Mohamed,Jasusi,
Bon Voyage.
Lakini kabla hujaondoka mimi nakuomba unijibu kitu kimoja.
Vipi kitabu cha Hamza Njozi "Mwembecha Killings" kipigwe marufuku lakini cha Mbogoni "The Cross Versus the Crescent" kiruhusiwe kusomwa?
Mohamed
Nimewasha gari tu nilikuwa sikajanyaga mafuta. Kitabu cha Njozi "Mwembechai Killings," nilikisoma kwenye mtandao baada ya Mkapa kukipiga marufuku. Tufauti ya vitabu hivi viwili, cha Njozi na cha Mbogoni ni kwamba Mbogoni amekuwa more rational katika utafiti wake, wakati Njozi amejikita zaidi katika kuonyesha Uislamu unaonewa. Nitakupa mfano mmoja. Kati ya picha za vijana waliopigwa na polisi katika maandamano ya Mwembechai, kuna kijana mmoja ambaye ni Mtanzania, lakini kwa kumwangalia tu huwezi jua kuwa huyu ni Muislamu au ni Mkristo. Lakini Njozi kishafanya conclusion kuwa yule kijana ni Islam. Hataji jina lake au mtaa anaoishi hakuweka. Kwangu mimi Mtanzania, yule kijana angeweza kuw ni Mkristo aliyekuwa "caught up in the crossfire" unless uniulize Mkristo alikuwa anatafuta nini katika ujirani wa Waislamu. Huo ni mfano mmoja tu. Mwingine ni maongezi ya Nyerere na padri Rweyemamu baada ya mkutano wa Tabora ambako alikutana na viongozi wa kanisa Katoliki ambao walikuwa na mashaka juu ya azimio la Arusha na sera za ujamaa. Mbogoni kaweka muktadha wa kuonyesha kuwa Wakatoliki walitaka kuuonyesha ujamaa kama Ukomunisti na yale mazungumzo ambapo Mwalimu anaweka bona fides zake kama mfuasi muaminifu wa kanisa Katoliki ninyi mmeutumia au mmeugeuza kujaribu kuonyesha kuwa Nyerere alikuwa anatumikia au anaendeshwa na kanisa Katoliki. That is a huge difference. Wakati ambapo Njozi katumia hisia za kichochezi, Mbogoni katumia usomi wake kuweka kila suala bayana. Lakini hapana, sikuunga mkono kabisa uamuzi wa Mkapa kukipiga marufuku kitabu cha Njozi kwa sababu siamini kuwa Watanzania ni mazezeta wa akili. Wana uwezo wa kupambanua. Basi ngoja nikimbie kwa sababu makabrasha yamenitinga. Nikipata muda, kama mjadala unaendelea bado, nitachangia.