Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Bismillah,

wanajanvi naona mnazunguka saana pasipo kutuliza vichwa vyenu mkamsoma Mohammed Said vizuri anakotokea na kwa nini amekatalia kipande cha ardhi yake kuwa historia..Na muda mrefu nimekuwa najiuliza kama kuna haja ya kupasua jipu hili lakini nadhani umefika muda muafaka nizungumzie kulikoni...Itakuwa hadithi ndefu kidogo naomba uvumilivu wenu..

Nimemsoma sana Mohammed Said na nadhani lengo lake la awali ni historia ya Wazee wake ktk mchango wa Uhuru wa Tanganyika, wazee ambao baada ya Uhuru leo hii wamesahaulika - FORGOTTEN HEROES - ktk historia ya nchi yetu lakini hakutafuta sababu zaidi ya maelezo alosimuliwa na jamaa zao wenyewe, ama misukosuko ilotokea kuwa sababu ya maswali mengi anayojiuliza lakini hukwepa kipande cha matukio kati ya mwaka 1963 hadi kufikia 1967, matukio ambayo yalisababisha na upande huo huo anaoutetea na muhimu sana kuyaelewa toka upande wa pili ili kuhitimisha.

Mohammed Said anazungumzia wazee wake kina Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Yusuf Badi, Dossa Aziz, Sheikh Mohamed Ramia, Bi Tatu biti Mzee, Dharura biti Abdulrahman, na Sheikh Hassan bin Amir ambao kweli wamesahaulika ktk historia ya nchi yetu na wala hakuna kumbukumbu zao ama baadhi yao Kitaifa..Madai haya ni regit na naweza kuelewa wapi Mohammed Said kasimama dhidi ya historia ya Tanganyika iliyopo ana inayonadiwa sana na waandishi wa vitabu na habari..

Nafikiri hadi hapa wengi tunaweza kukubaliana naye na haswa mtu kama Abdulwahid Sykes, Dosa Aziz wakati watu kama Julius Nyerere, John Rupia, Oscar Kambona, Paul Bomani na wengine kibao ni maarufu hata kwa kizazi hiki kipya wanajua mchango wa watu hawa katika Uhuru wa Tanganyika kupitia historia yetu..Katika hili bila kutaja dini zao nakubaliana sana na Mohammed na ndio maana nikauliuza historia ya Cecil Matola na mbona kiongozi huyu kasaulika?..

Kikubwa anachokosolewa Mohammed Said ni pale alipotengua lengo la awali na kulifanya swala hili kuwa la imani ya dini (conclusion yake) na kwamba hawa viongozi wamesahaulika kwa sababu ni Waislaam ama serikali imepotosha mchango wa Waislaam ktk harakati za Uhuru wa Tanganyika hivyo kuifanya hoja nzima ya TAA na TANU kuwa ya kidini zaidi ya chama cha siasa...

Nachomuomba Mohammed Said ni kimoja tu ya kwamba, hata historia ya Zanzibar haiwezi kuwa historia sahihi kama hutazungumzia viongozi waarabu wa Hizbu party. Na mtu yeyote kipenzi wa Hizbu anaweza kuja hapa na kudai haoni sababu kwa nini Karume maarufu kuliko Shamte, akatumia hata race card ya kama tunavyowasoma Wazanzibar wengi wakizungumzia Mapinduzi kama ilikuwa njama ya watu weusi dhidi ya Wazanzibar wenye asili ya Kiarabu na kadhalika..Yote haya yanaweza kuwa na ukweli lakini lengo la mwandishi linapokuwa linalenga kuonyesha dhulma fulani ni muhimu sana kwetu kupima hiyo dhulma inayodaiwa kisha tujenge hoja zinazopinga ama kuhalalisha dhulma hiyo..

Mimi nachoweza kumwambia Mohammed Said, historia ulopewa ya wazee wako kuna mengi umefichwa ama wewe mwenyewe umeamua kuiacha pembeni lakini kati ya kundi kubwa la wazee wako toka mwaka 1964 kufikia mwaka 1967 walikuwa tayari wamejitenga na chama TANU, walikuwa tayari wakitaka kufanya Mapinduzi dhidi ya chama TANU ambacho kiliongozwa na Nyerere walikuwemo waislaam wengi sana viongozi vile ivle, na Waislaam karibu mikoa yote walipingana na dhana ama lengo la hawa wazee wako waliojitenga...Hivyo, unapojitoa ktk chama kumbuka pia unapoteza haki zote ulostahili kupewa na historia yako inakuwa na picha tofauti kama ilivyokuwa kwa kina Mtenvu na Kambona.

Hatuwezi kuwa na historia njema ya Kambona zaidi ya kwamba alitaka kuipindua nchi. Na vile vile hatuwezi kuwa na historia nzuri ya kundi la watu walitaka kuanziusha vurugu nchini kwa kutumia sanduku la Udini ila naweza sana kukubaliana na wewe kwamba kuna viongozi wetu waliokuwa na mchango mkubwa sana ktk harakati za Uhuru wetu wamesahauliwa. Hawa ndio wanatakiwa kuitwa mashujaa na hawa ndio wanatakiwa kuenziwa kwa kila sifa ya Uzalendo na hata kusherehekewa ktk Memorial day!.

Nilichoweza kujifunza mimi kutoka vitabu vya Mohammed Said ni kwamba - Historia ya Tanganyika inapotea na ipo haja na sababu kubwa ya vitabu kama cha John Lliffe - A Modern History of Tanganyika kiwe ktk vitabu vinavyotakiwa kufundishwa mashuleni iwe Primary school au Secondary. Lakini haya maswala ya Udini au kutumia Uarabu kudai haki ya Uzanzibar haiwezi kujenga umoja wa kitaifa bali unabomoa hata imani ndogo ya uzalendo iliyokuwepo..Leo hii ukimwambia Mgazija kwamba Waarabu ndio waasisi wa Uhuru wa Zanzibar na Shamte alikaribishwa tu, sijui kama kutakalika.

Maasalaam!

Mkandara,

Maneno mazuri.

Nami nakuwekea maneno yangu hapa chini:
Wazee wangu hawakujitoa TANU bali walitolewa kwa hila na fitna. Hawa wafuatao ni baadhi ya wazee wangu walowekwa kizuizini: Abdillah Schneider Plantan, SheikhAbdulkarim Abdulwahid, Maalim Popo Saleh, Suleiman Masudi Mnonji, Ali Migeyo,Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Shariff Hussein Badawiy, Shariff Mwinyibaba,Shariff Adnan, Bilali Rehani Waikela, Sheikh Jumanne Bias, Maalim Matar,Abdalah Mwamba, Sheikh Hashim Haji Abdallah, Sheikh Nurdin Hussein, SalumAbdallah Popo, Sheikh Mzee Ali Comoriam, Sheikh Al Amin Maftah, Rajab Kiguu chaMbuzi na wengine wengi. Lakini ukweli ulikuwa kwamba si wote katika walewaliokamatwa na kuwekwa kizuizini walijihusisha na siasa. Baadhi yao walikamatwakwa sababu tu walikuwa wakishirikiana na wale waliodhaniwa ni wapinzani waNyerere. Maalim Matar na Shariff Adnan walifungwa jela kwa sababu tu walihusikana msikiti wa Badawiy mjini Dar es Salaam ambako Sheikh Hassan bin Amir, wakatihuo akichukuliwa kuwa ndiyo roho ya waumini wa Tanganyika, alikuwa ikiendeshamadrasa yake kila magharibi pale msikitini. Shariff Hussein na nduguyeMwinyibaba walihamishiwa Kenya, walikotoka si kwa sababu walikuwawamejishughulisha katika harakati za kuipinga serikali, ila lakini kwa sababuwalikuwa waangalizi wa msikiti wa Badawiy. Sheikh Mzee Ali Comorian alitiwa kizuizini kwa sababu kila mara alikuwaakifuatana na Sheikh Hassan bin Amir kama vile alikuwa kivuli cha sheikh. Huendakile kilichomfanya Nyerere kuwatia kizuizini masheikh na wengine kuhamishwa nikufuata ule msemo wa Biblia usemao, "yule ambae hayuko nasi basi ni dhidiyetu."Jinsi siasa na za Tanzaniazilivyobadilika na jinsi Nyerere alivyoanza kuonyesha uadui dhidi ya Waislamkulimsikitisha sana Abdulwahid. Alishindwa kuelewa uhasama huu ulikuwa unatokawapi. Alihisi kuwa anahusika na yale yaliyokuwa yanawapata Waislam. Mawazo hayayalimzonga kama jinamizi. Kwa ufahamu wake alikuwa anadhani matatizo yote yaudini walikuwa wameyashinda toka miaka ya 1950. Mwaka 1953 Abdulwahid akiwaMuislam na akiungwa mkono na Al Jamiatul Islamiyya aligombea kiti cha urais waTAA na Nyerere, Mkatoliki. Abdulwahid alishindwa uchaguzi ule. Waislamhawakuuchukulia uchaguzi ule kama uchaguzi kati ya Muislam na Mkristo. Kilichotazamwani uwezo wa wagombea. Nyerere alikuwa amemzidi Abdulwahid na kwa ajili hiialichaguliwa kuiongza TAA. Abdulwahid alikumbuka ugomvi wa Sheikh SuleimanTakadir wakati ule Mwenyekiti wa Baraza La Wazee wa TANU. Sheikh Takadiraliwaonya Waislam wachukue tahadhari kwani Nyerere atakuja kuwapendeleaWakristo wenzake pale atakaposhika madaraka. Kama walivyofanya Waislam wengi,Abdulwahid alimuunga mkono Nyerere na kumpinga Sheikh Takadir. Wakati uleAbdulwahid aliamini kama Waislam wengi walivyoamini kuwa Sheikh Takadir alikuwaanataka kuleta siasa za kibaguzi ambazo alikuwa anaziegemeza katika dini.Abdulwahid aliona udini aliokuwa anataka kuuleta Sheikh Takadir lilikuwa jamboambalo litailetea hatari Tanganyika.Abdulwahid alikufa mwaka 1968 wakati nchiilikuwa imegubikwa na hasama za chinichini kati ya Waislam na Wakristo ambaosasa walikuwa wamehodhi madaraka yote katika serikali. Umoja wa kitaifa, mojaya maadili ambayo yeye aliyapigania katika maisha yake yote katika siasaulikuwa unahatarishwa. Halikadhalika umoja wa Waislam ulikuwa unaelekeakuvunjika. Kulikuwepo na kuwekwa kizuizini kwa masheikh chini ya PreventiveDentation Act of 1962. Baadhi ya masheikh waliotiwa gerezani walikuwa watu waliomuunga yeye mwenyewe mkono wakatianaunda TANU. Baadhi yao aliwashawishi kumuunga mkono Nyerere na TANU katikakile kipindi kigumu cha harakati za kudai uhuru. Mwanakamati wa Kamati Ndogo yaSiasa ya TAA, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, kiongozi wa ngazi ya juu kabisa kwaWaislam alikuwa amekamatwa na kuondolewa nchini na kurudishwa kwao Zanzibar kwaamri ya Nyerere.[1]Sababu iliyotolewa ya kukamatwa kwa Sheikh Hassan bin Amir ilikuwa alikuwaati "akipanga njama ya kupinduaserikali."Sheikh Hassan bin Amir alikuwa kati yaWaislam wachache ambao walithubutu kusimama kidete dhidi ya serikali na kutoamawazo yake kuhusu jinsi serikali ilivyokuwa ikiwakandamiza Waislam. Kablahajafa Abdulwahid alikuwa akifikiwa na habari kuwa kulikuwa na kampeniiliyokuwa ikiendeshwa kwa makini sana naWakristo ndani ya chama kuufuta Uislam ndani ya TANU. [1]Abdulwahid alikuwa anafahamu matokeo yakuvunjika kwa umoja wa Waislam. Yeye alikuwa anajua vyema nguvu ya umoja waWaislam wakati walipokuwa wanapigania uhuru wa Tanganyika. Abdulwahidhalikadhalika alikuwa anafahamu nguvu ya wale waliokuwa nyuma na njama zile zakuwagawa Waislam katika makundi hasimu. Vilevile alikuwa anatambua hofu na watuwote waliokuwa nyuma ya njama zile. Alifahamu kuwa wale aliowapokea na kuwatiakatika harakati za kudai uhuru sasa walikua na hofu na Uislam. Kama Uislamulitumika kuwaondoa wakoloni Uislam hautashindwa kuwatoa wao madarakani. Uislamikiwa itkadi ya kupinga ukoloni sasa ilikuwa ni tishio kwa Ukristo katikaTanzania huru."

Mohamed

MS,

Hebu niambie hawa elites 'waislamu' tunaowaona leo katika nchi yetu..wao walisoma wapi? wamejazana kwenye uwaziri, U-DC-U-RC, Ubalozi, jeshini, biashara na kwingine kwingi..hwa walipata wapi fursa kama Nyerere alikuwa na njama dhidi ya waislamu? Jibu lako tafadhali kaka.

Masanja,

Wamejazana!

Mgawano wa madaraka ni 83% kwa 17%.

Source: Waraka wa Waislamu kwa Viongozi na Wapenda Haki Tanzania

Mohamed
 
Bob,

Mimi sina cha kuongeza ubarikiwe sana kwa hoja zako makini zilizokwenda shule. Sema jamaa akina invisible walishaondoa kale kadude ka thanks..wanatumia fesibuku ambayo wengine hatumo huko!

I wish kaka MS angekusoma na kukuelewa. Kikubwa ni kwamba ukishajenga hoja sensitive kama hii kwa kofia ya imani zetu ni vigumu sana watu kuafiki hoja zako kwa sababu..rightly or wrongly...wengi tunapoteza objectivity kama MS alivyodhihirisha.

In all, I deeply salute your analysis!

Bravo mkuu!

Bado Mohammed ana hoja kubwa sana..

Kwanini nyie mnashindwa kujiuliza kulikoni nyerere awaadhibu wanaharakati wenzake baada ya uhuru na wengi wao wawe waislamu?

Ilikuwa coincidence au alikuwa ana chuki na uoga wa kidini?

Alikuwa akiwadhulumu waislamu apate dhawabu kutoka kwa mungu wake or what?

Haya hamataki kujiuuliza lakini mko tayari kurukia kwenye udini wa Mohammed..why not opposite way?
 
Masanja,

Wamejazana!

Mgawano wa madaraka ni 83% kwa 17%.

Source: Waraka wa Waislamu kwa Viongozi na Wapenda Haki Tanzania

Mohamed

Mkubwa una maana gani mbona sijakupata? I mean angalia cabinet ya Kikwete na hata waliomtangulia. Unataka kuniambia kwamba kuna serikali yoyote ambayo iliwa-marginalize waislamu katika utumishi wa umma? Mkuu hebu nifafanulie, maana ki ukweli sielewi pale watu wanapolaumu bila kuangalia who are the 'powers' and decision makers' katika jamhuri yetu especially katika kipindi hiki.
 
Watumishi wa umma mgawanyiko ukoje? na sytem iliyotengenezwa na st.nyerere 24yrs followed by bond followers of the church doctrine haiwezi kuondolewa kwa haraka ..
 
MS,

Hivi kweli unaamini na unataka tuamini kwamba uhuru wa Tanganyika yetu tukufu uliletwa na waislamu na wala si watanganyika wenyewe bila kujali itikadi zao na imani zao? Ni mtu PUNGUANI anaweza kukubaliana na wewe kwa hoja hii. MS wewe ni msomi, lakini nakushauri kwa dhati kabisa hii chuki unayoipandikiza kwa kutumia uwezo na karama uliyopewa na Muumba (sijui kama ulisoma kwa kodi za wananchi-ningekuita msaliti-sorry mate-no better word to describe it) itakuja kukutafuna na wale wote wanaoangalia wenzao kwa misingi ya imani zao. Perhaps hujui unachokifanya. Perhaps unaandika kwa sababu wewe ni 'intellectual'. Perhaps unataka ufaidike na mauzo ya vitabu. perhaps..perhaps..perhaps..ziko nyingi tuu...ila mwisho wa yote.. lengo walijua wewe..... Lakini hapa ulipofika kuwafanya wadogo zetu waamini kwamba Tanzania hii imeasisiwa na kujengwa kwa misingi ya imani za watu si njema kabisa. Tanzania imejengwa/itajengwa na watanzania. Period. Mimi na wewe tutakufa. TANZANIA itadumu. Hata kama ikiuzwa- hata kama climate change ikiitafuna..wapo watakao dai kipande cha bahari kama sehemu ilipokuwa Tanzania. Ikiuzwa kwa mkoloni mambo leo..wapo watakaoingia msituni kudai 'uhuru' wa nchi yao kama walivyofanya wazee waliotutangulia.

Kama kweli wewe ni mtanzania mzalendo (and I am not questioning your patriotism at all), kwa nini usifanye analysis objectively? Ok, unasema umeangalia 'historia ya wazee wako', yet mtu hahitaji masters ya Morogoro Muslim University kujua lengo lako. Kwa nini usingewauliza/kuwahoji wengine ambao si 'wazee wako' ukapata upande wa pili wa shilling? Maana hakika umewa-condemn bila kuwasikiliza.

Kama walivyosema wengine humu ningekushauri ujaribu kuwa objective. Tanzania ikiripuka watakaoumia ni wote haijalishi unakaa Masaki, Oysterbay au Kongowe au Manzese uswahilini. Tuna jukumu la kukilinda hiki kipande chetu kinachoitwa Tanzania.

Ushauri wangu kwa wasomi wa taifa letu, kama wewe na mimi tutumie elimu yetu kulikomboa taifa letu na umasikini wa kudumu kuliko kuzidi kupandikiza chuki kwa kutumia minajili ya imani zetu. We already have enough problems jamani. We dont need more!

Naamini kabisa, huu mwendelezo wa kuangalia watu kwa majina na imani zao hautaondoa hiyo 'dhulma' ndugu yetu MS anayolia nayo kwenye maandishi yake humu na kwingineko.
 
Mkandara,

Maneno mazuri.

Nami nakuwekea maneno yangu hapa chini:
Wazee wangu hawakujitoa TANU bali walitolewa kwa hila na fitna. Hawa wafuatao ni baadhi ya wazee wangu walowekwa kizuizini: Abdillah Schneider Plantan, SheikhAbdulkarim Abdulwahid, Maalim Popo Saleh, Suleiman Masudi Mnonji, Ali Migeyo,Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Shariff Hussein Badawiy, Shariff Mwinyibaba,Shariff Adnan, Bilali Rehani Waikela, Sheikh Jumanne Bias, Maalim Matar,Abdalah Mwamba, Sheikh Hashim Haji Abdallah, Sheikh Nurdin Hussein, SalumAbdallah Popo, Sheikh Mzee Ali Comoriam, Sheikh Al Amin Maftah, Rajab Kiguu chaMbuzi na wengine wengi. Lakini ukweli ulikuwa kwamba si wote katika walewaliokamatwa na kuwekwa kizuizini walijihusisha na siasa. Baadhi yao walikamatwakwa sababu tu walikuwa wakishirikiana na wale waliodhaniwa ni wapinzani waNyerere. Maalim Matar na Shariff Adnan walifungwa jela kwa sababu tu walihusikana msikiti wa Badawiy mjini Dar es Salaam ambako Sheikh Hassan bin Amir, wakatihuo akichukuliwa kuwa ndiyo roho ya waumini wa Tanganyika, alikuwa ikiendeshamadrasa yake kila magharibi pale msikitini. Shariff Hussein na nduguyeMwinyibaba walihamishiwa Kenya, walikotoka si kwa sababu walikuwawamejishughulisha katika harakati za kuipinga serikali, ila lakini kwa sababuwalikuwa waangalizi wa msikiti wa Badawiy. Sheikh Mzee Ali Comorian alitiwa kizuizini kwa sababu kila mara alikuwaakifuatana na Sheikh Hassan bin Amir kama vile alikuwa kivuli cha sheikh. Huendakile kilichomfanya Nyerere kuwatia kizuizini masheikh na wengine kuhamishwa nikufuata ule msemo wa Biblia usemao, "yule ambae hayuko nasi basi ni dhidiyetu."Jinsi siasa na za Tanzaniazilivyobadilika na jinsi Nyerere alivyoanza kuonyesha uadui dhidi ya Waislamkulimsikitisha sana Abdulwahid. Alishindwa kuelewa uhasama huu ulikuwa unatokawapi. Alihisi kuwa anahusika na yale yaliyokuwa yanawapata Waislam. Mawazo hayayalimzonga kama jinamizi. Kwa ufahamu wake alikuwa anadhani matatizo yote yaudini walikuwa wameyashinda toka miaka ya 1950. Mwaka 1953 Abdulwahid akiwaMuislam na akiungwa mkono na Al Jamiatul Islamiyya aligombea kiti cha urais waTAA na Nyerere, Mkatoliki. Abdulwahid alishindwa uchaguzi ule. Waislamhawakuuchukulia uchaguzi ule kama uchaguzi kati ya Muislam na Mkristo. Kilichotazamwani uwezo wa wagombea. Nyerere alikuwa amemzidi Abdulwahid na kwa ajili hiialichaguliwa kuiongza TAA. Abdulwahid alikumbuka ugomvi wa Sheikh SuleimanTakadir wakati ule Mwenyekiti wa Baraza La Wazee wa TANU. Sheikh Takadiraliwaonya Waislam wachukue tahadhari kwani Nyerere atakuja kuwapendeleaWakristo wenzake pale atakaposhika madaraka. Kama walivyofanya Waislam wengi,Abdulwahid alimuunga mkono Nyerere na kumpinga Sheikh Takadir. Wakati uleAbdulwahid aliamini kama Waislam wengi walivyoamini kuwa Sheikh Takadir alikuwaanataka kuleta siasa za kibaguzi ambazo alikuwa anaziegemeza katika dini.Abdulwahid aliona udini aliokuwa anataka kuuleta Sheikh Takadir lilikuwa jamboambalo litailetea hatari Tanganyika.Abdulwahid alikufa mwaka 1968 wakati nchiilikuwa imegubikwa na hasama za chinichini kati ya Waislam na Wakristo ambaosasa walikuwa wamehodhi madaraka yote katika serikali. Umoja wa kitaifa, mojaya maadili ambayo yeye aliyapigania katika maisha yake yote katika siasaulikuwa unahatarishwa. Halikadhalika umoja wa Waislam ulikuwa unaelekeakuvunjika. Kulikuwepo na kuwekwa kizuizini kwa masheikh chini ya PreventiveDentation Act of 1962. Baadhi ya masheikh waliotiwa gerezani walikuwa watu waliomuunga yeye mwenyewe mkono wakatianaunda TANU. Baadhi yao aliwashawishi kumuunga mkono Nyerere na TANU katikakile kipindi kigumu cha harakati za kudai uhuru. Mwanakamati wa Kamati Ndogo yaSiasa ya TAA, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, kiongozi wa ngazi ya juu kabisa kwaWaislam alikuwa amekamatwa na kuondolewa nchini na kurudishwa kwao Zanzibar kwaamri ya Nyerere.[1]Sababu iliyotolewa ya kukamatwa kwa Sheikh Hassan bin Amir ilikuwa alikuwaati "akipanga njama ya kupinduaserikali."Sheikh Hassan bin Amir alikuwa kati yaWaislam wachache ambao walithubutu kusimama kidete dhidi ya serikali na kutoamawazo yake kuhusu jinsi serikali ilivyokuwa ikiwakandamiza Waislam. Kablahajafa Abdulwahid alikuwa akifikiwa na habari kuwa kulikuwa na kampeniiliyokuwa ikiendeshwa kwa makini sana naWakristo ndani ya chama kuufuta Uislam ndani ya TANU. [1]Abdulwahid alikuwa anafahamu matokeo yakuvunjika kwa umoja wa Waislam. Yeye alikuwa anajua vyema nguvu ya umoja waWaislam wakati walipokuwa wanapigania uhuru wa Tanganyika. Abdulwahidhalikadhalika alikuwa anafahamu nguvu ya wale waliokuwa nyuma na njama zile zakuwagawa Waislam katika makundi hasimu. Vilevile alikuwa anatambua hofu na watuwote waliokuwa nyuma ya njama zile. Alifahamu kuwa wale aliowapokea na kuwatiakatika harakati za kudai uhuru sasa walikua na hofu na Uislam. Kama Uislamulitumika kuwaondoa wakoloni Uislam hautashindwa kuwatoa wao madarakani. Uislamikiwa itkadi ya kupinga ukoloni sasa ilikuwa ni tishio kwa Ukristo katikaTanzania huru."

Mohamed

Mkuu labda hujaelezwa vizuri habari hizi lakini labda nikuulize wewe wakati hawa wazee wako wanatiwa ndani ilikuwaje Tewa yeye akahamishwa na kuwa balozi nje asiwekwe ndani?.. Hivi kwa akili yako wewe unafikiri hawa wazee waliwekwa ndani kwa kuonewa tu?...siri ilitoka ndani na yaliyofuata yalikuwa utekelezaji wa information zilizokwisha kusanywa..Mambo yote haya yalitokea baada ya Abdilwahid kufariki!
 
MS,

Hivi kweli unaamini na unataka tuamini kwamba uhuru wa Tanganyika yetu tukufu uliletwa na waislamu na wala si watanganyika wenyewe bila kujali itikadi zao na imani zao? Ni mtu PUNGUANI anaweza kukubaliana na wewe kwa hoja hii. MS wewe ni msomi, lakini nakushauri kwa dhati kabisa hii chuki unayoipandikiza kwa kutumia uwezo na karama uliyopewa na Muumba (sijui kama ulisoma kwa kodi za wananchi-ningekuita msaliti-sorry mate-no better word to describe it) itakuja kukutafuna na wale wote wanaoangalia wenzao kwa misingi ya imani zao. Perhaps hujui unachokifanya. Perhaps unaandika kwa sababu wewe ni 'intellectual'. Perhaps unataka ufaidike na mauzo ya vitabu. perhaps..perhaps..perhaps..ziko nyingi tuu...ila mwisho wa yote.. lengo walijua wewe..... Lakini hapa ulipofika kuwafanya wadogo zetu waamini kwamba Tanzania hii imeasisiwa na kujengwa kwa misingi ya imani za watu si njema kabisa. Tanzania imejengwa/itajengwa na watanzania. Period. Mimi na wewe tutakufa. TANZANIA itadumu. Hata kama ikiuzwa- hata kama climate change ikiitafuna..wapo watakao dai kipande cha bahari kama sehemu ilipokuwa Tanzania. Ikiuzwa kwa mkoloni mambo leo..wapo watakaoingia msituni kudai 'uhuru' wa nchi yao kama walivyofanya wazee waliotutangulia.

Kama kweli wewe ni mtanzania mzalendo (and I am not questioning your patriotism at all), kwa nini usifanye analysis objectively? Ok, unasema umeangalia 'historia ya wazee wako', yet mtu hahitaji masters ya Morogoro Muslim University kujua lengo lako. Kwa nini usingewauliza/kuwahoji wengine ambao si 'wazee wako' ukapata upande wa pili wa shilling? Maana hakika umewa-condemn bila kuwasikiliza.

Kama walivyosema wengine humu ningekushauri ujaribu kuwa objective. Tanzania ikiripuka watakaoumia ni wote haijalishi unakaa Masaki, Oysterbay au Kongowe au Manzese uswahilini. Tuna jukumu la kukilinda hiki kipande chetu kinachoitwa Tanzania.

Ushauri wangu kwa wasomi wa taifa letu, kama wewe na mimi tutumie elimu yetu kulikomboa taifa letu na umasikini wa kudumu kuliko kuzidi kupandikiza chuki kwa kutumia minajili ya imani zetu. We already have enough problems jamani. We dont need more!

Naamini kabisa, huu mwendelezo wa kuangalia watu kwa majina na imani zao hautaondoa hiyo 'dhulma' ndugu yetu MS anayolia nayo kwenye maandishi yake humu na kwingineko.

Kwanini unamshambulia Mohammed kuwa ni mdini???

Kwanini usimshambulie Nyerere kuwa ni mdini?? kwa kuwadhulumu wazee wake na wengine wengi wao wakiwa waislam??

Kwanini unaogopa nyerere kufanya udini ilikuwa hatari kwa taifa na Mohammed kuuelezea makosa hayo iwe hatari??

Mkuu acheni double standards nchi itajengwa na wanaosema ukweli na haki..
 
Topical, nakupa dokezo kidogo tu, ungekuwa makini kidogo tu ungetambua kuwa toka hii thread ianze hakuna anayepoteza muda wake kukujibu, jaribu kujiuliza ni kwa nini ?
 
Mkuu labda hujaelezwa vizuri habari hizi lakini labda nikuulize wewe wakati hawa wazee wako wanatiwa ndani ilikuwaje Tewa yeye akahamishwa na kuwa balozi nje asiwekwe ndani?.. Hivi kwa akili yako wewe unafikiri hawa wazee waliwekwa ndani kwa kuonewa tu?...siri ilitoka ndani na yaliyofuata yalikuwa utekelezaji wa information zilizokwisha kusanywa..Mambo yote haya yalitokea baada ya Abdilwahid kufariki!

Mkandara,

Unazungumzia jambo usilokuwa na ujuzi nalo.

Babu yangu ni mmoja kati ya wazalendo waliwekwa kizuizini kwa "kuchanganya dini na siasa na kwa kutaka kupindua serikali. Rashid Kheri Bagdelleh ndiye alikuwa Mkuu wa Mkoa Tabora na yeye na baba yangu walikuwa marafiki toka utoto wao. Tuna mengi tuliyafahamu kuhusu fitna ile ndiyo maana nakuambia unazungumza jambo usolijua.

Tewa alipelekwa China kama njia ya kuvunja nguvu EAMWS na kuhujumu mradi wa kujenga Chuo Kikuu cha Waislam. Soma hapa chini yalomkuta Tewa:
"Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka wa 1965,muasisi wa TANU Tewa Said Tewa alishindwa uchaguzi katika jimbo lake lauchaguzi Kisarawe. Aliyemshinda alikuwa mwanasiasa asiyefahamika, H.A.Ramadhani Dollah. Bibi Titi Mohamed vilevile alipoteza kiti chake cha Rufijikwa mtu ambae vilevile afahamiki, A.M. Mtanga. Kulikuwa na uvumi wakati ulekuwa ulikuwepo na udanganyifu katika kuhesabu kura. Tewa na Titi walikuwa kwawakati ule viongozi wa EAMWS.Tewa anasema hakushindwa uchaguzi, matokeo yakeyalicheleweshwa kwa siku mbili. Inasemekana fitna dhidi ya Tewa na Titi ilikuwaikiongozwa na Julius Nyerere pamoja na baadhi ya viongozi wa juu wa TANU. Baadaya ukimya wa karibu miaka thelathini Bibi Titi anasema kuwa sababu yakuangushwa kwa kwake katika siasa ni kuwa alimpinga Nyerere katika HalmashauriKuu ya TANU wakati Nyerere alipokuwa anatafuta kuungwa mkono na Waislam ndaniya chama aivunje EAMWS. (Angalia Rai 29 Desemba, 1994)."

Mohamed

Mkubwa una maana gani mbona sijakupata? I mean angalia cabinet ya Kikwete na hata waliomtangulia. Unataka kuniambia kwamba kuna serikali yoyote ambayo iliwa-marginalize waislamu katika utumishi wa umma? Mkuu hebu nifafanulie, maana ki ukweli sielewi pale watu wanapolaumu bila kuangalia who are the 'powers' and decision makers' katika jamhuri yetu especially katika kipindi hiki.

Masanja,

Waislam sasa tunazungumza na serikali tunasubiri jibu kutoka kwao.

Mohamed
 
Nyerere alipokuwa anazungumzia Ubepari alikuwa anazungumzia Wazungu. Alipewa misaada ya chakula na Wazungu kwa ajili ya WTZ alikataa, lakini anashindwa kusema kwa nini yeye alipochukuliwa kama ELITE wa TZ kwenda kusoma kwa nini alikubali?

Nyerere ni MYTH kubwa ya Historia ya TZ.

Sasa hivi kinachotakiwa kufanyika ni kutoa misaada ya mikubwa ili kuwezesha mpango maalum wa TEXT book ambazo zitafundishwa ktk shule nyingi za TZ, tukianzia na shule za Kiislamu kuelezea historia ambayo inafichwa na serikali ya TZ.

Nyinyi mnaondelea kumshabikia Nyerere endeleeni, na sisi tunaendelea na mpango wetu wa kuandika historia ya kweli, inshaAllah.

nafikiri wewe ni miongoni mwa watu walio kosa hoja kabisa katika hii mada......beter keep quite na ujifunze katika hoja zinazotolewa!
 
Mkandara,

Unazungumzia jambo usilokuwa na ujuzi nalo.

Babu yangu ni mmoja kati ya wazalendo waliwekwa kizuizini kwa "kuchanganya dini na siasa na kwa kutaka kupindua serikali. Rashid Kheri Bagdelleh ndiye alikuwa Mkuu wa Mkoa Tabora na yeye na baba yangu walikuwa marafiki toka utoto wao. Tuna mengi tuliyafahamu kuhusu fitna ile ndiyo maana nakuambia unazungumza jambo usolijua.

Tewa alipelekwa China kama njia ya kuvunja nguvu EAMWS na kuhujumu mradi wa kujenga Chuo Kikuu cha Waislam. Soma hapa chini yalomkuta Tewa:
"Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka wa 1965,muasisi wa TANU Tewa Said Tewa alishindwa uchaguzi katika jimbo lake lauchaguzi Kisarawe. Aliyemshinda alikuwa mwanasiasa asiyefahamika, H.A.Ramadhani Dollah. Bibi Titi Mohamed vilevile alipoteza kiti chake cha Rufijikwa mtu ambae vilevile afahamiki, A.M. Mtanga. Kulikuwa na uvumi wakati ulekuwa ulikuwepo na udanganyifu katika kuhesabu kura. Tewa na Titi walikuwa kwawakati ule viongozi wa EAMWS.Tewa anasema hakushindwa uchaguzi, matokeo yakeyalicheleweshwa kwa siku mbili. Inasemekana fitna dhidi ya Tewa na Titi ilikuwaikiongozwa na Julius Nyerere pamoja na baadhi ya viongozi wa juu wa TANU. Baadaya ukimya wa karibu miaka thelathini Bibi Titi anasema kuwa sababu yakuangushwa kwa kwake katika siasa ni kuwa alimpinga Nyerere katika HalmashauriKuu ya TANU wakati Nyerere alipokuwa anatafuta kuungwa mkono na Waislam ndaniya chama aivunje EAMWS. (Angalia Rai 29 Desemba, 1994)."

Mohamed

Na ndio nakwambia ya kwamba hii ni historia ulosimuliwa wewe na watu waliotaka wewe ufahamu hivyo. Labda nikuulize una umri gani? maanake nijuavyo mimi sisi wote tumesimuliwa, hivyo kama alivyosema JK ukiambiwa kitu Usifuate ya Gong'ota, kuwa kama Mbayuwayu changanya za za kwako!.. tatizo wewe Gong'ota hutaweza kufikiri kaa Mbayuwayu!..

Tewa Said Tewa hakuwa kikwazo cha EAMS isipokuwa alikuwa pandikizi la TANU ndani ya EAMWS ktk maswala yanayohusu jumuiya hiyo na kati ya wazee wote ulowataja hakuna ambaye hakuwa mwanachama wa AMNUT, sasa unapoleta ya Biti Titi unakwenda wakati mwingine kabisa na yeye pia alikuwa na matatizo yake ya kisiasa acha hayo ya kushiindwa uchaguzi..
 
Na ndio nakwambia ya kwamba hii ni historia ulosimuliwa wewe na watu waliotaka wewe ufahamu hivyo. Labda nikuulize una umri gani? maanake nijuavyo mimi sisi wote tumesimuliwa, hivyo kama alivyosema JK ukiambiwa kitu Usifuate ya Gong'ota, kuwa kama Mbayuwayu changanya za za kwako!.. tatizo wewe Gong'ota hutaweza kufikiri kaa Mbayuwayu!..

Tewa Said Tewa hakuwa kikwazo cha EAMS isipokuwa alikuwa pandikizi la TANU ndani ya EAMWS ktk maswala yanayohusu jumuiya hiyo na kati ya wazee wote ulowataja hakuna ambaye hakuwa mwanachama wa AMNUT, sasa unapoleta ya Biti Titi unakwenda wakati mwingine kabisa na yeye pia alikuwa na matatizo yake ya kisiasa acha hayo ya kunsindwa uchaguzi..

Bwana Mkandara,

Tubishane kwa mengine si haya ya TANU.

Mimi nina asili na chama hiki na nadhani ushaona kuwa najua.
Lakini sikuzuii kuamini upendavyo.

Ndiyo maana nimeikataa historia rasmi na nimekuja na ya wazee wangu hadi leo hakijaandikwa kitabu kupinga kitabu changu.
Zungumzeni mengine lakini si hii TANU na siasa za Dar es Salaam na yalokuja baada ya uhuru.

Mohamed

Mohammed Said, huwezi kuibadilisha historia kwa jinsi utakavyo hata sisi tunajua vile vile. Bibi Titi hahusiki kabisa na maswala nayozungumzia yeye scandal yake iko na kina Michael Kamaliza waliotaka kupindua serikali mwaka 1969, hatuzungumzii haya kwa sababu pamoja na kushindwa uchaguzi mwkaa 1965 she remained party official na muhimu ktk chama hadi tuhuma za mwaka 1969.

Hao wazee wako walitaka kuipindua seriikali na Nyerere alitonywa na Sheikh Kassim bin Jumaa na kuthibitishwa na Tewa Said Tewa hizi ni habari zilizotoka ndani ya EAMWS. Kwa hiyo kama hutaki historia inajionyesha walikamatwa kwa kosa ya kutaka kuipindua serikali. Wewe kama una ushahidi kuonyesha haikuwa kweli utoe hapa kwa sababu mimi najua watu wote ulokamatwa walihusika na walikuwa wanachama wa AMNUT, wengine wamejitoa TANU. Ni sawa na aloyafanya Ghadaffi unaweza yachukua kwa mtazamo wowote ule upendao.

Kulikuwepo na walokamatwa bila hatia? hilo sijui wewe mwenye taarifa hizi twambie watu hao nahawakuhusika kwa vipi?.. maana kutokuwa kiongozi haina maana huungi mkono mapinduzi. Mimi leo hii naunga mkono kabisa kuondolewa kwa CCM na serikali inaweza kuniweka ktk kitabu cheusi kama mpinzani hatari nayetakiwa kushughulikiwa. Being right or wrong itakuwa ktk macho ya mhadithiwa!
 
Topical, nakupa dokezo kidogo tu, ungekuwa makini kidogo tu ungetambua kuwa toka hii thread ianze hakuna anayepoteza muda wake kukujibu, jaribu kujiuliza ni kwa nini ?

Nijiulize nini?

Ni kwasababu hawana majibu..besides kumbe wewe uko hapa unafanya kazi ya kuhesabu nani anamjibu nani?
 
Bwana Mkandara,

Tubishane kwa mengine si haya ya TANU.

Mimi nina asili na chama hiki na nadhani ushaona kuwa najua.
Lakini sikuzuii kuamini upendavyo.

Ndiyo maana nimeikataa historia rasmi na nimekuja na ya wazee wangu hadi leo hakijaandikwa kitabu kupinga kitabu changu.
Zungumzeni mengine lakini si hii TANU na siasa za Dar es Salaam na yalokuja baada ya uhuru.

Mohamed

Mohamed Said hawezi kubishana na mtu kuhusu TANU kwani Mohamed Said ndiye pekee mwenye asili ya TANU ? Mohamed Said ana jeuri ya kuikataa historia ya wengine kwani hakuna kitabu kimeandikwa kupinga kitabu chake chenye hadithi alizosimuliwa utotoni na wazee wake, lakini hapo hapo kitabu chake anadai kukiandika kupinga historia rasmi kama anavyoiita. Na sasa anatupiga marufuku kuzungumzia historia ya TANU na siasa za Dar es Salaam na yalokuja baada ya uhuru ? Talk of the absurd, kuna ufedhuli kuliko huu wa Mohamed Said - halafu akiitwa mpuuzi anadai katukanwa ! Eti anatoa darsa, darsa my foot ! Mods nawaombeni samahani but JF is where we call a spade a spade and Mohamed Said is a fake anayejaribu kutumia Udini kupandikiza mbegu ya chuki miongoni mwa Watanzania, period.
 
Kwanini unamshambulia Mohammed kuwa ni mdini???

Kwanini usimshambulie Nyerere kuwa ni mdini?? kwa kuwadhulumu wazee wake na wengine wengi wao wakiwa waislam??

Kwanini unaogopa nyerere kufanya udini ilikuwa hatari kwa taifa na Mohammed kuuelezea makosa hayo iwe hatari??

Mkuu acheni double standards nchi itajengwa na wanaosema ukweli na haki..

1. Namshambulia Mohammed kwa Udini kwa sababu niyasoma maandishi yake..Kama wewe huoni Udini kwa nini unazungumzia Waislaam safi hivi na wakristu sio safi kwa makosa ya Nyerere..au Udini una maana tofauti!

2. Siwezi kumshambilia Nyerer kwa sababu sijaona usemi wake, maandishi yake na wala tabia yake ilonifanya nikaamini ana Udini isipokuwa kafanya mengi ya kunifanya nishangae kama kweli mkristu na mdini, moja wapo ni kuwanyang'anya shule zao, kuvunja uhusiano na Israel, na mengine mengi tu ambayo mtu mwenye udini asingeweza kuyafanya.

3. Double standard zipi?... mimi nachoweza kuwalaumu ni WATU hapa JF ambao mnaweza tu kumlaumu Nyerere lakini sio Sheikh Hassan bin Amir, kina Adam Nassib, kina Amri Abeid Kaluta, kina Kawawa, Mwapachu, Mwinyi, JK na wengine kibao ambao wamebakia ndani ya chama ambacho walikiona toka mwanzo kinaongozwa na kanisa, tena wao wakifanya mengi ya ajabu zaidi.. Mimi nachofanya mkuu wangu ni explore reality kama kuna swala ama jambo nimeliandika isivyo naomba unisahihishe kwa maana hakuna nalotoa kichwani mwangu bali limetokea au lipo na sote tunalijua.
 
Mohamed Said hawezi kubishana na mtu kuhusu TANU kwani Mohamed Said ndiye pekee mwenye asili ya TANU ? Mohamed Said ana jeuri ya kuikataa historia ya wengine kwani hakuna kitabu kimeandikwa kupinga kitabu chake chenye hadithi alizosimuliwa utotoni na wazee wake, lakini hapo hapo kitabu chake anadai kukiandika kupinga historia rasmi kama anavyoiita. Na sasa anatupiga marufuku kuzungumzia historia ya TANU na siasa za Dar es Salaam na yalokuja baada ya uhuru ? Talk of the absurd, kuna ufedhuli kuliko huu wa Mohamed Said - halafu akiitwa mpuuzi anadai katukanwa ! Eti anatoa darsa, darsa my foot ! Mods nawaombeni samahani but JF is where we call a spade a spade and Mohamed Said is a fake anayejaribu kutumia Udini kupandikiza mbegu ya chuki miongoni mwa Watanzania, period.

Hamaki matusi.

Lakini nisemacho ni kuwa kuhusu TANU mimi historia naijua na ushahidi ni kuwa nimeandika kitabu na nina "papers" hesabu yake sizijui katika somo hili.

Kama mtu ataona kwa mie kusema haya ni jeuri hiyo ni bahati mbaya.

Kuhusu darsa naam ninatoa humu JF na nimetoa kwingi duniani Alhamdulilah achilia za majlis na Vyuo Vikuu.
Maalim wangu Sheikh Haruna (Mungu amrehemu) akisema: "Basi ukisikia tusi limetoka jua ushamshinda."

Mohamed
 
Back
Top Bottom