokuwa mtoto mdogo. Akimfahamu SheikhHassan bin Amir kama mwalimu na mtu aliyeshiriki katika ukombozi waTanganyika. Msimamo wake heshima nahadhi yake mbele ya Waislam ipo juu kabisa. Inspekta Jenerali wa Polisialimwambia waziri kuwa haitawezekana kwake yeye kutii amri ile kwa sababu yeyehaamini kuwa tuhuma zile dhidi ya Mufti Sheikh Hassan bin Amir ni za kweli.Nyerere alifahamishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani kuwa Inspekta Generali waPolisi, Hamza Aziz amekataa kutii amri yake ya kumkamata Mufti. Nyerere alitoaamri kwa Usalama wa Taifa kumkamata Sheikh Hassan bin Amir. Hii ilikuwa nikinyume na utaratibu kwa kuwa Usalama wa Taifa hawana mamlaka ya kukamata watu.Usiku wa manane siku hiyo hiyo Sheikh Hassan binAmir alikamatwa na makachero wa Usalama wa Taifa akapelekwa uwanja wa ndege nakurudishwa Zanzibar. [1]Inaelekea kulikuwa na mpango uliokuwa umetayarishwa kabla ya serikali yaMapinduzi Zanzibar kumpokea Sheikh Hassan bin Amir. Inasemekana mara kadhaaKarume alipata kumueleza Sheikh Hassan bin Amir kuwa Nyerere alikuwa hamtakinchini kwake na akawa anamshauri arudi nyumbani Zanzibar. Sheikh Hassanalikataa ushauri ule hadi alipokamatwa na kurudishwa kwa nguvu. Karume alimpaSheikh Hassan bin Amir hadhi zote alizostahili kama ulamaa na akamruhusukuendesha madras. Lakini Zanzibar ilikuwa imebadilika.Mapinduzi ya mwaka 1964yalikuwa yameingiza katika Zanzibar fikra potofu zilizokuwa zinapinga Uislam.Karume mwenyewe alikuwa ametoa amri ya kuchoma vitabu vyote vya dini. Nakala zaQurían Tukufu zilichomwa moto pamoja na taka za mji. Muslim Academy chuokilichokuwa kikisomesha masomo ya dini kilifungwa. Mashine za kuchapa kwa lughaya Kiarabu zikatupwa kutoka Government Press. [1] Maulama wengi na wanafunziwa Sheikh Hassan bin Amir walikuwa wamekimbia Zanzibar kwenda kuishiuhamishoni. Zanzibar haikuwa tena kitovu cha elimu na maarifa ya Kiislam.Sheikh Hassan bin Amir akawa sasa mfungwa katika nchi yake mwenyewe kwa kuwahakuwa na ruhusa ya kuondoka visiwani hapo na kurejea Tanzania bara. Mara baadaya kukamatwa kwa Sheikh Hassan bin Amir, Adam Nasibu akatangaza kufanyika kwamkutano ambao ulikuja kujulikana kama Mkutano wa Waislam wa Taifa. Mkutanoambao ilitangazwa utafanyika Iringa kuanzia tarehe 12-15 Desemba, 1968. Agendakuu ya mkutano ule ilikuwa kujadili katiba kwa ajili ya jumuiya mpya yaWaislam.Baada ya kukamatwa kwa Sheikh Hassan Bin AmirTewa Said Tewa gazeti moja la Kiingerezalilimfuata ili afanye mazungumzo nalo.Tewa alimfahamisha mwandishi kuwa kulikuwa na hofu juu ya maendeleoyanayofanywa na Waislam na mikutano mikubwa ya Waislam iliyokuwa ikifanyikanchi nzima.[1]Waislam waliokuwa na vyeo katika serikali walikataa kabisa kuisaidia Tume ya Kikwima kwa njia yeyotewakidai kuwa kufanya hivyo ni sawasawa na kuchanganya dini na siasa. Waislamhawa walikaa pembeni kama watazamaji huku Nyerere kwa taratibu akivunja uongoziwa EAMWS na kutayarisha watu wakekuwaongoza Waislam. Kundi la Adam Nasibu lilikataa kukutana na Tume ya Kwikima.Maulamaa wa Kiislam ambao walikuwa na hadhi na uwezo wa kuleta sulhu katikasakata ile hawakuweza kufanya hivyo kwa kuwa walikuwa wanajua fika kuwaaliyekuwa akivunja EAMWS hakuwa Adam Nasibu, yeye na wenzake walikuwawakitumiwa tu. Kundi la Adam Nasibu lilikuwa halitaki chochote ila EAMWSivunjwe na badala yake iundwe jumuiya itakayokuwa chini ya kivuli cha serekali.[1]Vilevile kukawa na uvumi kuwa Muislam yeyote ambae atakaejejihusisha nashughuli za EAMWS atawekwa kizuizini na serekali. Tume ya Kikwima haukuwezakupuuza vitisho hivyo kwa sababu serekali ilishawahi kuwaweka vizuizinimasheikh.Tume ya Kwikima ilikuwa inafahamu lile kundi laAdam Nasibu halikuwa na nguvu wala uwezo wa kuivunja EAMWS. Kufuatia kutangazwakwa mkutano wa Iringa wa kundi la Adam Nasibu, Tume ya Kwikima ilitoa taarifayake tarehe 11 Desemba ñ siku moja kabla ya mkutano wa Iringa kuanza. [1]Taarifa ambayo ilitolewa kwa Waislam wote, iliitisha mkutano mkuu wa EAMWSambao ulikuwa ufanyike mwezi Februari mwaka unaofuata kujadili na kutoa uamuziwa mwisho kuhusu ëmgogoroí. [1]Tarehe ya mkutano ilibadilishwa hapobaadae na kuwa Januari kutokana na umuhimu wa ëmgogoroí uliokuwa ukikabiliEAMWS. Gazeti la TANU baada ya kusoma taarifa ya Kwikima iliamua kutoa maoniyake kuhusu taarifa ile kwa kusema kuwa haikuwa sawa.[1] Huu ulikuwa mpangouliosukwa mapema kuonyesha kuwa uongozi wa EAMWS ulikuwa na ubadhirifu. Jumalile lile Aga Khan ambae ndiye aliyekuwa akishambuliwa na kundi la Adam Nasibu,baada ya kutambua kuwa EAMWS isingeweza kamwe kuokolewa, akiwa Paris, Ufaransaalijiuzulu nafasi yake kama patron wa EAMWS."[1]