Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Hili swali la muda uliotumika kufanya utafiti na hatimaye kuandika kitabu cha Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes ni swali ambalo hoja mbalimbali dhidi ya Nyerere zinasimama. Bw. Said hawezi kujibu swali kwa uwazi na haki bila kusababisha swali pekee ambalo anajua kuwa litamfunga yeye na credibility nzima ya utafiti wake. Ni katika swali hili hoja nzima ya "udini" na "ukandamizaji wa Waislamu chini ya Nyerere" zinasimama. Ningefurahi kuona wale wanaotaka ukweli wa historia ya Tanganyika kama inavyosimuliwa na Bw. Said wamhimize basi japo kidogo ajibu tu hata bila maelezo ya kina..
 
aah yeshakuwa hayo tena shehe? yawezekana hukumbuki muda uliochukua kuandika kitabu chako?

Mwanakijiji, najua kwa nini ungependa ajibu swali hilo lakini si ajabu hata hilo halifahamu kwa sababu, if you can read between the lines, hizi anazoleta humu kama simulizi za wazee wake ni matokeo ya mpango wa muda mrefu sana. Kama nilivyosema mwanzo ni maandishi yaliyofinyangwa na kuungwaungwa kwa nia moja tu, kuipotosha jamii na si kazi ya mtu mmoja.

Majibu anayoyatoa kwa maswali kadhaa yanamuumbua ni wapi anapata reference na naweza kukuambia ilikuwa ni swala tu la muda mwafaka, haya mambo yamepikwa, yakaiva na sasa yanawekwa mezani na mwenye njaa kama kawaida akikuta meza tayari anafikiria kula tu hata chakula kikiwa na sumu. Nimejaribu kupima uwezo wa huyu Mohamed Said jinsi anavyojibu maswali anaji betray kwa sababu labda hakujitayarisha kuupata upinzani kama anaoupata humu.

Mohamed Said ni mtu hatari, amekubali kutumiwa tu katika ajenda ambayo huenda ni kubwa kuliko tunavyofikiria. Nina hakika great thinkers wa humu ndani tukiunganisha dots kama kawaida yetu, tutaweza kuuanika huu mpango mchafu na chanzo chake, ni swala la muda tu na tukumbuke kuwa mchelea mwana hulia mwenyewe. Jaribu kutafuta hizi mada zake ambazo kwa sasa hazionekani humu JF na alivyokuwa akitetea hoja zake.

  1. Christian Hegemony and the Rise of Muslim Militancy in Tanzania..
  2. Kitabu: Maisha na Nyakati za A Sykes
Tanzania, be warned.
 

Hata mimi naamini kabisa kuwa ni swali ambalo hawezi kulijibu kwa uwazi na haki. Kwani hoja zake zote dhidi ya Nyerere zinasimama kwenye hilo...
 
Lakini nikiangalia huu mjadala kiupana na in a big picture naliona tatizo lile lile tulilonalo waafrika kuhusu historia. Watu hawaandiki hivyo simulizi ndiyo huchukua nafasi. Kinachosikitisha ni kwamba hii ni historia ya miaka 50 tu ni juzi kabisa na wengi waliokuwepo nyakati hizo bado wako hai. Lakini ukisoma humu ndani ya mjadala utafikiri yanazungumziwa mambo ya nchi mbili au tatu tofauti kabisa na yalitokea miaka 500 iliyopita.

Wakuu kwa wale wasiofahamu ni kwamba ANC ya Afrika kusini mwanzilish
i Pixley ka Isaka Seme anajulikana na watu wachache sana hata ndani ya South Africa. Katika waanzilishi walikuwemo pia wamalawi. Ukienda pale Apartheid museum zote 2 ile ya Soweto na ya Gold reef city utakuta historia zao.

Ukija kwa mtu aliyemleta Mandela ANC, Walter Sisulu umaarufu wake ni less than 1% ukilinganisha na wa Mandela. By the way ni wangapi humu mnafahamu kwamba Walter Sisulu alikuwa halfe caste, au colored kama wanavyoita wenyewe South Africa? Je mmewahi kusikia coloreds (It is an official race in South Africa) wakilalamika kwamba historia yao kugombea uhuru SA imepotoshwa eti kwa sababu Sisulu hatajwi sana kama Mandela? Ukiongea haya unaambiwa eti unapata tabu kusikia historia fulani what a cheap shot?


 
Utapataje common ground wakati mnaita mfumo tulio nao mfumokristo? Mtapataje common ground wakati mna admit kuwa Sheikh Mohammed anayo asasi ya siri? Kama mnataka common ground usiri ni wa nini? Ayamwage hapa Mohammed tuyajadilie. Anakuja huku kama mwuungwana mwenye hekima asiyependa matusi lakini pembeni mnaandaa ajenda za siri halafu hapa unazungumzia common ground? Alichofanya Nyerere kinapaswa kuenziwa na kuendelezwa na kila mtu anayeitakia mema Tanzania. Ali level the playing field. Takadir na Mtemvu walikuwa wabaguzi. Kwao Utanganyika wao uliishia kwenye Uislamu. Walikuwa radhi uhuru wa Tanganyika ucheleweshwe mpaka Waislamu watakapokuwa tayari kushika nafasi za uongozi. Huo ni nini kama si ubaguzi? Mtemvu yeye alitaka Tanganyika iwe ya Watanganyika. Full stop. Mmalawi, Mzambia, Mkenya na Mkongo asingeruhusiwa kupata uraia wa Tanganyika. Ni Nyerere ndiye aliye "define" uraia wetu na kwa kuona mbali leo hawa Wahindi waliokuwepo tangu enzi za ukoloni ni ndugu zetu. Talk about common ground!
 
Mag3,'
Kwangu mimi hapa umemaliza kila kitu. Chochote kingine kile kitakuwa ni hadidu za rejea.
 
Mohammed,
Nahitimisha ushiriki wangu katika mjadala huu kwa kukuuliza mara nyingine tena swali moja tu: Umezipamba sana juhudi za Abdulwahid Kleist
katika ukombozi wa Tanganyika. Hata umeandika kitabu juu ya juhudi hizo na kuweka jina lake. Sasa kuna mahali ulisema kuna nyaraka za maandishi yake huyo huyo Abdulwahidi lakini familia yake imekataa kukupa hizo nyaraka. Je, unafikiri ni kwa nini familia ya mtu unayemsifia sana hawajakuamini vya kutosha kukupa nyaraka na memoranda za personal messages zake? Kama mwanahistoria ningefikiria kuwa familia yake ingefurahi kuona kuwa hizo nyaraka zimo mikononi mwa mtafiti makini kama wewe, au?
 
Mzee Said, tunakuomba usiweke vipande vya habari. Tunavyo katika magazeti na vitabu ikiwa ni pamoja na hapa JF. Ukiulizwa swali jibu swali, wewe ni mwandishi na moja ya sifa za uandishi ni kuweza kuwasiliana na hadhira yake kwa ufupi na ueledi(concise and precise). Usifanye maandishi yako kuwa ni reference muhimu kwetu, ni muhimu kwako na wale wanaomeza bila kujua lengo lako. Usijaze kurasa tafadhali.

Pili naona kuna wnaJF bado wanasita kuamini kuwa lengo la Mohamed ni udini. Mkuu Mkandara amekuja 'wima'kama wengi walivyosimama wima kupinga upotoshaji na udhalilishaji wa dini unaofanywa na mtu au watu wenye chuki kuu mioyoni mwao. Mkuu kasema uislam unasimama peke yake bila jina la mtu, na ukweli ni kuwa Mtume Muhamad S.A.W hakuutangaza Uislam kwa jina lake licha ya karama alizomruzuku mwenyezi, sijui Mohamed anayatoa wapi katika Quran, hadithi, sunna kuwa Uislam lazima uambatanishwe na majina

Lugha anayoielewa Mohamed ninapotoa hoja ni ile ya kumnukuu mwenyewe maana utaratibu wake ni wa kwenda mbele na nyuma, kubadili hadithi(flip flop), na huwa anasema hanielewi kwa matusi ya sisi watu wa pwani, ikiwa na maana mimi jinga fulani hivi.

Soma hii
Mohamed Said 2697723:Hakuna Muislam anaeweza kuthubutu kutangaza Uislam kwa jina la mtu. Sijafanya hivyo na wala siwezi kuthubutu
halafu soma hii
Mohamed Said; IngawaWaislam ndiyo walioleta uhuru wa Tanganyika, manufaa ya uhuru ni madogo sana kwao
anaendelea hivi
Mohamed Said: Huko umekwenda wewe mie haja ni kuonyesha mchango wa wazee wangu katika uhuru wa Tanganyika,alikuwepo Sheikh Yusuf Badi, alikuwepo Salum Mpunga, alikuwepo Yusuf Chembela nk
Ikifika hapo kama huamini udini ndio unaomuongoza Mohamed na anatumia majina kuutangaza Uisla basi hutamwelewa kamwe!

Ukitaka kujua anavyomchukia Nyerere kwa hila na kwa kina ndani ya nafsi yake, lakini akinasibisha kwetu kuwa ana mheshimu, soma hii nikupe analysis. Sisi watu wa Pwani huwa hatusemi ;mshamba wee!' tunasema hajajua kula chapati. Sisi huwa hatusemi ;mjinga' tunasema hajaelewa. Sisi wa Makorara huwa hatusemi 'mwendawazimu' tunasema ameghafilikiwa. Soma Wawili wamevaa suti na tai. John Rupia hana utambulisho, Saadan Kandoro hana utambulisho. Nyerere amevaa soksi hadi magotini. Haina tabu, kavaa kweli lakini kumbuka ni Mohamed huyo huyo aliyewahi kusema, Nyerere akija Dar si lolote si chochote(ushahidi upo) na kwamba alipewa pesa za kitoweo n.k. Kwasisi watu wa pwani hii ndiyo lugha yetu msituone wanafiki.

Angalia hapa chini Uislam unavyoingia halafu unavyochanganywa na hisia za mwanadamu ili kukidhi haja za matakwa ya kiroho.
Mohamed Said;2697723]Mkandara, Ila nitafahamisha moja ya mafunzo ya Uislam. Allah anawaasa Waislam "wasidhulumu na wasikubali kudhulumiwa."
Mohamed anaposema Nyerere amevunja baraza la wazee wa TANU, lakini hajui majina ya wajumbe wa kamati kuu iliyokaa na Nyerere kufikia uamuzi. Kwamba anamhukumu Nyerere kwa dhana bila uthibitisho, halafu anasema Uislam unakataa dhulma ile ile anayoitenda yeye kwa kuhukumu pasi na ushaidi. Tuhuma zinandelea
Christian lecturers at Dares Salaam University are discouraging students from making references to thosetwo books
Kila mtu asiye mwislam ni mkristo amekataa kitabu chake kisitumike, dhulma! kama angetaja majina tungeelewa ni Uislam, lakini kwa kuongozwa na dhana ya 'wao' na kuwatuhumu maprofesa wa Physics na medicine kuwa ni wakristo na wamekataa kitabu chake inasikitisha mzee Said.
Watu wa bara wanasema 'roho mbaya' sisi watu wa Mabawa polisi tunasema, ah ah lugha ya kiungwana ni kusema hiyo ni fitna!!
Hutaki dhulma, ile ile unayoiandika kwa mkono wako!

Kwahiyo hakuna haja ya kudhani kuwa alimchukia Nyerere, tunachojiuliza ni kwanini? na kwanini chuki hii anaifanya sehemu ya dini!
Amekubali kuwa historia ni ya Gerezani, basi tukubaliane naye ila akisema neno Tanganyika, tumwambie Tanganyika si Kipata au Gerezani.

Huyo ndiye MSS na harakati za kupandikiza chuki, kuchochea vurugu. Akiitwa Mnyapala wa wazungu anasema katukanwa, labda kauli hii ya mwenzangu wa pwani kule Unguja ina lahaja ya yenye stara
Barubaru;2696526]Kwani ufahamu kuwa Shoka haliwezi kukata miti bila kuwekwa kipande cha mti (mpini)
 

Nguruvi3,

Ahsante kwa ushauri.

Hivi vipande ninavyoviweka ni "excerpts" kutoka kitabu changu na hujibu yale niliyoulizwa. Inawezekana wewe haikusaidii kwa maana yote yaliyo mle unayajua lakini nimesoma humu ukumbini wengi wakisema kuwa wananufaika na "excerpts" hizo.

Wala sisemi kuwa hizo ni rejea muhimu la hasha ni maandishi yangu tu na mtu anaweza kuyakubali au kuyakataa. Hatuwezi kugombana kwa hilo.

Hilo la udini nimelijibu mara nyingi na nitajibu tena. Mbona mabuku mengi tu yameandikwa kuhusu Kanisa na jinsi lilivyosaidia kumaliza biashara ya utumwa na sisi hatujasema kuwa huo ni udini?

Kuhusu kitabu changu kukataliwa si kimoja ukweli ni vitabu viwili hiki cha pili kilichapwa na Oxford University Press, Nairobi ni kitabu cha shule ya msingi kusomesha historia huku wanafunzi wanajifunza lugha ya Kiingereza kinaitwa "The Torch on Kilimanjaro." Maudhui ya kitabu ni historia ya Nyerere wakati wa kudai uhuru.

Wataalam wa Oxford wanashangaa vipi kiabu kizuri kama kile kimekataliwa na Wizara ya Elimu. Wao jibu hawana lakini jibu liko wazi wamefanya utafiti wao wenyewe na sasa wamejua.

Sijasema wazee wangu ndiyo wazalendo pekee. Nilichofanya ni kuandika walichofanya katika kupigania uhuru wa Tanganyika na laiti nisingelifanya hivyo historia hii ingepotea.

Ikiwa kuna mtu ambae anawajua wazalendo wengine ambao wamefanya makubwa lakini wamesahauliwa hakuna ubaya wakaandika habari zao watu wakasoma.

Mwisho nakuomba fanya utafiti wako mwenyewe juu ya hali ya Waislam ilivyo sasa hivi nchini nina hakika utajua kuwa mambo si kama yalivyokuwa zamani.

Tunalo tatizo ambalo lazima tulijadili tunapenda au hatupendi.

Mohamed
 

Jasusi,

Nyaraka zote nimesoma ila zile shajara (diary) zake ndiyo sikupewa. Huenda sikupewa kuzipitia kwa kuwa shajara huwa zina mengi mambo binafsi.

Baadhi ya hizi shajara Abdulwahid kaziandika katika hati mkato. Hizi ni zile kuanzia 1950 ambapo Special Branch ilikuwa iikimwandama. Hizi za hati mkato ingebidi atafutwe mtaalam wa kuzisoma.

Halikuwa suala la kutoaminika.


Mohamed
 
Jasusi,

Naomba nikusahihishe kidogo.

Sheikh Suleiman Takadir ndiye aliyekuwa na wasiwasi na hali ya baadae ya Waislam na hivyo akagombana na Nyerere. Mtemvu yeye hakugombana na Nyerere kwa ajili ya Uislam. Mtemvu hakutaka wageni washiriki katika siasa za Tanganyika.

Mohamed
 

Mnakasha ukishafikia hali kama hii ninayoiona sasa hivi ni dalili kuwa uko ukingoni.

Katika hali kama hii nashindwa kutoa mchango wa maana ninachofanya nasoma na
kutia fikra hizi katika kumbukumbu zangu huenda huko mbeleni Insha Allah nikaandika
kitabu kingine na hivi ndivyo vitu vya kunisaidia.

Nashukuru kwa mchango wako.

Mohamed
 
aah yeshakuwa hayo tena shehe? yawezekana hukumbuki muda uliochukua kuandika kitabu chako?

Mwanakijiji,

Ndugu yangu ahsante nimepata raha kujadiliana na wewe na Insha Allah tutajadiliana zaidi lakini mimi ni mtu wa akida na hupenda kuchunga mipaka yangu.

Huwa sikubali kufanya yale ambayo mimi nayaona si sawa kwa kuwa hayana tija.

Mohamed
 
Nguruvi3,
Mwisho nakuomba fanya utafiti wako mwenyewe juu ya hali ya Waislam ilivyo sasa hivi nchini nina hakika utajua kuwa mambo si kama yalivyokuwa zamani.
Tunalo tatizo ambalo lazima tulijadili tunapenda au hatupendi. Mohamed
Mzee Said Waislam hawana tatizo, ila kuna tatizo linalopandikizwa kwa waislam. Unapokwenda na kumwambia mtu ni second citizen na unajua hajui maana yake na wala hawezi kuhoji, yeye si tatizo tatizo ni mto habari. Kama Waislam ni second citizen, je wapagan na Atheist wao ni daraja gani, mbona hao huelezi

Mzee Said, umekiri kuwa mnazunguka mikoani kuelezea hali ya dhulma. Tumekuuliza mara mia dhulma zipi hutuelezi badala yake unajifungia diamond jubilee na kuandika nyaraka na kusambaza kwa siri.

Nimeona CD za masheikh mnaowatuma, kuna tatizo mzee Siad. Unapomtuma mtu aseme asichoweza kukitetea ni hatari na haina tija. Unakumbuka suala la kadhi lilivyokabidhiwa wamtaani na matokeo yake.
Sheikh anaposema serikali inajenga makanisa ukimuuliza kivipi anasema kasome kitabu cha Mohamed Said, ni hatari.

Lakini jiulize mzee wangu, mtu ameoza mtoto wa miaka 12 halafu maisha yakiwa hohe hahe anasema mfumo kristo.
Mnatumia pesa na muda kuzunguka mikoani kuelezea kisicho na ukweli, huko huko mikoani shule za waislam zinaongoza kutoka kusini!
Mnakaa kikao siku mbili kuandika tamko la ndoa ya mtu, halafu mnasema mnaonewa. Mnakaa siku nzima kuandika tamko la hijabu na sio kujadili mabinti wa kiislam wasioweza kuendelea na shule, halafu mnasema mnaonewa.

Tatizo lipo kuwa huenda mna nia nzuri, nasema huenda, kwa bahati mbaya ima hamjui muitekeleze vipi au mna ajenda za siri. Lakini uprising unayoiendesha ni hatari kwa taifa na wala haitatoa jibu la matatizo. Matatizo hayatatuliwi kwa kutafuta mtu wa kumsingizia, ni watu wakae chini waangalie nini cha kufanya na si lini kuleta vurugu.

Unaposema asilimia 76 ni wakatoliki bungeni, unasahau nani amechagua? kwa wasio na uwezo wa kuchambua watakuelewa vizuri sana na kujaa hasira, kwa walio na uelewa wa kuchambua kama waislam weledi wanaona haya kwa hoja hii. Too low mzee wangu! please.

Hatuchagui masheikh wala maaskofu hapo ndipo nawapenda Watanzania. Si ilikuwepo haki sawa kwa wote na wewe na wenzako mkiunga mkono CUF, jiulize iliwahi kuwa na mbunge Tanzania bara?

Wewe na wenzako si ndio miaka 10 mlikuwa mnaisema CCM na udhalimu, kauli hiyo imeishia wapi. Sasa tunasikia serikali, lakini miaka ya 60,70,80 mdhalimu alikuwa Nyerere. Sijui kwanini leo isemwe serikali na si 'Nyerere wa leo' double standard na flip flop.

Kinachonishangaza kwako ni kuwa more than 20 years unaongea kile kile hata kama kinapata challenge hujaribu kubadili, miaka 20 hujatoa solution yoyote zaidi ya kuchochea.

Na kibaya huchochei fikra unachochea watu kuchukua mikuki, halafu unarudi JF na kusema hali si njema, unaenda ulaya kuelezea matatizo kwa wazungu wale wale unaosema kila siku ni mkafir. Mzee Said, hivi nani anaifahamu Tanzania, mimi Nguruvi wa Kicheba Muheza au William wa New Hamshire.

Watu wanahisi huko ndiko unaenda kupata hela za kutengeneza CD za uprising, lakini mzee Said, jiulize hiyo ndiyo njia akina Abdul Sykes, Mshume Kiyate n.k waliotumia? Lini Sykes aliokota jiwe kumpiga mkoloni. Sasa wewe unapojenga chuki na jamii ni Uislam upi huo.

Mzee Said, Waislam hawana tatizo ila kuna tatizo linalochomekwa kwa waislam na kikundi cha watu kwa kusingizia Uislam ili kifikie malengo yake, kwa hili ipo siku kuna mtu hatajipiga kifua mbele kama unavyojipiga kwa wazee wako kwasababu ataona haya kunasibishwa na jina lako na historia haifichi kitu.

Mzee Said, usikwepe tatizo tafuta chanzo halisi cha tatizo. Toa solution si kuchochea hasira bila sababu. Nasema bila sababu kwasababu wewe unayeandaa mada na mkakati huwezi kujibu au kutetea hoja, mwenzangu mimi pangu pakavu atafanya nini.
 
Nguruvi3,

Ahsante kwa juhudi zako lakini bahati mbaya unatoa majibu wewe.

Yule Waislam tunaemtuhumu kwa dhulma kakaa kimya.

Mohamed
 
Kwa wale wanaopinga maneno ya MS tunaomba watoe ushahidi wa VITENDO ambavyo Nyerere alivifanya kuwatendea HAKI Waislamu.

Kama Nyerere hakuwa MDINI kwa nini Wakristo ndiyo walikuwa wanaongoza ktk Idara Serikalini?

Kama Nyerere hakuwa MDINI kwa nini kila Waziri ktk wizara ya Elimu alikuwa Mkiristo?

Kama Nyerere hakuwa MDINI kwa nini Wakristo wanamwita "Mtakatifu" kwa kumpa fadhila alozowafanyia?

Kama Nyerere hakuwa MDINI mbona mnakasirika akiambiwa MDINI?
 
Nguruvi3,

Ahsante kwa juhudi zako lakini bahati mbaya unatoa majibu wewe.

Yule Waislam tunaemtuhumu kwa dhulma kakaa kimya.

Mohamed
Dhulma zipi? maana unajibu kitu unachoulizwa, kama hakuna swali au hoja unatoaje majibu.
Ndiyo maana mimi huweka ushahidi wa kuthibitisha Mzee Said ana chuki au ni mdini. Haitoshi mimi kusema mzee Said ni mdini halafu nikutake utoe majibu.

Pili, mnamtuhumu nani ? Nyerere, Serikali, CCM au Wakatoliki. Tukishajua hapo, tuendelee kwa tuhuma zipi. Na tusiishie hapo tuambiwe nini kifanyike nini.

Hebu toa hoja moja tu kuhusu dhulma unaayohamasisha masheikh wakaieleze mikoani, halafu tupe ufumbuzi wake kwa mtazamo wako.

Lakini mzee Said, si unajua kuwa busara si la lazima kuongea hata kukaa kimya ni busara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…