Alaa ukiitwa kwa kazi uloifanya imekuwa tusi? unachojaribu kufanya hapa kitu gani haswa kama wewe una hakika na kazi yako ambayo kwetu sisi ni matusi makubwa unashangaa kipi?Kama hukuelewa ninachozungumza ustaarabu ni kuomba ufafanuzi sio kunitukana.
Katika sentensi yangu hapakuwa na tusi lakini haya tuwaachie wanaukumbi waamue
kati yetu nani katukana.
Mohamed
Hili sio swala la chuki hata kidogo,inaonekana somo la MS halijaeleweka.
Nyerere mpaka Mwinyi ana stahafu bado ananguvu nchii ametuchagulia mpaka rais wa awamu ya tatu kama mmesahau na alihaidi kabla ya kwenda London kutibiwa kwamba angemwona hata rais wa awamu ya nne.
Mzee MS,amewaambia kwa fumbo hapo juu "mwinyi alikuwepo tu ila "watu" walisha form a mechanism ya kuendesha mambo yao
Sanda Matuta,
Hali ya Mwinyi ilikuwa kama Insha Allah utakavyoona hapo chini:
"This was the time that Mwinyi confided to Prof. Malima that there werepeople within the office of the president who had duplicates keys to hisdrawers and were stealing documents. Mwinyi, Prof. Malima confided to my informantlooked scared and while he was reporting this to Prof. Malima, Mwinyi wasspeaking in very low tones, whispering as if fearing his office was bugged.Prof. Malima advised President Mwinyi to transfer that entire staff and bringin new people who would have allegiance to him. At this time Prof. Malimastarted to receive hate mails which he turned over to the Intelligence forinvestigation but nothing came out of those investigations."
Mohamed
Mkuu Mkandara,
Heshima kwako,miaka michache iliyopita nilipojiunga na JF nilijaribu kwa mbali ku-rise issue hii ya Nyerere ukani crash pamoja na wachangiaje wengine na kuniambia nilikua na "labda Nyerere kuna kitu alinifanya mimi binafsi au familia yangu" na kwakua sikua na utafiti wowote (kama Muhamed Said) nikaliwacha jambo lile.Nilijaribu kuleta kile ambacho nikua nikielezwa na kukisikia.
Ila kama lilivyo kila jambo dunia lazima litapata wa kulisemea hata kama mbele zaidi miaka mia,wakati wake umefika sasa kwa jambo hili.Labda uniambie wewe hukutani na maneno ya namna ya Muhamed Said huko uliko ila ni kitu cha kawaida sana wanapokaa watu wa imani sawa kuzungumzia mustakabari wa imani yao.
Usipate shida sana kutetea jambo lililo wazi muda ni muafaka upande ule mwingine kujua kwamba upand e huu wanalijua hili na wanalizungumza labda itasaidia kupunguza ama kuondoa tofauti hizi.
As for Muhamed Said,yeye ni mtu mdogo sana kuleta machafuko kwenye nchi hii,na nina imani hiyo sio nia yake kuletea vurugu baina yetu ila yafaa kuzungumza ile tupate common ground which will be based on mtual understanding for a lasting peace kama mababu zetu walivyo ishi zamani.Lakini kung'ang'ania kila kitu kiko sawa ni kuletelea msiba....
Mzee Mohamed,
Suala la mzee mwinyi kumnong'oneza malima juu ya kuingiliwa ofisini kwake tangu awali umeombwa umhoji ili upate habari toka kwa mhusika mwenyewe badala ya kutumia habari za kuambiwa na mtu mwingine.
Kumbuka hapa mzee mwinyi alikuwa ananong'ona, nani aliufahamu huo mnong'ono?
MM,
Yaani unataka vyanzo vyangu vya habari nivianike katika jamvi?
Nifanye hivyo na nibaki mtafiti...
Mohamed
Sanda Matuta,
Hali ya Mwinyi ilikuwa kama Insha Allah utakavyoona hapo chini:
"This was the time that Mwinyi confided to Prof. Malima that there werepeople within the office of the president who had duplicates keys to hisdrawers and were stealing documents. Mwinyi, Prof. Malima confided to my informantlooked scared and while he was reporting this to Prof. Malima, Mwinyi wasspeaking in very low tones, whispering as if fearing his office was bugged.Prof. Malima advised President Mwinyi to transfer that entire staff and bringin new people who would have allegiance to him. At this time Prof. Malimastarted to receive hate mails which he turned over to the Intelligence forinvestigation but nothing came out of those investigations."
Mohamed
Mag 3 Kwanini unaona tukubari RAI zako na tukatae hadithi na Muhamed Said!!!?
Unahisi kwa kijana wa miaka arobaini kila siku ana amka asubui na wimbo wa "Nyerere ni mpungufu wa fadhira" kila siku kutoka kwa wazazi na ndugu wa karibu na anakutana na "ngano" za MS na RAI zako ataamini kipi?
"Panapo ukweli uongo ujitenga" Muhamed saidi si kaleta juzi tu hizo hadithi zake angalia post zangu za mwaka 2007 haya mambo yapo inabidi mkubari ili tuanze upya.
Tena kuhusu hilo la chadema ndio wala usililete hapa mimi nalijua mwanzo mwisho

Hapana swali hapo sasa unajibu nini mahali pasipokuwa na swali?
Mohamed
Bila shaka yoyote kuna wana JF wengi labda wanajiuliza kwa nini sitaki kuwa na majibizano ya moja kwa moja na huyu mchochezi anayejiita Mohamed Said. Mwanzoni nilifikiri huyu bwana kweli ana nia ya kuandika historia ya watu waliochangia kwa namna mbalimbali katika harakati zetu kama Watanganyika kupigania uhuru wa nchi yetu. Hivyo mimi pamoja na wachangiaji wengine kwa nia njema kabisa tulijaribu sana kumwelimisha kuwa si kweli hao wazee wake wa Gerezani ndio waliotoa mchango mkubwa kuliko Watanganyika wengine. Dar es Salaam ambako ndiko yalikuwapo makao makuu ya serikali ya kikoloni, pamoja na kuwa mji mkuu wa Tanganyika, kalikuwa kamji kadogo chenye wakazi wasiofikia hata laki mbili. Dar es Salaam ilikuwa ndani ya Jimbo la Pwani, moja ya majimbo manane nchini Tanganyika, na liliunganisha ambayo hivi sasa yanajulikana kama Mkoa wa Morogoro, Mkoa wa Pwani na Mkoa wa Dar es Salaam yenyewe.
Kwa sababu lengo hasa la Mohamed Said halikuwa la kuandika historia ya kweli kama alivyodai mwanzoni, badala ya kutupongeza wengine tuliokuwa tukimpa somo kuhusu Watanganyika ambao yeye hayuko tayari kuwata kabisa ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya, akaanza kutukejeli kuwa na sisi kama tunataka tuandike historia yetu. Baada ya hapo tukamshauri kwamba kama ni hivyo, basi hiyo historia anayoiandika aseme wazi kabisa ni ya Wazee wake wa Gerezani na asithubutu kudai kuwa ni ya Watanganyika. La haula ! Mohamed Said kwa chuki ambayo imetawala hisia zake potofu, akashindwa kuficha tena hasa lengo lake - anapiga vita dhulma waliyofanyiwa na wanayoendelea kufanyiwa Waislaam pamoja na kwamba wenyewe ndio walitoa mchango mkubwa katika kudai uhuru. Mohamed Said, bila kificho, anadai haya ni mapambano dhidi ya mfumo Kristo ambao umetumiwa kukandamiza Uislaam toka na baada ya uhuru.
Mimi Mag3 nimejaribu kumweleza kuwa pamoja na kuwa na uelewa mkubwa wa mambo ya siasa katika miaka ya 1950's sikuwahi kuwasikia wala kuwaona hao wazee wa Mohamed wa Gerezani. Pamoja na kufika Dar es Salaam kwa mara ya kwanza mwazoni mwa miaka ya 1960 baada ya uhuru sikuwasikia hawa Wazee ukiacha Zuberi Mtemvu ambaye jitihada zake, pamoja na mapungufu yake ya kimkakati, hazikumfikisha mbali. Tumejaribu kumwelewesha Mohamed Said jinsi TAA ilivyoundwa mwaka 1929, malengo yake yaliyoainishwa katika katiba na uendeshwaji wake kwa kutojihusisha na mambo ya siasa. Wengine tumempa somo kuhusu maraisi wa TAA (waliokiongoza) tangu kuundwa kwake na Gavana Cameron hadi kuundwa TANU (chama cha siasa) mwaka 1954 na Mwenyekiti wa TANU tangu wakati huo hadi tunapata uhuru. Tumemwomba awataje hao wazee wake walioongoza hivyo vyama, yeye kakazania porojo za wazee wake !
How convenient kwa wenye mawazo potofu kama Mohamed Said kuwa mbinu za kuhusisha Ukristo na mfumo wa serikali baada ya uhuru hazingeweza kufanikiwa bila kwanza kumchafua Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Na kumchafua Mwalimu hakungeweza kufanikiwa bila kuzua kinachoitwa chuki yake dhidi ya Uislaam na hivyo kuwateka Waislaam ambao mathalan dini imehusishwa, watatetea mada mradi mtoa mada ni Muislaam mwenzao. Bahati nzuri Waislaam wa Tanzania walio wengi (hasa ninaoshirikiana nao - marafiki, ndugu na comrades) wanaelewa fika hizo mbinu chafu zenye kujali maslahi ya watu wachache na si taifa letu tunalolipenda la Tanzania na hawako tayari kuzibariki bila tafakari. Hii ni moja ya sababu inayonizuia kujibizana na Mohamed Said moja kwa moja (people might not notice the difference) na ninawaachia Waislaam hawa wenye mapenzi ya kweli na taifa letu, wachambue mchele na pumba katika haya ninayoyaandika.
Juzi kuna kundi la Waislaam wamejitokea na bila kificho wamewaagiza waumini wao wasikipigie Chadema kura ! Ni bahati gani tamko kama hili halikutolewa na kikundi chochote cha Kikristo, lakini nachelea kusema kwa uhakika kuwa lingetokea hilo hivi sasa tungekuwa tunaongelea mengine. Katika uchaguzi wa mwaka 2010 alianza mwandishi wa gazeti la serikali kwa jina Ali Mkumbwa akatumia maneno yenye mtizamo na mwelekeo kama huo lakini hadi leo anaendelea kuchapa kazi bila wasi wasi katika mfumo Kristo. Watu kama Mohamed Said tusiwapuuze, nyuma yake kuna kubwa zaidi ya hili la kudai kuandika historia ya kweli na bila shaka hii mada inavyoendelea anazidi kujifunua kwa sura yake halisi - nimesoma kwa makini michango yake ya karibuni ambayo yaonyesha kabisa kuwa anataka nini. Anadai Uislaam unawapa watu woga na anaonya kuhusu yatakayotukuta sisi wazalendo ambao tumetanguliza Utaifa mbele ya Udini anaoupaka rangi akisahau hiyo rangi haibadilishi umbile.
Tumemtolea Mohamed Said mifano kuwa katika harakati zote za kudai mabadiliko popote pale duniani kimfumo au kiutawala, lazima anatokea kiongozi ambaye hupata sifa za pekee na huyu si mwingine ila ni yule anayefanikisha malengo ya harakati hizo. Mtanganyika hakutakiwa kusafiri hadi Dar es Salaam ndio awajue Wazee wa Gerezani na laiti hao wazee wangekuwa maarufu kiasi hicho, hawangemhitaji Mwalimu Nyerere aje awaongoze lakini nakumbuka katika ujana wangu jina tu Nyerere lilivyoenea mpaka kijijini na hadi leo, CCM inapokwama inamtumia Nyerere kama mtaji wake. Kwa nini hata Lindi, jina la Nyerere litajwe kwenye kampeni na wagombea ni si la akina nani vile ! Abdul Sykes ! Jamani tuache hizi soga zisizokuwa na kichwa wala miguu, hadi watoto walizaliwa wakati huo wakaitwa Nyerere Mikindani hadi Kibondo, Usangi hadi Tukuyu na Mafia hadi Tumbatu. Na hapo bado Auckland hadi Edmonton, Kyoto hadi Guyana na Cape Town hadi Tripoli.
Nimeeleza Mwalimu alivyoona aibu kuongoza nchi huru na huku mji wake mkuu, ukiacha Uhindini na Uzunguni, wazawa wanaishi kwenue nyumba za makuti. "Operation Makuti" ilianzishwa makusudi kuwapa makazi bora hawa watu inaodaiwa Mwalimu hakutaka wapate maendeleo na hili ndilo lilikuwa lengo kubwa la kuanzishwa kwa Shirika la Nyumba. Wana JF mtafakari na muamue wenyewe kuhusu michango ya Watanganyika mbali mbali na "sacrifices" ambazo ilkuwa ni lazima zifanyike ili tuweze kujenga taifa lenye umoja na mshikamano. Kwa bahati nzuri au mbaya, Raisi wa chama cha siasa anaweza kuwa moja tu na Raisi wa nchi anaweza kuwa moja tu, na historia kamwe haitafuta ukweli kwamba Raisi wa Kwanza wa TANU na Raisi wa kwanza wa Tanganyika huru angeweza na alikuwa moja tu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wanaolilia wazee wao, wakumbuke tu kitu kimoja, mtu aliyeongoza harakati hizo alipatikana kwa kura baada ya kuwa na sifa kuwashinda wengine.
Bila shaka yoyote kuna wana JF wengi labda wanajiuliza kwa nini sitaki kuwa na majibizano ya moja kwa moja na huyu mchochezi anayejiita Mohamed Said. Mwanzoni nilifikiri huyu bwana kweli ana nia ya kuandika historia ya watu waliochangia kwa namna mbalimbali katika harakati zetu kama Watanganyika kupigania uhuru wa nchi yetu. Hivyo mimi pamoja na wachangiaji wengine kwa nia njema kabisa tulijaribu sana kumwelimisha kuwa si kweli hao wazee wake wa Gerezani ndio waliotoa mchango mkubwa kuliko Watanganyika wengine. Dar es Salaam ambako ndiko yalikuwapo makao makuu ya serikali ya kikoloni, pamoja na kuwa mji mkuu wa Tanganyika, kalikuwa kamji kadogo chenye wakazi wasiofikia hata laki mbili. Dar es Salaam ilikuwa ndani ya Jimbo la Pwani, moja ya majimbo manane nchini Tanganyika, na liliunganisha ambayo hivi sasa yanajulikana kama Mkoa wa Morogoro, Mkoa wa Pwani na Mkoa wa Dar es Salaam yenyewe.
Kwa sababu lengo hasa la Mohamed Said halikuwa la kuandika historia ya kweli kama alivyodai mwanzoni, badala ya kutupongeza wengine tuliokuwa tukimpa somo kuhusu Watanganyika ambao yeye hayuko tayari kuwataja kabisa ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya, akaanza kutukejeli kuwa na sisi kama tunataka tuandike historia yetu. Baada ya hapo tukamshauri kwamba kama ni hivyo, basi hiyo historia anayoiandika aseme wazi kabisa ni ya Wazee wake wa Gerezani na asithubutu kudai kuwa ni ya Watanganyika. La haula ! Mohamed Said kwa chuki ambayo imetawala hisia zake potofu, akashindwa kuficha tena hasa lengo lake - anapiga vita dhulma waliyofanyiwa na wanayoendelea kufanyiwa Waislaam pamoja na kwamba wenyewe ndio walitoa mchango mkubwa katika kudai uhuru. Mohamed Said, bila kificho, anadai haya ni mapambano dhidi ya mfumo Kristo ambao umetumiwa kukandamiza Uislaam toka na baada ya uhuru.
Mimi Mag3 nimejaribu kumweleza kuwa pamoja na kuwa na uelewa mkubwa wa mambo ya siasa katika miaka ya 1950's sikuwahi kuwasikia wala kuwaona hao wazee wa Mohamed wa Gerezani. Pamoja na kufika Dar es Salaam kwa mara ya kwanza mwazoni mwa miaka ya 1960 baada ya uhuru sikuwasikia hawa Wazee ukiacha Zuberi Mtemvu ambaye jitihada zake, pamoja na mapungufu yake ya kimkakati, hazikumfikisha mbali. Tumejaribu kumwelewesha Mohamed Said jinsi TAA ilivyoundwa mwaka 1929, malengo yake yaliyoainishwa katika katiba na uendeshwaji wake kwa kutojihusisha na mambo ya siasa. Wengine tumempa somo kuhusu maraisi wa TAA (waliokiongoza) tangu kuundwa kwake na Gavana Cameron hadi kuundwa TANU (chama cha siasa) mwaka 1954 na Mwenyekiti wa TANU tangu wakati huo hadi tunapata uhuru. Tumemwomba awataje hao wazee wake walioongoza hivyo vyama, yeye kakazania porojo za wazee wake !
How convenient kwa wenye mawazo potofu kama Mohamed Said kuwa mbinu za kuhusisha Ukristo na mfumo wa serikali baada ya uhuru hazingeweza kufanikiwa bila kwanza kumchafua Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Na kumchafua Mwalimu hakungeweza kufanikiwa bila kuzua kinachoitwa chuki yake dhidi ya Uislaam na hivyo kuwateka Waislaam ambao mathalan dini imehusishwa, watatetea mada mradi mtoa mada ni Muislaam mwenzao. Bahati nzuri Waislaam wa Tanzania walio wengi (hasa ninaoshirikiana nao - marafiki, ndugu na comrades) wanaelewa fika hizo mbinu chafu zenye kujali maslahi ya watu wachache na si taifa letu tunalolipenda la Tanzania na hawako tayari kuzibariki bila tafakari. Hii ni moja ya sababu inayonizuia kujibizana na Mohamed Said moja kwa moja (people might not notice the difference) na ninawaachia Waislaam hawa wenye mapenzi ya kweli na taifa letu, wachambue mchele na pumba katika haya ninayoyaandika.
Juzi kuna kundi la Waislaam wamejitokea na bila kificho wamewaagiza waumini wao wasikipigie Chadema kura ! Ni bahati gani tamko kama hili halikutolewa na kikundi chochote cha Kikristo, lakini nachelea kusema kwa uhakika kuwa lingetokea hilo hivi sasa tungekuwa tunaongelea mengine. Katika uchaguzi wa mwaka 2010 alianza mwandishi wa gazeti la serikali kwa jina Ali Mkumbwa akatumia maneno yenye mtizamo na mwelekeo kama huo lakini hadi leo anaendelea kuchapa kazi bila wasi wasi katika mfumo Kristo. Watu kama Mohamed Said tusiwapuuze, nyuma yake kuna kubwa zaidi ya hili la kudai kuandika historia ya kweli na bila shaka hii mada inavyoendelea anazidi kujifunua kwa sura yake halisi - nimesoma kwa makini michango yake ya karibuni ambayo yaonyesha kabisa kuwa anataka nini. Anadai Uislaam unawapa watu woga na anaonya kuhusu yatakayotukuta sisi wazalendo ambao tumetanguliza Utaifa mbele ya Udini anaoupaka rangi akisahau hiyo rangi haibadilishi umbile.
Tumemtolea Mohamed Said mifano kuwa katika harakati zote za kudai mabadiliko popote pale duniani kimfumo au kiutawala, lazima anatokea kiongozi ambaye hupata sifa za pekee na huyu si mwingine ila ni yule anayefanikisha malengo ya harakati hizo. Mtanganyika hakutakiwa kusafiri hadi Dar es Salaam ndio awajue Wazee wa Gerezani na laiti hao wazee wangekuwa maarufu kiasi hicho, hawangemhitaji Mwalimu Nyerere aje awaongoze lakini nakumbuka katika ujana wangu jina tu Nyerere lilivyoenea mpaka kijijini na hadi leo, CCM inapokwama inamtumia Nyerere kama mtaji wake. Kwa nini hata Lindi, jina la Nyerere litajwe kwenye kampeni na wagombea na si la akina nani vile ! Abdul Sykes ! Jamani tuache hizi soga zisizokuwa na kichwa wala miguu, hadi watoto walizaliwa wakati huo wakaitwa Nyerere Mikindani hadi Kibondo, Usangi hadi Tukuyu na Mafia hadi Tumbatu. Na hapo bado Auckland hadi Edmonton, Kyoto hadi Guyana na Cape Town hadi Tripoli.
Nimeeleza Mwalimu alivyoona aibu kuongoza nchi huru na huku mji wake mkuu, ukiacha Uhindini na Uzunguni, wazawa wanaishi kwenue nyumba za makuti. "Operation Makuti" ilianzishwa makusudi kuwapa makazi bora hawa watu inaodaiwa Mwalimu hakutaka wapate maendeleo na hili ndilo lilikuwa lengo kubwa la kuanzishwa kwa Shirika la Nyumba. Wana JF mtafakari na muamue wenyewe kuhusu michango ya Watanganyika mbali mbali na "sacrifices" ambazo ilkuwa ni lazima zifanyike ili tuweze kujenga taifa lenye umoja na mshikamano. Kwa bahati nzuri au mbaya, Raisi wa chama cha siasa anaweza kuwa moja tu na Raisi wa nchi anaweza kuwa moja tu, na historia kamwe haitafuta ukweli kwamba Raisi wa Kwanza wa TANU na Raisi wa kwanza wa Tanganyika huru angeweza na alikuwa moja tu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wanaolilia wazee wao, wakumbuke tu kitu kimoja, mtu aliyeongoza harakati hizo alipatikana kwa kura baada ya kuwa na sifa kuwashinda wengine.
Sanda Matuta, na wewe ulisimuliwa na wazee wako ama ulikuwapo ili nijue namna ya kukujibu. Kama ulikuwapo kwenye miaka ya 1950 hadi uhuru ulikuwa na umri gani ? Siulizi hivi kwa lengo baya, nataka tu nijue kama unaeleza uliyoshuhudia au uliyosimuliwa.
"Jina la Abdulwahid halitajwi kabisa katika historia ya kudai uhuru wa Tanganyika au katika historia ya kuasisi TANU. Juu ya haya yote Abdulwahid ndiye aliyewasha cheche za kuanzisha harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.
Mohamed
Sheikh mohamed,
nia yangu sio unitajie vyanzo vyako vya habari, maana hizi ni nyeti zinahitaji usiri. Zile ambazo si nyeti sana umekuwa ukibainisha vyanzo vyake.
Ninachokusudia hapa ni kutaka kufahamu kama umewahi kumhoji mzee mwinyi kuhusu jambo hilo, lengo ni kutanzua huu utata. Bila shaka utakuwa umenielewa!
Hii ilishafutwa kwani harakati za uhuru Tanganyika hazikuanzia Dar-es-Salaam kulikuwa na watu wengine nje ya Dar ambao nao katika maeneo yao walianzisha cheche za kudai uhuru. Ni sahihi kusema tu kuwa kwa eneo la Dar mzee Sykes yumkini ndiye aliyekuwa mwanzo wa cheche za uhuru.
Mwanakijiji,
Hilo linawezekama sana lakini litasimama vizuri na kuingizwa katika historia kama utapatikana ushahidi. Kila siku sishi kusema kuwa kama nanyi mna wazee wenu waliopigania uhuru itakuwa vyema kama mtaandika habari zao tuzisome hapa ukumbini.
Inaelekea hili limekushindeni maana naona maswali ya kupinga historia yangu iliyofanyiwa utafiti na na nyaraka zipo hadi leo.
Mohamed