Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mwanakijiji,
Hivi kuna mtu kakulazimisha kusoma?
Mohamed
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwanakijiji,
Hivi kuna mtu kakulazimisha kusoma?
Mohamed
aah yeshakuwa hayo tena shehe? yawezekana hukumbuki muda uliochukua kuandika kitabu chako?
Mwanakijiji, najua kwa nini ungependa ajibu swali hilo lakini si ajabu hata hilo halifahamu kwa sababu, if you can read between the lines, hizi anazoleta humu kama simulizi za wazee wake ni matokeo ya mpango wa muda mrefu sana. Kama nilivyosema mwanzo ni maandishi yaliyofinyangwa na kuungwaungwa kwa nia moja tu, kuipotosha jamii na si kazi ya mtu mmoja.
Utapataje common ground wakati mnaita mfumo tulio nao mfumokristo? Mtapataje common ground wakati mna admit kuwa Sheikh Mohammed anayo asasi ya siri? Kama mnataka common ground usiri ni wa nini? Ayamwage hapa Mohammed tuyajadilie. Anakuja huku kama mwuungwana mwenye hekima asiyependa matusi lakini pembeni mnaandaa ajenda za siri halafu hapa unazungumzia common ground? Alichofanya Nyerere kinapaswa kuenziwa na kuendelezwa na kila mtu anayeitakia mema Tanzania. Ali level the playing field. Takadir na Mtemvu walikuwa wabaguzi. Kwao Utanganyika wao uliishia kwenye Uislamu. Walikuwa radhi uhuru wa Tanganyika ucheleweshwe mpaka Waislamu watakapokuwa tayari kushika nafasi za uongozi. Huo ni nini kama si ubaguzi? Mtemvu yeye alitaka Tanganyika iwe ya Watanganyika. Full stop. Mmalawi, Mzambia, Mkenya na Mkongo asingeruhusiwa kupata uraia wa Tanganyika. Ni Nyerere ndiye aliye "define" uraia wetu na kwa kuona mbali leo hawa Wahindi waliokuwepo tangu enzi za ukoloni ni ndugu zetu. Talk about common ground!Mkuu Mkandara,
Heshima kwako,miaka michache iliyopita nilipojiunga na JF nilijaribu kwa mbali ku-rise issue hii ya Nyerere ukani crash pamoja na wachangiaje wengine na kuniambia nilikua na "labda Nyerere kuna kitu alinifanya mimi binafsi au familia yangu" na kwakua sikua na utafiti wowote (kama Muhamed Said) nikaliwacha jambo lile.Nilijaribu kuleta kile ambacho nikua nikielezwa na kukisikia.
Ila kama lilivyo kila jambo dunia lazima litapata wa kulisemea hata kama mbele zaidi miaka mia,wakati wake umefika sasa kwa jambo hili.Labda uniambie wewe hukutani na maneno ya namna ya Muhamed Said huko uliko ila ni kitu cha kawaida sana wanapokaa watu wa imani sawa kuzungumzia mustakabari wa imani yao.
Usipate shida sana kutetea jambo lililo wazi muda ni muafaka upande ule mwingine kujua kwamba upand e huu wanalijua hili na wanalizungumza labda itasaidia kupunguza ama kuondoa tofauti hizi.
As for Muhamed Said,yeye ni mtu mdogo sana kuleta machafuko kwenye nchi hii,na nina imani hiyo sio nia yake kuletea vurugu baina yetu ila yafaa kuzungumza ile tupate common ground which will be based on mtual understanding for a lasting peace kama mababu zetu walivyo ishi zamani.Lakini kung'ang'ania kila kitu kiko sawa ni kuletelea msiba....
Mag3,'Bila shaka yoyote kuna wana JF wengi labda wanajiuliza kwa nini sitaki kuwa na majibizano ya moja kwa moja na huyu mchochezi anayejiita Mohamed Said. Mwanzoni nilifikiri huyu bwana kweli ana nia ya kuandika historia ya watu waliochangia kwa namna mbalimbali katika harakati zetu kama Watanganyika kupigania uhuru wa nchi yetu. Hivyo mimi pamoja na wachangiaji wengine kwa nia njema kabisa tulijaribu sana kumwelimisha kuwa si kweli hao wazee wake wa Gerezani ndio waliotoa mchango mkubwa kuliko Watanganyika wengine. Dar es Salaam ambako ndiko yalikuwapo makao makuu ya serikali ya kikoloni, pamoja na kuwa mji mkuu wa Tanganyika, kalikuwa kamji kadogo chenye wakazi wasiofikia hata laki mbili. Dar es Salaam ilikuwa ndani ya Jimbo la Pwani, moja ya majimbo manane nchini Tanganyika, na liliunganisha ambayo hivi sasa yanajulikana kama Mkoa wa Morogoro, Mkoa wa Pwani na Mkoa wa Dar es Salaam yenyewe.
Kwa sababu lengo hasa la Mohamed Said halikuwa la kuandika historia ya kweli kama alivyodai mwanzoni, badala ya kutupongeza wengine tuliokuwa tukimpa somo kuhusu Watanganyika ambao yeye hayuko tayari kuwataja kabisa ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya, akaanza kutukejeli kuwa na sisi kama tunataka tuandike historia yetu. Baada ya hapo tukamshauri kwamba kama ni hivyo, basi hiyo historia anayoiandika aseme wazi kabisa ni ya Wazee wake wa Gerezani na asithubutu kudai kuwa ni ya Watanganyika. La haula ! Mohamed Said kwa chuki ambayo imetawala hisia zake potofu, akashindwa kuficha tena hasa lengo lake - anapiga vita dhulma waliyofanyiwa na wanayoendelea kufanyiwa Waislaam pamoja na kwamba wenyewe ndio walitoa mchango mkubwa katika kudai uhuru. Mohamed Said, bila kificho, anadai haya ni mapambano dhidi ya mfumo Kristo ambao umetumiwa kukandamiza Uislaam toka na baada ya uhuru.
Mimi Mag3 nimejaribu kumweleza kuwa pamoja na kuwa na uelewa mkubwa wa mambo ya siasa katika miaka ya 1950's sikuwahi kuwasikia wala kuwaona hao wazee wa Mohamed wa Gerezani. Pamoja na kufika Dar es Salaam kwa mara ya kwanza mwazoni mwa miaka ya 1960 baada ya uhuru sikuwasikia hawa Wazee ukiacha Zuberi Mtemvu ambaye jitihada zake, pamoja na mapungufu yake ya kimkakati, hazikumfikisha mbali. Tumejaribu kumwelewesha Mohamed Said jinsi TAA ilivyoundwa mwaka 1929, malengo yake yaliyoainishwa katika katiba na uendeshwaji wake kwa kutojihusisha na mambo ya siasa. Wengine tumempa somo kuhusu maraisi wa TAA (waliokiongoza) tangu kuundwa kwake na Gavana Cameron hadi kuundwa TANU (chama cha siasa) mwaka 1954 na Mwenyekiti wa TANU tangu wakati huo hadi tunapata uhuru. Tumemwomba awataje hao wazee wake walioongoza hivyo vyama, yeye kakazania porojo za wazee wake !
How convenient kwa wenye mawazo potofu kama Mohamed Said kuwa mbinu za kuhusisha Ukristo na mfumo wa serikali baada ya uhuru hazingeweza kufanikiwa bila kwanza kumchafua Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Na kumchafua Mwalimu hakungeweza kufanikiwa bila kuzua kinachoitwa chuki yake dhidi ya Uislaam na hivyo kuwateka Waislaam ambao mathalan dini imehusishwa, watatetea mada mradi mtoa mada ni Muislaam mwenzao. Bahati nzuri Waislaam wa Tanzania walio wengi (hasa ninaoshirikiana nao - marafiki, ndugu na comrades) wanaelewa fika hizo mbinu chafu zenye kujali maslahi ya watu wachache na si taifa letu tunalolipenda la Tanzania na hawako tayari kuzibariki bila tafakari. Hii ni moja ya sababu inayonizuia kujibizana na Mohamed Said moja kwa moja (people might not notice the difference) na ninawaachia Waislaam hawa wenye mapenzi ya kweli na taifa letu, wachambue mchele na pumba katika haya ninayoyaandika.
Juzi kuna kundi la Waislaam wamejitokea na bila kificho wamewaagiza waumini wao wasikipigie Chadema kura ! Ni bahati gani tamko kama hili halikutolewa na kikundi chochote cha Kikristo, lakini nachelea kusema kwa uhakika kuwa lingetokea hilo hivi sasa tungekuwa tunaongelea mengine. Katika uchaguzi wa mwaka 2010 alianza mwandishi wa gazeti la serikali kwa jina Ali Mkumbwa akatumia maneno yenye mtizamo na mwelekeo kama huo lakini hadi leo anaendelea kuchapa kazi bila wasi wasi katika mfumo Kristo. Watu kama Mohamed Said tusiwapuuze, nyuma yake kuna kubwa zaidi ya hili la kudai kuandika historia ya kweli na bila shaka hii mada inavyoendelea anazidi kujifunua kwa sura yake halisi - nimesoma kwa makini michango yake ya karibuni ambayo yaonyesha kabisa kuwa anataka nini. Anadai Uislaam unawapa watu woga na anaonya kuhusu yatakayotukuta sisi wazalendo ambao tumetanguliza Utaifa mbele ya Udini anaoupaka rangi akisahau hiyo rangi haibadilishi umbile.
Tumemtolea Mohamed Said mifano kuwa katika harakati zote za kudai mabadiliko popote pale duniani kimfumo au kiutawala, lazima anatokea kiongozi ambaye hupata sifa za pekee na huyu si mwingine ila ni yule anayefanikisha malengo ya harakati hizo. Mtanganyika hakutakiwa kusafiri hadi Dar es Salaam ndio awajue Wazee wa Gerezani na laiti hao wazee wangekuwa maarufu kiasi hicho, hawangemhitaji Mwalimu Nyerere aje awaongoze lakini nakumbuka katika ujana wangu jina tu Nyerere lilivyoenea mpaka kijijini na hadi leo, CCM inapokwama inamtumia Nyerere kama mtaji wake. Kwa nini hata Lindi, jina la Nyerere litajwe kwenye kampeni na wagombea na si la akina nani vile ! Abdul Sykes ! Jamani tuache hizi soga zisizokuwa na kichwa wala miguu, hadi watoto walizaliwa wakati huo wakaitwa Nyerere Mikindani hadi Kibondo, Usangi hadi Tukuyu na Mafia hadi Tumbatu. Na hapo bado Auckland hadi Edmonton, Kyoto hadi Guyana na Cape Town hadi Tripoli.
Nimeeleza Mwalimu alivyoona aibu kuongoza nchi huru na huku mji wake mkuu, ukiacha Uhindini na Uzunguni, wazawa wanaishi kwenue nyumba za makuti. "Operation Makuti" ilianzishwa makusudi kuwapa makazi bora hawa watu inaodaiwa Mwalimu hakutaka wapate maendeleo na hili ndilo lilikuwa lengo kubwa la kuanzishwa kwa Shirika la Nyumba. Wana JF mtafakari na muamue wenyewe kuhusu michango ya Watanganyika mbali mbali na "sacrifices" ambazo ilkuwa ni lazima zifanyike ili tuweze kujenga taifa lenye umoja na mshikamano. Kwa bahati nzuri au mbaya, Raisi wa chama cha siasa anaweza kuwa moja tu na Raisi wa nchi anaweza kuwa moja tu, na historia kamwe haitafuta ukweli kwamba Raisi wa Kwanza wa TANU na Raisi wa kwanza wa Tanganyika huru angeweza na alikuwa moja tu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wanaolilia wazee wao, wakumbuke tu kitu kimoja, mtu aliyeongoza harakati hizo alipatikana kwa kura baada ya kuwa na sifa kuwashinda wengine.
halafu soma hiiMohamed Said 2697723:Hakuna Muislam anaeweza kuthubutu kutangaza Uislam kwa jina la mtu. Sijafanya hivyo na wala siwezi kuthubutu
anaendelea hiviMohamed Said; IngawaWaislam ndiyo walioleta uhuru wa Tanganyika, manufaa ya uhuru ni madogo sana kwao
Ikifika hapo kama huamini udini ndio unaomuongoza Mohamed na anatumia majina kuutangaza Uisla basi hutamwelewa kamwe!Mohamed Said: Huko umekwenda wewe mie haja ni kuonyesha mchango wa wazee wangu katika uhuru wa Tanganyika,alikuwepo Sheikh Yusuf Badi, alikuwepo Salum Mpunga, alikuwepo Yusuf Chembela nk
Wawili wamevaa suti na tai. John Rupia hana utambulisho, Saadan Kandoro hana utambulisho. Nyerere amevaa soksi hadi magotini. Haina tabu, kavaa kweli lakini kumbuka ni Mohamed huyo huyo aliyewahi kusema, Nyerere akija Dar si lolote si chochote(ushahidi upo) na kwamba alipewa pesa za kitoweo n.k. Kwasisi watu wa pwani hii ndiyo lugha yetu msituone wanafiki.Mohamed Said;2694530]Abdulwahid anaonekana akiwa amevaa miwani ya jua akiwa amesimama kushotokwa Dossa Aziz; wote wamevaa suti na tai. Abdulwahid anaiangalia kamera. Raismstaafu Julius Kambarage Nyerere amevaa kaptura na soksi ndefu hadi magotini amekalia benchi mkono wa kushoto wa John Rupia. Aliyesimama nyuma ya Nyerere,Saadani Abdu Kandoro
Mohamed anaposema Nyerere amevunja baraza la wazee wa TANU, lakini hajui majina ya wajumbe wa kamati kuu iliyokaa na Nyerere kufikia uamuzi. Kwamba anamhukumu Nyerere kwa dhana bila uthibitisho, halafu anasema Uislam unakataa dhulma ile ile anayoitenda yeye kwa kuhukumu pasi na ushaidi. Tuhuma zinandeleaMohamed Said;2697723]Mkandara, Ila nitafahamisha moja ya mafunzo ya Uislam. Allah anawaasa Waislam "wasidhulumu na wasikubali kudhulumiwa."
Kila mtu asiye mwislam ni mkristo amekataa kitabu chake kisitumike, dhulma! kama angetaja majina tungeelewa ni Uislam, lakini kwa kuongozwa na dhana ya 'wao' na kuwatuhumu maprofesa wa Physics na medicine kuwa ni wakristo na wamekataa kitabu chake inasikitisha mzee Said.Christian lecturers at Dares Salaam University are discouraging students from making references to thosetwo books
Barubaru;2696526]Kwani ufahamu kuwa Shoka haliwezi kukata miti bila kuwekwa kipande cha mti (mpini)
Mzee Said, tunakuomba usiweke vipande vya habari. Tunavyo katika magazeti na vitabu ikiwa ni pamoja na hapa JF. Ukiulizwa swali jibu swali, wewe ni mwandishi na moja ya sifa za uandishi ni kuweza kuwasiliana na hadhira yake kwa ufupi na ueledi(concise and precise). Usifanye maandishi yako kuwa ni reference muhimu kwetu, ni muhimu kwako na wale wanaomeza bila kujua lengo lako. Usijaze kurasa tafadhali.
Pili naona kuna wnaJF bado wanasita kuamini kuwa lengo la Mohamed ni udini. Mkuu Mkandara amekuja 'wima'kama wengi walivyosimama wima kupinga upotoshaji na udhalilishaji wa dini unaofanywa na mtu au watu wenye chuki kuu mioyoni mwao. Mkuu kasema uislam unasimama peke yake bila jina la mtu, na ukweli ni kuwa Mtume Muhamad S.A.W hakuutangaza Uislam kwa jina lake licha ya karama alizomruzuku mwenyezi, sijui Mohamed anayatoa wapi katika Quran, hadithi, sunna kuwa Uislam lazima uambatanishwe na majina
Lugha anayoielewa Mohamed ninapotoa hoja ni ile ya kumnukuu mwenyewe maana utaratibu wake ni wa kwenda mbele na nyuma, kubadili hadithi(flip flop), na huwa anasema hanielewi kwa matusi ya sisi watu wa pwani, ikiwa na maana mimi jinga fulani hivi.
Soma hii halafu soma hii anaendelea hivi Ikifika hapo kama huamini udini ndio unaomuongoza Mohamed na anatumia majina kuutangaza Uisla basi hutamwelewa kamwe!
Ukitaka kujua anavyomchukia Nyerere kwa hila na kwa kina ndani ya nafsi yake, lakini akinasibisha kwetu kuwa ana mheshimu, soma hii nikupe analysis. Sisi watu wa Pwani huwa hatusemi ;mshamba wee!' tunasema hajajua kula chapati. Sisi huwa hatusemi ;mjinga' tunasema hajaelewa. Sisi wa Makorara huwa hatusemi 'mwendawazimu' tunasema ameghafilikiwa. Soma Wawili wamevaa suti na tai. John Rupia hana utambulisho, Saadan Kandoro hana utambulisho. Nyerere amevaa soksi hadi magotini. Haina tabu, kavaa kweli lakini kumbuka ni Mohamed huyo huyo aliyewahi kusema, Nyerere akija Dar si lolote si chochote(ushahidi upo) na kwamba alipewa pesa za kitoweo n.k. Kwasisi watu wa pwani hii ndiyo lugha yetu msituone wanafiki.
Angalia hapa chini Uislam unavyoingia halafu unavyochanganywa na hisia za mwanadamu ili kukidhi haja za matakwa ya kiroho. Mohamed anaposema Nyerere amevunja baraza la wazee wa TANU, lakini hajui majina ya wajumbe wa kamati kuu iliyokaa na Nyerere kufikia uamuzi. Kwamba anamhukumu Nyerere kwa dhana bila uthibitisho, halafu anasema Uislam unakataa dhulma ile ile anayoitenda yeye kwa kuhukumu pasi na ushaidi. Tuhuma zinandelea Kila mtu asiye mwislam ni kristo na amekataa kitabu chake kisitumike, dhulma! kama angetaja majina tungeelewa ni Uislam lakini kwa kuongozwa na dhana ya 'wao' hata kama ni profesa wa Physics midhali ni mkristo naye amekaa kitabu chake.
Watu wa bara wanasema 'roho mbaya' sisi watu wa Mabawa polisi tunasema, ah ah lugha ya kiungwana ni kusema hiyo ni fitna!!
Hutaki dhulma, ile ile anayoiandika kwa mkono wako.
Kwahiyo hakuna haja ya kudhani kuwa alimchukia Nyerere, tunachojiuliza ni kwanini? na kwanini chuki hii anaifanya sehemu ya dini!
Amekubali kuwa historia ni ya Gerezani, basi tukubaliane naye ila akisema neno Tanganyika, tumwambie Tanganyika si Kipata au Gerezani.
Huyo ndiye MSS na harakati za kupandikiza chuki, kuchochea vurugu. Akiitwa Mnyapala wa wazungu anasema katukanwa, labda kauli hii ya mwenzangu wa pwani kule Unguja ina lahaja ya yenye stara
Mohammed,
Nahitimisha ushiriki wangu katika mjadala huu kwa kukuuliza mara nyingine tena swali moja tu: Umezipamba sana juhudi za Abdulwahid Kleist
katika ukombozi wa Tanganyika. Hata umeandika kitabu juu ya juhudi hizo na kuweka jina lake. Sasa kuna mahali ulisema kuna nyaraka za maandishi yake huyo huyo Abdulwahidi lakini familia yake imekataa kukupa hizo nyaraka. Je, unafikiri ni kwa nini familia ya mtu unayemsifia sana hawajakuamini vya kutosha kukupa nyaraka na memoranda za personal messages zake? Kama mwanahistoria ningefikiria kuwa familia yake ingefurahi kuona kuwa hizo nyaraka zimo mikononi mwa mtafiti makini kama wewe, au?
Mwanakijiji, najua kwa nini ungependa ajibu swali hilo lakini si ajabu hata hilo halifahamu kwa sababu, if you can read between the lines, hizi anazoleta humu kama simulizi za wazee wake ni matokeo ya mpango wa muda mrefu sana. Kama nilivyosema mwanzo ni maandishi yaliyofinyangwa na kuungwaungwa kwa nia moja tu, kuipotosha jamii na si kazi ya mtu mmoja.
Majibu anayoyatoa kwa maswali kadhaa yanamuumbua ni wapi anapata reference na naweza kukuambia ilikuwa ni swala tu la muda mwafaka, haya mambo yamepikwa, yakaiva na sasa yanawekwa mezani na mwenye njaa kama kawaida akikuta meza tayari anafikiria kula tu hata chakula kikiwa na sumu. Nimejaribu kupima uwezo wa huyu Mohamed Said jinsi anavyojibu maswali anaji betray kwa sababu labda hakujitayarisha kuupata upinzani kama anaoupata humu.
Mohamed Said ni mtu hatari, amekubali kutumiwa tu katika ajenda ambayo huenda ni kubwa kuliko tunavyofikiria. Nina hakika great thinkers wa humu ndani tukiunganisha dots kama kawaida yetu, tutaweza kuuanika huu mpango mchafu na chanzo chake, ni swala la muda tu na tukumbuke kuwa mchelea mwana hulia mwenyewe. Jaribu kutafuta hizi mada zake ambazo kwa sasa hazionekani humu JF na alivyokuwa akitetea hoja zake.Tanzania, be warned.
aah yeshakuwa hayo tena shehe? yawezekana hukumbuki muda uliochukua kuandika kitabu chako?
Mzee Said Waislam hawana tatizo, ila kuna tatizo linalopandikizwa kwa waislam. Unapokwenda na kumwambia mtu ni second citizen na unajua hajui maana yake na wala hawezi kuhoji, yeye si tatizo tatizo ni mto habari. Kama Waislam ni second citizen, je wapagan na Atheist wao ni daraja gani, mbona hao hueleziNguruvi3,
Mwisho nakuomba fanya utafiti wako mwenyewe juu ya hali ya Waislam ilivyo sasa hivi nchini nina hakika utajua kuwa mambo si kama yalivyokuwa zamani.
Tunalo tatizo ambalo lazima tulijadili tunapenda au hatupendi. Mohamed
Dhulma zipi? maana unajibu kitu unachoulizwa, kama hakuna swali au hoja unatoaje majibu.Nguruvi3,
Ahsante kwa juhudi zako lakini bahati mbaya unatoa majibu wewe.
Yule Waislam tunaemtuhumu kwa dhulma kakaa kimya.
Mohamed