Bismillah,
wanajanvi naona mnazunguka saana pasipo kutuliza vichwa vyenu mkamsoma Mohammed Said vizuri anakotokea na kwa nini amekatalia kipande cha ardhi yake kuwa historia..Na muda mrefu nimekuwa najiuliza kama kuna haja ya kupasua jipu hili lakini nadhani umefika muda muafaka nizungumzie kulikoni...Itakuwa hadithi ndefu kidogo naomba uvumilivu wenu..
Nimemsoma sana Mohammed Said na nadhani lengo lake la awali ni historia ya Wazee wake ktk mchango wa Uhuru wa Tanganyika, wazee ambao baada ya Uhuru leo hii wamesahaulika - FORGOTTEN HEROES - ktk historia ya nchi yetu lakini hakutafuta sababu zaidi ya maelezo alosimuliwa na jamaa zao wenyewe, ama misukosuko ilotokea kuwa sababu ya maswali mengi anayojiuliza lakini hukwepa kipande cha matukio kati ya mwaka 1963 hadi kufikia 1967, matukio ambayo yalisababisha na upande huo huo anaoutetea na muhimu sana kuyaelewa toka upande wa pili ili kuhitimisha.
Mohammed Said anazungumzia wazee wake kina Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Yusuf Badi, Dossa Aziz, Sheikh Mohamed Ramia, Bi Tatu biti Mzee, Dharura biti Abdulrahman, na Sheikh Hassan bin Amir ambao kweli wamesahaulika ktk historia ya nchi yetu na wala hakuna kumbukumbu zao ama baadhi yao Kitaifa..Madai haya ni regit na naweza kuelewa wapi Mohammed Said kasimama dhidi ya historia ya Tanganyika iliyopo ana inayonadiwa sana na waandishi wa vitabu na habari..
Nafikiri hadi hapa wengi tunaweza kukubaliana naye na haswa mtu kama Abdulwahid Sykes, Dosa Aziz wakati watu kama Julius Nyerere, John Rupia, Oscar Kambona, Paul Bomani na wengine kibao ni maarufu hata kwa kizazi hiki kipya wanajua mchango wa watu hawa katika Uhuru wa Tanganyika kupitia historia yetu..Katika hili bila kutaja dini zao nakubaliana sana na Mohammed na ndio maana nikauliuza historia ya Cecil Matola na mbona kiongozi huyu kasaulika?..
Kikubwa anachokosolewa Mohammed Said ni pale alipotengua lengo la awali na kulifanya swala hili kuwa la imani ya dini (conclusion yake) na kwamba hawa viongozi wamesahaulika kwa sababu ni Waislaam ama serikali imepotosha mchango wa Waislaam ktk harakati za Uhuru wa Tanganyika hivyo kuifanya hoja nzima ya TAA na TANU kuwa ya kidini zaidi ya chama cha siasa...
Nachomuomba Mohammed Said ni kimoja tu ya kwamba, hata historia ya Zanzibar haiwezi kuwa historia sahihi kama hutazungumzia viongozi waarabu wa Hizbu party. Na mtu yeyote kipenzi wa Hizbu anaweza kuja hapa na kudai haoni sababu kwa nini Karume maarufu kuliko Shamte, akatumia hata race card ya kama tunavyowasoma Wazanzibar wengi wakizungumzia Mapinduzi kama ilikuwa njama ya watu weusi dhidi ya Wazanzibar wenye asili ya Kiarabu na kadhalika..Yote haya yanaweza kuwa na ukweli lakini lengo la mwandishi linapokuwa linalenga kuonyesha dhulma fulani ni muhimu sana kwetu kupima hiyo dhulma inayodaiwa kisha tujenge hoja zinazopinga ama kuhalalisha dhulma hiyo..
Mimi nachoweza kumwambia Mohammed Said, historia ulopewa ya wazee wako kuna mengi umefichwa ama wewe mwenyewe umeamua kuiacha pembeni lakini kati ya kundi kubwa la wazee wako toka mwaka 1964 kufikia mwaka 1967 walikuwa tayari wamejitenga na chama TANU, walikuwa tayari wakitaka kufanya Mapinduzi dhidi ya chama TANU ambacho kiliongozwa na Nyerere walikuwemo waislaam wengi sana viongozi vile ivle, na Waislaam karibu mikoa yote walipingana na dhana ama lengo la hawa wazee wako waliojitenga...Hivyo, unapojitoa ktk chama kumbuka pia unapoteza haki zote ulostahili kupewa na historia yako inakuwa na picha tofauti kama ilivyokuwa kwa kina Mtenvu na Kambona.
Hatuwezi kuwa na historia njema ya Kambona zaidi ya kwamba alitaka kuipindua nchi. Na vile vile hatuwezi kuwa na historia nzuri ya kundi la watu walitaka kuanziusha vurugu nchini kwa kutumia sanduku la Udini ila naweza sana kukubaliana na wewe kwamba kuna viongozi wetu waliokuwa na mchango mkubwa sana ktk harakati za Uhuru wetu wamesahauliwa. Hawa ndio wanatakiwa kuitwa mashujaa na hawa ndio wanatakiwa kuenziwa kwa kila sifa ya Uzalendo na hata kusherehekewa ktk Memorial day!.
Nilichoweza kujifunza mimi kutoka vitabu vya Mohammed Said ni kwamba - Historia ya Tanganyika inapotea na ipo haja na sababu kubwa ya vitabu kama cha John Lliffe - A Modern History of Tanganyika kiwe ktk vitabu vinavyotakiwa kufundishwa mashuleni iwe Primary school au Secondary. Lakini haya maswala ya Udini au kutumia Uarabu kudai haki ya Uzanzibar haiwezi kujenga umoja wa kitaifa bali unabomoa hata imani ndogo ya uzalendo iliyokuwepo..Leo hii ukimwambia Mgazija kwamba Waarabu ndio waasisi wa Uhuru wa Zanzibar na Shamte alikaribishwa tu, sijui kama kutakalika.
Maasalaam!