FF,Unajua ikiwa mtu utaishi karibu na hawa watu utajua jinsi walivyokuwa hawatujui kabisa. Mimi binafsi mara chungu mzima nimejitahidi kuwaleza Dar es Salaam ilivyokuwa, wazee wetu walikuwa watu wa namna gani. Nini ustaarabu wa watu wa pwani na dini ya Kiislam. Mengi mengi sana.
Wameaminishwa kuwa Waswahili hawawezi kitu ndiyo sasa hiyo historia ya "superman" sasa leo kusikia kumbe mambo hayakuwa kama walivyoelezwa mshtuko waliopata ni mkubwa sana. Mimi hili nimelishuhudia hapo Dar es Salaam University nawaambia babu yangu alikuwa katika harakati hizi miaka mingi sana kabla. Nawaeleza habari za Mzee Kleist wamepigwa na butwaa.
Basi hiyo imekwenda hadi katika uhusiano wa mtu kwa mtu. Haya mie nakutananayo kila siku. Umeshuhudia humu ukumbini wewe mwenyewe shida walizonazo hawa ndugu zetu.Leo kuhadithia habari hizi zishakuwa ati ni "porojo."Hawa wakiishi na watu na watu hawa ndiyo wazee wetu sisi.Mohamed
Mzee Said unapoteza uelekeo na pengine vijana wamekuvuta na kuingia katika mtego wao.
Sidhani kuwa umeweka makala hapa ili watu wasome tu, vinginevyo wangesoma vitabu na magazeti. Elewa kuwa kuulizwa maswali au hoja si matusi wala upungufu wa kuelewa ni weledi wa fikra na tashwishi ya kufahamu.
Watu wamesema makala zako zina lengo la udini, umejaribu kukanusha mara nyingi bahati mbaya unajisahau vijana wanapokushangilia na kujikuta unatoa siri za moyoni. Hiyo haina shida na ni haki kabisa kwa mtazamo wa kila mmoja, lakini inaondoa thamani ya kile unachotaka kukilingania kwa wasomaji.
Unaposema hawa watu, ni akina nani? makala zako inawezekana hazijasomwa na waislam na hata kama wamesoma pengine hawakuweza kuzielewa kuliko watu wengine. Kwahiyo si haki kusema hawa watu, hiyo ni kuligawa taifa na sijui kama ndio lengo la vitabu vyako.
Wale wanaosema porojo wana hoja kwasababu hutaki kujibu maswali yanayoonekana kukinzana na uandishi au dhima yako.
Umesema(ushahidi upo) kwa maneno yako siyo 'only credible version' na ukaongezea kuwa 'una mapungufu uliyoyafanya' sasa unapoelewa hivyo kwanini usiwe tayari kukubaliana au kutokubaliana kwa hoja? badala ya name calling, despise na matusi ya kifasihi ingawa wewe hupendi kutusiwa hata kidogo. This kind of narcism and hatred haipo katika uislam.
Kupitia mnakasha huu watu wamejifunza mengi si kutoka kwako bali kwa kila mmoja alivyojaaliwa. Haina maana waliochangia sio waislam au ni waislam tu bali ni watanzania. Kwa kauli zako ni uungwana kama utaomba radhi kwa jitihada za kuwagagawa watu 'wale na sisi'
Mzee Said, kama maswahaba walitofautina, maimam wakatofautiana hadi kukatokea akina Shafi, Hanafi, Hambali, Maliki n.k lakini bado hawakudhihakiana au kutengana kwa' wale na sisi', vipi jamii iliyojaa mchanganyiko kama yetu ishindwe kuwa na tofauti?
Najaribu kufuatilia communication skills yako halafu nailinganisha na ya akina marhum Didat, with all due respect I draw a clear contrast.
Na mwisho naomba usiamnishe watu kuwa unawaambia ukweli, ukweli mtupu. Ni vema usema unaandika unachokifahamu. Kama maneno yako ni kweli tupu inakuwaje useme'not only credible version' na kukubali mapungufu?
Tafadhali jibu maswali unayoulizwa na si kuzunguka zunguka. Unapokataa kujibu maswali unazidi kuondoa credibility ya makala zako na ikifika hapo tunajiuliza kwanini vitabu vyako vitumike katika mtaala wa shule yoyote!
Ni mwalimu au profesa gani anayeweza kutumia reference ya mwandishi ambayo imeficha baadhi ya ukweli,ina hisia za chuki, inatuhuma zisizothibitika na kwa upande mwingine mwandishi ima hataki au hawezi na pengine hajui kwanini ameandika kifungu fulani.
Ahsante