Mag3,
Naomba nikusahihishe. Nyerere na Nkrumah hawakupata kukutana masomoni. Wazee wangu hawahadithii porojo. Walichokijua kuhusu Nyerere si siri kwa watu walioishi miaka ile ni vitu ambavyo vikijulikana na kila mtu. Kusema kuwa TANU ilianzishwa na Abdulwahid Sykes hili kwa wakati ule wala halikuwa jambo nyeti wala haikuwa jambo nyeti kusema kuwa Al Jamiatul Islamiyya ilitoa fedha kuchangia safari ya Nyerere UNO. Haya yote yalikuwa mambo ya kawaida na watu wakiyajua. Kamati ya ndani ya TAA ilikuwa ikiwajua "intellectuals" wake wa ni Abdu, Steven Mhando, Mwapachu, Sheikh Hassan bin Amir... Siku hizo Nyerere hajafika Dar es Salaam na hizo nyaraka zipo na ndizo nilizotumia kuandika kitabu.
Sasa tuje Tabora. Nyerere hakuasisi African Association Tabora na wala sitokuita muongo kwa kusema hivyo najua ni kosa la kawaida hukuwa na nia mbaya na hujui kwa undani historia ya Tanganyika. Hebu soma hii hapa chini:
"Tarehe 3 Machi, 1945 African Associationmjini Tabora ilifungua ofisi yake ikiwa na na viongozi wafuatao: Hamisi Simbe (Rais), Ramadhani Nasibu (Makamu waRais), M. K. Hemed (katibu), Chamngíanda Usingizi (Mwenyekiti), Fimbo Mtwana(Mweka Hazina) na Rashidi Mussa (Mkaguzi wa Hesabu). African Association, kamailivyokuwa asili ya kilabu iliyotokana nayo, ilishikwa na Wamanyema. Hivyindivyo Wamanyema walivyokuja kuongoza siasa Tanganyika. Julius Nyerere, wakatihuo akifundisha St. Maryís School, alishuhudia sherehe za uzinduzi wa AfricanAssociation.[1]Nyerere hakutambua hata kidogo wakati huo kuwa alikuwa akishuhudia sehemu yahistoria kazi yake mwenyewe ikijifungua mbele ya macho yake."
Mwaka 1947 palitokea mgomo mkubwa hapo Tabora na Nyerere hakuoenekana popote. Viongozi hawa wa mgomo huu wengi walikuwa katika AA na babu yangu, Salum Abdallah ndiye aliyeongoza huo mgomo. Sasa hapa uongo uko wapi? Uongo utakuja tu kama mtu atasema Nyerere alijihusisha na harakati hizi za wananchi na aliongoza mgomo dhidi ya wakoloni.
Umeandika vitu vingi lakini naamini kwa haya niliyoweka hapa wanaukumbi weshapata picha zetu.
Insha Allah nasubiri mengine na nitachangia pale inapobidi.
Mohamed