Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa


Mkandara,

Maneno mazuri.

Nami nakuwekea maneno yangu hapa chini:
Wazee wangu hawakujitoa TANU bali walitolewa kwa hila na fitna. Hawa wafuatao ni baadhi ya wazee wangu walowekwa kizuizini: Abdillah Schneider Plantan, SheikhAbdulkarim Abdulwahid, Maalim Popo Saleh, Suleiman Masudi Mnonji, Ali Migeyo,Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Shariff Hussein Badawiy, Shariff Mwinyibaba,Shariff Adnan, Bilali Rehani Waikela, Sheikh Jumanne Bias, Maalim Matar,Abdalah Mwamba, Sheikh Hashim Haji Abdallah, Sheikh Nurdin Hussein, SalumAbdallah Popo, Sheikh Mzee Ali Comoriam, Sheikh Al Amin Maftah, Rajab Kiguu chaMbuzi na wengine wengi. Lakini ukweli ulikuwa kwamba si wote katika walewaliokamatwa na kuwekwa kizuizini walijihusisha na siasa. Baadhi yao walikamatwakwa sababu tu walikuwa wakishirikiana na wale waliodhaniwa ni wapinzani waNyerere. Maalim Matar na Shariff Adnan walifungwa jela kwa sababu tu walihusikana msikiti wa Badawiy mjini Dar es Salaam ambako Sheikh Hassan bin Amir, wakatihuo akichukuliwa kuwa ndiyo roho ya waumini wa Tanganyika, alikuwa ikiendeshamadrasa yake kila magharibi pale msikitini. Shariff Hussein na nduguyeMwinyibaba walihamishiwa Kenya, walikotoka si kwa sababu walikuwawamejishughulisha katika harakati za kuipinga serikali, ila lakini kwa sababuwalikuwa waangalizi wa msikiti wa Badawiy. Sheikh Mzee Ali Comorian alitiwa kizuizini kwa sababu kila mara alikuwaakifuatana na Sheikh Hassan bin Amir kama vile alikuwa kivuli cha sheikh. Huendakile kilichomfanya Nyerere kuwatia kizuizini masheikh na wengine kuhamishwa nikufuata ule msemo wa Biblia usemao, "yule ambae hayuko nasi basi ni dhidiyetu."Jinsi siasa na za Tanzaniazilivyobadilika na jinsi Nyerere alivyoanza kuonyesha uadui dhidi ya Waislamkulimsikitisha sana Abdulwahid. Alishindwa kuelewa uhasama huu ulikuwa unatokawapi. Alihisi kuwa anahusika na yale yaliyokuwa yanawapata Waislam. Mawazo hayayalimzonga kama jinamizi. Kwa ufahamu wake alikuwa anadhani matatizo yote yaudini walikuwa wameyashinda toka miaka ya 1950. Mwaka 1953 Abdulwahid akiwaMuislam na akiungwa mkono na Al Jamiatul Islamiyya aligombea kiti cha urais waTAA na Nyerere, Mkatoliki. Abdulwahid alishindwa uchaguzi ule. Waislamhawakuuchukulia uchaguzi ule kama uchaguzi kati ya Muislam na Mkristo. Kilichotazamwani uwezo wa wagombea. Nyerere alikuwa amemzidi Abdulwahid na kwa ajili hiialichaguliwa kuiongza TAA. Abdulwahid alikumbuka ugomvi wa Sheikh SuleimanTakadir wakati ule Mwenyekiti wa Baraza La Wazee wa TANU. Sheikh Takadiraliwaonya Waislam wachukue tahadhari kwani Nyerere atakuja kuwapendeleaWakristo wenzake pale atakaposhika madaraka. Kama walivyofanya Waislam wengi,Abdulwahid alimuunga mkono Nyerere na kumpinga Sheikh Takadir. Wakati uleAbdulwahid aliamini kama Waislam wengi walivyoamini kuwa Sheikh Takadir alikuwaanataka kuleta siasa za kibaguzi ambazo alikuwa anaziegemeza katika dini.Abdulwahid aliona udini aliokuwa anataka kuuleta Sheikh Takadir lilikuwa jamboambalo litailetea hatari Tanganyika.Abdulwahid alikufa mwaka 1968 wakati nchiilikuwa imegubikwa na hasama za chinichini kati ya Waislam na Wakristo ambaosasa walikuwa wamehodhi madaraka yote katika serikali. Umoja wa kitaifa, mojaya maadili ambayo yeye aliyapigania katika maisha yake yote katika siasaulikuwa unahatarishwa. Halikadhalika umoja wa Waislam ulikuwa unaelekeakuvunjika. Kulikuwepo na kuwekwa kizuizini kwa masheikh chini ya PreventiveDentation Act of 1962. Baadhi ya masheikh waliotiwa gerezani walikuwa watu waliomuunga yeye mwenyewe mkono wakatianaunda TANU. Baadhi yao aliwashawishi kumuunga mkono Nyerere na TANU katikakile kipindi kigumu cha harakati za kudai uhuru. Mwanakamati wa Kamati Ndogo yaSiasa ya TAA, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, kiongozi wa ngazi ya juu kabisa kwaWaislam alikuwa amekamatwa na kuondolewa nchini na kurudishwa kwao Zanzibar kwaamri ya Nyerere.[1]Sababu iliyotolewa ya kukamatwa kwa Sheikh Hassan bin Amir ilikuwa alikuwaati "akipanga njama ya kupinduaserikali."Sheikh Hassan bin Amir alikuwa kati yaWaislam wachache ambao walithubutu kusimama kidete dhidi ya serikali na kutoamawazo yake kuhusu jinsi serikali ilivyokuwa ikiwakandamiza Waislam. Kablahajafa Abdulwahid alikuwa akifikiwa na habari kuwa kulikuwa na kampeniiliyokuwa ikiendeshwa kwa makini sana naWakristo ndani ya chama kuufuta Uislam ndani ya TANU. [1]Abdulwahid alikuwa anafahamu matokeo yakuvunjika kwa umoja wa Waislam. Yeye alikuwa anajua vyema nguvu ya umoja waWaislam wakati walipokuwa wanapigania uhuru wa Tanganyika. Abdulwahidhalikadhalika alikuwa anafahamu nguvu ya wale waliokuwa nyuma na njama zile zakuwagawa Waislam katika makundi hasimu. Vilevile alikuwa anatambua hofu na watuwote waliokuwa nyuma ya njama zile. Alifahamu kuwa wale aliowapokea na kuwatiakatika harakati za kudai uhuru sasa walikua na hofu na Uislam. Kama Uislamulitumika kuwaondoa wakoloni Uislam hautashindwa kuwatoa wao madarakani. Uislamikiwa itkadi ya kupinga ukoloni sasa ilikuwa ni tishio kwa Ukristo katikaTanzania huru."

Mohamed


Inna Lillahi wainna ilaihi rajihunnah
 
Nauliza hv nyerere ndo aloteta huo mfumo kristu.?wakolön walitugawa ili watutawale na ikumbukwe kwamba wakolon walikuwa wazungu kwa hyo ni wakristu..nyerere kajitahid kuweka usawa kupitia azimio la arusha mkaleta la zanzibar afu mnasema nyerere kaleta mfumo kristu asa angewasaidiaje..au labda mtu aniambie kuwa nyerere ndo alovunja azimio la arusha?
 
Nguruvi3,

"It is strange thatKawawa’s book does not have references to his personal papers which are notonly important to Kawawa’s life history but to the history of Tanganyika aswell. Magotti did not even interview Kawawa’s contemporaries still living likeAlly Sykes and Victor Mkello a fellow trade unionist now on his death bed. This was Magotti’s greatest omission................''
Mohamed

Hhahahaaha...sasa MS you are a very strange person bro! kwani huyu Magotti anatofauti gani na wewe? It is the precise thing of what people have accused you in this thread. Kuandika bila kuhoji upande wa pili! Perhaps, na wewe ungetake trouble kufanya yale unayomtuhumu Magotti tungekuwa na narrative tofauti. Lakini majibu yako ni yale ya 'na wengine wakaandike historia yao...' Basi na Magotti atasema hivyo hivyo!!

Nafurahi kuona kwamba na wewe umeigundua hiyo double standard, tragically wewe hujioni kwamba you have done exactly the same thing! Na implication yake ingawa unai admitt kwenye kitabu cha Kawawa..kwako huioni! Duh...

Tatizo MS you 'know alot of things', lakini unasahau kwamba humu JF watu tunasoma kama wewe na kufanya 'analysis' so we dont simply swallow stuffs! Ndo maana watu hapa wanakujibu kwa hoja. Strange world? uhhh???
 
Hakuna kinachobadilishwa wala kubatilishwa bali inaongezwa yale yalio ondolewa kwa makusudi kabisa kwa nia maalu.

Kumbuka hata mbuyu ulianza kama mchicha. Miaka 50 kazi kwenu kila kitu kipo hadharani.
Yaliondolewa wapi na nani? Tunamshukuru Mungu asiye na DINI ambaye ameifikisha TANZANIA hapa ilipo. Hatuna DINI ya TAIFA, hatuchagui wala kuteua viongozi wetu kwa kushauriana na Maaskofu wala Masheikh. Tunachanganyika vilivyo kuanzia ndoa, familia, makazi, shule, ajira, misiba, starehe, humu JF, michezo, miziki,....
 
Nauliza hv nyerere ndo aloteta huo mfumo kristu.?wakolön walitugawa ili watutawale na ikumbukwe kwamba wakolon walikuwa wazungu kwa hyo ni wakristu..nyerere kajitahid kuweka usawa kupitia azimio la arusha mkaleta la zanzibar afu mnasema nyerere kaleta mfumo kristu asa angewasaidiaje..au labda mtu aniambie kuwa nyerere ndo alovunja azimio la arusha?

Soma vizuri posts utajuwa tatizo liko wapi. Kwa ufupi azimio la arusha lilikuwa ni kuuleta mfumokristo "mkitaka msitake" na si kuliondoa.
 
Yaliondolewa wapi na nani? Tunamshukuru Mungu asiye na DINI ambaye ameifikisha TANZANIA hapa ilipo. Hatuna DINI ya TAIFA, hatuchagui wala kuteua viongozi wetu kwa kushauriana na Maaskofu wala Masheikh. Tunachanganyika vilivyo kuanzia ndoa, familia, makazi, shule, ajira, misiba, humu JF, michezo, miziki,....

Soma kitabu cha Sivalon.
 
Na ndio nakwambia ya kwamba hii ni historia ulosimuliwa wewe na watu waliotaka wewe ufahamu hivyo. Labda nikuulize una umri gani? maanake nijuavyo mimi sisi wote tumesimuliwa, hivyo kama alivyosema JK ukiambiwa kitu Usifuate ya Gong'ota, kuwa kama Mbayuwayu changanya za za kwako!.. tatizo wewe Gong'ota hutaweza kufikiri kaa Mbayuwayu!..


Tewa Said Tewa hakuwa kikwazo cha EAMS isipokuwa alikuwa pandikizi la TANU ndani ya EAMWS ktk maswala yanayohusu jumuiya hiyo na kati ya wazee wote ulowataja hakuna ambaye hakuwa mwanachama wa AMNUT, sasa unapoleta ya Biti Titi unakwenda wakati mwingine kabisa na yeye pia alikuwa na matatizo yake ya kisiasa acha hayo ya kushiindwa uchaguzi..

Mkandara,

ndugu yangu elewa utafiti siku zote unapingwa kwa utafiti na sio hisia kutoka kichwani mwako. Kama unavyomuona Mohamed Said anaweka mpaka data na source zake kwetu sote na wewe jitahidi sana kama una data au source zozote tuwekee.

Kwani wengi tunamjua Nyerere akitaka lake liwe halitumia kila hila na linafanikiwa. Enzi za Nyerere saa hizi Mohamed Said tusingekuwa nae kabisa au sote hapa tungekuwa tunamkimbia. Kwani Nyerere angetukama wote pamoja na jamii na maswahiba zake wote kisha kutupoteza. Ni nani asiyejua hayo.

Ni nani asiyejua kuwa Nyerere hakupenda kufanya kazi na watu wasomi wanaojiamini alipenda wasomi wasiojiamini na waoga ili aweze kuwaendesha atakavyo yeye. Na hicho ndio mbegu mbaya aliyoipandikiza kwenye uchumi wa Tanganyika mpaka sasa mnakuwa masikini asiyat.

Kumbuka sasa tupo dunia ya uwazi na ukweli. Mohamed said anafanya kazi ambayo wengi waislam walishindwa kuifanya. Kwani waislam wameamrishwa wanapoona maovu basi wayakemee ima kwa mikono yao, au mdomo wao au kwa imani dhaifu kuyachukia moyoni mwao.

Mohamed amekemea kwa mkono wake kwa kupoteza muda na mali zake (fedha) kufanya utafiti na kisha kuuweka hadharani na hata JK Nyerere ameupata na kuusoma kwa kina sana lakini hakuwa na la kukosoa. Kwani kila kitu kina karne yake.

nakupongeza sana Mohamed Said. Allah akubariki sana.
 
Unajua wakuu, mkitaka tusonge mbele kama taifa tuache hizi siasa mfilisi za CCM za kugawa watu kwa makundi na dini zao. Sasa kuna ndugu zangu hapa akina Barubaru mnaona CCM na serikali yake kama ndo adui nambari wani wa uislamu. Hapo hapo mnashindwa kuelewa kwamba hiyo serikali ya CCM kwa mda mrefu (mpaka leo) imekuwa ikiongozwa na waislamu na wasio waislamu. Mfano, leo hii safu karibu yote ya tanzania ya viongozi wa juu ni waislamu (atleast ndivyo wanavyojitambulisha).....Lakini bado tunalia kwa kunyanyaswa na 'mfumo kristo'. Sasa hebu niulize..ukombozi wa waislamu utatoka wapi? Maana wanaopewa nafasi..bado wanaonekana as if wao sio waislamu......I honestly dont understand this!

Sasa 'makafir' kama Masanja hapa tunasema tuungane watanzania wote tuiwajibishe serikali tuliyoichagua. Tunaambiwa tuna chuki na waislamu kwa sababu tunam-attack Kikwete ambaye ni muislamu. Ok, tunasema ngoja tutafute chama mbadala..labda tuone kama kina nafuu..tunaambiwa hicho ni cha wakatoliki kwa sababu kuna Dr. Slaa. Sasa hebu Barubaru twambie...kama watanzania tufanye nini kuondoa hiyo dhulma ambayo waislamu mnalia nayo kila siku? maana you guys it seem you want to eat your cake and have it at the same time. Mfano...taifa letu hata kama ni masikini bado tunaongozwa na sheria. You cant impose your will on others. Sasa jamani mlitaka JK aruhusu mahakama ya Kadhi wakati katiba hairuhusu? People get life jamani....

Mimi naamini, Tanzania challenges zinazotuface hazina dini wala kabila. Mafisadi ni waislamu, wakristo na wasio na dini. Ni hizi mentalities za kutaka special treatment nadhani ndo maana hata hao 'waislamu' wakifika huko madarakani wana-ignore 'kelele' za wenzao maana wanajua kabisa hazina mashiko.

Tuungane tulijenge taifa! Once you consider your self or allow people to define you as a victim of anything-you will always be a victim. Ndo maana hapa watu wanalia na historia ya miaka 50-100 iliyopita, baada ya kuangalia watoto wao na taifa letu tutasonga mbele vipi katika miaka 50 ijayo. Tragic indeed!

Katika hili ahali yangu hakuna siasa hapa.
Kinachotakiwa ni kuhakikisha keki ya taifa inaliwa na wote kwa usawa pasi na dhulma wala ubaguzi wa aina yoyote. Kwani siku zote kwenye dhulma hakuna haki. Na pasipo na haki basi hakuna amani.

Sasa sote tuombe amani ya kweli sio ya kinafiki.
 
Mkandara,

ndugu yangu elewa utafiti siku zote unapingwa kwa utafiti na sio hisia kutoka kichwani mwako. Kama unavyomuona Mohamed Said anaweka mpaka data na source zake kwetu sote na wewe jitahidi sana kama una data au source zozote tuwekee.

Kwani wengi tunamjua Nyerere akitaka lake liwe halitumia kila hila na linafanikiwa. Enzi za Nyerere saa hizi Mohamed Said tusingekuwa nae kabisa au sote hapa tungekuwa tunamkimbia. Kwani Nyerere angetukama wote pamoja na jamii na maswahiba zake wote kisha kutupoteza. Ni nani asiyejua hayo.

Ni nani asiyejua kuwa Nyerere hakupenda kufanya kazi na watu wasomi wanaojiamini alipenda wasomi wasiojiamini na waoga ili aweze kuwaendesha atakavyo yeye. Na hicho ndio mbegu mbaya aliyoipandikiza kwenye uchumi wa Tanganyika mpaka sasa mnakuwa masikini asiyat.

Kumbuka sasa tupo dunia ya uwazi na ukweli. Mohamed said anafanya kazi ambayo wengi waislam walishindwa kuifanya. Kwani waislam wameamrishwa wanapoona maovu basi wayakemee ima kwa mikono yao, au mdomo wao au kwa imani dhaifu kuyachukia moyoni mwao.

Mohamed amekemea kwa mkono wake kwa kupoteza muda na mali zake (fedha) kufanya utafiti na kisha kuuweka hadharani na hata JK Nyerere ameupata na kuusoma kwa kina sana lakini hakuwa na la kukosoa. Kwani kila kitu kina karne yake.

nakupongeza sana Mohamed Said. Allah akubariki sana.

Barubaru,

Amin, Amin, Amin ndugu yangu Amin.
Allah aturidhie na atupe ushindi na aiweke nchi yetu kwenye salama na amani kila mtu aishi kwa haki na usawa na dhulma zote zitokomee.

Amin.

Mohamed
 
Mkandara,

ndugu yangu elewa utafiti siku zote unapingwa kwa utafiti na sio hisia kutoka kichwani mwako. Kama unavyomuona Mohamed Said anaweka mpaka data na source zake kwetu sote na wewe jitahidi sana kama una data au source zozote tuwekee.

Kwani wengi tunamjua Nyerere akitaka lake liwe halitumia kila hila na linafanikiwa. Enzi za Nyerere saa hizi Mohamed Said tusingekuwa nae kabisa au sote hapa tungekuwa tunamkimbia. Kwani Nyerere angetukama wote pamoja na jamii na maswahiba zake wote kisha kutupoteza. Ni nani asiyejua hayo.

Ni nani asiyejua kuwa Nyerere hakupenda kufanya kazi na watu wasomi wanaojiamini alipenda wasomi wasiojiamini na waoga ili aweze kuwaendesha atakavyo yeye. Na hicho ndio mbegu mbaya aliyoipandikiza kwenye uchumi wa Tanganyika mpaka sasa mnakuwa masikini asiyat.

Kumbuka sasa tupo dunia ya uwazi na ukweli. Mohamed said anafanya kazi ambayo wengi waislam walishindwa kuifanya. Kwani waislam wameamrishwa wanapoona maovu basi wayakemee ima kwa mikono yao, au mdomo wao au kwa imani dhaifu kuyachukia moyoni mwao.

Mohamed amekemea kwa mkono wake kwa kupoteza muda na mali zake (fedha) kufanya utafiti na kisha kuuweka hadharani na hata JK Nyerere ameupata na kuusoma kwa kina sana lakini hakuwa na la kukosoa. Kwani kila kitu kina karne yake.

nakupongeza sana Mohamed Said. Allah akubariki sana.
Barubaru,
Ukiweka kando chuki zako mbili dhidi ya Mwalimu. Ukaufungua ubongo wako utagundua kuwa UNAONGOPA na KUMSINGIZIA mambo mengi sana Mwalimu. Mwalimu aliwaweka ndani wahalifu tu. Mwalimu wala hakuwachukia wasomi. Alijenga vyuo vikuu vya nini sasa! Mohamed huyu unayemsema hapa amekuwepo tangu enzi za Mwalimu na UDINI wake huuhuu. Na sio yeye tu.
Najua unamchukia Mwalimu kwa Ukristo wake na pia kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao ninyi wa-Oman na Waarabu wengine mnadhani hata mapinduzi ya Zanzibar yana mkono wa Mwalimu. Hamtamsamehe. Mkipata mijadala na hoja kama hii mnakomaa kwelikweli.
 
1. Maandishi na ushahidi wa vitabu mbalimbali unaotolewa either kwa mazungumzo yake nyerere na matokeo ya siasa zake yanaonyeshwa si na Mohammed tu pia waandishi wengine kuwa alikuwa mdini sana..sijaona kwenye maandishi ya Mohammed akisema wakristo wote ni wabaya na waislamu wote ni malaika atakuwa amekosea ..udini wake nini kuulezea historia ya wazee wake ambao walitokea kuwa waislamu? kuna shida kueleza mchango wa uislamu kwa uhuru wa nchi yetu?? huo ndio udini wenyewe kuchukia ukweli kwakuwa unaonekana kuukuza uislam?? what worries you and others? if I may ask?

2. Kunyang'anya shule inaweza ikawa kitu kizuri lakini haina maana kama unatengeneza utaratibu katika serikali ili kuwabagua wananchi kuwajaza wakristo serikalini kwa hila huku ukiwabagua wakristo ..ni sawa na kuruka moshi na kukanya'anga moto..kunyang'anya shule hakuna maana kama unakubali wakristo wandeshe seminary zao wakati huo huo unavunja jumuiya ya kiislamu yenye maendeleo makubwa na kuweka mamluki wachumia tumbo kwa faida ya kanisa kama anavyoeleza Mohammed kwenye vitabu vyake..

3. Hao JF watalaumu mtu bila wewe kuleta evidence (researched) kwamba hao watu walihusika katika kuhujumu watu fulani au Taifa?? kama alivyofanya Mohammed kwa nyerere au unataka tusikilize ngojera za mtaani na kukuamini???

Acheni kumshambulia Mohammed kwa Udini wakati huo huo mnashindwa kumshambulia Nyerere kwa udini wapi na wapi?? mnabaki na double standards???

Siku zote anayesema fulani mchawi basi mchawi ni yeye. Kwani alijuaje kuwa ni mchawi?.

Tatizo ni wavivu wa kusoma vitabu bali wamezoea kubebwa na mfumo wa kupenda kurahisishiwa kila kitu. Msomeni kitabu cha Padre Silvalon ameweka bayana kila kitu.
 
Hhahahaaha...sasa MS you are a very strange person bro! kwani huyu Magotti anatofauti gani na wewe? It is the precise thing of what people have accused you in this thread. Kuandika bila kuhoji upande wa pili! Perhaps, na wewe ungetake trouble kufanya yale unayomtuhumu Magotti tungekuwa na narrative tofauti. Lakini majibu yako ni yale ya 'na wengine wakaandike historia yao...' Basi na Magotti atasema hivyo hivyo!!

Nafurahi kuona kwamba na wewe umeigundua hiyo double standard, tragically wewe hujioni kwamba you have done exactly the same thing! Na implication yake ingawa unai admitt kwenye kitabu cha Kawawa..kwako huioni! Duh...

Tatizo MS you 'know alot of things', lakini unasahau kwamba humu JF watu tunasoma kama wewe na kufanya 'analysis' so we dont simply swallow stuffs! Ndo maana watu hapa wanakujibu kwa hoja. Strange world? uhhh???

Masanja,

Mei sisomwi JF tu.
Hapa naja kwa msimu.

Mimi kila wakiingia wanafunzi wapya vyuoni Marekani na Ulaya na ikiwa somo watakalochukua ni African History, Islam and Politics basi jua nasomwa na kitabu changu mwalimu anafundishia.

Hilo la kwanza mimi nina "paper" katika somo hili hesabu yake sizijui.

Jambo la pili.

Hushangai kila akitajwa mtu nakuwekea bandiko lake tena ni "paragraph" moja tu.
Huu ni utafiti wa "lifetime."

Fananisha utapata jibu.

Mohamed
 
Tusihangaike sana na Maandishi haya ya Mzee Mohamed ambayo yamekuwepo zaidi ya miaka 10 iliyopita na hayakuleta madhara wala kuibadili HISTORIA ya NCHI yetu. Pengine tunayakuza bila sababu. TANZANIA itabaki bila DINI. Hatutagawana vyeo, madaraka, elimu, viwanja, mashamba,...., kwa misingi ya DINI.

WC,

Alokwambia historia haijabadilika nani?
Toka huko uliko fungua macho, sikiliza, soma utatambua nyakati zimepita.

Kuna shule za Waislam zinatoa zawadi ya Sheikh Hassan bin Amir kwa mwanafunzi bora.
Kuna zawiyya zinaitwa Sheikh Suleiman Takadir nk. nk.

Kabla ya sasa ulisikia neno "mfumokristo" likirushwa hewani na radio mubashar "live?"

Ndugu yangu uko dunia gani?

Mohamed
 
Huku mzee nilishaaga kwa kudhani kwamba tumeelewana na MS na mashabiki wake. Lakini nilipochungulia nikaona bandiko lako, kwa kweli ni hitimisho zuri sana, lakini naomba niongezee kitu kidogo ambacho niliona kwenye mjadala huu.

Kwanza kuna dhana mbili ambazo ndizo zinaongoza mjadala mzima na tafakuri ya MS kwenye kuwasilisha mada yake ya "Udini wa wakristu" na ile mada ya pili ya "Uonevu dhidi ya waislamu". Dhana mbili zinazoongoza mada za MS ni "uislamu ni dini bora kuliko nyingine" na " Mfumo bora wa kuendesha nchi ni kwa kutumia mfumo wa Kiislamu"

Dhana hizi mbili ndizo MS anazitumia kujengea hoja zake nyingi. Ndiyo maana alitaka kuonyesha ni kwa kuwa kwao waislamu ndiyo maana Kinjekitile, Chabruma, na Mkwawa walipigana na wakoloni wa Kijerumani.

MM,

Shida kubwa itakukuta kusimama na mimi katika mnakasha.
Nimekusoma.

Huwezi kuivunja historia niloandika kwa bandiko katika JF.
NARUDIA...andika kitabu au angalau "paper."



Mohamed
 
Barubaru,
Ukiweka kando chuki zako mbili dhidi ya Mwalimu. Ukaufungua ubongo wako utagundua kuwa UNAONGOPA na KUMSINGIZIA mambo mengi sana Mwalimu. Mwalimu aliwaweka ndani wahalifu tu. Mwalimu wala hakuwachukia wasomi. Alijenga vyuo vikuu vya nini sasa! Mohamed huyu unayemsema hapa amekuwepo tangu enzi za Mwalimu na UDINI wake huuhuu. Na sio yeye tu.
Najua unamchukia Mwalimu kwa Ukristo wake na pia kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao ninyi wa-Oman na Waarabu wengine mnadhani hata mapinduzi ya Zanzibar yana mkono wa Mwalimu. Hamtamsamehe. Mkipata mijadala na hoja kama hii mnakomaa kwelikweli.

WC,

Huko ni kuishiwa na Sera.

Lakini nitakudondolea kidogo tu. Mimi nimefanya kazi enzi za Nyerere mara tu baada ya kumaliza UDSM shahada ya uchumi na nimefanya nae kwa ukaribu sana nikiwa kitengo cha Bajeti wizara ya fedha (muungano). Namjua vilivyo.

Lakin tuache hayo. Mimi nakwambia mtu yeyote makini na aliyekuwa anajiamini na kuthamini taratibu na kaanun za taaluma yake Nyerere hakumpenda .

Mfano ni waziri wetu wa fedha Edwin Mtei, Abdurahman Babu,Idi Simba (enzi za azimio la Arusha) na wengine wengi sana ambao Mohamed said amewabainisha na kuwataja.

Na ninaposema Nyerere nu muasisi wa Ulanguzi wa bidhaa hapo Tanganyika nafikiri sitakuwa nimesema uongo. Kwani haijawahi tokea ulanguzi wa kitu chochote iwe sabuni, kiberiti au hata chakula kabla ya uhuru 1961.Watu wakti wa ukoloni waliishi maisha bora sana na kila kitu kilikuwa kinapatikana madukani. Na ulanguzi huo ndio sasa umekuwa na kupevuka na kuwa ufisadi.

sasa nibainishie ni kipi nitachomtuhumu Nyerere ambacho si cha kweli?

Suala la muungano nafikiri nimeliweka bayana kwenye barza za faida za muungano kwa Znz?

Lakini likuuliza tokea huko awali na hujanipa jibu. Je unajuwa TZ kwanini ni masikini wakati ndio ilikuwa nchi tajiri kabla uhuru kuliko nchi zote za afrika mashariki na kati?
 
Huyo ndiyo Mkandara .'ashomile'..! Inasikitisha sana kuona jinsi taasisi nyingi za waislam zilivyokosa watu wa calibre ya Mkandara...!

Sweke34,

Ni kwa kuwa hujui.

Ingekuwa hapa ni uwanja wangu ningekupa kisa cha Ubay bin Kaab.
Kwako wewe kumsifia Mkandara kuwa Muislam "hodari" umemmaliza.

Na ukisikia siku mimi nimesifiwa na watu kama nyinyi basi jua hamna kitu nishawageuka Waislam.
Hii ndiyo historia ya Uislam na ndiyo Qur'an yenyewe na ndiyo kauli yake Allah SW.

Kama Mkandara ni Muislam khasa jua kwake leo ni siku ya msiba mkubwa.
Mtafute Muislam yeyote akupe kisa cha Mtume SAW na Ubayy bin Kaab utaelewa haya nilokueleza.

Kutokujua nako hakika kuna raha yake.
"Ignorance is bliss."

Mohamed
 
Nimesema hivi ukichora mstari kutoka kwa "wazee" wa Mohammed Said na wale waliotaka kuondoka TANU kupitia AMNUT mwaka 1958 na wale waliomkataa Nyerere mara ya kwanza alipotambulishwa kwao early 1950s utakuwakuta kuwa niw atu wale wale. Chuki dhidi ya Ukatoliki wa Nyerere haikuanza 1962 kwenye congress ya Waislamu wote na wala siyo Waislamu wote wa Dar walikuwa na chuki dhidi ya Nyerere. Ndio maana waliowashinda AMNUT mwaka 1958 walikuwa ni Wazee Waislamu wa Tanga.

Ukiniuliza mimi hadi leo huoni akiwataja wazee hawa kwa heshima. Barubaru anawajua sana wazee wa Tanga lakini ni ndio hawa ambao majina yao hayatajwi lakini kiukweli kabisa naweza kuwaita ndio MASHUJAA WA UHURU kwa maana ya kwamba kama wangekubali AMNUT nchi ingegawanyika. NI hawa wazee wa Tanga walioona mbali zaidi kuwa Tanganyika ni moja na wote tuna maslahi ndani yao. Katika kitabu cha Bw. Said anasimulia vizuri sana jinsi Nyerere alivyoonesha ushawishi mkubwa na kuweza kuwazidi siasa kina Mtemvu kwenye ule Mkutano wa Tabora. Mashehe wa Tanga hawatajwi sana japo walikuwa na mchango mkubwa sana.

Ningefurahi kusikia kama Barubaru anaweza kutusaidia kutoka upande huo.

Bw. Said angetaka kuandika historia ya wale "MASHUJAA WALIOSAHAULIWA" kwa kweli angekuja nahistoria tamu sana ya wazee 'wetu'. Asingeangalia dini zao kabisa lakini hilo lingevunja vunja kabisa kile alichotaka kusema ambacho kwa uhakika kabisa hajawahi kupata changamoto ambazo anazipata hapa. Nimeangalia kwenye youtube nyingi anapozungumza mbele ya vijana ambao maskini wa Mungu hawana hili wala lile zaidi ya kuitia na kuonesha kushangazwa. Vijana hawa ambao wengine hawajui kabisa historia ya nchi yetu imetoka wapi lakini wako tayari kuaminishwa histohisa ambayo inapendekezwa kwao kuwa ni historia.

Kwa kutumia 'authority' ya kuwa vitabu vyake vinachapishwa na kusomwa sehemu mbalimbali duniani Bw. Said anawaaminisha wasikilizaji wake kuwa anachosema ni kweli. Kwa sisi wengine tunajua kabisa kuwa vyuo vikuu kama vya Marekani vina vitabu vya kila aina na vyenye dhana mbalimbali si lazima vikubaliane na dhana hizo. Wenyewe wanaita "academic freedom". Ndio maana utakuta vitabu vinavyozungumzia masomo ya ajabu ajabu lakini kwa vile ni vyuo vikuu vinakubalika kwa sababu ndio kufunguana mawazo. Kwa wale vijana wa mitaani ambao wana kiu na kujua historia yao wanajikuta wanakubali masimulizi haya hasa kwa vile jamaa alikuwa ametoa mihadhara kwenye vyuo mbalimbali.

Nina uhakika wa asilimia mia Bw. SAid hawezi kuita mhadhara wa wazi na wasomi wa historia ya Tanzania akaweza kujitetea zaidi ya mbinu hii mpya "na nyie nendeni kaandikeni". Madai yake mengi hawezi kuyatetea, ushahidi wake hawezi kuutetea, na mahitimisho mbalimbali hayana msingi wa kihistoria.

Lengo lililo ni jepesi tu - kupandikiza chuki kwa Waislamu dhidi ya Kanisa na Wakristu. Ni kwa kufanya hivi tu ndio anapata uwezo wa kuzunguka na kuaminisha watu. Lakini Watanzania wakikataa hii chuki - ambayo imepata mashabiki hata wasomi wa hali ya juu na maafisa wa juu katika taasisi zetu mbalimbali - watapoteza nguvu ya sumu hii. Ni sawasawa na simulizi moja la kwenye Star Trek ambapo silaha moja ilikuwa na madhara zaidi kama wale wanaoshambuliwa nayo na wao wanaonesha aggressive behavior. Kwa hasira na kutaka kupigana ndivyo silaha ya adui yao ilivyokuwa inazidi kupata nguvu. Lakini Patrick Stewart (Capt. Jean Luc Picard) anawaambia kina Worf na maofisa wengine "to empty all aggressive thoughts" ndivyo yule adui yao alivyoshindwa kutumia silaha yake. Kwani kila akijaribu kuwaprovoke wapigane naye wao waliweka silaha zao chini na badala yake wakarudisha amani na upendo na kumshinda.

Chuki ya kidini ambayo Bw. Said anajitahidi sana kuipanda kwa mbinu ya upotoshaji wa hali ya juu wahistoria hata hivyo haiwezi kuachiliwa kimya kama wanavyofanya baadhi ya viongozi wetu. Bali inatakiwa ijibiwe kwa nguvu ya hoja ambazo zinasimama zenyewe. Baba wa Taifa aliwahi kusema kuwa "hoja dhaifu hushindwa kwa kuoneshwa kuwa ni hoja dhaifu na huondolewa kwa hoja nzuri zaidi". Hoja ya kuwa Kanisa na WAkristu ndio tatizo la Waislamu nchini inavutia. Inaonesha ina ukweli na kwa namna fulani inakubaliana na hisia za watu. Lakini inaposogezwa karibu kwenye darubini watu wanatambua mara moja kuwa hicho ni kisingizio tu. Na ndipo hapa Watanzania wamekuja pamoja wenye threads hizi zote kupinga hoja za Bw. Said, kuzionesha kuwa ni dhaifu na kuzikosoa pasipo huruma.

Na tuelewane vizuri kabisa. Hoja zinazopingwa siyo historia au sehemu ya historia ambayo Bw. Said anaisimulia. Kutuambia habari za kina Sykes, Plantan, Tambaza na wengine ni sehemu ya historia yetu. Bw. Said yeye anafanya ni historia ya Waislamu wakati kwa kweli kabisa ni urithi wetu sote kwani hawa wote ni wazee 'wetu' tena ni WETU kwa herufi kubwa. Ni sawasawa na Wamarekani ambao mwanzoni waliona kuwa sikukuu ya Martin Luther King Jr. ilikuwa ni sikukuu ya Watu weusi tu. Lakini sasa hivi Wamarekani weupe kwa weusi, wanjano na wa kahawia wote wanamkubali MLK Jr kama shujaa wao. Leo hii watu mbalimbali ambao miaka michache nyuma walionekana ni wa kikundi fulani tu wanaonekana ni wa Taifa zima kwa sababu mchango wao ni mchango wa historia ya Marekani. Ni sawa sawa na Wazungu kule Afrika ya Kusini. Unafikiri Wazungu hawamuenzi Mandela? Well walimfunga gerezani lakini leo hawamuenzi? You bet they do! kwa sababu ni historia yao ni mzee wao na wanaona fahari kuwa naye.

Sasa leo hii Bw. Said anataka kuwafanya mashujaa wa historia yetu kuwa ni mashujaa wa watu wa Dar peke yao. Anajaribu kuwagawa mashujaa wa historia yetu katika makundi ya Waislamu na Wakristu! Ili kiwe nini? Well... soma sentensi ifuatayo vizuri: Nyerere awe shujaa wa Wakristu na Abdulwahid Sykes awe shujaa wa Waislamu! Bahati mbaya hawezi kuwa na Sykes katika kiwango hicho kwa kadiri ya kwamba Nyerere naye bado yupo juu. Said hawezi kusema jema lolote la Nyerere, hawezi kukiri mambo yoyote mazuri ambayo Nyerere aliwafanyia Waislamu, hawezi kuthubutu kukiri kuwa Nyerere alikuwa na unique role (yeye anaseme 'leading role'). Kwake yeye Sykes ndiye muasisi wa Tanganyika na Nyerere alikaribishwa tu. There nothing special about Nyerere. Unfortunately, some of our young politicians as well some educated/miseducated elite wameingia kwenye mtego huu.

Bahati mbaya ni kuwa Watanzania wametambua mtegu huu mwepesi. Tunatambua mchango wa wazee wetu wengi ambao hawajulikani. Nakumbuka niliwahi kuandika nyuma kuwa labda wakati umefika kuwa restore to honor baadhi ya waasisi wa taifa letu. Wote wale ambao walitoa mchango mkubwa kabla ya Uhuru regardless of what happened after independence warudishiwe heshima yao na hadhi yao irudi. Ukiondoa wale ambao labda ambao hawakuweza kabisa kurudishwa katika historia. Na hili haliwezekani isipokuwa.

1. Tuwe wa kweli kwa historia. Tuwataje wote na binafsi kweli kabisa ningependa kweli kuwasikia watu wa familia za kina Aziz, Mwapachu, Sykes wanasema nini kuhusu haya. Kwa ukimya wao wametoa baraka kuwa na wao wanaamini kuwa kweli Nyerere alikuwa na chuki dhidi ya Waislamu.
2. Tusahihishe na kuhoji histohisia inayoendesha na Bw. Said ambayo inapambwa kama historia.
3. Wasomi wetu wajibu changamoto ya Bw. Said ya kuandika historia yetu nzima bila kuiogopa. Ni kweli bado hatujazama sana katika historia yetu inavyopaswa hasa linapokuja kwenye suala la harakati za kupigania uhuru.
4. Binafsi naamini kama kuna kipindi cha historia yetu ambacho kinahitaji kusomwa vizuri ni 1961-1971 (Miaka 10 ya kwanza). Ni kipindi hiki matukio yote muhimu ambayo yameifanya Tanzania ya leo iwe yametokea na ni matukio ambayo yangeweza kujaza juzuu za vitabu. Fikiria
- Uhuru
- Mapinduzi ya Zanzibar
- Muungano
- Kuasi kwa Jeshi
- Uamuzi wa Chama Kimoja
- Azimio la Arusha
- Expulsion of prominent figures from the Party

Haya mambo yote ni ya kihistoria sana na wakati umefika kuanza kuyaangalia na si rahisi kuyaangalia moja moja bali ni mambo ambayo japo labda yanaoverlap yanahitaji kuangalia moja nje ya jingine.

Mwanakijiji,

narejea tena kusema unakuwa uwatendei haki wanajamii hususan wale wenye kiu kubwa sana ya kuona na kuyasoma yale yaliyosahaulika katika historia ya uhuru wa Tanganyika. Na kumbuka kwa msomi huwa siku zote hakosoi kitu pasi na kuonyesha njia sahihi ni ipi. Kwani tunaamini uongo ukikaa muda mrefu basi unageuka kuwa kweli.

Naungana na Mohamed Said hapa anaposema.
MM,

Shida kubwa itakukuta kusimama na mimi katika mnakasha.
Nimekusoma.

Huwezi kuivunja historia niloandika kwa bandiko katika JF.
NARUDIA...andika kitabu au angalau "paper."



 
Back
Top Bottom