Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Wanaukumbi,

Kuna uzi niliambiwa kuwa mimi sijui chochote kuhusu Sablak na wenzake wa huko Meru. Nikamwaga hapa jamvini habari za Abdulwahid Sykes na Sablak kama nilvyosoma katika nyaraza za marehemu Abdu na Tanzania National Archives. Ninachosikitika ndugu zangu ni ukimya wenu.

Jamani kuweni na huruma kwani mcheza kwao hutunzwa. Hivi imekushindeni hata kusema, "Mkuu Mohamed tumekosoma." Vibaya hivyo ndugu zanguni. Nipeni motisha kidogo.

Hilo kama hamliwezi basi nipeni mji au niruhusini nitoe salam.

Mohamed

PS: Kuna mwingine akaja na Nyerere kuandika katiba nikamwaga data. Katiba ya TANU wazee wamenyanyambua ya Nkrumah. Kimya! Sisikii kitu.
MS

Sheikh MS,

Mada yako ilikuwa nzuri sana kama USINGELIINGIZA HARUFU YA UDINI..Hapo ndipo ulipochafua.
Ukishaanza tu kubagua kati ya UISLAMU na UKRISTO basi kwa Watanzania tulio wengi umeshapoteza mwelekeo.
Tungelikusoma vizuri sana kama usingeleta hoja za ubaguzi wako wa kidini.

Labda ufute kauli zako za Kidini ndipo tutaanza kukusoma vizuri na kukupa miji na majiji.
Kwa sasa mimi nasema I am sorry!
 
Kwa heshima na taadhima, Bwana Mohamed Said, ni upotoshaji wa hali ya juu kujaribu kutujuza eti ni wakazi wa mtaa wa Gerezani, Dar es Salaam walianzisha harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika. Aidha kuwapa Waislamu dhima (role) mahsusi ya ukombozi wetu, bila kuwahusisha Watanganyika wengine, ni 'distortion' ya historia ya nchi yetu.

Tanzania ya sasa ina wataalam wengi, na wengi wao ni wahadhiri katika vyuo vikuu kama Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sokoine, Dodoma, Mzumbe na Tumaini. Ningependekeza maprofesa wa historia katika vyuo vikuu hivi, watuandikie vitabu, badala ya Bwana Mohamed Said ambaye anaonekana ana madhumuni ya kutuletea ujumbe wa kidini na dhima ya Uislamu katika maendeleo yetu.

Sisi ambao tuna umri wa watu wazima, tunakumbuka matukio kama ya Japhet Kirilo aliyehutubia UNO (Umoja wa Mataifa), New York kuhusu tatizo la Ardhi la Meru Corridor, michango ya kumsafirisha Julius Nyerere kwenda UNO kudai uhuru pia na harakati za vyama vya siasa vya kikanda, kukusanya mawazo ili ujumbe wa Trusteeship Council ya UNO ulipozuru Tanganyika upate representations.

Uhuru wa nchi yetu pia ulichangiwa na wazalendo walioanzisha na kuongoza vyama vikuu vya ushirika. Mohamed Said amemtaja Paul Bomani wa Victoria Federation of Co-operative Unions. KNCU ya huko Moshi, BNCU ya huko Bukoba na shirikisho la aina hiyo hiyo huko Tukuyu chini ya uongozi wa Jeremiah Kasambala, vyote hivi vilidhihirisha umoja wa wazalendo kujikomboa kiuchumi.
 
Kigarama,

Wakati mwingine huwa sijibu kwa kuwa nimesoma kejeli na dharau maneno ya kutukana. Huamua kuepusha shari. Sheikh wangu Maalim Haruna kanifunza kama ukishaona katika mnakasha mwenzio anatoa kejeli, lugha kali basi jua kashindwa na wewe unachotakiwa kufanya ni kuondoka vinginevyo atakutoa ngeu.

Umemtukana babu yangu ndiyo maana nimekukalia kimya.

Mimi si mtu wa kupigana mieleka na kuburuzwa katika matope ya nguruwe.

Mimi muungwana.

Mohamed
MS kila ukibanwa inakuwa umetukanwa!! Mimi pia ni muungwana hebu nielewesha ni wapi nilikosa adabu kiasi cha kumtusi babu yako ili nami niombe radhi kama waungwana wote wafanyavyo. Lakini swali langu lipo palepale, hao wazee wa Gerezani wana asili (wazawa) ya Gerezani au ni Wamanyema, wanubi na Wanyamwezi waliokuja Dar es salaam wakiwa ni wapagazi wa wajerumani?

Maana siye ambao tunajua Historia ya Kariakoo tunajua hata jina lenyewe, kuna baadhi ya maandiko yanasema linahusiana na kutoholewa kwa neno la Kiingereza "Carrier Call" kwani kariakoo si Kizaramo wala si Kimanyema. Kwa hiyo wazee wa Gerezani bila shaka walikuwa ni wapagazi wa Kimanyema, Kinubi na Kinyamwezi walioletwa pwani na wajerumani.

Kama unakumbuka kwenye bandiko langu moja niliuliza kama wewe na Sheikh ponda mna undugu, FaizaFoxy akakujibia kwamba undugu wenu unajengwa kwa kuwa wewe ni pia ni MUislamu na Ponda hali kadhalika. Lakini swali langu lilikuwa ni kuhusu Umanyema.
 
Mohamed Saidi alikuwa na hoja ya msingi kuwa historia ya kutafuta uhuru haikuandikwa yote au kikamilifu, kwamba kuna mambo mengi yalifanyika na hayakuandikwa,
Mohamed Siad yupo sahihi kuandika historia yake ya Wazee wa Gerezani ambao walikuwa Waislamu, Wamanyema("sio wakuja"), Tatizo kubwa analolifanya kiuandishi ni kutaka kuifanya iwe ndio Historia rasmi ya Taifa la Tanzania/Tanganyika,
Historia ya kutafuta Uhuru wa Tanzania ilikuwa ya Watu wote, wa dini, rangi na kabila zote,

Mohamed Saidi atakuwa sahihi kama akisema anaandika Historia ya wazee wake na Waislamu wa Gerezani katika Harakati za kutafuta Uhuru,
 
MS kila ukibanwa inakuwa umetukanwa!! Mimi pia ni muungwana hebu nielewesha ni wapi nilikosa adabu kiasi cha kumtusi babu yako ili nami niombe radhi kama waungwana wote wafanyavyo. Lakini swali langu lipo palepale, hao wazee wa Gerezani wana asili (wazawa) ya Gerezani au ni Wamanyema, wanubi na Wanyamwezi waliokuja Dar es salaam wakiwa ni wapagazi wa wajerumani?

Maana siye ambao tunajua Historia ya Kariakoo tunajua hata jina lenyewe, kuna baadhi ya maandiko yanasema linahusiana na kutoholewa kwa neno la Kiingereza "Carrier Call" kwani kariakoo si Kizaramo wala si Kimanyema. Kwa hiyo wazee wa Gerezani bila shaka walikuwa ni wapagazi wa Kimanyema, Kinubi na Kinyamwezi walioletwa pwani na wajerumani.

Kama unakumbuka kwenye bandiko langu moja niliuliza kama wewe na Sheikh ponda mna undugu, FaizaFoxy akakujibia kwamba undugu wenu unajengwa kwa kuwa wewe ni pia ni MUislamu na Ponda hali kadhalika. Lakini swali langu lilikuwa ni kuhusu Umanyema.

Kaka/Dada Kigarama
inaonekana una kitu unataka kukielezea ama kukifafanua lakini msingi wako unabase kwenye majibu ya Bw. Mohamed Said
sidhani kama utapata majibu unayoyataka ni kheri wewe mwenywe ukaelezea kile unachokijua aua kukifahamu
 
Mohamed Saidi atakuwa sahihi kama akisema anaandika Historia ya wazee wake na Waislamu wa Gerezani katika Harakati za kutafuta Uhuru,
Mbona akikiri hivyo hii thread tungeomba ifungwe maana ingekuwa haina maana tena. kuna mfululizo (Series) wa vitabu vya zamani kidogo ambavyo nadhani Mohamed Said anavifahamu, vinaitwa watu mashuhuri wa Tanganyika. Kwenye Vitabu hivyo watu wanaosimuliwa wengi walifanyakazi na Kanisa Katoliki au walikuwa ni Wakatoliki, mmojawapo ni Adriano Atman ambaye alikuwa ni Daktari huko Karema kwenye mwambao wa ziwa Tanganyika.

Ukisoma masimulizi hayo bila shaka utagundua kwamba ni wakatoliki wanasimulia visa vya watu wao "mashuhuri" na wala hakuna mahali kumeandikwa watu hawa "mashuhuri" wameachwa kwenye mkondo mkuu (Main stream) wa Historia ya ya Tanganyika kwa sababu ya Ukatoliki wao.
 
Kaka/Dada Kigarama
inaonekana una kitu unataka kukielezea ama kukifafanua lakini msingi wako unabase kwenye majibu ya Bw. Mohamed Said
sidhani kama utapata majibu unayoyataka ni kheri wewe mwenywe ukaelezea kile unachokijua aua kukifahamu

Ni kweli kuna kitu nataka kukielezea lakini kwa sasa inatosha tu kufanya hivi ninavyofanya kwani Mag3 na Mwanakijiji wanafanya kazi kubwa sana ya kuleta nukuu za vitabu,machapisho, tafiti na masimulizi mbalimbali. Mimi nimeamua kufuatilia (Bila ya maagano na Mag3 na Mwanakijiji) ni kwa nini Mohamed Said huwa hajibu maswali ya msingi anayoulizwa.

Athari (Effect) na taathira (Impact) ya haya anayoyafanya MS huwezi kuiona au kuijua mpaka uwasikilize Kina Sheikh Kundecha na kundi lake au usikilize Redio kama Redio Imaani, Radio Qiblatain au Radio Quran au usome Gazeti la Al Nurru. Kuna wakati unaweza kufikiri kwamba kesho hii nchi inaweza kuripuka. Hoja ya mfumo "Kristu" inayoshabikiwa sana siku hizi mwanzilishi wake ni MS.

Ninachotaka kusema ni kwamba hawa kina MS wamefanikiwa kuwaaminisha baadhi ya waislam kwamba matatizo yoooote yamesababishwa na mfumo Kristu ambao uliasisiwa na Mwalimu Nyerere na kwa kuwagandamiza waislamu na kukiteka chama chao cha TANU. Lakin kwa upande mwingine MS na wenzake wanajisifia kwa kukubalika na wazungu ambao wakiwa na waislamu wenzao wanawaita Makafiri.

Kazi ya nukuu nimewaachia Mag3 na Mzee Mwanakijiji ambao wanaifanya kwa uzuri sana.
 
Kweli kabisa nyerere aliasisi ubaguzi wa kidini ndio maana leo wakatoliki wanataka kumpa awe mtakatifu amefanyia kanisa gazi kubwa kuliko taifa..letu na watu wake
 
Wanaifanya "uzuri sana" kwa kunukuu vitu vya visivyokuwepo? Na ukiwabana na ukweli, post zinachakachuliwa! Au hujaisoma post #162 ya mwanakijiji? Iliyojibiwa na post #167 na Mohamed Said. Naomba zisome halafu useme kazi nzuri ni ipi?

Kisha baada ya hayo, Jee? Wazee wa Gerezani, waasisi wa siasa za kudai madaraka, hawana haki ya kuandikwa kwenye historia? Au Mohamed Said anafanya makosa kuwaandika?

Tatizo lenu ni lipi haswa?, maana mara hiki mara kile.

Jee, tukisema Nyerere alifundishwa kucheza dansi na wazee Gerezani nalo mtapinga?
 
Ni kweli wazee wa gerezani walimfunduisha Nyerere kucheza dance na Nyerere akawafundisha siasa na mbinu za kupigania uhuru na hatimaye ukapatikana.

Nyerere kawatoa wazee wa gerezani kutoka TAA ya kilabu cha kupeana chai hadi kuwa TANU chama cha siasa!
 
Kweli kabisa nyerere aliasisi ubaguzi wa kidini ndio maana leo wakatoliki wanataka kumpa awe mtakatifu amefanyia kanisa gazi kubwa kuliko taifa..letu na watu wake
Kuasisi udini kivipi yaani kanisa lake kwa imani ya dini yake kutaka kumpa hadhi ya utakatifu ni udini? Mbona Mwinyi anaitwa Alhaji kwa sababu ya kwenda kuhiji Maka huo ni udini?

Kazi gani aliyolifanyia Kanisa ni ipi. Kutaifisha shule za kanisa na Hospitali zao? Udini Mzee Mwanakijiji alishawahi kuuelezea vizuri sana huko nyuma. Udini ni ile hali ya mtu kufanya mambo kwa upendeleo kwa misingi ya dini bila ya kujali sifa hitajiwa. Kama kuna waalimu wawili wenye sifa sawa wanataka kuajiriwa wewe ukamchagua mmoja hata kama hana sifa ila kwa sababu ni wa dini yako huo ndiyo udini.

Mtu kutetea dini yake si udini, mtu kuswali swala tano au kuwa mlokole si udini bali ni ucha mungu. Udini ni kutenda mambo kibaguzi kwa misingi ya dini yako. kwa mfano kama mtu anaamini kwamba waislamu wote wako sahihi na wakristo wote ni wakosaji kwa sababu tuu ya dini yao huo ndiyo udini.
 
Mkuu udini wa nyerere uko wazi..na uko recored soma vitabu vya Mohamed Said utaona alivyofanya kazi kidini na si kwa ajili ya taifa..

Pamoja na definition uliyotoa..udini ni hali ya mtu kumchukia mtu mwingine na mafanikio yake kwasababu ya dini yake..

Sasa nyerere alitaifisha shule na hosptiali za waislamu zote pamoja na za wakristo lakini akawaachia wakristo baadhi ya seminari. zao lakini kwa waislamu hakuacha hata moja ...

Nyerere aliwapa wakristo nafasi ya uongozi hasa wizara ya elimu (recored kwenye books) si kwasababu ya uweledi wake ila ukatoliki wake ili asaidie wakristo wasome zaidi kuliko waislamu for 23 years..

Nyerere alifuta taasisi za kidini za kiislam (recorded) zeney mafanikio makubwa na mtandao mkubwa wa kifedha na matawi kwa ajili ya kuogopa kutanuka kwa uislam zaidi ya ukristo (udini huo)

Nyerere alinyima taasisi za kiislam kutopata misaada kutoka nje wakati akiacha taasisi za kanisa kupokea misaada hiyo kwa chuki zake na uwoga wa kukua uislam,

Alifuta mahakama ya kadhi etc..list ni kubwa mkuu..
 
Wanaifanya "uzuri sana" kwa kunukuu vitu vya visivyokuwepo? Na ukiwabana na ukweli, post zinachakachuliwa! Au hujaisoma post #162 ya mwanakijiji? Iliyojibiwa na post #167 na Mohamed Said. Naomba zisome halafu useme kazi nzuri ni ipi?
Kwanza kabisa huwa sielewi kama wewe FaizaFoxy umepotoshwa na MS au ndiyo mko pamoja kweny kazi ya kupotosha. Maana ya majibu na maelezo ni vitu viwili tofauti kabisa.Mwanakijiji aliuliza swali MS akatoa Maelezo bila ya kuwa na jibu ndani yake. siyo kila maelezo ni majibu.

Kisha baada ya hayo, Jee? Wazee wa Gerezani, waasisi wa siasa za kudai madaraka, hawana haki ya kuandikwa kwenye historia? Au Mohamed Said anafanya makosa kuwaandika?
Hakuna makosa kuandika historia ya hawa waasisi wa siasa za kudai madaraka na siyo kudai UHURU.

Tatizo lenu ni lipi haswa?, maana mara hiki mara kile.
Mada ni moja lakini ina vipengele vyake vingi tu.

Jee, tukisema Nyerere alifundishwa kucheza dansi na wazee Gerezani nalo mtapinga?
Suala la kucheza dansi ni suala la kibinafsi zaidi. Mimi mwenyewe sijui kucheza dansi ,nije unifundishe kucheza ili kina MS wa baadaye waje kuandika kwamba nilifundishwa kucheza Dansi na FaizaFoxy!!
 
Kweli kabisa nyerere aliasisi ubaguzi wa kidini ndio maana leo wakatoliki wanataka kumpa awe mtakatifu amefanyia kanisa gazi kubwa kuliko taifa..letu na watu wake

Hiko ni wazi na kweli tupu. Nyerere kaiacha hii nchi hohehahe, senti mbovu ya kigeni BOT hakuna, imewashwa moto kuficha yaliyoficha. Lakini on the other side, Kanisa katoliki leo Tanzania ni kanisa kubwa kuliko lingine lolote lina hodhi ardhi kuliko taasisi yoyote baada ya Serikali.

Utakatifu ndio huo, kwa lipi la kuifanyia nchi awe mtakatifu?

Ni kwa yale aliolifanyia kanisa ndio litampelekea kupewa utakatifu, na muujiza ni kigezo kimojawapo cha kupewa utakatifu, Nyerere watamtungia muujiza upi? Tafakari.
 
Kwanza kabisa huwa sielewi kama wewe FaizaFoxy umepotoshwa na MS au ndiyo mko pamoja kweny kazi ya kupotosha. Maana ya majibu na maelezo ni vitu viwili tofauti kabisa.Mwanakijiji aliuliza swali MS akatoa Maelezo bila ya kuwa na jibu ndani yake. siyo kila maelezo ni majibu.

Hakuna makosa kuandika historia ya hawa waasisi wa siasa za kudai madaraka na siyo kudai UHURU.

Mada ni moja lakini ina vipengele vyake vingi tu.

Suala la kucheza dansi ni suala la kibinafsi zaidi. Mimi mwenyewe sijui kucheza dansi ,nije unifundishe kucheza ili kina MS wa baadaye waje kuandika kwamba nilifundishwa kucheza Dansi na FaizaFoxy!!

Kuwa Nyerere ntakufundisha.

Hilo jibu na swali unalolileta ni tofauti kabisa na yaliyomo kwenye hizo post, hamuoni haya kuchakachuwa? jee mmesha chakachuwa kama mlivyopinda la kuwaunganisha wazee wa gerezani?
 
Kwa heshima na taadhima, Bwana Mohamed Said, ni upotoshaji wa hali ya juu kujaribu kutujuza eti ni wakazi wa mtaa wa Gerezani, Dar es Salaam walianzisha harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika. Aidha kuwapa Waislamu dhima (role) mahsusi ya ukombozi wetu, bila kuwahusisha Watanganyika wengine, ni 'distortion' ya historia ya nchi yetu.

Tanzania ya sasa ina wataalam wengi, na wengi wao ni wahadhiri katika vyuo vikuu kama Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sokoine, Dodoma, Mzumbe na Tumaini. Ningependekeza maprofesa wa historia katika vyuo vikuu hivi, watuandikie vitabu, badala ya Bwana Mohamed Said ambaye anaonekana ana madhumuni ya kutuletea ujumbe wa kidini na dhima ya Uislamu katika maendeleo yetu.

Sisi ambao tuna umri wa watu wazima, tunakumbuka matukio kama ya Japhet Kirilo aliyehutubia UNO (Umoja wa Mataifa), New York kuhusu tatizo la Ardhi la Meru Corridor, michango ya kumsafirisha Julius Nyerere kwenda UNO kudai uhuru pia na harakati za vyama vya siasa vya kikanda, kukusanya mawazo ili ujumbe wa Trusteeship Council ya UNO ulipozuru Tanganyika upate representations.

Uhuru wa nchi yetu pia ulichangiwa na wazalendo walioanzisha na kuongoza vyama vikuu vya ushirika. Mohamed Said amemtaja Paul Bomani wa Victoria Federation of Co-operative Unions. KNCU ya huko Moshi, BNCU ya huko Bukoba na shirikisho la aina hiyo hiyo huko Tukuyu chini ya uongozi wa Jeremiah Kasambala, vyote hivi vilidhihirisha umoja wa wazalendo kujikomboa kiuchumi.

Kilasara,
Umesema kweli kabisa nakuunga mkono kwa hoja yako wala sina ubishi.

Mimi niliandika historia ya wazee wangu baada ya kuona historia hiyo imepuuzwa.

Kitabu changu kinaitwa, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika," Minerva Press, London 1998.

Ndani nimeeleza yale ambayo wengi hawakuwa wanayajua. Kitabu kilifanyiwa review katika Cambridge Journal of African History na John Iliffe na katika majarida mengine Ulaya na Marekani. "The East African" walikifanyia "seralisation" mwezi Desemba 1998 kwa majuma matatu mfululizo. Nimealikwa kwingi Ulaya, Afrika na Marekani kufanya mihadhara kutokana na kitabu hiki.

Wala haijanijia kuwa hii ndiyo "the histrory" hata kidogo mara nyingi nasisitiza hili. Huu ni mchango wangu kwa wazee wangu ambao wengi wamekufa wakidhani kuwa historia yao haitakujafahamika na kizazi kijacho.

Nawahimiza wenzangu kama mnacho ambacho hakipo katika historia huu ndiyo wakati wa kuandika ili tuhifadhi historia ya nchi yetu. Sasa hao uliowataja walimu wa vyo vikuu walishindwa siku nyingi kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika. Hebu soma hii hapa chini:

"Mwaka wa 1974 Rais Julius Nyererealiwatwisha Chuo Cha Kivukoni jukumu la kuandika historia ya TANU. Chuo hikikilianzishwa kama shule ya kuwasomesha makada wa TANU katika mambo ya itikadi,propaganda na uhamasishaji umma wakiiga mfano wa Ruskin College ya Uingereza.Chuo Cha Kivukoni kwa ajili hii kisingeweza kufanya utafiti huru walakuandika historia sahihi ya TANU. Mwaka1976, katika mkutano wa kumi na sita wa TANU Nyerere alisisitiza tena kuandikwakwa historia rasmi ya TANU. Lakini historia rasmi ziku zote zimekuwa zakupotosha kama anavyoeleza Maslov:"Kuwafuta watu waliopita ni kasoronyingine katika maandishi yanayohusu historia ya Chama Cha Kikomunisti chaUrusi. Katika vitabu na makala za utafiti, kama vile ni sheria, watu waliomuhimu katika historia huwa wanaorodheshwa katika katika ëorodhaí na baadhi yaohawatajwi kabisa.[1]Historia ya Chama Cha Kikomunisti cha Urusi haina tofauti na historia ya TANU.Mwaka 1985, Rais Nyerere alipokuwa anamtunukia digrii ya heshima BasilDavidson, alitoa changamoto kwa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kuandika historiaya kweli ya Tanzania. Mwaka 1988, katika sherehe ya kuadhimisha miakathelathini ya Azimio la Tabora, Nyerere aliwasifu wanachama wa mwanzo wa TANUambao walijiunga na chama kati ya mwaka 1954 na mwaka 1958. Nyerere alisema:"Hicho kilikuwa kipindi kigumu sana katika historia ya Chama chetu na ni watuwachache sana walikuwa na ujasiri wa kujiunga na chama na kukifanyika kazií." [1]Jambo la kustaajabisha katika kauli ya Nyerere ni kuwa wakati yeye anawasifuwatu waliojiunga na TANU katika ya mwaka wa 1954 na 1958 yeye binafsihajawaenzi wale ambao siyo tu walijiunga na TANU bali ndiyo waasisi wa TANUyenyewe. Kwa hali hii inakuwa vigumu kuamini kama kauli yake ilikuwa inatokakwenye dhati ya nafsi yake.Katika kuunga mkono kauli ya Nyererekuhusu kuwakumbuka mashujaa wa uhuru wa Tanganyika, na kwa kutaka kuitikia ilechangamoto yake ya kutaka historia ya kweli ya TANU andikwe kama alivyosemamwaka wa 1974 na 1985, mwandishi alichapisha makala katikaAfrica Events [1]ambayo Abdulwahid na wazalendo wengine wa TANU zilielezwa habari zao. Katikamakala yale mwandishi alifanya jambo ambalo kabla yake lilikuwa halijafanywa namwandishi yeyote. Mwandishi alisema kuwa Waislam ndiyo walikuwa mstari wa mbalekatika kupigania uhuru. Wakati ule ilikuwa mwiko kabisa kunasibisha Uislam auWaislam na harakati za kudai uhuru. Mwandishi alipewa kemeo kali kutoka kwamwanahistoria wa CCM, Dr Mayanja Kiwanuka,[1] kiongozi wa jopo lililoandikaHistoria ya Chama Cha TANU 1954-1977, kitabu kinachoeleza historia rasmi yaChama. Mwanahistoria wa Chama ChaMapinduzi alikuwa na haya ya kusema dhidi ya mwandishi:"... makala inadai kuwa ingawa WaislamTanzania walitoa mchango muhimu katika harakati za kudai uhuru, zipo juhudi zamakusudi za kufifilisha mchango wao. Kutokana na hayo, makala nzima ina nganoili kuipa nguvu fikra zake, zaidi kwa kutaja majina ya wazalendo wa TANU ambaoimetokea kuwa ni Waislam. Ukuu wa TANU, na hasa ukuu wa kiongozi-muasisi wake,Mwalimu Nyerere, ni kuwa, baada ya muda mfupi tu toka kuasisiwa (TANU), ikawezakuwaunganisha watu katika vuguvugu la utaifa lenye nguvu, lau kama watu haowalikuwa tofauti kwa kabila, utamaduni na dini zao. Nia ya Said ni kupandiza chuki,kwa bei yoyote ile, ukweli kwake yeye si kitu muhimu."[1]Hizi ndizo fikra za Kiwanuka, ambaealiaminiwa na CCM kusimamia utafiti na uandishi wa historia mahsusi ya TANU.Kilichomkera ni kusema kuwa Waislam ndiyo waliokuwa mstari wa mbele katikakudai uhuru wa Tanganyika. Kwa ajili ya kuwataja Waislam, makala ya utafitiikawa sawasawa na ngano, yaani hadithi. Mwandishi akatuhumiwa kusema uongo.Kiwanuka hakuweza kuuepuka msimamo wa Chama wa kutia mkazo katika kumsifu mtummoja, Nyerere peke yake katika kuasisi TANU - "Ukuu wa TANU, na hasa ukuu wakiongozi-muasisi wake, Mwalimu Nyerere." Wakati akiandika maneno haya Kiwanukaalikuwa Katibu Msaidizi katika Idara ya Propaganda na Uhamasishaji Umma katikaChama Cha Mapinduzi. Mwandishi alijibu mashambulizi ya Kiwanuka kwa kuelezakuwa yote aliyoyaandika ni matokeo ya utafiti.[1] Kufuatia majibu hayaKiwanuka aliandika fedhuli kwa kumuita mwandishi "mwanahistoria asiye kuwa nakimo" na akamtisha mwandishi kwa kuapa kuwa endapo atajaribu kuibadilishahistoria ya Tanzania atamwandama yeye na ndugu zake.[1] Baada ya mjadala huu bainaya mwandishi na Kiwanuka, watu wengi walijitokeza kumuunga mkono mwandishi nahuo ndiyo ukuwa mwisho wa ubishi. Kingine cha kustaajabisha ni kuwa anaeiweka historia kwa kufanya utafitina kuiandika sawa, ndiyo anayetishwa na wale waliopotosha historia wanaachiwawaendelee kuipotosha historia na kuifanyia fisadi kadri watakavyo. Kiwanukaakiwa mwanafunzi Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, aliandika tasnifu kuhusuuhusiano wa Waislam na Wakristo Tanzania. Tasnifu hii ni muhimu kwa kilamwanafunzi wa historia ya uhuru wa Tanzania, hasa miaka kumi ya mwanzo baada yauhuru. [1]Kutokana na makala za mwandishizilizokuwa zinaitafsiri upya historia ya Tanzania kwa kuuweka mbele Uislam kamaitikadi ya kupinga dhulma ya aina yoyote pamoja ukoloni, Fr. Peter Smith,mtaalamu wa uhusiano kati ya Waislam na Wakristo katika Kanisa Katoliki, katikajuhudi za kupinga ukweli huo, alijibu kwa makala mbili.[1] Katika makala mojaalisema: "Kuna historia mpya zinazoandikwa hivisasa zinazojaribu kuonyesha kuwa vuguvugu la mwanzo kuiunga mkono TANU lilikuwavuguvugu la Kiislam. Ukweli ni kuwa Waislam walihusika, halikadhalika Wakristoñ vuguvugu lilikuwa la utaifa, ingawa halikuwa la kupinga dini, lilikuwa nivuguvugu la kisekula."[1].Father Smith wa Kanisa Katoliki na CCMinaelekea wote wana mawazo sawa katika utata huu wa historia ya Waislam nauhuru wa Tanganyika.[1]Wote wawili, Kiwanuka, mwanahistoria wa CCM na Padri Smith, mtaalamu wa Uislamkatika Kanisa Katoliki wanatoa mawazo yao binafsi. Hawaangalii historiainadhihirisha ukweli gani. Hakuna anaekataa kuwa Wakristo walikuwepo. Ukweli nikuwa majina ya Kikristo yapo katika historia ya uhuru wa Tanganyika. Lakiniwalikuwa ni wachezaji wa pembeni si katikati ya jukwaa. Kitabu hiki kimeonyeshanafasi ya Waislam na Uislam katika kupambana na ukoloni, mchango wao katikakuunda TANU, kukipa chama wanachama na katika kuutumia Uislam wenyewe kamaitikadi ya mapambano. Baraza la Wazee wa TANU Jimbo la Dar es Salaam chini yamwenyekiti wake wa kwanza Sheikh Suleiman Takadir lilikuwa na wajumbe mia mmojana sabini na tatu, wote Waislam.[1]Kutokana na Kiwanuka, mwandishi katikakumbukumbu ya miaka ishirini toka Abdulwahid afariki dunia, aliamua kuandikahistoria fupi ya maisha yake.[1] Abdulwahid ili kukomesha upinzani wote kwawakati ule na hapo baadae kuhusu nafasi ya Abdulwahid katika kuasisi TANU nakudai uhuru wa Tanganyika. Makala hii ilifuatiwa na kumbukumbu iliyotolewa nawatoto wake katika gazeti la CCM - Uhuru, na gazeti la serikali ñ Daily News. [1]Wahariri wa magazeti ya Chama na serikali waliposoma wasifu wa Abdulwahidtayari wakawa wameshatatizwa na habari zilizokuwa katika kumbukumbu ile. Tatizokubwa lilikuwa habari zilizoandikwa katika kumbukumbu ile zilizokuwazinahusisha jina la Abdulwahid na matukio muhimu katika historia ya Tanganyika.Mhariri wa Daily News, Reginald Mhango, alimpigia simu mtoto wa Abdulwahid,Kleist na kumweleza kuwa hatoweza kuchapisha kumbukumbu ile hadi amepata idhinikutoka Dodoma, Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi. Hakijulikani kilichofanyikalakini kwa bahati nzuri kumbukumbu zote mbili zilichapishwa na kutokea katikamagazeti yote, ya chama na serikali siku ya pili yake baada ya kufanya mabadilisho fulani fulani. Mwaka a 1986, miaka miwili kabla, baadaya takriban miaka ishirini na tano ya ukimya, Ally Sykes alikubali kufanyamajadiliano na mwandishi wa Kiingereza Paula Park. Park akachapisha majadilianoaliyofanya na Ally Sykes kuhusu ukoo wa Sykes na mchango wao katika historia ya uhuru wa Tanganyika.[1]Makala ile iliposomwa Ally Sykes akawa anapata simu kutoka kwa marafiki zake nakwa wafanyabiashara wenzake wakitaka uhakika kama yale yaliyoandikwa katikagazeti lile kweli yeye ameyasema. Haukupita muda mrefu, maofisa wa Idara yaUhamiaji walimtembelea Park na kumuomba aondoke nchini. Hivi ndivyo mambo yalivyo na mwandishiamekuwa akiulizwa maswali mengi na watu mbalimbali kuhusu ukweli ya yalealiyokuwa akiyaandika katika mchango wa Abdulwahid katika uhuru wa Tanganyika.Wasiwasi huu umekuwapo lau kama mwandishi amefanya rejea nyingi na za kutoshakutoka magazeti ya zamani, vitabu,majarida na kumbukumbu zingine za wakati waukoloni. Juu ya wasiwasi wote uliokuwapo hakuthubutu kujitokeza yeyote kupingayake mwandishi aliyoandika kuhusu historia ya Abdulwahid katika TANU na uhuruwa Tanganyika. Hata mwanahistoria wa CCM hakunyanyua kalamu yake. Hali hii yaCCM kuikataa historia yake na wakati huo huo ikidai kuwa haijaweza kuihifadhihistoria yake inatoa mvuto fulani kwa watafiti kutaka kujua kulikoni. Ukweli wakuwa CCM imeandika historia yake lakini hapo hapo imeonekana upo upungufumkubwa unaweka wazi suala la utafiti ufanywe na watafiti huru ili ukweli upatekujitokeza. Somo la historia ya uhuru wa Tanganyika bado lipo wazi kwa utafitizaidi."

Mohamed
 
MOHAMED S,unaingia katika vitabu vya historia kama muasisi wa "MFUMO KRISTO"

SoA,

Mgunduzi wa mfumokristo ni marehemu Sheikh Malik na watu walisaidia sana kuwaamsha Waislam ni marehemu Mussa Mdidi na Burhani Mtengwa na vijana wengine wa Warsha.

Hao mimi ni walimu wangu nimejifunza mengi kutoka kwao.

Mohamed
 
Sasa nyerere alitaifisha shule na hosptiali za waislamu zote pamoja na za wakristo lakini akawaachia wakristo baadhi ya seminari. zao lakini kwa waislamu hakuacha hata moja ...

Naomba uwe mkweli, tutajie hizo shule na hospitali za Waislaam alizotaifisha Mwalimu Nyerere halafu tukupe somo. Wakati wa kupigania uhuru kulikuwa na shule maarufu tatu za Sekondari nazo ni Tabora, Pugu na Minaki. Kwa bahati zote zilijengwa katika majimbo anayodai Mohamed Said yaliachwa nyuma kielimu na wakoloni.
  1. Tabora ilikuwa ya serikali
  2. Pugu ilijengwa na Wakatoliki - St. Francis College
  3. Minaki ilijengwa na Waprotestant - St. Andrews College
 
Mkuu udini wa nyerere uko wazi..na uko recored soma vitabu vya Mohamed Said utaona alivyofanya kazi kidini na si kwa ajili ya taifa..
Watu wengine humu ndani hupenda kujadili viwango vya elimu vya wenzao, lakini mimi napenda kujadili viwango vya utashi na dhamira njema vya wachangiaji wenzangu. Hivi kama Nyerere kweli angekuwa na Udini angekubali kumwachia madaraka ya Urais wa Tanzania Alhaji Ally Hassan Mwinyi Mwaka 1995? Ilikuwaje huyu Nyerere mdini adondoshe chozi pale aliposema "watu kama Rashid hawazliwi kila mara, labda mara moja kila baada ya Karne" Hivi Lowassa si Mkristo. Ilikuwaje Nyerere mdini amkubali Salim Ahmed Salim dhidi ya Lowassa?

Pamoja na definition uliyotoa..udini ni hali ya mtu kumchukia mtu mwingine na mafanikio yake kwasababu ya dini yake..
Hivi Dibangula aliposema Yesu si mwana wa Mungu alikuwa ni mdini au alikuwa anatetea dini yake? Waislamu wanapomchukia Salman Rushdie ni wadini?

Sasa nyerere alitaifisha shule na hosptiali za waislamu zote pamoja na za wakristo lakini akawaachia wakristo baadhi ya seminari. zao lakini kwa waislamu hakuacha hata moja ...
Waislamu walikuwa na shule ngapi zilizotaifishwa? Wakristo walikuwa na shule angalau kwenye kila mkoa na nyingine zilikuwa ndani ya maeneo ya kuabudia ya makanisa. Idadi ya shule za kanisa zilizotaifishwa na Nyerere ni mara tatu ya zile za kiislamu zilizotaifishwa.
Nyerere aliwapa wakristo nafasi ya uongozi hasa wizara ya elimu (recored kwenye books) si kwasababu ya uweledi wake ila ukatoliki wake ili asaidie wakristo wasome zaidi kuliko waislamu for 23 years..
Hivi kina Prof. Kapuya, DR.. Asharose na wengineo walisoma enzi za Mwalimu au Mwinyi?

Nyerere alifuta taasisi za kidini za kiislam (recorded) zeney mafanikio makubwa na mtandao mkubwa wa kifedha na matawi kwa ajili ya kuogopa kutanuka kwa uislam zaidi ya ukristo (udini huo)
Hata wingi wa makanisa umeanza enzi za Mwinyi. Lakini si kila taasisi ya kiislamu ilifutwa. Na hakuna mahali pameandikwa hata kwenye hivyo vitabu vya Mohamed Said unavyotuchagiza tuvisome ambamo kumeandikwa kwamba ni Nyerere yeye mwenyewe aliwaambia "futeni hii taasisi ya Kiislamu"

Nyerere alinyima taasisi za kiislam kutopata misaada kutoka nje wakati akiacha taasisi za kanisa kupokea misaada hiyo kwa chuki zake na uwoga wa kukua uislam,
Alizinyimaje kupata msaada kutoka nje. Tangu Nyerere aondoke madarakani ni miaka 26 sasa, tofauti ni nini?

Alifuta mahakama ya kadhi etc..list ni kubwa mkuu..
Hili mjadala wake ni Mreeeeeeeefu sana!!
 
Back
Top Bottom