Hapa kwa Nyakanga,
Hazishi nyimbo. Lete swali.
Mohamed
Hiyo asilimia 83 ni statistics zinazopatikana wapi nami nikajionee?
Go figure...indeed strange that he thought he would get away with this...
Kwa kweli mtapata tabu labda mfanye kama alivyokushaurini FF.
Andikeni kitabu.
Nendeni kwa Mama Maria, Mkapa na wengine wengi sana.
Mimi nimekupeni "cue" nishakusafishieni njia.
Sasa hicho kitabu chenu ndiyo kitakuwa jibu la kitabu changu.
Lakini kwa kutaka kujibu kitabu changu kwa sentensi katika JF mtakesha na mimi.
Mwenzenu mimi baada ya kuona wazee wangu wametolewa katika historia nimeandika hilo buku leo unaona nyote mmemjua Mshume Kiyate, Sheikh Hassan bin Amir, Rashid Sisso, Tatu bint Mzee, Bi Mluguru bint Mussa na wengine wengi.
Mmejua kuwa hotuba ya Nyerere iliandikwa toka 1950. Mmejua kuwa kuna historia ya TANU iliyoandikwa siku za mwanzo za uhuru ikapotea na mengine mengi...
Vipi mtachukua hii changamoto?
Mohamed
Una evidence kuwa JK fisadi? Mnamzushia tu JK kila siku subirini kesi ya Ridhiwani na Dr Slaa imalizike mtaelewa JK kama fisadi au la. Hao niliwataja kila mmoja ana liscandal lake kuanzia waliouza wanyama na ardhi kwa waarabu hadi kwa wauzaji wa nyumba za serikali. Turudi katika mada mnacho cha kukosoa kuhusu kazi mohamed said.
Hili ni swali zuri sana; kwa kweli siyo changamoto kama unavyoiona na ni changamoto ambayo naamini itakuja kujibiwa na Waislamu wengine. Toka mwanzo wa historia yetu yamekuwepo makundi mbalimbali ya kisiasa. Hata kwenye suala la dini ni hivyo hivyo. Kitu ambacho wengi tumefanikiwa katika mjadala huu ni kuonesha kuwa:
a. Ulichoandika katika kitabu hiki siyo historia bali ni simulizi tu ambalo halina ushahidi wa historia zaidi ya hisia.
b. Unatumia dini kuangalia historia na kuweka tafsiri ya kidini kwa kutumia historia na kudai "wazee" wako si kwa sababu ni wazee wa historia yetu bali ni kwa sababu ya kuwa unakubaliana nao kuwa ni dini moja.
c. Wapo watu ambao nina uhakika nao wazee wao walikuwa ni Waislamu na walikuwa upande mwingine kabisa wa kina Takadir na kina Sheikh Amir.
Hivyo watakuja Watanzania ambao wataiokoa historia yetu kutoka mikononi mwa mtazamo wa kidini na kuiweka mahala pake hasa. Wale ambao watawaunganisha wazee wetu katika umoja wao na uzalendo wao siyo kwa dini zao bali kwa Utanganyika na Utanzania wao. Litakapotokea hilo kitabu chako kitabakia kama simulizi la majaribio tu na mapungufu yake yatawekwa bayana. Ninatumaini hili litatokea mapema zaidi.
Wewe kama hujui kitu ukae kimya using'ang'anie upupu kwa kuwa raisi ni wa dini yako.
Mbna mkapa anatuhuma za kuihujumu serikali na wakrito hawamtetei?
Mdondoaji utadondolewa.
Mwanakijiji,
Usiwe na haraka safari yetu Waislamu bado ni ndefu serikali haijakubali kuwa tuna tatizo. Hadi hapo watakapokiri kuna tatizo na kutaka ushauri kipi kifanyike hapo ndipo tutazungumza nini kifanyike.
Kwa sasa tujikite katika kuisihi serikali iamke tuiepushe nchi yetu na vurugu.
Mohamed
In your way of thinking but in the intellectual way of thinking Mwanakijiji you are dead wrong soma huyu jama amesemaje kuhusu kazi ya Mohamed Said:-
In recent years historians of nationalism, like historians of science, have been turning to the stories of the losers. In studies of South Asia as well as Africa, authors such as Allman, Geiger and Mbembe have sought to escape the triumphalist trap of assuming that nationalist politics were shaped solely by the men who eventually took power. A focus on historical dead-ends can illuminate the contingencies that shaped nationalism, and can also help explain many postcolonial political conflicts. Mohamed Said's book is one such study.
Kitabu kinachozungumziwa hapa ni Life and Times of Abdulwahid Sykes...... ambacho wasomi wa JF mnasema ni simulizi, takataka blah blah. hamna lenu moja nimewaambie fanyeni na nyie publication tuzisome na sio kuleta ukosoaji usio na kichwa wala miguu.
Mkapa hatoki kwenye tuhuma zinazomtuhumu ana Anben, Mchuchuma, na madudu mengi humo ndani. Kikwete ana nini? Tangu 2006 tuhuma zote zinaishia katika cloud of speculation and allegation zisizo na msingi. Hebu taja basi JK ana nini maana sizijui kabisa. JK simtetei na sifurahishwi na namna anavyowashughulikia mafisadi kwani amekuwa mwoga katika kuwashughulikia mafisadi ila namtetea kama nyie mnaleta tuhuma kwasababu ya dini yake hapo siwaachi nakula na nyie sahani moja.
Hii si picha ya Mwarabu. Ni Mmisri wa kale kabla nchi haijavamiwa na Waarabu. Masalia wao ndio Waethiopia wa leo na Wanubi wa Sudan. Na wewe kajifunze historia.
Soma post niliyobandika hiyo picha nilisema Mwaarabu? Unanchekesha!
Have you read the book Mdondoaji?
Haaa haaa haa! leo hii kuna member waislaam wengi CCM kuliko wakati wowote! na wameyabeba mabango kwa ajili ya CCM... Wengine tunao humu JF, wengi wameondoka hata CUF na hawataki hata kusikia, halafu unataka kusema vitu vilivyotungwa na mtu akilini wakati hajui ukweli umesimama wapi?
Deep green finance ilikuwa ya nani?
Kupotezwa kwa ushaidi wa BOT ambao alikuwa nao Balali?nani alihusika?
Wahindi kupewa reli kama asante ya magari ya mahidra yaliyopga kampen za jakaya?
Mwanakijiji,
Nikusahihishe kidogo.
Diamond 2 Waislam tumekubaliana wakati wa kulalamika umekwisha.
Sasa ni wakati wa "kushughulika vizuuuri."
Mohamed
Mhhh kweli comment nyingine unaweza kudhani mtu kachoka au kajisahau.Mohamed Said said:Mwanakijiji,
Swali hilo mbona nyie ndiyo wa kulijua zaidi kwa kuwa ndiyo mmeshika madaraka kwa 83%.
Masikini ya mungu sisi nafasi zetu wahudumu, wapika chai, madereva, shamba boy sasa hayo mambo ya huko maofisini ya ufisadi, sijui nini tutayajuaje?
Mohamed
Yes ila mara moja why? Usiniulize kuhusu mapungufu yake kuna mapungufu nimeyaona Mwanakijiji but he has done a substantial amount of work which highlight there is a need to revisit the history of nationalism in Tanganyika.
Mdondoaji - umesema jambo kubwa sana. Miye binafsi - na nimelisema hili huko nyuma - Mchango wa Bw. Said katika kuandika historia "yetu" ni mkubwa sana kuliko hata anavyojua. Ni kweli kuna mapungufu mengi - na mengine naweza kusema ni makubwa sana - katika kitabu chake lakini all in all ni kitabu ambacho binafsi ningependa kisomwe na watu wengi zaidi lakini kisomwe kwa kutumia uwezo wa kuhoji na umakini wa kutambua ni wakati gani kinachosemwa ni historia na wakati gani ni hisia na hasa kuelewa mapema kabisa the underlying theme ya kitabu chenyewe - kuonesha kuwa Nyerere hakuwa na mchango wa kipekee katika historia ya Uhuru kulinganisha na waasisi wengine wa Taifa letu.
Ninakuhakikishia baadhi ya matatizo mengi ambayo tunayazungumza tatizo lake ni CCM na hili mimi na Said tunakubaliana sana. Tofauti ni kuwa siamini kama CCM ina interests wala uwezo wa kushughulikia matatizo hayo ya kihistoria wakati yeye anaamini kuwa serikali hii hii inaweza kushughulikia matatizo hayo. Sijui uko upande gani katika hilo lakini sentensi yako hapo is telling.
Jasusi, Umepatia kwelikweli. Waislam tunadai uhuru anakuja mtu anatueleze ati sijui Gavana kanunua Rolls Royce mpya na ma Pronvicial Commissioner wote katika majimbo kawamwaga na ma Humber. Sisi hilo tatizo letu? Tunadai uhuru kwanza hilo ndilo la kutushughulisha sisi. EPA nk hizo ofisi zote wamekalia wao sie tumo huko? Hatuna muda wa kucheza mkole usio kuwa wetu. Kwani wenye ngoma yao wametualika? Mohamed
By Mohamed Said
Mwanakijiji, Swali hilo mbona nyie ndiyo wa kulijua zaidi kwa kuwa ndiyo mmeshika madaraka kwa 83%.
Masikini ya mungu sisi nafasi zetu wahudumu, wapika chai, madereva, shamba boy sasa hayo mambo ya huko maofisini ya ufisadi, sijui nini tutayajuaje?
Mohamed
But what makes you think CCM ni tatizo? Nini source ya CCM kuwa tatizo? Hili ndio swali la msingi tujiulize na ndio nilijiuliza wakati nasoma kitabu cha Sheikh Mohamed Said. Kwa bahati mbaya nilikisoma nikiwa nje ya nchi nikakiacha huko kwani ulikuwa ukionekana nacho Dar hatari tupu. Sijui siku hizi hali ikoje ila nimekusudia kukinunua nikiweke katika maktaba yangu nitakisoma tena mbeleni .
another song , another rythm in this thread...im not going anywhere.....Mkapa hatoki kwenye tuhuma zinazomtuhumu ana Anben, Mchuchuma, na madudu mengi humo ndani. Kikwete ana nini? Tangu 2006 tuhuma zote zinaishia katika cloud of speculation and allegation zisizo na msingi. Hebu taja basi JK ana nini maana sizijui kabisa. JK simtetei na sifurahishwi na namna anavyowashughulikia mafisadi kwani amekuwa mwoga katika kuwashughulikia mafisadi ila namtetea kama nyie mnaleta tuhuma kwasababu ya dini yake hapo siwaachi nakula na nyie sahani moja.
corruption, greed, intoxication of power, impunity, abuse of power, indignity, I could go on and on.. hata hivyo labda utasema tatizo ni "kanisa"! Ni jibu zuri kihisia lakini halielezei ukweli kwani matatizo ambayo tunayaona Tanzania leo hii yanatokea Jordan (Waarabu wa Jordani na wale wa Palestina); tunaliona Misri (Waislamu walioko madarakani dhidi ya wale ambao hawako madarakani), tunaliona Syria (Waislamu Vs Waislamu) na kote huko utaona kuwa hao kule hawawezikulalamikia "kanisa"! Wanalielewa tatizo lao ni mfumo wa utawala. Ndio maana utaona nchi hata za Kikatoliki (Brazil, Chile, Ufilipino) zinajikuta na matatizo yale yale ya kimfumo wa utawala!
Ni sisi Tanzania tu tunataka kuaminishwa tatizo ni "kanisa" na wapo wanaokubali hivyo. Nakuhakikishia Bw. Said akivuka tu mstari wa kuangalia "kidini" na kuona ni tatizo la ufisadi kama mfumo utashangaa ni jinsi gani kila kitu kitamake sense. Itaelezea umaskini siyo wa Waislamu tu bali hata wa jamii nyingi za jadi, utaelezea umaskini na uduni wa maisha katika Jiji letu kuu la Dar, utaelezea ni kwanini wapo Wakristu wengi tu ambao wanaona kabisa mfumo uliopo hauwanufaishi wao kama raia wa Tanzania na katika hilo wako sawa kabisa na Waislamu na Wasioamini dini hizi mbili.
Tatizo lililopo ni kutoka huko kwenye kuangalia "dini" na kuangalia mfumo wetu ulivyoharibiwa na ufisadi. Lakini huko ni kugumu kwa sababu hata wewe unaamini kabisa "wakristu ni mafisadi zaidi" as if mafisadi wa hivyo wanafanya hivyo kwa sababu ni Wakristu. Nina uhakika hutaweza kukubali tukisema Waislamu ni mafisadi zaidi huko Misri, Syria au Libya kwa sababu watawala wengi wanaotuhumiwa ufisadi ni Waislamu! It doesn't make any sense but to some of you my friends it does and that in itself is a colossal tragedy of the first order.