makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,218
Wanaukumbi,
Kuna uzi niliambiwa kuwa mimi sijui chochote kuhusu Sablak na wenzake wa huko Meru. Nikamwaga hapa jamvini habari za Abdulwahid Sykes na Sablak kama nilvyosoma katika nyaraza za marehemu Abdu na Tanzania National Archives. Ninachosikitika ndugu zangu ni ukimya wenu.
Jamani kuweni na huruma kwani mcheza kwao hutunzwa. Hivi imekushindeni hata kusema, "Mkuu Mohamed tumekosoma." Vibaya hivyo ndugu zanguni. Nipeni motisha kidogo.
Hilo kama hamliwezi basi nipeni mji au niruhusini nitoe salam.
Mohamed
PS: Kuna mwingine akaja na Nyerere kuandika katiba nikamwaga data. Katiba ya TANU wazee wamenyanyambua ya Nkrumah. Kimya! Sisikii kitu.
MS
Sheikh MS,
Mada yako ilikuwa nzuri sana kama USINGELIINGIZA HARUFU YA UDINI..Hapo ndipo ulipochafua.
Ukishaanza tu kubagua kati ya UISLAMU na UKRISTO basi kwa Watanzania tulio wengi umeshapoteza mwelekeo.
Tungelikusoma vizuri sana kama usingeleta hoja za ubaguzi wako wa kidini.
Labda ufute kauli zako za Kidini ndipo tutaanza kukusoma vizuri na kukupa miji na majiji.
Kwa sasa mimi nasema I am sorry!