Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa


Sheikh Mohammed.. nikupe pole kwa mitusi uliyoporomoshewa na Mag3. Licha ya kukiri kama umri wake ni mkubwa zaidi ya wa kwako lakini majibu yake yaliyoambatana na kejeli ni kiashiria kama kuna walakini kwa mchangiaji huyu. Woga anaozidi kuoonyesha kwa kuficha jina lake na kujiita mag3 ni kielelezo kingine cha kumtambua aina ya mtu unayejadiliana nae.

Ikiwa anashindwa hata kuthubutu kutaja jina lake na kuishia kuporomosha matusi ni dalili ya mtu muoga anaethubutu kutoa matusi nyuma ya pazia.

Ila nukta ya kukumbuka.... kitendo chake cha kukiri kama yeye licha ya umri huooo mkubwa alioutaja ya kuwa hajawahipo kusikia majina ya bwana wakubwa hawa uliowataja ni kielelezo kingine cha kujua kiwango cha uweledi wa historia ya nchi hii. Ila napata faraja kama .. mtu huyu na wengine wenye muelekeo wake watafaidika sana kwenye munakasha huu.

Mods
Nimestushwa kuona thread hii ilihali kuna thread mama inaendelea.... falsafa ya kuanzisha thread hii sijaijua. Maana huku ni madongo tu baina ya pande mbili..ilihali kwenye ile thread mama kuna mtiririko wa majadiliano ya madda husika. Ushauri wangu..hii thread iunganishwe na ile ya awali

Shkh Yahya.
 

nafurahi kuwa zile hoja zinazostahili kujadiliwa na watu wenye hadhi ya forum hii zimeanza kujitokeza tena na kwa kweli zinachokonoa bongo na fikra za watu hadi inatia msisimko.

kuna ushahidi wa wazi kuwa kuna vipande vya historia vimezuiwa ama kupotoshwa kwa makusudi(sielewi ni kwa maslahi ya nani) na tumekuwa miaka yote tukiaminishwa kwamba harakati za kupigania uhuru ziliasisiwa,kuratibiwa na hata kufanikishwa na MWALIMU!! siku zote tumeshindwa kujiuliza maswali madogo tu kuwa kwa nchi kubwa kama TZ ambayo ilikuwa haina miundombinu kama ilivyo sasa, mwalimu aliwezaje kupata fedha,wenyeji n.k mpaka TANUikaweza kukubalika nchi nzima.
nisingepedna kuingia ndani zaidi lakini naamini kitu kimoja ambacho hata mwalimu nyerere alikuwa anakiamini nacho ni wakati makabila madogomadogo, masikini na yasiyo na elimu ya tanzania yakiunganisha nguvu na fedha zao kwa ajili ya mapambano dhidi ya ukoloni,, na wakati mwalimu nyerere akiwa sambamba na wananchi wenzke toka katika jamii hizi masikini,, yale makabila yanayojiona leo hii kuwa ni makabila ya wasomi,wenye fedha na madaraka ndio yaliyokuwa hayataki kujishughulisha na harakati za kupigania uhuru na hawakuwa tayari hata kutoa michango ya fedha kusaidia harakati hizo,kwa vile wengi wao walikuwa wanafanya kazi katika serikali ya kikoloni, hawakuona ubaya wa ukoloni na hivyo hawakuona maana ya uhuru,
wale wachache wenye upeo na uelewa wa hali ya juu( nyerere,paul bomani,rashid kawawa,abbas mtemvu, abdul sykes.oscar kambona n.k) walikuwa wanapata support kubwa toka makabila madogodogo na yasiyo maarufu hivi sasa.

ushahidi uko wazi kwani hata mikutano muhimu kabisa ya TANU ilikuwa ikifanyika maeneo hayo,ofisi za kwanza kabisa za TANU zilifunguliwa maeneo hayo na hata wanaharakati wa mwanzo kabisa wa sisa za kudai uhuru walitoka maeneo hayo.

Hata mwalimu angekuwa hai leo na umuulize kama ni busara sisi wa TZ tumchague raisi kutoka makabila fulanifulani(siyataji) mwalimu angesema HAPANA tena kwa herufi kubwa kabisa kwani makabila haya yana sifa kubwa tatu nazo ni 1.usaliti-haswa kama usaliti wake utampa faida ya kifedha 2.uoga- haswa kama uoga wake utamfaya asipoteze kile anachokipata kwa muda huo. 3. ubinafsi- kwa kuamini kwa sababu wao wengi wamesoma na wanafedha basi wao ndio bora na haki kuliko wengine na kudhani kwamba wao ndio mabwana nasisi wengine tubaki kuwa watwana
 
Banned 4 ever,
Mbona na wewe umekuja na theories zako ambazo hazina mashiko? Wasukuma ni kabila dogo? Unajua wewe mchango wao katika harakati za uhuru? Wahaya ni kabila dogo, na hawa mchango wao je? Na Wachagga, na Wanyakyusa?

Ni kweli wafanyikazi katika serikali ya wakoloni hawakuruhusiwa kushiriki katika harakati za kupigania uhuru, lakini kuna waliothubutu kwa kutoa michango yao kwa siri.
 
Nimefika hapo kwenye red highlight nikapoteza mvuto wa thread yako. Nenda kaongopee wajinga wenzako huko. Na acha kupotosha uhalisia wa historia yetu. I am sure historia ya ukweli itakuwa wazi si muda mrefu. mmejitahidi sana kufanya historia ya kweli lakini time to ome out is on.
 


Nguruvi3,

..umenikumbusha vipindi vya michezo ya redio enzi zile za RTD[radio tanzania dar-es-salaam]

..hawa walikuwa na vipindi vya maigizo redioni ambapo waliigiza mapambano ya Mtwa Mkwawa,Mtemi Isike, Mangi Meli, etc etc.

..mgomo wa kodi ya MBIRU ulikuwa ni moja ya matukio yaliyoigizwa ktk vipindi hivyo vya redio.

..kitu cha kufurahisha ni kwamba mgomo wa MBIRU ulitumia dhana ya NON VIOLENCE. wananchi walikusanyika bomani kwa DC bila kufanya vurugu yoyote ile.

..kiongozi wa mgomo wa Mbiru alikuwa ni Paulo Mashambo ambaye alikuwa mwalimu na Mchungaji wa Kanisa la Wasabato. Pamoja na hayo mgomo huo ulijumuisha watu wa imani mbalimbali. Kumbuka, kati ya makabila yenye mchanganyiko wa imani za Kiislamu na Kikristo kwa kiwango kikubwa ni hili la Wapare.

..mgomo wa MBIRU ulidumu kwa zaidi ya MIEZI MIWILI!!!

..kumbukumbu haziwekwi tu, lakini hivi mgomo wa Mbiru una tofauti kubwa na yale yaliyofanyika mwaka huu Tahrir square?

..hawa wazee waliweza vipi ku-organize wanaume wa wilaya nzima ya Pare kwa muda mfupi, mfano wa Tahrir square, bila facebook wala Twitter??!!


Mag3,

..Katibu Mkuu wa Pare Union, akiitwa Elias Kissenge, alikuja kuwa Katibu Mkuu wa Tanu, kipindi fulani.

..mikoani Tanu ilirithi mitandao iliyokuwa imeshaanzishwa na hivi vyama vidogo vidogo vya kikabila.

..pia kuna migogoro ilikuwa inafukuta baina ya Muingereza na wazalendo ambayo nayo ilirahisisha mapokezi ya Tanu huko mikoani. Particularly hapo nikumbushe mgogoro wa ardhi ktk eneo la Wasukuma.


 
Naona kila wanapojaribu huwa wanashindwa hata pa kuanzia na wanaamuwa kuanza na matusi. Pole Sheikh Mohamed kwa kutusiwa bila sababu.

Halafu wamejaribu kufika mpaka Upare wakakumbana na TAA sasa waeleze hao wapare kwanini waliungana na TAA na waasisi wa TAA ni kina nani.

Naona wanakuja na hadithi zisizo na mpango wala kichwa wala miguu. Wasomi hao. Wanashangaza!
 

Huyo shehe wako kakudanganya, mimi ninavyo wajua waisilamu hawana mchezo wakidai hoja yao hatakama haina msingi, wako tayari hatakufa kusimamia anochokiamini hata kama ni ushenzi, yuko teyari kukuua ili usimsumbue, kama huyo shehe wako angekuwa hai nadhani kwa sasa angeshakuwa chriatian tena born again.
 


Tatizo lako linaloonekana hapa ni uelewa wako mdogo. Ni kweli kabisa watanganyika walipigania ardhi yao bila kujali dini zao na ndo maana watu wa Dar ambao wengi wao walikuwa wenye maamuzi ya juu walikuwa wa dini fulani lakini walimfuata julius nyerere akiwa wa dini tofauti pale pugu kuja kushirikiana nao. na kumbuka kwanza alikataa kwa sababu yeye alikuwa ameajiriwa na huku akihoji kuhusu kipato lakini wazee wa Dar walijitolea na kuingiza mifukoni kwao na kumlipa nyerere mshahara.

Kumbuka hao watu walifikia hata kufunga saumu kumuombea nyerere mema. Ila sasa baada tu ya kupata uhuru, wewe mwenyewe unajionea hali halisi ya hizo jamii.

Na ndo maana hata unathubutu bila HATA AIBU kusema eti walikuwa nyuma kisiasa na porojo zingine. unakera kwa kweli.
 

Mohamed Said anapotaja wazee wake anaonesha na nini walikifanya na dalili anaziweka wazi, sasa huyo aliyeambiwa na wazee wake bila kutupa dalili za hao wazee walikuwa kina nani walikuwa na harakati zipi, tumuamini vipi?
 

Wacha kupoteza mtiririko thread... huna la kuchangia baki msimaji ..
 
Changia hoja acha kuleta porojo za kipuuzi.
 

Tumeona Mohamed Said akitubwagia kinaga ubaga vitabu alivyoandika na "papers" alizoandika, mihadhara aliyoitowa / hudhuria vyuo mbali mbali duniani, Jee, na wewe upo tayari kutuwekea hapa ili tujuwe "credibility" yako katika historia? au ndio wakudonyoa donyoa mtandaoni? na ya kuhadithiwa na wazee wako ambao hata dalili hautupi walikuwa na harakati zipi katika siasa au jamii wakati huo? Tuwekee wazi ili tusikuone kama ni mpiga porojo tu.
 

Mchangiaji mkubwa wa harakati za kugombea uhuru alikuwa akiitwa John, muumini wa kanisa Anglikana (sio mkatoliki au muislamu).

Katibu Mkuu wa kwanza ambae alizunguka nchi nzima kuhamasisha watu alikuwa anaitwa Oscar, muumini wa kanisa Anglikana... lakini hawa uwaoni wewe unamuona yule mzee tunayeambia alikuwa akikusanya nyanya na kabechi kupeleka nyumbani kwa Mwalimu!

Unayekera ni wewe.

Amandla.
 
Naona wengine hawataki tu kumuelewa Mag3. Ni hivi:
  1. Mwaka 1957, kulikuwa na watanganyika waafrika 8,665,336 nchi nzima.
  2. Wasukuma walikuwa asilimia 12.6 ya watanganyika waafrika, kwa hiyo walikuwana idadi ya 1,091,832.
  3. Mwaka huo huo, mji wa Dar es Salaam ulikuwa na watu 128,742; Tanga 38,053; Mwanza 19,877;Tabora 15,361; Moshi 13,726; Arusha 10,038 na Bukoba 5,276.
  4. Mwaka huo ni asilimia 4.4 ya wakazi wa Tanganyika ndio waliokuwa wanaishi mijini.
  5. Kutokana na ukweli huu, hao watu ambao Mohamed Said anawapigia debe waliokuwa wakiishi kwenye kitongoji kimoja tu cha mji wa Dar es Salaam wasingeweza kufanya lolote hata kama waswahili wote wa Dar es Salaam, Tanga na Tabora wangewaunga mkono.
  6. Miaka ile huku walikokuwa wakiishi watanganyika wengi, mswahili alikuwa anachukuliwa kama mtu asiyeweza kuaminika ndiyo maana wakina Sykes wasingeweza kuwashawishi watu wa huko kuungana nao. Mtu ambaye wangemwamini ni mshamba mwenzao na hasa kama atatambulishwa na watu wa kwao wanaowaamini. Mtu mwenye sifa hii alikuwa Julius Kambarage Nyerere na pengine Oscar Kambona. Sehemu za pwani, Bibi Titi Muhamed alichangia mno kuvuta wanawake na wame zao kuingia TANU.
Ndi maana, tunawashangaa watu wanaotaka kutuambia kuwa bila hao jamaa wa gerezani na misheni kota, mpambano usingefanikiwa. Ni matusi makubwa.

Amandla.....
 

Naona umekuja na hadithi ndeefu na takwimu nyingi lakini hoja dhaifu sana. Mohamed Said anasema hao wazee wa hicho "kitongoji" ndio waliosahauliwa katika historia na ndio yeye ameamuwa kushika kalamu na kuandika historia yao na vipi walishiriki kikamilifu katika harakati za kujitwalia madaraka na hizo harakati walizianza kabla ya Nyerere kukaribishwa kuungana nao.

Kumbuka kuwa hicho "kitongoji" ndio kilikuwa mstari wa mbele katika harakati, hicho "kitongoji" ndio kilikuwa mwanzo wa vyama kama TAA kilicho zaa TANU, hicho "kitongoji" (Ashaakum si matusi) ndicho kilichomvalisha suruali Nyerere, nasikia alikuja na kaptura, na picha zake za zamani kweli zinaonesha akivaa kaptura ya Khaki na soksi ndefu mpaka karibu ya magoti na viatu vyeusi (kama wale wanaocheza ngoma za Kinyasa kama umebahatika kuwaona).

Kinachowekwa sawa ni kuwa siasa za harakati za kudai madaraka hazikuanzia kwa Nyerere na wala Nyerere sio muasisi wa hizo harakati, hao wazee wa hicho kitongoji ndio waasisi wa harakati zote zilizotufikisha kupewa madaraka na Umoja wa Mataifa. Ni matusi makubwa zaidi kuwaacha hao wazee katika historia hususan kwa mtoto wao Mohamed Said, msomi na mtunzi wa historia anaetambulika vyuo vingi vikuu duniani na ambae ameshaandika vitabu na "papers" nyingi zinazotumika katika vyuo vikuu. Ma sha Allah.
 
Wewe nawe una lako utakuwa masalia ya RIZ1 mie naanza hata kuwa na wasiwasi wa hizi harakati za kujivua gamba maana ikumbukwe 2005 tuliskia mengi sana kuhusu Sumaye na Salim lakini baada ya uchaguzi kashfa zile zikaja kujulikana ulikuwa uzandiki na chuki ya kundi fulani dhini ya watu fulani ili Kikwete apite kiurahisi! Sasa tunaanza kuambiwa ati Nyerere hakupewa usaidizi na makabila makubwa wakati ndiyo hayo yaliyompa idadi ya kuimiza wakoloni saa ya uhuru imewadia! Sisi si watoto wadogo humu ndani zile siasa zenu za Bagamoyo za maji taka zitashindwa maana tunawaangalia vizuri na kuwasoma itakapowadia muda mtajua msimamo wetu ni upi! Ila kwa kuwahakikishia tu hoja zenu nyie watu wa Azimio la Bagamoyo hazina mshiko na ni za kitoto sana...
 
Mwingine huyu! Kwanini wasimfunze kuvaa kanzu na sio suruali ya Mwingereza (ambapo JKN aliijua alipokuwa huko kwa Mwingereza akisoma) maana mnachopigania hapa ni udini! Mawazo mafupi yanadhani Nyerere alikuwa hajui suruali na sio mtindo wa wakati huo kuvaa kaptula na stockings! Ikumbukwe Nyerere alikuwa ametoka kusoma Scotland! Na kuna uwezekano yeye ndiye alifundisha hao wazee kuvaa vitu kama suruali na chupi maana kanzu zilikuwa zikivaliwa utupu...!
 
Nakubaliana na Bwana Said na wachangiaji wengine kwamba kuna namna mbalimbali za uandishi wa historia. Hata hivyo, historia yoyote lazima ilenge kuunganisha jamii, na siyo kuisambaratisha. Hapo ndipo ninapotofautiana na Said. Nina hakika kwamba hata hicho anachotaka kutuaminisha kwamba ni mchango wa waislamu katika kuleta uhuru, siyo historia kamilifu ya waislamu. Ninachomaanisha hapa ni kwamba yeye anadhani "waislamu" ni wale waishio mikoa ya pwani tu, huku akisahau kwamba kuna waislamu wengine huko Tabora, Ujiji, Singida, Upareni, Karagwe, n.k.

Mimi binafsi sina tatizo na Bwana Said kuandika historia mbadala. Tatizo ninaliliona ni kutumia udini as a point of departure. Hili ni jambo hatari sana, na nashindwa kufahamu kwa nini Bwana Said haoni hatari anayoitengeneza. Said namfahamu binafsi. Ni mtu mzima mwenye akili zake, tena nzuri tu. Kwahiyo napata shida kidogo anapojivunia kwa aina ya uandishi anaofanya. Bwana Said, utambue kwamba duniani kote hakuna historia iliyokamilika. Historia ni mtazamo, na ni hali ya kawaida kabisa wanajamii kutofautiana mitazamo. Hata hivyo, wanajamii hao hao hufikia sehemu ya kukubaliana kutumia aina fulani ya historia, si kwa sababu ni sahihi sana, bali tu kwa sababu inawahakikishia mshikamano, usalama, na mahusiano mema. Historia yoyote yenye dalili za uchochezi haiwezi kukubalika kwa mtu yeyote mwenye akili timamu, hata kama ingekuwa ndiyo tafsiri halisi ya mambo yalivyotokea.

Hebu futailia hata kwenye familia na ukoo wako. Utakuta mambo mengi makubwa yaliyotendeka huko nyuma, lakini, kwa busara za wazee, walidhani wayaache kama yalivyo ili kudumisha mshikamano wa jamii zao. Sote tunajua kilichotokea Rwanda. Tunajua pia gharama kubwa wanayoitumia sasa hivi kujaribu kuirejesha nchi yao kwenye mshikamano. Gharama hizo ni pamoja na kuchambua kitu gani wakiandike na kipi wakiache kwa manufaa ya vizazi vyao vijavyo. Kwa hiyo, akitokea mnyarwanda mmoja mkereketwa, akataka kuandika hali halisi ilivyotokea (mfano, fulani ndiye alimchinja fulani, n.k.), hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kukubaliana kwamba "historia" ya aina hiyo iwe sehemu ya historia rasmi ya nchi. Itatusaidia nini kujua hali halisi, kama hiyo hali halisi mwisho wake ni vurugu, uvunjifu wa amani, na kuvunja utaifa?

Mimi ninawafahamu wazee kadhaa wa kwetu walioshiriki kuleta uhuru wetu, lakini wako nje ya historia rasmi. Pamoja na hayo, sioni busara ya kuchokonoa sana mambo ya aina hiyo kwa sababu mwisho wake ni kuleta vurugu na uvunjifu wa amani. Tanzania ina makabila zaidi ya 120, na naamini kwamba kila kabila lilikuwa na mtu aliyeshiriki kupigania uhuru. Lakini, kama kawaida ya historia zote, huwezi kumuingiza kila mtu. All histories are selective by nature. History is not just the study of the past, but the study of "significant" past. Simaanishi kwamba mchango wa waislamu haukuwa "significant." Naheshimu sana mchango wa waislamu. Hata hivyo, nadhani historia yetu imebeba majina kama Kawawa, Adam Sapi Mkwawa, n.k. Je, hao si waislamu? Waislamu lazima watoke mtaa wa Gerezani?

Bado nisingepata shida kama Bwana Said angejenga hoja kwamba baadhi ya waislamu "muhimu" wamesahauliwa na historia rasmi iliyopo. Hilo linawezekana, kwani history is constantly made and remade. Uandishi wa historia ni kazi ya mwanadamu, na hakuna mwanadamu aliyekamilika. Pamoja na hayo, nisingependa kujiaminisha kwamba wote waliosahauliwa kwenye hitsoria rasmi ya nchi wamesahauliwa kwa sababu ya dini zao, makabila yao, au kanda wanazotoka. Kama Bwana Said anadhani ana ushahidi wa kutosha juu ya hao waliosahaulika, angetusaidia sana endapo angetuhamasisha (na hasa wale wanaohusika na mitaala mashuleni/vyuoni) ili hayo majina anayodhani yamesaulika yaingizwe kwenye mchakato wa mitaala mipya ijayo. Hili linaweza kufanyika bila uchochezi wala kupandikiza mbegu za udini wala mfarakano. Nchi yetu tayari iko ICU kutokana na ufisadi na "siasa uchwara." Tukiongeza na haya ya udini sijui tutafika wapi.


Nawasilisha.
 
GU
Bora umemjibu huyo bibi .... Nilishangaa sana huyu mama alivyokurupuka Udini ni kitu kibaya sana .... Yaani Nyerere katoka scotland na alikuwa ni mwalimu halafu unasema alikuwa hajui kuvaa suruali. Sasa hao wanafunzi aliokuwa anawafundisha si walikuwa hawavai nguo kabisa.. FF mama usikurupuke kumbuka kuwa hapa wapo watu makini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…