Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Hivi hicho chama kilianzishwa kwa masilahi ya Waislamu peke yao?.......iweje mtu ajiulize kuwa huyu bwana hatakuja kutujali? kutujali alikuwa akimaanisha akina nani? na kwa misingi ipi?.....ya uanzilishi wa chama au Uislamu wao?
Hizi ndizo huitwa "prejudices"
Kwa nini watu waingie wasiwasi Watanganyika wengine kuingia Barazani?........huo umoja wa Kitaifa la Tanganyika unakuwaje hapo?
..........Sheikh Takadir alihitaji nini hasa.....kwa kuwa yeye na Waislamu wenzake walianzisha chama basi wasije wengine kuongoza chama? ambacho madhumuni yake ni kushika uongozi wa nchi yenye watu wenye imani na makabila mbali mbali.......ambao nao pia walipigana vilivyo ili kupata uhuru wa Tanganyika..........
Mkasa wa Nyerere na Sheikh Suleiman Takadir unaendelea. Baada ya hayo likaja sakata la All Muslim National Union of Tanganyika (AMNUT). Usiwe na haraka subiri hadi mwisho huenda baadhi ya maswali yako yakawa yamejibiwa humu ndani. Kwa miaka mingi sana TANU ilikuwa inaogopa hata kueleza ugomvi huu wa Sheikh Suleiman Takadir na Nyerere. Endelea na historia ya TANU New Street, Dar es Salaam, 1958 sasa inaingia 1959...:
Mwafrika,[1] gazeti la kila wiki chiniya uhariri wa Heri Baghdelleh na Robert Makange, lilichapisha habari za SheikhSuleiman Takadir katika ukurasa wa kwanza, likitangaza kufukuzwa kwake kutokaTANU kwa wino mzito, picha yake akiwa amevaa kanzu na kofia ya mkono akikodoamacho ikachapishwa gazetini.[1]Picha ya Sheikh Takadir iliwekwa pale ili wote wauone uso wa ëmsalitií anaetakakuchelewesha uhuru kwa kutaka Waislam wapewe uthibitisho wa hali yao yabaadae kwa sababu ya mchango wao katikaharakati za kudai uhuru. Mtu mmoja tu ndiyo aliyejitokeza kumuunga mkono SheikhTakadir na huyo alikuwa Ramadhan Mashado Plantan. Akiandika katika gazeti lakela Zuhra alihoji ile harara ya Nyerere kuwatumbukiza wananchi ndani ya uchaguziwa kura tatu ingawa ilikuwa wazi kuwa yale masharti ya kupiga kura yalikuwa yakuchukiza na ile haraka ambayo kwayo Sheikh Takadir alifukuzwa kutoka TANU.[1]Wakati wa mkasa wa Sheikh Takadir,Mwafrika lilikuwa likifaidi mauzo makubwa kwa sababu TANU ilisusia gazeti laBaraza gazeti la kila wiki la serikali. Baghdelleh na Makange walikuwa wamechapishamakala moja ambayo serikali iliiona ni ya uchochezi. Baghdelleh na Makangewalipatikana na hatia na kufungwa miezi sita gerezani. [1] TANU ililipa kisasi kwakuwataka wananchi wasusie gazeti la Baraza. Hakuna Mwafrika aliyenunua gazetihilo na kwa ajili hii yake mauzo ya Mwafrika yalipanda sana, hivyo kuipa sakataya Sheikh Takadir katika Mwafrika nafasi kubwa gazetini. Baraza ilikuwa katikaukingo wa kufa kabisa kama isingelikuwa juhudi na mbinu za kidiplomasia zameneja wake, Page Jones na Meneja wa Tanganyika Standard, Nihill waliokwendamakao makuu ya TANU kusuluhisha baina ya gazeti hilo la serikali na TANU.Nihill alifanya mazungumzo na makamu wa rais wa TANU, John Rupia; kaimu katibumwenezi, Amos Kissenge; katibu wa TANU Youth League, Dr. Michael Lugazia; DossaAziz na Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya TANU Idd Faiz. Hawa viongoziwaandamizi wa TANU walitoa amri ya kusitisha ususiaji wa gazeti la Baraza. Kwa kitendo hiki TANU ilikuwa imeojielezavyema na ilikuwa imeonyesha nguvu zake. Katika kipindi hiki mashambulizi kwa waleWaislam walionekana wanaipinga TANU na Nyerere yalizidishwa. Sheikh HusseinJuma makamu wa rais wa UTP alikuwa na pacha mwenzake, Sheikh Hassan Juma.Sheikh Hassan Juma alikuwa akiendesha madrasa pamoja na shule ikiitwa AlHassanein Muslim School, moja ya majaribio ingawa hafifu ya Waislamkujiendeleza katika elimu. Shule nyingi zilikuwa mikononi mwa wamisionari.Watoto wengi waliozaliwa mjini Dar es Salaam baada ya vita ya pili walisomeshwaQurían katika Al Hassanein chini ya Sheikh Hassan Juma. Wazazi waliwatoa watotowao katika shule hii kwa sababu waliihusisha madrasa hii na upinzani dhidi yaTANU. Watoto hawa hawakuishia katika kuacha kuhudhuria madrasa bali walitunganyimbo za kebehi ambazo waliziimba kwasauti kubwa walipokuwa wakipita katika shule yao ya zamani ili kuwakebehi,Sheikh Hussein Juma na nduguye pacha Sheikh Hassan. Wazee wao hawakuona haja yakuwakataza watoto wao tabia hii isiyofaa. Kwa kawaida ilionekana kwamba yeyotealiyekuwa anaipinga au hakujinasibisha na TANU, alikuwa adui.Huu ndiyo ukuwa mwanzo wa upinzani wachini chini dhidi ya TANU. Mwaka 1959, Ramadhani Mashado Plantan, mharirihodari wa gazeti la Zuhra wakati mmoja gazeti hili likiwa ndiyo sauti ya TANUna wananchi wa TAnganyika, pamoja na kikundi kidogo cha Waislam akiwemo SalehMuhsin walijiuzulu kutoka TANU na kuunda chama chao cha upinzani, All MuslimNational Union of Tanganyika (AMNUT).[1]Wanachama wengine waasisi walikuwa Abdallah Mohammed ambaye alichaguliwa kuwarais na Plantan akiwa katibu. Plantan alijitolea chumba kimoja nyumbani kwakeKirk Street, Gerezani kama ofisi ya kwanza ya AMNUT. Mara tu baada ya kuundwakwa AMNUT, ulizuka mgogoro katika uongozi na ofisi hiyo ilibidi ihamishwekutoka nyumbani kwa Plantan hadi Libya Street, eneo lenye Wahindi wengikatikati ya mji. Uongozi mpya ulikuja madarakani na katibu mpya AbduwahidAbdulkarim. Abduwahid Abdulkarim, kijana mwenye umri wa miaka 25 alichaguliwakuchukua nafasi ya Plantan. Abdallah Mohamed alibakia na cheo chake kama rais.AMNUT haikuweza kumudu kodi ya nyumba katika eneo lile la matajiri wa Kihindi.AMNUT ikaihamisha ofisi yake na kwenda Kariakoo, Narungíombe Street, karibu namsikiti wa Sheikh Idris bin Saad."
Mohamed
