Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Nimeipenda hii nukuu: "as long as you stand to correct history, the same will correct you."
 
--------------------

Jasusi,

Walichokuwa wanakitafuta Waingereza ni kutia mjiti katika ya Waislam na Wakristo ili ipatikane farka. Waislam wangelikataa kushiriki katika uchaguzi ule chama kingemeguka na Nyerere angepwelewa.

Sasa hapa kigetoka chama kingine ambacho kingeingia katika kura tatu na chama hiki kingelikuwa na Wakristo kwani Waislam wangelibaki wengi katika TANU.

Hili lingetendeka lingevuruga mstakbali wa nchi yetu kabisa.

Kwa wazee wetu kukubali TANU iwalete watu kutoka nje kuja kusimama kuingia katika Legco na Waislam wabaki nje ya chombo hicho ilikuwa busara kwa maana kuwa ile farka iliepukwa na wananchi wakabaki wamoja.... [/COLOR]
Hapa hujajibu swala lililoibuliwa na mwenzio.

Imesemwa uliwahi kudai kwamba Kura Tatu, ambayo tunajua Nyerere aliwakazania kwa udi na uvumba wenzake waikubali, ililengwa kuwabagua waislam. Lakini pia sehemu nyingine umesomeka ukidai kwamba Kura Tatu ulikuwa ni "uamuzi wa busara."

Kwa hiyo, Jasusi ameuliza, lipi ni lipi?

Kwa maneno mengine tuseme ulikosea msimamo wa kwanza au wa pili, au Jasusi ndio kakosea kuwakilisha mawazo yako, au wewe ndio misimamo yako ni ya kudanganya danganya?
 
Niwie radhi labda sikulielewa swali. Ikiwa swali ni "Je TANU ilfanya uamuzi wa busara kuingia katika kura tatu jibu ni ndiyo ulikuwa uamuzi wa busara.

Mohamed
 
Kigarama, nashukuru sana maana nimeandika kitu kama hiki katika makala ya Mohamed Said ile inayoendelea thread nyingine.

Nimehoji kuwa ni vema kama Matimbwa alitoa mchango huo na tunauthamini sana, lakini kwa bahati mbaya kama ilivyo ada ya Mzee Said pesa hizo sio hoja, hoja ni kuinasibisha na jina la Salum na wala si Matimbwa, hapo unajua kinaendelea nini.
Katika makala zake Mohamed amemtaja John Rupia kama mtu aliyetoa kiwanja cha ujenzi, lakini huwezi kumsikia John akitajwa kwasababu ni John. Hapo ndipo tunapohoji sana makala za Mohamed na 'Biasness'.

Ukitaka kuona mkanganyiko zaidi, ni pale Mohamed Said anaposema hotuba ya Nyerere UNO iliandikwa na Sykes na kufanyiwa editing Mzumbe kabla hajaenda nayo UNO. Hili laweza kuwa ni kweli lakini linazaa maswali mengine. Nyerere alipofika Dar alikuwa ni msomi mzuri tu aliyehitimu Makerere na Edimburgh. Inaingia akilini zaidi kuwa ufahamu wake wa mambo ya kimataifa ulikuwa mkubwa sana kuliko wenzake wengi.

Labda ingeandikwa kuwa hotuba iliandikwa kwa ushirikiano wa abc ningeelewa zaidi. Sidhani Nyerere alikuwa mtu wa kuandikiwa hotuba aende akaisome tu bila ye yeye kuwa na ushiriki wa kujua nini anaenda kuongelea.

Na kuthibitisha kuwa hotuba iliandikwa kwa ushirikiano naomba nimnukuu mzee Said '........Sykes aliandika na kuituma kwa basi Mzumbe na kisha kurudishwa kwakwe.....' Sasa kama aliandika na ikafanyiwa edit Mzumbe ni wazi kulikuwa na ushirikiano wake na wenzake, ushirikiano ambao nadhani ulimgusa aliyetakiwa kwenda kutoa hotuba UNO.

Hii haina maana Sykes hakuandika au hakuna nakala ya hotuba! maana yake halisi na anachotaka kusema Mohamed ni kuendelea kumdhalilisha Nyerere kama alivyowahi kusema ' wazee walimjua Nyerere wakati akiwa si lolote si chochote' na pia ' ......Kiyate akampa pesa za kwenda kariakoo kununua mboga n.k.

Ukisoma makala za mzee Said sehemu inayomhusu Nyerere inanasibishwa sana na ubaya. In short, his intention is to potray the negative image about Mwalimu, despise him, above all to make Nyerere as public enemy number one. Mohamed hates Nyerere to the core.
Mzee Said strives to make his grievance as a 'public issue'.
As long as you stand to correct the history, the same will correct you.

Ndugu yangu Nguruvi3, ningekuwa FaizaFoxy ningemwambia huyu Mohamed Said kuwa "ananchekesha". Naanza kuamini kabisa kuwa Mohamed Said hakumfahamu kabisa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wala historia yake zaidi ya porojo alizosimuliwa na Wazee wake. Kabla sijaingia kwa undani katika historia historia ya Mwalimu Nyerere ambayo kama Mohamed Said angefanya utafiti japo kidogo wa kutaka kuijua hiyo historia katu hangetoa hiyo kashfa kwamba Mwalimu alisoma tu hotuba aliyoandikiwa ! Lakini kwa kuwa anathubutu kudai hivyo, kuna maswali manne ya msingi hapa:
  • Kwa nini kabla ya kuanzishwa TANU na licha ya kipindi kifupi walichomfahamu Mwalimu, wazee wa Mohamed walikubali awe nahodha wao na kumkabidhi chombo chao TAA akiongoze kama Raisi wake mwaka 1953 ? Walikuwa hawana mwenye sifa na uzoefu zaidi yake ?
  • Katika huo uchaguzi bila shaka wagombea walipewa nafasi ya kujieleza, je hali likuwaje baada ya Mwalimu Nyerere kujieleza ?
  • Baada ya kuanzishwa kwa TANU mwaka 1954, uchaguzi wa Raisi wa kwanza wa TANU uliwahusisha akina nani kama wagombea au Nyerere alikosa mpinzani ? Je wajumbe waliomkataa Mwalimu Nyerere walikuwa wangapi na ni akina nani ?
  • Je yawezekana kuwa kweli kwamba Wazee wa Mohamed hawakuwahi kumsikia Mwalimu Nyerere kabla ya 1952 ?
Between 1943 and 1945 Nyererre attended Makerere University, in Uganda's capital Kampala, obtaining a teaching certificate. It was around this time that he took his first steps towards a political career - in 1945 he formed Tanganyika's first student group, an offshoot of the African Association, AA, (a pan-African group first formed by Tanganyika's educated elite in Dar es Salaam, in 1929). Nyerere and his colleagues began the process of converting the AA towards a nationalistic political group.

Mohamed Said anaongelea vijana walioleta Changamoto ndani TAA lakin hawataji wasomi hawa kama Mwalimu Nyerere badala yake amejikita kwa waliotoka KAR baada ya vita vya pili ! Ukweli ni kwamba wengi wa hao Wazee walipigwa butwaa kwa ujuzi na uwezo mkubwa wa Mwalimu siyo tu katika kujieleza lakini kubwa zaidi mikakati aliyokuwa tayari ameitayarisha tangu awali akiwa Makerere. Kulingana na maandishi ya Prof. Haroub Othman, " Makerere was at that time the highest institution of learning in East Africa, and constituted an important period for Mwalimu Nyerere in formulating the objectives and principles that guided him later on in his life."

Mwalimu Nyerere alifundisha Tabora kwa miaka mitatu ( 1945 - 1948) kabla hajapewa Scholarship kwenda Uingereza kuendelea na msomo mwaka 1949 akiwa Mtanganyika wa kwanza kusomea MA in Economics. Je kwa miaka hiyo mitatu akiwa Tabora alifanya nini kwa sababu kulingana na simulizi za wazee wa Mohamed Mwalimu Nyerere hakuna sehemu juhudi zake Tabora zinapewa umuhimu wowote na kumbe ni yeye aliyeanzisha tawi la AA Tabora.

Once he had gained his teaching certificate, Nyerere returned to Tanganyika to take up a teaching post at Saint Mary's, a Catholic mission school in Tabora. He opened a local branch of the AA, and was instrumental in converting the AA from its pan-African idealism to the pursuit of Tanganyikan independence. To this end, the AA restyled itself in 1948 as the Tanganyika African Association, TAA.

Vijana wasomi wa Kiafrika nyakati hizo walikuwa na kawaida ya kuwa na majadiliano ya pamoja kuhusu mustakhabali wa bara la Afrika na walijikita sana katika jinsi ya kushiriki katika harakati za kudai uhuru. Mara nyingi walipeana mawaidha na mikakati iliyohusu uendeshwaji wa vyama vya siaisa na utayarishwaji wa katiba na hivyo si ajabu katiba nyingi za vyama vilivyoanzishwa zilifanana fanana. Katika misingi hii si ajabu katiba ya nyingi kufanana, kwa nini tunashindwa kuona uwezekano wa Mwalimu kushiriki katika kuidraft katiba ya Ghana kwani Mwalimu Nyerere na Kwame Nkuruma hawakukutana barabarani, walikutana masomoni.

In 1949 Nyerere left Tanganyika to study for an MA in economics and history at the University of Edinburgh. He was the first African from Tanganyika to study at a British university and, in 1952, was the first Tanganyikan to gain a degree. At Edinburgh Nyerere became involved with the Fabian Colonial Bureau (a non-Marxist, anti-colonial socialist movement based in London). He watched intently Ghana's path to self-government, and was aware of the debates in Britain on the development of a Central African Federation (to be formed from a union of North and South Rhodesia and Nyasaland). Three years of study in the UK gave Nyerere an opportunity to vastly widen his perspective of pan-African issues. Graduating in 1952, he returned to teach at a Catholic school near Dar es Salaam. On 24 January he married primary school teacher Maria Gabriel Majige.

Kwa mtu anayejua historia ya Nyerere hawezi kuthubutu kutoa madai ya kipuuzi kama anavyofanya Mohamed Said, madai potofu ambayo hakuna namna ya kuyaelezea zaidi ya chuki za kidini zinazotokanana na simulizi za wazee zisizokuwa na msingi wowote. Mwalimu alikuwa na uwezo mkubwa wa kujieleza na ndiye kiongozi barani Afrika aliyeweza kuwakabili viongozi wa mataifa makubwa on one to one basis. Na wote kuanzia Indira Gandhi wa India, Mao Tse Tung wa China, Olof Palme wa Scandinvia, John Kennedy wa Marekani, Malkia Elizabeth wa United Kingdom na kutoka kila pembe ya dunia aliweza kukabiliana nao hoja kwa hoja na wakamkubali. Sasa hawa Wazee wa Gerezani wanapata ujasiri gani wa kupandikiza hizi mbegu za chuki kwa mtoto wao dhidi ya Baba wa Taifa ! Wangekuwa hai tungewahoji but ... how convenient kwa Mohamed Said !

Nitaendelea.......! Baada ya kutoka masomoni mwaka 1952.
 
... Ikiwa swali ni "Je TANU ilfanya uamuzi wa busara kuingia katika kura tatu jibu ni ndiyo ulikuwa uamuzi wa busara.
Ha ha hahahaaaa....

Hapana!

Hilo sio swali. Unajifanya huelewi, wazungu wanasema huna intellectual honesty, huna maadili ya kiakili.

Swali ni, uliwahi kudai kwamba Kura Tatu ya Mkoloni ambayo Kambarage aliitetea kwa dhati iliyosababisha mpaka maswaiba wake wakakimbia chama, Zuberi Mtemvu n.k., ililenga kuwabagua Waislam. Leo unatuambia Kura Tatu ulikuwa uamuzi wa busara.

Je, madai yako ya awali ya ubaguzi dhidi ya Waislam ni kukosea kwa bahati mbaya au Jasusi hawakilishi mawazo yako kwa usahihi, au kuna reconciliation katika misimamo yako miwili, kwamba kuwabagua Waislam lilikuwa ni jambo la busara au ni wewe ndio una misimamo ya kinafki, kichochezi na ya uongo wa kuchomewa jehanam?
 
Taso,

Nimeulizwa swali na mie nimetoa jibu. Ikiwa jibu hukulipenda hilo ni jambo la kawaida hatutovutana kwa hilo.

Mohamed
 
Ndugu yangu Nguruvi3, ningekuwa FaizaFoxy ningemwambia huyu Mohamed Said kuwa "ananchekesha". Naanza kuamini kabisa kuwa Mohamed Said hakumfahamu kabisa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wala historia yake zaidi ya porojo alizosimuliwa na Wazee wake. Kabla sijaingia kwa undani katika historia historia ya Mwalimu Nyerere ambayo kama Mohamed Said angefanya utafiti japo kidogo wa kutaka kuijua hiyo historia katu hangetoa hiyo kashfa kwamba Mwalimu alisoma tu hotuba aliyoandikiwa ! Lakini kwa kuwa anathubutu kudai hivyo, kuna maswali manne ya msingi hapa:
  • Kwa nini kabla ya kuanzishwa TANU na licha ya kipindi kifupi walichomfahamu Mwalimu, wazee wa Mohamed walikubali awe nahodha wao na kumkabidhi chombo chao TAA akiongoze kama Raisi wake mwaka 1953 ? Walikuwa hawana mwenye sifa na uzoefu zaidi yake ?
  • Katika huo uchaguzi bila shaka wagombea walipewa nafasi ya kujieleza, je hali likuwaje baada ya Mwalimu Nyerere kujieleza ?
  • Baada ya kuanzishwa kwa TANU mwaka 1954, uchaguzi wa Raisi wa kwanza wa TANU uliwahusisha akina nani kama wagombea au Nyerere alikosa mpinzani ? Je wajumbe waliomkataa Mwalimu Nyerere walikuwa wangapi na ni akina nani ?
  • Je yawezekana kuwa kweli kwamba Wazee wa Mohamed hawakuwahi kumsikia Mwalimu Nyerere kabla ya 1952 ?
Mohamed Said anaongelea vijana walioleta Changamoto ndani TAA lakin hawataji wasomi hawa kama Mwalimu Nyerere badala yake amejikita kwa waliotoka KAR baada ya vita vya pili ! Ukweli ni kwamba wengi wa hao Wazee walipigwa butwaa kwa ujuzi na uwezo mkubwa wa Mwalimu siyo tu katika kujieleza lakini kubwa zaidi mikakati aliyokuwa tayari ameitayarisha tangu awali akiwa Makerere. Kulingana na maandishi ya Prof. Haroub Othman, " Makerere was at that time the highest institution of learning in East Africa, and constituted an important period for Mwalimu Nyerere in formulating the objectives and principles that guided him later on in his life."

Mwalimu Nyerere alifundisha Tabora kwa miaka mitatu ( 1945 - 1948) kabla hajapewa Scholarship kwenda Uingereza kuendelea na msomo mwaka 1949 akiwa Mtanganyika wa kwanza kusomea MA in Economics. Je kwa miaka hiyo mitatu akiwa Tabora alifanya nini kwa sababu kulingana na simulizi za wazee wa Mohamed Mwalimu Nyerere hakuna sehemu juhudi zake Tabora zinapewa umuhimu wowote na kumbe ni yeye aliyeanzisha tawi la AA Tabora.

Vijana wasomi wa Kiafrika nyakati hizo walikuwa na kawaida ya kuwa na majadiliano ya pamoja kuhusu mustakhabali wa bara la Afrika na walijikita sana katika jinsi ya kushiriki katika harakati za kudai uhuru. Mara nyingi walipeana mawaidha na mikakati iliyohusu uendeshwaji wa vyama vya siaisa na utayarishwaji wa katiba na hivyo si ajabu katiba nyingi za vyama vilivyoanzishwa zilifanana fanana. Katika misingi hii si ajabu katiba ya nyingi kufanana, kwa nini tunashindwa kuona uwezekano wa Mwalimu kushiriki katika kuidraft katiba ya Ghana kwani Mwalimu Nyerere na Kwame Nkuruma hawakukutana barabarani, walikutana masomoni.

Kwa mtu anayejua historia ya Nyerere hawezi kuthubutu kutoa madai ya kipuuzi kama anavyofanya Mohamed Said, madai potofu ambayo hakuna namna ya kuyaelezea zaidi ya chuki za kidini zinazotokanana na simulizi za wazee zisizokuwa na msingi wowote. Mwalimu alikuwa na uwezo mkubwa wa kujieleza na ndiye kiongozi barani Afrika aliyeweza kuwakabili viongozi wa mataifa makubwa on one to one basis. Na wote kuanzia Indira Gandhi wa India, Mao Tse Tung wa China, Olof Palme wa Scandinvia, John Kennedy wa Marekani, Malkia Elizabeth wa United Kingdom na kutoka kila pembe ya dunia aliweza kukabiliana nao hoja kwa hoja na wakamkubali. Sasa hawa Wazee wa Gerezani wanapata ujasiri gani wa kupandikiza hizi mbegu za chuki kwa mtoto wao dhidi ya Baba wa Taifa ! Wangekuwa hai tungewahoji but ... how convenient kwa Mohamed Said !

Nitaendelea.......! Baada ya kutoka masomoni mwaka 1952.

Mag3,

Naomba nikusahihishe. Nyerere na Nkrumah hawakupata kukutana masomoni. Wazee wangu hawahadithii porojo. Walichokijua kuhusu Nyerere si siri kwa watu walioishi miaka ile ni vitu ambavyo vikijulikana na kila mtu. Kusema kuwa TANU ilianzishwa na Abdulwahid Sykes hili kwa wakati ule wala halikuwa jambo nyeti wala haikuwa jambo nyeti kusema kuwa Al Jamiatul Islamiyya ilitoa fedha kuchangia safari ya Nyerere UNO. Haya yote yalikuwa mambo ya kawaida na watu wakiyajua. Kamati ya ndani ya TAA ilikuwa ikiwajua "intellectuals" wake wa ni Abdu, Steven Mhando, Mwapachu, Sheikh Hassan bin Amir... Siku hizo Nyerere hajafika Dar es Salaam na hizo nyaraka zipo na ndizo nilizotumia kuandika kitabu.

Sasa tuje Tabora. Nyerere hakuasisi African Association Tabora na wala sitokuita muongo kwa kusema hivyo najua ni kosa la kawaida hukuwa na nia mbaya na hujui kwa undani historia ya Tanganyika. Hebu soma hii hapa chini:

"Tarehe 3 Machi, 1945 African Associationmjini Tabora ilifungua ofisi yake ikiwa na na viongozi wafuatao: Hamisi Simbe (Rais), Ramadhani Nasibu (Makamu waRais), M. K. Hemed (katibu), Chamngíanda Usingizi (Mwenyekiti), Fimbo Mtwana(Mweka Hazina) na Rashidi Mussa (Mkaguzi wa Hesabu). African Association, kamailivyokuwa asili ya kilabu iliyotokana nayo, ilishikwa na Wamanyema. Hivyindivyo Wamanyema walivyokuja kuongoza siasa Tanganyika. Julius Nyerere, wakatihuo akifundisha St. Maryís School, alishuhudia sherehe za uzinduzi wa AfricanAssociation.[1]Nyerere hakutambua hata kidogo wakati huo kuwa alikuwa akishuhudia sehemu yahistoria kazi yake mwenyewe ikijifungua mbele ya macho yake."

Mwaka 1947 palitokea mgomo mkubwa hapo Tabora na Nyerere hakuoenekana popote. Viongozi hawa wa mgomo huu wengi walikuwa katika AA na babu yangu, Salum Abdallah ndiye aliyeongoza huo mgomo. Sasa hapa uongo uko wapi? Uongo utakuja tu kama mtu atasema Nyerere alijihusisha na harakati hizi za wananchi na aliongoza mgomo dhidi ya wakoloni.

Umeandika vitu vingi lakini naamini kwa haya niliyoweka hapa wanaukumbi weshapata picha zetu.

Insha Allah nasubiri mengine na nitachangia pale inapobidi.

Mohamed
 
Ha ha hahahaaaa....

Hapana!

Hilo sio swali. Unajifanya huelewi, wazungu wanasema huna intellectual honesty, huna maadili ya kiakili.

Swali ni, uliwahi kudai kwamba Kura Tatu ya Mkoloni ambayo Kambarage aliitetea kwa dhati iliyosababisha mpaka maswaiba wake wakakimbia chama, Zuberi Mtemvu n.k., ililenga kuwabagua Waislam. Leo unatuambia Kura Tatu ulikuwa uamuzi wa busara.

Je, madai yako ya awali ya ubaguzi dhidi ya Waislam ni kukosea kwa bahati mbaya au Jasusi hawakilishi mawazo yako kwa usahihi, au kuna reconciliation katika misimamo yako miwili, kwamba kuwabagua Waislam lilikuwa ni jambo la busara au ni wewe ndio una misimamo ya kinafki, kichochezi na ya uongo wa kuchomewa jehanam?

Taso,

Nimeulizwa swali na mie nimetoa jibu. Ikiwa jibu hukulipenda hilo ni jambo la kawaida hatutovutana kwa hilo.

Mohamed

Kukiri kuwa ulikosea ni uungwana Brother MS...
 
Umesema kweli.

Kukosea ni jamabo la kawaida kwetu binadamu wala siwezi kuona aibu kwa kufanya kosa.

Mohamed
 
Ni kweli hata sie wafuatiliaji wa mjadala tumeliona hilo, lakini "two wrongs don't make it right" muungwana M'hd deserved an apology then ndo hayo maelezo yangefuata..
Aksante..
 
Wana JF hii hapa chini ni sehemu ndogo ya ushuhuda wa mtu aliyeitwa Father Arthur H. Wille, M.M. alivyokutana na kumfahamu Mwalimu Nyerere. Sababu yangu ya kutoa ushuhuda huu ni kwamba huyu alikuwa na bahati ya kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na baadhi ya Wazee wa Mohamed Said. Hebu jaribuni kutafakari maneno anayosema yalitamkwa na Abdul Sykes pamoja na Abbas Sykes wakimwelezea Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika hayo mazungumzo.
Within three months of returning to Dar es Salaam Julius joined the Tanganyikan African Association. He had been a member of this organization when he was at Makerere. A much respected British Governor, Sir Donald Cameron, had established the Tanganyikan African Association as a social club for civil servants.

It continued to be involved in this way, but never with the purpose of seeking independence. As Julius got to know TAA better, he found that it was merely a social club interested mainly in giving tea parties for expatriates who were going on leave.
As a newcomer to Dar es Salaam Julius was seen as one with the people. He was in contrast to Chief David Makwaia, who was the favorite politician of the then Governor Edward Twining. Chief David Makwaia was a university graduate. Like many Africans with university education at this time, they became sophisticated. Chief Makwaia preferred to be with the Europeans. He was elected to the Legislative Council of the governor.

Julius quickly gained leadership and was elected president of TAA. He began by educating his followers to think about independence. Chief Patrick Kunambi who knew him well said that his leadership was not based on what Julius promised “because Julius practically never promised anything.”

Another associate of his, Abdul Sykes, once said, “Nyerere made us start to think: all we wanted was independence.” Because of this goal of independence Nyerere and his colleagues reorganized TAA as a political party, the Tanganyika African National Union, on July 7, 1954. It became better known as TANU and the date of it founding, the seventh day of the seventh month became Saba Saba (in Swahili “seven-seven”).

His colleagues unanimously elected Julius as president of TANU. He was 32 years old at the time. One of the founding members of TANU, Abbas Sykes said, “He came at the right time. Usually if a man went away to university when he came back he would not be one with us; he would be very sophisticated. But here was a man who had the same kind of education — higher in fact, because he had an M.A. instead of a B.A. — who was willing to be with his people.This humility— ‘I’m willing to serve you’— made everyone forget that he was from up-country and that he wasn’t a Muslim.”

There are as many Christians as Muslims in Tanganyika (now Tanzania) as a whole, but the coastal region is heavily Muslim.

Huyo ndiye Mwalimu Julius Nyerere lakini huyu anayeongelewa kwa kebehi na Mohamed Said sijui ni Nyerere yupi !
 
Mzee Mwanakijiji;2690367]Bw. Said, Nyerere alikuja Dar-es-Salaam kwa mara ya kwanza mwaka gani?

Mag3;2690168]Ndugu yangu Nguruvi3, ningekuwa FaizaFoxy ningemwambia huyu Mohamed Said kuwa "ananchekesha". Naanza kuamini kabisa kuwa Mohamed Said hakumfahamu kabisa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wala historia yake zaidi ya porojo alizosimuliwa na Wazee wake. Kabla sijaingia kwa undani katika historia historia ya Mwalimu Nyerere ambayo kama Mohamed Said angefanya utafiti japo kidogo wa kutaka kuijua hiyo historia katu hangetoa hiyo kashfa kwamba Mwalimu alisoma tu hotuba aliyoandikiwa !
1.Kwa nini kabla ya kuanzishwa TANU na licha ya kipindi kifupi walichomfahamu Mwalimu, wazee wa Mohamed walikubali awe nahodha wao na kumkabidhi chombo chao TAA akiongoze kama Raisi wake mwaka 1953 ? Walikuwa hawana mwenye sifa na uzoefu zaidi yake ?

2. Katika huo uchaguzi bila shaka wagombea walipewa nafasi ya kujieleza, je hali likuwaje baada ya Mwalimu Nyerere kujieleza ?

3.Baada ya kuanzishwa kwa TANU mwaka 1954, uchaguzi wa Raisi wa kwanza wa TANU uliwahusisha akina nani kama wagombea au Nyerere alikosa mpinzani ? Je wajumbe waliomkataa Mwalimu Nyerere walikuwa wangapi na ni akina nani ?

4.Je yawezekana kuwa kweli kwamba Wazee wa Mohamed hawakuwahi kumsikia Mwalimu Nyerere kabla ya 1952

Kwa mtu anayejua historia ya Nyerere hawezi kuthubutu kutoa madai ya kipuuzi kama anavyofanya Mohamed Said, madai potofu ambayo hakuna namna ya kuyaelezea zaidi ya chuki za kidini zinazotokanana na simulizi za wazee zisizokuwa na msingi wowote. Mwalimu alikuwa na uwezo mkubwa wa kujieleza na ndiye kiongozi barani Afrika aliyeweza kuwakabili viongozi wa mataifa makubwa on one to one basis. Na wote kuanzia Indira Gandhi wa India, Mao Tse Tung wa China, Olof Palme wa Scandinvia, John Kennedy wa Marekani, Malkia Elizabeth wa United Kingdom na kutoka kila pembe ya dunia aliweza kukabiliana nao hoja kwa hoja na wakamkubali. Sasa hawa Wazee wa Gerezani wanapata ujasiri gani wa kupandikiza hizi mbegu za chuki kwa mtoto wao dhidi ya Baba wa Taifa ! Wangekuwa hai tungewahoji but ... how convenient kwa Mohamed Said !
Mzee Said kama ulivyosema mcheza kwao hutuzwa, sasa kuna maswali hapo juu ya MM na Mag3. Moja la MM na manne ya Mag3. Tafadhali sana yajibu kabla uzi haujasonga mbele ili usisahau.

Nimekuwa nafikiri, hivi huyu mtu aliyekuwa na degree yake nyakati hizo aliwezaje kuandikiwa hotuba. Halafu tunaambiwa hotuba haipatikani popote! Huko nyuma tuliambiwa na Mohamed kuwa Sykes anakumbukumbu zote na ameziweka vema sana sijui ilikuwaje draft ya hotuba ya UNO hakuwa nayo.

Lakini hata kama ikipatikana bado sahihi itakuwa na ya kiongozi wa TANU aliyetoa hotuba hata kama imeandikwa na akina marhum Sykes, marhum mzee dalali mshume Kiyate n.k.

Nakumbuka mwaka 1962, mwaka mmoja baada ya uhuru Nyerere alikutana na Mzee Mandela wakati anakwenda Adis Ababa na akamuonya kuwa akirudi South Africa watamfunga. Ndiye kiongozi wa mwisho kukutana naye kabla ya kuingia gerezani. Sasa huyu Nyerere aliyeweza kuwasiliana na vigogo kama Mandela katika miaka 1960 alishindwaje kuandika hotuba au kushirikiana na wenzake kuandika hadi alipoandikiwa na wazee wa Gerezani! Hivi Nyerere akiwa na degree yake na exposure katika international protocol and politics alikubalije kusoma hotuba kutoka kwa wazee wetu wa Gerezani! ambayo yeye hakushiriki kuiandika.

Kama aliweza kuandikiwa hotuba basi Nyerere asingekuwa na sifa za kuwa ' statesman' kama alivyjulikana. Ushahidi wa uwezo wake wa kuongoza ni pamoja na kuwa miongoni mwa viongozi wa nchi masikini za group 77. Kwa wale wanaJF wa Arusha ile hotel ya 77 ilijengwa mahususi kwa mkutano mwaka 1976 na declaration iikuwa Arusha programme for Self-Reliance and frame work for Negotiations.

Akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa frontline states kwa ajili ya ukombozi wakati huo kamati ikiongozwa na brigadier Hashim Mbita.
Mwalimu alichaguliwa kuwa katika viongozi sita kushughulikia suala la disarmament akiwa na akina Olfe Palm, Indira Gandhi n.k
Nyerere akawa mwenyekiti wa OAU katika kipindi OAU ipo katika mgogoro mkubwa sana
Nyerere akawa mwenyekiti wa south south commission
n.k n.k

Sasa najiuliza uwezo huo wa kuwa 'international figure' aliupata akiwa 'job on training' au ni kitu alichokuwa nacho. Maana anapoandikiwa hotuba na wazee wetu wa Gerezani inafikirisha kidogo.
 
Nguruvi3,

Kwa kweli lazima nikiri kuwa una juhudi sana na natambua kuwa akili yako inakataa kabisa kuamini haya ninayosema.

Insha Allah nitajitahidi kujibu maswali yale ambayo ninayo yale ambayo sina majibu unisamehe.

Kwanza lazima nikurudishe kwa taratibu uelewe kitu kimoja kuhusu hii nyaraka. Nyaraka ile hakuandikiwa Nyerere bali alikusudiwa Governor Twining katika Constitutional Development Commitee ya 1950.Kwa kuwa nimekuona swali hili limekuvuruga sana akili yako nakushauri usome kitabu cha Cranford Pratt, "The Critical Phase in Tanzania 1945 -1968, Cambridge UniversityPress kitabu hiki kimezunguza kwa undani sana na amewataja waandishi. Kitabu kinaweza kupatikana Dar University Library.

Kuhusu kupotea kwa nyaraka hii kwa kweli kama inavyokushangaza wewe hata mie na si kuwa imepotea hii peke yake nimeona jalada la Abdu Sykes, Hamza Mwapachu CCM Library Dodoma karatasi zote zimenyofolwa hazipo. Unaweza na wewe kwenda hapo uthibitishe.
Nilipata kuandika makala Africa Events, London katika miaka ya 1980s na nikaeleza kwa kirefu tatizo hili. Sasa nina maelezo mengu tu kwa watu waliohusika na historia ya TANU lakini sioni kama ipo haja kwa sasa kuyaweka bayana.

Umezungumza kuhusu nyaraka za Sykes. Hii nyaraka haipo wala watoto wa Hamza Mwapachu hawana hii document lakini wanaifahamu vizuri sana na wamemsikia baba yao akizungumza kuhusu hiyo document kwa kuisifia kuwa katika yote waliyofanya wakati wa TANU ile ndiyo ilikuwa komesha. Hata Pratt ambae yeye aliiona na kuiosoma kaisifia. Utasoma kitabu utajione mwenyewe. Haya yote yalifanyika 1950 Nyerere hayupo katika "circle" ile.

Mwisho napenda kukusitizia kuwa hayo yote mengine ambayo Nyerere aliyafanya baada ya kushika nchi hakuna wa kuyapinga na sifa hizo hakika zinamstahiki yeye peke yake.

Lakini hata kama haya hamyakubali mimi sina neno hiyo ni khiyari yenu. Ikiwa mimi nimeikataa historia rasmi na nikaandika kitabu nitakuwa na haki gani ya kukulazimisheni nyinyi mkubali historia ya wazee wangu?

Hayo mswalimengine kwa kweli nai maswali ya kawaida sana majibu wala hayahitaji nitoe mimi kuwa Nyerere kaja lini Dar es Salaam nk. nk.

Mohamed

Wana JF hii hapa chini ni sehemu ndogo ya ushuhuda wa mtu aliyeitwa Father Arthur H. Wille, M.M. alivyokutana na kumfahamu Mwalimu Nyerere. Sababu yangu ya kutoa ushuhuda huu ni kwamba huyu alikuwa na bahati ya kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na baadhi ya Wazee wa Mohamed Said. Hebu jaribuni kutafakari maneno anayosema yalitamkwa na Abdul Sykes pamoja na Abbas Sykes wakimwelezea Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika hayo mazungumzo.

Huyo ndiye Mwalimu Julius Nyerere lakini huyu anayeongelewa kwa kebehi na Mohamed Said sijui ni Nyerere yupi !

Mag3,

Hakuna wa kupinga hayo lakini usiishie hapo utakosa mengi. Fanya utafiti wa historia nzima hapo ndipo utakutana na mambo. Hivi kweli unataka tuchukulia paragraph mbili tatu ndiyo historia nzima ya harakati? Jibu ni kuwa hapana. Lazima tufanye uchambuzi na utafiti kujua nini kilikuwa nini na nani alifanya nini.

Sasa tujiulize hao wasomi hivyo ndivyo walivyosema kuhusu Nyerere na washirika wenzake.Yeye mwenyewe Nyererekasema nini?

Huu ndiyo usomi.

Ahali yangu Moh'd Said,

Hakika ni lazima ufahamu kuwa unabishana na watu na kutoa darsa kwa watu ambao mna tofauti sana kimtazamo.

Awali ya yote wewe umezama zaidi katika utafiti hususan wa Historia ya tanganyika na wenzako wapo kusikia jambo tu kutoka chanzo chochote kisicho na mashiko kisha kuja barzani na kuanza kubisha. Hakika sote tunakubali kabisa kuwa kwa mtu makini pamoja na kusikia mengi katika historia ya Tanganyika ni lazima ufanye jitihada mbalimbali za uchunguzi wa habari hizo kisha kuja na historia iliyo ya kweli na kuacha yale ya uongo na kutia chumvi.

Lakini pia kwa wasomi wa historia imejibainisha wazi kabisa kuwa Wakoloni wa Kiingereza walipokuja kuitawala Afrika ya mashariki kwa maana ya Uganda, Kenya na Tanganyika walitumia mbinu ya divide and rule.

Kwa upande wa Kenya na Uganda mbako kila nchi ilikuwa na makabila machahce sana yasio zidi 7 kwa kila nchi. Hapa walitumia ukabila na huo ndio tatizo la wazi mpaka leo kenya na uganda kuna ukabila sana na hili ni kovu la madhara ya ukoloni wa mwingireza ndani ya nchi hizo.

Kwa Upande wa Tanganyika ambako kulikuwa na makabila zaidi ya 70 walishindwa kutumia mbinu hiyo. Hivyo Tanganyika walitumia UDINI kwani kulikuwa na dini mbili kuu yaani uislam na ukristo.Hakika hicho ni kitu kinachofahamika kwa wana historia wengi sana na kwa kuwa wazungu hawa walikuwa wakristo hivyo waliubeba sana ukristo kwa kula hali kitu kilichopelekea waislam kuliona hilo na kuanza kudai uhuru wao. Hicho hakina siri kwani waislam wengi sana walishiriki kudai uhuru ukilinganisha wa wakristo ambao walikuwa wasomi.

Sasa kama wote tunaweza kukubali kuwa kenya na uganda kuna ukabila sana na wenyewe wameshaliona hilo na sasa wanajaribu kuliondoa. Vipi Tanganyika wanaficha ukweli kuwa kuna UDINI mabo ni kovu la ukoloni? Je mnafikiri mtaweza kulificha kwa kuifuta historia? lazima mjue kuwa hamuwezi kuificha wala kuifuta historia ya kweli ya nchi yenu. Kwani historia ni kama pembe la Ng'ombe.

Tuwe wa kweli na kusahihisha pale mlipoteleza ili kuleta mustakabali mzuri wa nchi yenu. Kwani hakuna mtu anayelala maisha yake yote ipo siku atazindika na hilo lipo wazi Tanganyika kwa sana. UDINI UDINI kila pahala kuanzia makazini mpaka kwenye siasa.

Poleni sana
 
Nimeuweka tena uzi huu hapa ule naona umevurugika.
Nguruvi3,

Kwa kweli lazima nikiri kuwa una juhudi sana na natambua kuwa akili yakoinakataa kabisa kuami haya ninayosema.

Insha Allah nitajitahidi kujibu maswali yale ambayo ninayo majibu yale ambayosina majibu unisamehe.

Kwanza lazima nikurudishe kwa taratibu uelewe kitu kimoja kuhusu hii nyaraka.Nyaraka ile hakuandikiwa Nyerere bali alikusudiwa Governor Twining katikaConstitutional Development Commitee ya 1950.Kwa kuwa nimekuona swali hililimekuvuruga sana akili yako nakushauri usome kitabu cha Cranford Pratt,"The Critical Phase in Tanzania 1945
-1968,"Cambridge UniversityPress kitabu hiki kimezunguza kwa undani sana na amewatajawaandishi. Kitabu kinaweza kupatikana Dar University Library.

Kuhusu kupotea kwa nyaraka hii kwa kweli kama inavyokushangaza wewe hata mie nasi kuwa imepotea hii peke yake nimeona jalada la Abdu Sykes, Hamza Mwapachu CCMLibrary Dodoma karatasi zote zimenyofolewa hazipo. Unaweza na wewe kwenda hapouthibitishe.

Nilipata kuandika makala Africa Events, London katika miaka ya 1980s nanikaeleza kwa kirefu tatizo hili. Sasa nina maelezo mengI tu kwa watuwaliohusika na historia ya TANU lakini sioni kama ipo haja kwa sasa kuyawekabayana.

Umezungumza kuhusu nyaraka za Sykes. Hii nyaraka haipo wala watoto wa HamzaMwapachu hawana hii document lakini wanaifahamu vizuri sana na wamemsikia babayao akizungumza kuhusu hiyo document kwa kuisifia kuwa katika yote waliyofanyawakati wa TAA ile ndiyo ilikuwa komesha. Hata Pratt ambae yeye aliiona nakuiosoma kaisifia. Utasoma kitabu utajione mwenyewe. Haya yote yalifanyika 1950Nyerere hayupo katika "circle" ile.

Mwisho napenda kukusitizia kuwa hayo yote mengine ambayo Nyerere aliyafanyabaada ya kushika nchi hakuna wa kuyapinga na sifa hizo hakika zinamstahiki yeyepeke yake.

Lakini hata kama haya hamyakubali mimi sina neno hiyo ni khiyari yenu. Ikiwamimi nimeikataa historia rasmi na nikaandika kitabu nitakuwa na haki gani yakukulazimisheni nyinyi mkubali historia ya wazee wangu?

Hayo maswali mengine kwa kweli ni maswali ya kawaida sana majibu walahayahitaji nitoe mimi kuwa Nyerere kaja lini Dar es Salaam nk. nk.

Mohamed

ilishikwa na Wamanyema. Hivyindivyo Wamanyema walivyokuja kuongoza siasa Tanganyika.

Kuna mahali ndugu yangu nilikuuliza hao wazee wako wa Gerezani ni "wazawa" wa Gerezani au walikuwa ni wamanyema,wanubi na wanyamwezi waliokuja Dar wakiwa ni wapagazi wa Wajerumani? Ndugu yangu ukanikalia kimya. lakini hata hapa umenitatiza, wamanyema waliongoza siasa za Tanganyika au waliongoza siasa za TANU? Maana kwa uwelewa wangu hata sehemu nyingine kulikuwa na watu wenye ushawishi mkubwa sana na huko kote ni wamanyema walikuwa "wanaongoza" siasa zao?
 
Ahali yangu Moh'd Said,

Hakika ni lazima ufahamu kuwa unabishana na watu na kutoa darsa kwa watu ambao mna tofauti sana kimtazamo.

Awali ya yote wewe umezama zaidi katika utafiti hususan wa Historia ya tanganyika na wenzako wapo kusikia jambo tu kutoka chanzo chochote kisicho na mashiko kisha kuja barzani na kuanza kubisha. Hakika sote tunakubali kabisa kuwa kwa mtu makini pamoja na kusikia mengi katika historia ya Tanganyika ni lazima ufanye jitihada mbalimbali za uchunguzi wa habari hizo kisha kuja na historia iliyo ya kweli na kuacha yale ya uongo na kutia chumvi.

Lakini pia kwa wasomi wa historia imejibainisha wazi kabisa kuwa Wakoloni wa Kiingereza walipokuja kuitawala Afrika ya mashariki kwa maana ya Uganda, Kenya na Tanganyika walitumia mbinu ya divide and rule.

Kwa upande wa Kenya na Uganda mbako kila nchi ilikuwa na makabila machahce sana yasio zidi 7 kwa kila nchi. Hapa walitumia ukabila na huo ndio tatizo la wazi mpaka leo kenya na uganda kuna ukabila sana na hili ni kovu la madhara ya ukoloni wa mwingireza ndani ya nchi hizo.

Kwa Upande wa Tanganyika ambako kulikuwa na makabila zaidi ya 70 walishindwa kutumia mbinu hiyo. Hivyo Tanganyika walitumia UDINI kwani kulikuwa na dini mbili kuu yaani uislam na ukristo.Hakika hicho ni kitu kinachofahamika kwa wana historia wengi sana na kwa kuwa wazungu hawa walikuwa wakristo hivyo waliubeba sana ukristo kwa kula hali kitu kilichopelekea waislam kuliona hilo na kuanza kudai uhuru wao. Hicho hakina siri kwani waislam wengi sana walishiriki kudai uhuru ukilinganisha wa wakristo ambao walikuwa wasomi.

Sasa kama wote tunaweza kukubali kuwa kenya na uganda kuna ukabila sana na wenyewe wameshaliona hilo na sasa wanajaribu kuliondoa. Vipi Tanganyika wanaficha ukweli kuwa kuna UDINI mabo ni kovu la ukoloni? Je mnafikiri mtaweza kulificha kwa kuifuta historia? lazima mjue kuwa hamuwezi kuificha wala kuifuta historia ya kweli ya nchi yenu. Kwani historia ni kama pembe la Ng'ombe.

Tuwe wa kweli na kusahihisha pale mlipoteleza ili kuleta mustakabali mzuri wa nchi yenu. Kwani hakuna mtu anayelala maisha yake yote ipo siku atazindika na hilo lipo wazi Tanganyika kwa sana. UDINI UDINI kila pahala kuanzia makazini mpaka kwenye siasa.

Poleni sana

Ahsante sana.

Marehemu Sheikh Mohamed Ayoub alikuwa anaiita elimu kuwa ni amana na amana lazima itolewe kwa mweyewe pindi atakapoitaka. Hawa ndiyo wenyewe wa historia ile kupitia Nyerere na sisi tuna amana yao ndiyo hii sasa tunawajeshea hapa.

Sheikh Mohamed Ayoub alikuwa akisomesha kuanzia baada ya fajr hadi kupita isha akisema hii ni amana ya watu Allah kesho ataniuliza kama nilirejesha kwa wenyewe.

Nasi tunajifunza kwa hawa masheikh zetu uadilifu.

Hakuna wa kutulaumu kuwa tumedhulumu amana ya watu.

Mohamed
 
Kuna mahali ndugu yangu nilikuuliza hao wazee wako wa Gerezani ni "wazawa" wa Gerezani au walikuwa ni wamanyema,wanubi na wanyamwezi waliokuja Dar wakiwa ni wapagazi wa Wajerumani? Ndugu yangu ukanikalia kimya. lakini hata hapa umenitatiza, wamanyema waliongoza siasa za Tanganyika au waliongoza siasa za TANU? Maana kwa uwelewa wangu hata sehemu nyingine kulikuwa na watu wenye ushawishi mkubwa sana na huko kote ni wamanyema walikuwa "wanaongoza" siasa zao?

Kigarama,

Wakati mwingine huwa sijibu kwa kuwa nimesoma kejeli na dharau maneno ya kutukana. Huamua kuepusha shari. Sheikh wangu Maalim Haruna kanifunza kama ukishaona katika mnakasha mwenzio anatoa kejeli, lugha kali basi jua kashindwa na wewe unachotakiwa kufanya ni kuondoka vinginevyo atakutoa ngeu.

Umemtukana babu yangu ndiyo maana nimekukalia kimya.

Mimi si mtu wa kupigana mieleka na kuburuzwa katika matope ya nguruwe.

Mimi muungwana.

Mohamed
 
Back
Top Bottom