Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Jasusi,

Bon Voyage.

Lakini kabla hujaondoka mimi nakuomba unijibu kitu kimoja.

Vipi kitabu cha Hamza Njozi "Mwembecha Killings" kipigwe marufuku lakini cha Mbogoni "The Cross Versus the Crescent" kiruhusiwe kusomwa?

Mohamed
Mohamed,
Nimewasha gari tu nilikuwa sikajanyaga mafuta. Kitabu cha Njozi "Mwembechai Killings," nilikisoma kwenye mtandao baada ya Mkapa kukipiga marufuku. Tufauti ya vitabu hivi viwili, cha Njozi na cha Mbogoni ni kwamba Mbogoni amekuwa more rational katika utafiti wake, wakati Njozi amejikita zaidi katika kuonyesha Uislamu unaonewa. Nitakupa mfano mmoja. Kati ya picha za vijana waliopigwa na polisi katika maandamano ya Mwembechai, kuna kijana mmoja ambaye ni Mtanzania, lakini kwa kumwangalia tu huwezi jua kuwa huyu ni Muislamu au ni Mkristo. Lakini Njozi kishafanya conclusion kuwa yule kijana ni Islam. Hataji jina lake au mtaa anaoishi hakuweka. Kwangu mimi Mtanzania, yule kijana angeweza kuw ni Mkristo aliyekuwa "caught up in the crossfire" unless uniulize Mkristo alikuwa anatafuta nini katika ujirani wa Waislamu. Huo ni mfano mmoja tu. Mwingine ni maongezi ya Nyerere na padri Rweyemamu baada ya mkutano wa Tabora ambako alikutana na viongozi wa kanisa Katoliki ambao walikuwa na mashaka juu ya azimio la Arusha na sera za ujamaa. Mbogoni kaweka muktadha wa kuonyesha kuwa Wakatoliki walitaka kuuonyesha ujamaa kama Ukomunisti na yale mazungumzo ambapo Mwalimu anaweka bona fides zake kama mfuasi muaminifu wa kanisa Katoliki ninyi mmeutumia au mmeugeuza kujaribu kuonyesha kuwa Nyerere alikuwa anatumikia au anaendeshwa na kanisa Katoliki. That is a huge difference. Wakati ambapo Njozi katumia hisia za kichochezi, Mbogoni katumia usomi wake kuweka kila suala bayana. Lakini hapana, sikuunga mkono kabisa uamuzi wa Mkapa kukipiga marufuku kitabu cha Njozi kwa sababu siamini kuwa Watanzania ni mazezeta wa akili. Wana uwezo wa kupambanua. Basi ngoja nikimbie kwa sababu makabrasha yamenitinga. Nikipata muda, kama mjadala unaendelea bado, nitachangia.
 
Ndugu zangu, nawaageni katika mnakasha huu kwa kuwashauri msome kitabu "The Cross versus The Crescent" Religion and Politics in Tanzania from the 1880s to the 1990s. Kimeandikwa na Lawrence E.Y. Mbogoni na kimechapishwa na Mkuki na Nyota Publishers. Mohamed hana monopoly ya ukweli kwenye historia ya Ukoloni, Ukristo na Uislamu nchini Tanzania. Na naongezea tu, it is more rational and educational. It has been a good debate and I believe we will achieve a peaceful Tanzania where no one is judged by the colour of his skin or the faith of his belief.
Asante Jasusi, huu mnakasha naamini umewafungua macho wengi. Mimi binafsi niliingia humu kwa kusita sana kwa sababu kama kuna kitu nakiheshimu na siwezi kukibeza ni imani ya mtu. Lakini historia yoyote ile inayodaiwa kuandikwa irrationally kwa kutanguliza Udini, huyo mwandishi sina namna nyingine ya kumwita isipokuwa mpuuzi.

Kama wewe, na mimi naaga huu mnakasha lakini kwa onyo kwa Watanzania wenzangu ambao nina mapenzi kwao bila kutazama dini zao, makabila yao, rangi zao na jinsia zao, tukiiruhusu hii mbegu inayopandikizwa na huyu mchochezi ikue na kuchanua basi tukae tayari kuvuna matunda yake kwani maadam tutakuwa tumelikoroga, itabidi tulinywe.

Nawashukuru wote mliochangia na hasa wale ambao wanatambua mchango wa Watanganyika wote kwa ujumla wao katika kupigania uhuru wa taifa letu kutoka mikononi mwa mkoloni mweupe. Na sasa historia inajirudia kwani tunajikuta kwenye mapambano ya kujinasua kutoka mikononi mwa wakoloni lakini hawa wakiwa weusi ambao ni sisi wenyewe tumewakabidhi madaraka.
 
Mohamed,
Nimewasha gari tu nilikuwa sikajanyaga mafuta. Kitabu cha Njozi "Mwembechai Killings," nilikisoma kwenye mtandao baada ya Mkapa kukipiga marufuku. Tufauti ya vitabu hivi viwili, cha Njozi na cha Mbogoni ni kwamba Mbogoni amekuwa more rational katika utafiti wake, wakati Njozi amejikita zaidi katika kuonyesha Uislamu unaonewa. Nitakupa mfano mmoja. Kati ya picha za vijana waliopigwa na polisi katika maandamano ya Mwembechai, kuna kijana mmoja ambaye ni Mtanzania, lakini kwa kumwangalia tu huwezi jua kuwa huyu ni Muislamu au ni Mkristo. Lakini Njozi kishafanya conclusion kuwa yule kijana ni Islam. Hataji jina lake au mtaa anaoishi hakuweka. Kwangu mimi Mtanzania, yule kijana angeweza kuw ni Mkristo aliyekuwa "caught up in the crossfire" unless uniulize Mkristo alikuwa anatafuta nini katika ujirani wa Waislamu. Huo ni mfano mmoja tu. Mwingine ni maongezi ya Nyerere na padri Rweyemamu baada ya mkutano wa Tabora ambako alikutana na viongozi wa kanisa Katoliki ambao walikuwa na mashaka juu ya azimio la Arusha na sera za ujamaa. Mbogoni kaweka muktadha wa kuonyesha kuwa Wakatoliki walitaka kuuonyesha ujamaa kama Ukomunisti na yale mazungumzo ambapo Mwalimu anaweka bona fides zake kama mfuasi muaminifu wa kanisa Katoliki ninyi mmeutumia au mmeugeuza kujaribu kuonyesha kuwa Nyerere alikuwa anatumikia au anaendeshwa na kanisa Katoliki. That is a huge difference. Wakati ambapo Njozi katumia hisia za kichochezi, Mbogoni katumia usomi wake kuweka kila suala bayana. Lakini hapana, sikuunga mkono kabisa uamuzi wa Mkapa kukipiga marufuku kitabu cha Njozi kwa sababu siamini kuwa Watanzania ni mazezeta wa akili. Wana uwezo wa kupambanua. Basi ngoja nikimbie kwa sababu makabrasha yamenitinga. Nikipata muda, kama mjadala unaendelea bado, nitachangia.

Jasusi,

Ahsante.

Ila kaeni mkijua kuwa haya yote niliyoandika humu na walioandika wengine kukupeni tahadhari siku moja ndiyo utakuwa ushahidi wetu na hapatakuwa na mtu wa kutuambia Waislam, "Mbona hamkututahadharisha kabla?"

Mohamed
 
Mag3,

Shukrani sana kwa observation yako. Kuna watu hapa wanajitosa kujaribu kujibu kila post ili waonekane wanafahamu mambo kumbe hawajui wanatafuta nini na wanaelekea wapi! Wanapeperushwa na upepo tena kirahisi sana hawajielewi wanasimamia nini.

Na huu ni uthibitisho wa dhahiri kwamba agenda inayojaribu kusukumwa hapa ina lengo la kuwagawa watanzania ili tabaka fisadi liendelee kutuibia, na baadhi ya watu hapa bila kuchanganya na zao wanameza tu vitu vizima vizima.
 
Asante Jasusi, huu mnakasha naamini umewafungua macho wengi. Mimi binafsi niliingia humu kwa kusita sana kwa sababu kama kuna kitu nakiheshimu na siwezi kukibeza ni imani ya mtu. Lakini historia yoyote ile inayodaiwa kuandikwa irrationally kwa kutanguliza Udini, huyo mwandishi sina namna nyingine ya kumwita isipokuwa mpuuzi.

Kama wewe, na mimi naaga huu mnakasha lakini kwa onyo kwa Watanzania wenzangu ambao nina mapenzi kwao bila kutazama dini zao, makabila yao, rangi zao na jinsia zao, tukiiruhusu hii mbegu inayopandikizwa na huyu mchochezi ikue na kuchanua basi tukae tayari kuvuna matunda yake kwani maadam tutakuwa tumelikoroga, itabidi tulinywe.

Nawashukuru wote mliochangia na hasa wale ambao wanatambua mchango wa Watanganyika wote kwa ujumla wao katika kupigania uhuru wa taifa letu kutoka mikononi mwa mkoloni mweupe. Na sasa historia inajirudia kwani tunajikuta kwenye mapambano ya kujinasua kutoka mikononi mwa wakoloni lakini hawa wakiwa weusi ambao ni sisi wenyewe tumewakabidhi madaraka.

Ila kaeni mkijua kuwa haya yote niliyoandika humu na walioandika wengine kukupeni tahadhari siku moja ndiyo utakuwa ushahidi wetu na hapatakuwa na mtu wa kutuambia Waislam, "Mbona hamkututahadharisha kabla?"

Mohamed
 
Asante Jasusi, huu mnakasha naamini umewafungua macho wengi. Mimi binafsi niliingia humu kwa kusita sana kwa sababu kama kuna kitu nakiheshimu na siwezi kukibeza ni imani ya mtu. Lakini historia yoyote ile inayodaiwa kuandikwa irrationally kwa kutanguliza Udini, huyo mwandishi sina namna nyingine ya kumwita isipokuwa mpuuzi.

Kama wewe, na mimi naaga huu mnakasha lakini kwa onyo kwa Watanzania wenzangu ambao nina mapenzi kwao bila kutazama dini zao, makabila yao, rangi zao na jinsia zao, tukiiruhusu hii mbegu inayopandikizwa na huyu mchochezi ikue na kuchanua basi tukae tayari kuvuna matunda yake kwani maadam tutakuwa tumelikoroga, itabidi tulinywe.

Nawashukuru wote mliochangia na hasa wale ambao wanatambua mchango wa Watanganyika wote kwa ujumla wao katika kupigania uhuru wa taifa letu kutoka mikononi mwa mkoloni mweupe. Na sasa historia inajirudia kwani tunajikuta kwenye mapambano ya kujinasua kutoka mikononi mwa wakoloni lakini hawa wakiwa weusi ambao ni sisi wenyewe tumewakabidhi madaraka.

Endeleeni kutetea wanafiki na watu waliodhulumu wananchi wa Tanzania kwasababu ya dini zao baada ya kuwaamini ..

Wamewadhulumu kwa mambo madogo (kama historia) na mambo makubwa ambayo yatafichuliwa siku zijazo..

Sisi waislamu wasomi tutaendelea na juhudi za kuelemisha jamii yetu na watanzania wapenda amani kuhusu

Dhulma na ufisadi wa kanisa kwa rasilimali za nchi na kodi zetu hadi hapo haki itakapoenea

Kwa hekima au kwa nguvu..
 
Ila kaeni mkijua kuwa haya yote niliyoandika humu na walioandika wengine kukupeni tahadhari siku moja ndiyo utakuwa ushahidi wetu na hapatakuwa na mtu wa kutuambia Waislam, "Mbona hamkututahadharisha kabla?"

Mohamed

Watakuja tu mezani..

Kinachoatakiwa ni kuendeleza harakati hizi

hadi kifo kitakapotuchukua..
 
Topical,

Insha Allah Amin kwa sote.

Walokimbia uwanja wa vita na kuonyesha migongo na visigino vyao ni wao.
Sisi bado tumesimama na silaha zetu mikononi.

Alhamdulilah tumewarehemu wazee wetu kwa taadhima zote.

Leo majina yaliyokuwa hayatajwi sasa yamo humu kwa dunia nzima kuyasoma na kuwajua kuwa hawa ndiyo waliopigania uhuru wa Tanganyika kwa hali na mali zao.

Tumeeleza na dhulma zilizodumu toka uhuru.

Haya yote si haba.

Kila atakapotajwa Nyerere tarehe 9 Desemba kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wako watu ndani ya nafsi zao watasema, "Walikuwapo wengine ila hawatajwi."

Wataukumbuka mnakasha huu.

Mohamed
 
Jasusi,

Ahsante.

Ila kaeni mkijua kuwa haya yote niliyoandika humu na walioandika wengine kukupeni tahadhari siku moja ndiyo utakuwa ushahidi wetu na hapatakuwa na mtu wa kutuambia Waislam, "Mbona hamkututahadharisha kabla?"

Mohamed
ok, we will see the way u are going to implement ur agenda. kumbe mmeshapanga tayari . niambie utekelezaji unaanza lini ili tujiandae
 
Kuna mtu aliyetokea kusikojulikana ambaye mpaka sasa ameacha sintofahamu ni wapi hasa aliipotokea na kuwaachia wana historia wabashiri ni wapi alitokea. Mtu huyo ambaye kwa maelezo yake walikuwa kwenye vita na wenzake watatu wakakimbizwa na maadui wao na hatimaye kutawanyika, mmoja akaenda Kaskazini, mwingine Kusini na Mmoja akafika eneo la Udzungwa mahali kunaitwa Ng'uruwe.

Mtu huyu ambaye jina lake halijulikani mpaka sasa alipewa majina mawili na wenyeji wa Udzungwa jina moja aliitwa Mfwimi = Mwindaji kwani alikuwa ni mwindaji hodari sana na jingine Muyinga yaani mtu aliyefika mahali kwa kutangatanga. Mtu anahisiwa kwamba inawezekana alikuwa ni mtu wa pwani kwani alipofika Ng'uruwe alikuwa na furushi la Chumvi, lakini dhana nyingine mtu huyu anaweza kuwa alikuwa ni Mkamba kutokana na umbo lake kubwa.

Mfwimi au Muyinga alizaa na Semduda mtoto wa mtawala wa eneo la Ng'uruwe mtoto aliyezaliwa akaitwa Muyinga. Muyinga akamzaa Maliga na Mkini, Maliga akamzaa Kilonge ambaye akawazaa watoto wawili, Ngaonalupembe na Munyigumba. Munyigumba alimuua Ngaonalupembe wakati mkewe akiwa mjamzito. Baada ya kufanya mauaji hayo Mnyigumba alisema mtoto atakayezaliwa atajwe kuwe ni wake

Mke wa Ngaonalupembe ambaye alikuwa ni Sekinyaga Semlimwandi alizaa mtoto wa Ngaonalupembe akiwa anaishi na Munyigumba, mtoto huyo aliitwa Kong'oke. watoto wa Mnyigumba ambao alizaa na mke wake Sengimba ni Mkwawa na Mpangile. Baadaye Mkwawa alikuja kumuua Kong'oke.

Baadhi ya watoto wa Mkwawa ni hawa

1. Sapi ambaye baadaye alisilimu na kuitwa Yusuph. Mama yake ni Semsilamgunda

2. Ligiliwe ambaye naye alisilimu akaitwa Mohamed. Mama yake ni Mganga Senyenza

3 Pancrass- Mkristo. Mama yake ni Semelele Msangu toka ukoo wa kina Melele.

4. Ananasi - Mkristo

5. Boniface - Mkristo

6. Mwanzali ambaye alisilimu akaitwa Athumani

7. Kilemaganga alikuwa ni mwanamke na aliolewa kwenye ukoo wa chifu wa Usangu Melele.

Ilikuwaje watoto wa Mkwawa wengine wakawa waislamu na wengine wakawa wakristo? Wakati yeye Mwenyewe hakuwa Muislamu wala Mkristo!!
 
Akutukanae hakuchagulii tusi na mdomo haumkatai bwana wake. Wenzako wengine wanawakataza wanafunzi wao kusoma kitabu cha Abdulwahid Sykes na kufanya rejea. Lakini mambo ndiyo haya:

BOOKS
1. TheLife and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the MuslimStruggle against British Colonialism in Tanganyika,Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati zaWaislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.2. Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi 20063. Contributing author AfricanAnthology, The Mermaid of Msambweni,Oxford University Press, 2008 Nairobi 4. Uamuzi wa Busara, Abantu Publications, Dar es Salaam, 2009
5. BrokenDreams, Phoenix Publishers, Nairobi, The Life of Ally KleistSykes (Forthcoming)

PART OFRESEARCH PAPERS/ARTICLES

1. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events(London).
2. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement(1988) Africa Events (London).3. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
4. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
5. Tanzania - The "Secular" UnsecularState (1995)Change (Dar es Salaam).
6. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A MuslimRiddle (Paper presented at theConference of the Global World of the Swahili InterculturalDialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
7. IslamicEducation and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit inTanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000'(Paper presented at InternationalSymposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organisedby the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture(IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15[SUP]th[/SUP] – 17[SUP]th[/SUP] 2003).
8. Sheikh Hassanbin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 –1968) (Paper presented at Youth CampOrganised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) andTanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27[SUP]th[/SUP] February – 4[SUP]th[/SUP]March 2004).
9. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience ofthe late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (PaperPresented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University ofAgriculture (SUA) Morogoro 11[SUP]th[/SUP]April 2004).
10. Terrorism in East Africathe Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and AfricanDevelopment University of Ibadan, Nigeria 8[SUP]th[/SUP] - 10th February 2006).
11. The Legacy of Sheikh AhmedDeedat (Paper Presentedat International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa,University of Johannesburg 1 - 3 September, 2006 (the paper was also presented atIslamic Propagation Centre International, Durban).
12. Speaker: ChristianHegemony and the Rise of Muslim Militancy in Tanzania, University of Iowa,A Celebration of East Africa Conference organised by African Studies Programand the US Department of Education through the Undergraduate StudiesInternational and Foreign Language UISFL University of Iowa 22/26 April 2011.
13. Speaker: Islamand Politics in Tanzania Half a Century Later, Northwestern University,Evanston, Illinois 11[SUP]th[/SUP] April, 2011.
14. Speaker: "Erecters of Milestones and Builders ofMonuments in Tanganyika's History," Muslim University of Mororgoro, 26 May 2011
AWARDS

Awarded Certificate ofAppreciation by United States Information Services (USIS) for research intopolitical history of Tanganyika and made Member Library of Congress,Washington, DC.

Mohamed

Ukiniluiza mimi kama wewe kweli ndiyo Mwandishi wa hivyo vitabu na "papers" kwenye lugha ya Kiingereza, nitapinga kabisa. Vyote hivyo ni ghostwritten kwani uwezo huo wa Uandishi na Usomi huna Mohamed Said. Navyoweza kusema kazi ulizoandika mwenyewe ni simulizi kwa lugha ya Kiswahili kama zile zinazochapishwa kwenye gazeti la "Mwananchi". Narudia tena, wewe si lolote bali ni intellectual imposter tu na mpotoshaji tu.
 
Kuna mtu aliyetokea kusikojulikana ambaye mpaka sasa ameacha sintofahamu ni wapi hasa aliipotokea na kuwaachia wana historia wabashiri ni wapi alitokea. Mtu huyo ambaye kwa maelezo yake walikuwa kwenye vita na wenzake watatu wakakimbizwa na maadui wao na hatimaye kutawanyika, mmoja akaenda Kaskazini, mwingine Kusini na Mmoja akafika eneo la Udzungwa mahali kunaitwa Ng'uruwe.

Mtu huyu ambaye jina lake halijulikani mpaka sasa alipewa majina mawili na wenyeji wa Udzungwa jina moja aliitwa Mfwimi = Mwindaji kwani alikuwa ni mwindaji hodari sana na jingine Muyinga yaani mtu aliyefika mahali kwa kutangatanga. Mtu anahisiwa kwamba inawezekana alikuwa ni mtu wa pwani kwani alipofika Ng'uruwe alikuwa na furushi la Chumvi, lakini dhana nyingine mtu huyu anaweza kuwa alikuwa ni Mkamba kutokana na umbo lake kubwa.

Mfwimi au Muyinga alizaa na Semduda mtoto wa mtawala wa eneo la Ng'uruwe mtoto aliyezaliwa akaitwa Muyinga. Muyinga akamzaa Maliga na Mkini, Maliga akamzaa Kilonge ambaye akawazaa watoto wawili, Ngaonalupembe na Munyigumba. Munyigumba alimuua Ngaonalupembe wakati mkewe akiwa mjamzito. Baada ya kufanya mauaji hayo Mnyigumba alisema mtoto atakayezaliwa atajwe kuwe ni wake

Mke wa Ngaonalupembe ambaye alikuwa ni Sekinyaga Semlimwandi alizaa mtoto wa Ngaonalupembe akiwa anaishi na Munyigumba, mtoto huyo aliitwa Kong'oke. watoto wa Mnyigumba ambao alizaa na mke wake Sengimba ni Mkwawa na Mpangile. Baadaye Mkwawa alikuja kumuua Kong'oke.

Baadhi ya watoto wa Mkwawa ni hawa

1. Sapi ambaye baadaye alisilimu na kuitwa Yusuph. Mama yake ni Semsilamgunda

2. Ligiliwe ambaye naye alisilimu akaitwa Mohamed. Mama yake ni Mganga Senyenza

3 Pancrass- Mkristo. Mama yake ni Semelele Msangu toka ukoo wa kina Melele.

4. Ananasi - Mkristo

5. Boniface - Mkristo

6. Mwanzali ambaye alisilimu akaitwa Athumani

7. Kilemaganga alikuwa ni mwanamke na aliolewa kwenye ukoo wa chifu wa Usangu Melele.

Ilikuwaje watoto wa Mkwawa wengine wakawa waislamu na wengine wakawa wakristo? Wakati yeye Mwenyewe hakuwa Muislamu wala Mkristo!!

Nilimuuliza swali MS kuhusu huyo Pancras akaja na jibu yeye hazungumzii watoto as if watoto huwa wanajipa majina. Anyways mkuu asante kwa kutuletea hiyo brief history. Suala ni kwamba kama Mkwawa alikuwa traditionalist, mwislam au mkristo who cares????? The only problem ni pale mtu anapotaka kuendesha ajenda ya udini kwa kutumia kila gain on freedom iliyowahi kupatikana ndani ya Tanganyika.
 
Ndiyo maana nilimueleza mohamed said kama anataka kuendekeza makundi makundi basi ajikite kwenye Ukabila na koo na sio dini. Hakuna sehemu afrika watu walipigania uhuru kwa misingi ya Dini. Hata Matatizo yaliyopo somalia yenye 99.9% muslim na historia yake imejengeka kikoo na sio kidini.

Lakini Mohamed said anajua akiongela propagangda za wamanyema, wazaramu kutengwa na Nyerere hatapa kile anachokitaka. Anaamua kutumia dini ili aguse hisia zaa wale wa kigoma tbora lindi mwanza kagera. Lkini Mohamed said sidhanikama kweli anataa kusimaia historia ya historia ya waislam wa kigoma, Tabora, kagrea na Kwingineko.

Kama ni kundi au jamii ya watu wanatakiwa kuwa wa kwanza kumnyoshea Nyerere Kidole basi ni wale machief wa makabila na mila mbali mbali alizovunja. Lakini hilo halina nguvu sababu wote tunazijua.

@ Swali kwa Mohmed said
Je

  • Ulikuwa uamauzi mzuri kufutiliaa mbali tawala za machief wa mila na tamaduni mbali mbali za Tanzania ?
  • ilikuwa sahii serikali kufuta mfumo wa sheria za tawala za machief hawa kama kina kuwa na mahakama zao?
 
Wakuu naona mjadala wetu umefikia ukingoni, hoja zimeletwa , zimechambuliwa, zimenyumbulishwa sometimes individuals wameshutumiana, wametishana, wamekasirikiana etc. Kilichobakia sasa ni dilly dallying na kurudi kule kule tulikotoka. Kama nilivyoahidi hili litakuwa bandiko langu la mwisho katika mada hii. Na Kama nilivowahi kusema huko mwanzo ni mambo ya aibu kwa watanzania kujadili mijadala kwa mitazamo ya kidini au kufikiria kidini dini (them and us), it is sick, low and primitive.

General Advice
Kama ni kweli kuna “dhulma” specific towards waislamu iliyoexist kwa zaidi ya miongo mitano, namna pekee ya ku-level mambo ni thru affirmative action. Kuanzia sasa kuwe na nafasi za upendeleo bungeni kwa waislamu (Viti maalum), kuwe na nafasi maalum za sekondari, kidato cha sita na chuo kikuu kwa waislamu, makazini nako serikalini iwe nusu kwa nusu waislam + wakristo na madhehebu mengine. Kwenye sekta binafsi tufanye kama South Africa “it should reflect the country’s demographic”. Ikumbukwe “dhulmati” Nyerere alishafanya hii affirmative action kiuchumi kupitia azimio la Arusha na kwenye elimu kukawa na uwiano sawa katika mikoa yote Tanzania kutoa wanafunzi kwenda shule za sekondari za serikali. Pale pugu kuna watu kutoka jamii za wahadzabe, wamasai, wamang’ati walikuwa wanaletwa form 1 hawajui hata kusoma vizuri. Unless kama MS una ushauri tofauti kuhusu hii so called “dhulma” ya “mfumo kristo” lakini to me it should be affirmative action all the way to counter the so called “inequalities”

Acknowledgement
Napongeza kaka Mohamed Said kwa kuandika japo sikubaliani na baadhi ya contents ya mada zake. Maandishi ni tatizo la Tanzania na si dogo mambo mengi tunayobishana hapa yangekuwa yameandikwa kulikuwa hakuna sababu ya zogo. Ukisoma humu zaidi ya 95% ya references ni maandishi ya nje ya bongo. Pia bro Mag3 kwa kuleta hii thread na wachangiaji wote. Lakini pia naomba nimkumbushe Mohamed Said kwamba kuitwa kutoa mhadhara kwenye vyuo vikuu au taasisi za vyuo vikuu haimaanishi usomi au Ukweli juu ya unachozungumza. MS unapaswa kuelewa kuwa hata Idd Amin baada ya kukimbia Uganda alikuwa akiitwa na vyuo vikuu vingi tu kuzungumzia his side of the story au Ukiandika leo kitabu ukasema say “Jesus never existed, it is just a myth” utaitwa kwenye vyuo vikuu mbali mbali kupiga mihadhara.

Contradictions
Mohamed Said katika maandiko yake na references zake kuna kujichanganya kwingi sana mfano
1. MS anasema kanisa nini serikali ndani ya serikali, kanisa likiamua ndiyo mwisho. Haishii hapo anatoa mfano uchaguzi mkuu mwaka jana. Kanisa lilitoa “election manifesto ya nani anafaa kuchaguliwa” na wakamsimamisha Dr. Slaa ambaye ni former padre ili apambane na mwislam JK. Hatima yake wote tunaijua Dr. Slaa alishindwa sasa hili kanisa ambalo ni kila kitu walishindwaje kuhakikisha mgombea wao anakuwa raisi?

2. Mohamed Said zaidi ya mara moja anadai sababu ya shule nyingi za kiislamu kutofanya vizuri inatokana na MoU kwa shule za kikristo, kwamba walimu wote wazuri wanaenda kwenye shule za kikristo kwa sababu kuna maslahi mazuri kutokana na MoU wakati huo huo anauliza nani wanafanya kazi huko kwenye hizo shule na hospitali za wakristo? Sasa ukijiuliza objectively ina maana kuna walimu wazuri wanakataliwa shule husika kwa sababu ya dini zao, je hao wanafundisha wapi?

3. Mohamed Said anatuhumu kwamba sheria ya ugaidi imetungwa kuwalenga waislamu, lakini inashangaza mpaka sasa raisi mwislamu, makamu mwislamu, jaji mkuu mwislam hajaenda mahakamani kuhakikisha sheria hiyo inakuwa repealed. Hao niliowataja ni kwamba wana power kuhakikisha haki kama ipo kuhusu jambo hilo inatendeka.

4. MS anasema mojawapo ya dhulma ni kuwa bunge asilimia 85 ni katoliki na hiyo 15 ni wengine. Wote tunafahamu wabunge wanachaguliwaje lakini MS hatuambii ni kwa namna gani wabunge hao wanapatikana fraudulently thru the so called “mfumo kristo”

5. MS anatuambia kwamba wakristo especially wakatoliki wameshikilia 83% ya fursa zote Tanzania na wengine 17% lakini hatuambii namba hiyo ameipataje? Na why 83% why not 90%, 60% or either 100%.

6. MS anaishutumu serikali kwamba hawawezi kufanya jambo lolote zuri au kuwajibika kwa hoja zitolewazo na waislam kwa sababu ya “mfumo kristo” lakini anataka serikali hiyo hiyo ilete solutions.

7. MS hajibu maswali magumu aidha kwa kuzunguka zunguka au kusema na nyie muandike vitabu vyenu. Hivi ingeuwa ni hivyo huu mjadala si ungekuwa uliisha siku nyingi maana tungekuwa tunapost hongesa, safi sana, big up etc. Mfano ni swali nililomuuliza mara tano kuhusu hii profile (Bonyeza hapa) kama ni yake hajajibu mpaka sasa and I know why.

8. Mohamed said kama ilivyo kwa baadhi ya wamarekani au “wasauzi” wanoona kila kitu in black and white (Black this, white that, white this….) anawatazama watanzania kwa uislamu na ukristo na hapa ndipo amegota and yet anataka kucommand authority kwamba anaisaidia serikali (anayoituhumu kutosikia llolote kutoka kwa mwislam) iepukane na vita inayonukia anasahau kwamba unlike the skin color you can’t tell somebody’s religion by just the looks.

Hits and Misses
Kumekuwa na lots of hits and misses kutoka kwa wachangiaji kuoka hii mada lakini ntazielezea miss kubwa mbili.
Ni wazi kuwa kwa hii mifumo ya kibinadamu ni lazima mfumo uundwe na ulindwe ili uendelee ku-exist. Kwa maana hiyo basi kutokana na maandishi ya MS, so called “mfumo kristo”

1. Ulianzishwa na Nyerere – Huge Miss
2. Wanaoulinda mfumo huo ni wale wote according to MS wasio na majina ya kiislamu. Maana kwa analysis za MS jina linatosha kujua wewe ni dini gani na unasympathize na nani– Huge miss

Ushauri Binafsi
Si mara moja nilijikuta nikiwa attacked personally (with exception of MS) na ndugu zangu hapa chini, Hivyo nimeona ni bora kuwapa ushauri badala ya eye for an eye.

1. MS -
sasa ni wakati muafaka kutoka kwenye hisia na kuwa analytical kisayansi, kutoka kwenye simulizi na kuweka historia kwa maana ya historia, kuacha kutumia maneno kama inasemekana, huenda, nahisi katika uandishi. Na hasa kama una nia ya kwenda UN kama ulivyosema mwenyewe, which I believe you will have to maana huwezi kuweka CCM na haki katika sentensi moja

2. Faiza Foxy –
Ndugu yangu unahitaji ku-attend therapy haraka iwezekanavyo on anger management na pia juu ya how to feel secure. This is just a friendly advice.

3. Mdondoaji –
Partial Knowledge is dangerous.

4. Topical –
Pamoja na kwamba nimeshakushauri huko nyuma (hahaha ahaha!!!) Jiamini, kuwa na high self esteem. Kujenga hoja si lazima uungwe mkono au ujiunge mkono kwa Id’s tofauti tofauti.

Kila laheri, wajibu wetu uni kuijenga Tanzania kuhakikisha inakuwa mahali salama, yenye fursa kwa wote na inayostawi kwetu na vizazi vijavyo. Tukutane kwenye mada zingine.
 
Kuna mtu aliyetokea kusikojulikana ambaye mpaka sasa ameacha sintofahamu ni wapi hasa aliipotokea na kuwaachia wana historia wabashiri ni wapi alitokea. Mtu huyo ambaye kwa maelezo yake walikuwa kwenye vita na wenzake watatu wakakimbizwa na maadui wao na hatimaye kutawanyika, mmoja akaenda Kaskazini, mwingine Kusini na Mmoja akafika eneo la Udzungwa mahali kunaitwa Ng'uruwe.

Mtu huyu ambaye jina lake halijulikani mpaka sasa alipewa majina mawili na wenyeji wa Udzungwa jina moja aliitwa Mfwimi = Mwindaji kwani alikuwa ni mwindaji hodari sana na jingine Muyinga yaani mtu aliyefika mahali kwa kutangatanga. Mtu anahisiwa kwamba inawezekana alikuwa ni mtu wa pwani kwani alipofika Ng'uruwe alikuwa na furushi la Chumvi, lakini dhana nyingine mtu huyu anaweza kuwa alikuwa ni Mkamba kutokana na umbo lake kubwa.

Mfwimi au Muyinga alizaa na Semduda mtoto wa mtawala wa eneo la Ng'uruwe mtoto aliyezaliwa akaitwa Muyinga. Muyinga akamzaa Maliga na Mkini, Maliga akamzaa Kilonge ambaye akawazaa watoto wawili, Ngaonalupembe na Munyigumba. Munyigumba alimuua Ngaonalupembe wakati mkewe akiwa mjamzito. Baada ya kufanya mauaji hayo Mnyigumba alisema mtoto atakayezaliwa atajwe kuwe ni wake

Mke wa Ngaonalupembe ambaye alikuwa ni Sekinyaga Semlimwandi alizaa mtoto wa Ngaonalupembe akiwa anaishi na Munyigumba, mtoto huyo aliitwa Kong'oke. watoto wa Mnyigumba ambao alizaa na mke wake Sengimba ni Mkwawa na Mpangile. Baadaye Mkwawa alikuja kumuua Kong'oke.

Baadhi ya watoto wa Mkwawa ni hawa

1. Sapi ambaye baadaye alisilimu na kuitwa Yusuph. Mama yake ni Semsilamgunda

2. Ligiliwe ambaye naye alisilimu akaitwa Mohamed. Mama yake ni Mganga Senyenza

3 Pancrass- Mkristo. Mama yake ni Semelele Msangu toka ukoo wa kina Melele.

4. Ananasi - Mkristo

5. Boniface - Mkristo

6. Mwanzali ambaye alisilimu akaitwa Athumani

7. Kilemaganga alikuwa ni mwanamke na aliolewa kwenye ukoo wa chifu wa Usangu Melele.

Ilikuwaje watoto wa Mkwawa wengine wakawa waislamu na wengine wakawa wakristo? Wakati yeye Mwenyewe hakuwa Muislamu wala Mkristo!!
Mkuu mbona majina yote ya wale waliosilimu ni ya kiasili? hawa hawakuwa na dini kabla ya hapo kama ndugu zao Wakristu ambao hawakusilimu?...
 
Hili jina la "Mohamed Said" ni la kutilia mashaka. Iweje Mbantu tena Mtanganyika mwenye uchungu na nchi yake asitumie jina lake la ukoo la Kibantu akiwa kama Mwandishi? Obviously something fishy seems to be going on here. Vitabu na "papers" zote kwenye lugha ya Kiingereza vimeandikwa na watu au mtu mwingine, na "Mohamed Said" anapewa credit for authorship sababu "Mohamed Said" happens to be a very generic name among Muslims na inakuwa rahisi kwake kualikwa nje ya nchi etc kutumia jina la "Mohamed Said" ukilinganisha na tuseme kama angekuwa anajiita "Mohamed Said Mbukuzi".

Nasema kazi za uandishi anazodai kuandika "Mohamed Said" ni bogus unless atuwekee angalu video moja akichangia maada au chochote kwa lugha ya Kiingereza kwenye moja ya warsha, presentations, au mikutano lukuki ya Kisomi anazodai kuhudhuria nje ya nchi ( na kama anavyo-boast mwenyewe kwa jinsi passport yake ilivyojaa mihuri.)
 
Ama kweli wewe ni ni mpotoshaji wa hali ya juu, kwa kuwa Mohamed Said hajui Kiingereza? unaweza kuweka ushahidi wowote kuwa hajaandika yeye?

Najuwa huji na jibu kwani hata mwanzo ulipokuja kichwa kichwa nikakuuliza maswali hujaja na jibu hata moja.
 
Ujumbe wangu ni kwa "Mohamed Said", na wewe siyo "Mohamed Said". Hata hivyo, kwa kukumbushana tu, nasubiri video ya "Mohamed Said" akitoa mchango wowote kwa lugha ya Kiingereza kwa mbwembwe zake zote kama anavyoandika kwenye "Papers" na "Vitabu" vyake akitumia lugha hiyo.
 
Back
Top Bottom