Prof Griff
JF-Expert Member
- Aug 29, 2008
- 6,772
- 5,258
Duh mkuu wangu bado unaliendeleza barza.... Heee ama kweli wajua kuuza kitabu... Kwa hili la Hanga nakuomba sana tena sana funga safari nenda Zanzibar mtafute Nassoro Moyo atakueleza kwa ufasaha kilichotokea (kama atapenda) maana yeye na marehemu H. Hanga walikuwa kundi moja..
Duh mkuu wangu bado unaliendeleza barza.... Heee ama kweli wajua kuuza kitabu... Kwa hili la Hanga nakuomba sana tena sana funga safari nenda Zanzibar mtafute Nassoro Moyo atakueleza kwa ufasaha kilichotokea (kama atapenda) maana yeye na marehemu H. Hanga walikuwa kundi moja..
Ile kwamba Hanga alilawitiwa gerezani kabla ya kifo chake, lawama yote ni kwa JKN yote sababu ya "Muungano" ambao ulikuwa ni "hirizi tosha ya kumkinga Karume?" Swali ni jee, "hirizi" in what sense? Hapa ni wazi Mwandishi anachukulia kwamba presumed super-natural effects za "hirizi" are real and effective, and could be taken in a literal sense.
Hivi huyu Mag3 alishaelezea ile Historia yake ya makabila 50 ya Mara kudai Uhuru?
FF,
Mag3 bado hajaeleza habari za Musoma.
Mie bado nazisubiri kwa hamu.
Imekuwa bora umemkumbusha.
Mohamed
PS: Bi Faiza ukumbi umepooza we miss you plenty. MS
Nipo ndugu yangu, nilipigwa ban nikawa sionekani lakini napita napita humu kupata darsa, tuko pamoja.
Mohamed Said,
..tuhuma dhidi ya Kassim Hanga zilikuwa ni nini?
..unakumbuka ni tuhuma gani Nyerere alizitoa dhidi ya Hanga kwenye mkutano wa hadhara?
..Kwanini Nyerere hakumuacha huku bara kama ilivyokuwa kwa Abdulrahman Babu?
..yuko Col.Mahfudhi naye alikuwa anatakiwa Zanzibar lakini akaishia huku Bara, na baadaye akawa assigned kijeshi Mozambique.
..nauliza haya maswali kwasababu style ya Nyerere ilikuwa siyo kuua. Yeye kama alikuwa hakutaki basi alikutupa kizuizini kama ilivyotokea kwa kina Christopher Kassanga Tumbo, na Joseph Kassela Bantu, ambao walikaa kizuizini kwa miaka 20+.
Sheikh Mohamed Said,
..Thanx.
..nimesoma kile kingine "kuusuta uongo..."
..there r very sad things that have been reported in the book.
..tatizo ni kukosekana kwa ujasiri miongoni mwa wa-Zenj kukubali kwamba tatizo linaanza na wao wenyewe.
..in the end mwandishi anamtupia lawama zote Mwalimu Nyerere.
..the author is even claiming that there was no racism in Zanzibar!!!
..sasa hiki kitabu cha Ghassany kina lipi jipya ambalo halijaripotiwa kule kwenye "kuusuta uongo..."?
Kitu kimoja nilicho na hakika nacho kwa asilimia 100% ni kwamba wale wote wenye mapenzi ya kweli kwa taifa letu la Tanzania wanasita sana kuchangia hii hoja inayofinyangwafinyangwa na huyu anayejiita Mohamed Said. Bila kumung'unya maneno nayaita madai ya Mohamed Said la kutoa elimu ya historia ya kweli ni porojo hatari iliyojaa uchochezi ambayo lengo lake hasa ni kuleta uhasama wa kidini miongoni mwa wananchi. Sijui anachotegemea kufaidika nacho kwa kupanda hii mbegu ya hatari ambayo nina hakika mtu kama Mohamed Said anajua fika madhara yake.
Mohamed Said ni kama kipofu ambaye baada ya kusimuliwa na wazee kwamba tembo ni mnyama mkubwa kuliko wanyama wengi anapata nafasi ya kumpapasa tembo. Kwa bahati mbaya anaupapasa mguu wa tembo na si mwili wote halafu katika imani yake anadai anao uwezo wa kutoa somo kuhusu umbo la mnyama tembo na ushuhuda wake, kuwa tembo ni kama gogo la mti mkubwa, ndio ukweli na anayesema tofauti hajui kitu. Watu wote wanaolalamikiwa na Mohamed Said kuwa walisahauliwa, wengi wao walikuwa wakazi wa Dar es Salaam eneo la Gerezani.
Kabla ya uhuru Tanganyika iligawanywa katika majimbo makuu manane na katika majimbo yote hayo, jimbo la pwani kwa ujumla lilikuwa moja ya majimbo yaliyokuwa nyuma kimaendeleo kiuchumi, kielimu na kisiasa na hiyo ni licha ya kuwa makao makuu ya serikali ya kikoloni yalikuwa Dar es Salaam. TAA ilianzishwa na watumishi wa serikali (civil servants) na kwa wakati wote kazi kubwa ya TAA ilikuwa ni kulalamika ikidai haki ya wafanyakazi bila upendeleo na hasa ubaguzi wa rangi katila utumishi kubwa ukiwa uonevu dhidi ya wazawa, mtu mweusi.
Jimbo la Ziwa ni moja ya majimbo yaliyokuwa mbele kiuchumi, kielimu na kisiasa na kama kuna kitu kinaweza kudaiwa kuwa kilisahaulika katika harakati ya kupigania uhuru ni mchango wa Jimbo la Ziwa (Bukoba, Mwanza, Mara na Shinyanga) Jimbo la Ziwa ndilo lililoongoza kwa idadi ya watu, idadi ya makabila, idadi ya mali asili na idadi ya machifu ambao nafasi yao ilikuwa kubwa tu katika kuhamasisha watu. Moja wa watu ambao mchango wao nitautaja kidogo tu ingawa alifanya jitihada kubwa labda zaidi ya wazee wa Mohamed Said ni Paul "Kishamapanda" Bomani.
Historia ya harakati za uhuru ni zaidi ya porojo za Mohamed Said, watu walipigania uhuru kama Watanganyika na bila kubaguana kikabila, kidini wala kijinsia. Ndio maana mimi sitaki kabisa kuwa na majibizano na huyu Mohamed Said moja kwa moja ila kwa kuwa hoja ileletwa JF, akae tayari kupewa somo kuhusu umbile zima la mnyama tembo na sio mguu moja wa tembo alioupapasa. Hapa mimi nitaongea sana kuhusu mchango wa Jimbo la Ziwa na baadaye kuonyesha jinsi maadui wa nchi yetu wanavyowatumia kidini watu kama huyu Mohamed Said.
Baadaye nitaeleza jinsi Mkoa wa Mara yenye makabila karibu hamsini yalivyoweza kushirikiana bila mfarakano na kuitikia mwito wa Mwalimu Nyerere katika hizo harakati za kudai uhuru. Je mwamko wa wakazi wa jimbo la Ziwa ulikuwaje na mapokezi gani aliyapata kila wakati Mwalimu aliporudi kwenye hili jimbo ambalo idadi ya wakazi wake kwenye miaka ya 50s ilikuwa mara tatu ya majimbo mengi Tanganyika kama Pwani. Pia nitaonyesha ni wakati gani walianza kuyasikia hayo majina anayodai Mohamed Said ya wazee wa Gerezani Dar es Salaam !
jK,JK,
Nakushauri ukisome kitabu cha Dr Harith Ghassany "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru" utapata yote humo ndani.
Mohamed
jK,
Nakushauri utapoteza muda wako bure kusoma kitabu cha Dr Harith Ghassany. Ni upotoshaji mwingine wa historia. Kama title yake inavyosema, baada ya kuondolewa ukoloni Zanzibar uhuru wa kikweli haujapatikana. If you believe that, go ahead and read the book, but don't say I didn't warn you.
jK,
Nakushauri utapoteza muda wako bure kusoma kitabu cha Dr Harith Ghassany. Ni upotoshaji mwingine wa historia. Kama title yake inavyosema, baada ya kuondolewa ukoloni Zanzibar uhuru wa kikweli haujapatikana. If you believe that, go ahead and read the book, but don't say I didn't warn you.
dah hadithi bado zinaendelea na kujirudia!!.....sasa naamini kuwa lile kabila ni wabishi......maswali hawajibu....."darsa" tu kwa kwenda mbele, iwe pumba iwe mchele.....ni kanyaga twende...duh
Ustaadh Moh'd naona unamwaga nondo sio polepole. Haya endeleeni kutujuza hizi habari.
Hoja ilikuwa ni kama Mkwawa alikuwa ni Muislam au la, na wala hoja haikuwa mkwawa alipataje utawala wa Wahehe. Kuna wengi sikuwataja kama kina Mayagila, mdegela, Mdemu na wengineo. Inshaalah watakuwemo kwenye Historia fupi ya Mkwawa.Muulizeni Kigarama mbona hajamtaja Muhenga wala Mwambambe kwani inasemekana Mwambambe alikuwa anaonekana ni nuksi na dosari katika historia ya wahehe. Tutaendelea kesho wacha niwaacheni leo nilikuwapo wakuu.