Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Hamaki matusi.

Lakini nisemacho ni kuwa kuhusu TANU mimi historia naijua na ushahidi ni kuwa nimeandika kitabu na nina "papers" hesabu yake sizijui katika somo hili.

Kama mtu ataona kwa mie kusema haya ni jeuri hiyo ni bahati mbaya.

Kuhusu darsa naam ninatoa humu JF na nimetoa kwingi duniani Alhamdulilah achilia za majlis na Vyuo Vikuu.
Maalim wangu Sheikh Haruna (Mungu amrehemu) akisema: "Basi ukisikia tusi limetoka jua ushamshinda."

Mohamed
Mohammed said,
Tumekusoma sana na tunashukuru kwa darsa lakini mbona hutaki nawe kusoma yetu ili hali wewe mwenyewe umetaka nasi tuzungumze historia tunayoijua sisi? Sii ndivyo Mdondoaji alivyo suggest nasi tuje na historia yetu au unataka nasi tuandike kitabu fani isokuwa yetu. Mimi nadhani tukubali kutokubaliana itasaidia zaidi maana uloandika tumeyasoma na hakika binafsi naunga mkono sana watu kama Abdulwahid Sykes na Cecil Matola kusahaulika ktk historia ni makosa makubwa sana.

Hawa watu walitakiwa kupewa heshima zote za kitaifa na hasa sikukuu ya Mashujaa wetu iwahusu zaidi wao pamoja na Nyerere kwani hatuwezi kupindisha ukweli wa mchango wa Nyerere hata kama.. Na nitasema tena na tena Walibya pamoja na makosa yote ya Ghaddaff hawataweza kuiondoa historia ya mazuri aloyafanya kwa sababu tu alimwondoa Mfalme ambaye leo wanataka sana kumrudisha..

Jana nikitazama taarifa ya habari za Libya, nimeona wakionyesha bendera za Al qaeda zikipepea miji ya Libya na wazungu sasa wanaanza kujiuliza kama ndio ujio wa Sheria law na makazi mapya ya Al qaeda..Alaaa! sasa mlokuwa mkiyapigia makofi ni yapi?
 
1. Namshambulia Mohammed kwa Udini kwa sababu niyasoma maandishi yake..Kama wewe huoni Udini kwa nini unazungumzia Waislaam safi hivi na wakristu sio safi kwa makosa ya Nyerere..au Udini una maana tofauti!

2. Siwezi kumshambilia Nyerer kwa sababu sijaona usemi wake, maandishi yake na wala tabia yake ilonifanya nikaamini ana Udini isipokuwa kafanya mengi ya kunifanya nishangae kama kweli mkristu na mdini, moja wapo ni kuwanyang'anya shule zao, kuvunja uhusiano na Israel, na mengine mengi tu ambayo mtu mwenye udini asingeweza kuyafanya.

3. Double standard zipi?... mimi nachoweza kuwalaumu ni WATU hapa JF ambao mnaweza tu kumlaumu Nyerere lakini sio Sheikh Hassan bin Amir, kina Adam Nassib, kina Amri Abeid Kaluta, kina Kawawa, Mwapachu, Mwinyi, JK na wengine kibao ambao wamebakia ndani ya chama ambacho walikiona toka mwanzo kinaongozwa na kanisa, tena wao wakifanya mengi ya ajabu zaidi.. Mimi nachofanya mkuu wangu ni explore reality kama kuna swala ama jambo nimeliandika isivyo naomba unisahihishe kwa maana hakuna nalotoa kichwani mwangu bali limetokea au lipo na sote tunalijua.

1. Maandishi na ushahidi wa vitabu mbalimbali unaotolewa either kwa mazungumzo yake nyerere na matokeo ya siasa zake yanaonyeshwa si na Mohammed tu pia waandishi wengine kuwa alikuwa mdini sana..sijaona kwenye maandishi ya Mohammed akisema wakristo wote ni wabaya na waislamu wote ni malaika atakuwa amekosea ..udini wake nini kuulezea historia ya wazee wake ambao walitokea kuwa waislamu? kuna shida kueleza mchango wa uislamu kwa uhuru wa nchi yetu?? huo ndio udini wenyewe kuchukia ukweli kwakuwa unaonekana kuukuza uislam?? what worries you and others? if I may ask?

2. Kunyang'anya shule inaweza ikawa kitu kizuri lakini haina maana kama unatengeneza utaratibu katika serikali ili kuwabagua wananchi kuwajaza wakristo serikalini kwa hila huku ukiwabagua wakristo ..ni sawa na kuruka moshi na kukanya'anga moto..kunyang'anya shule hakuna maana kama unakubali wakristo wandeshe seminary zao wakati huo huo unavunja jumuiya ya kiislamu yenye maendeleo makubwa na kuweka mamluki wachumia tumbo kwa faida ya kanisa kama anavyoeleza Mohammed kwenye vitabu vyake..

3. Hao JF watalaumu mtu bila wewe kuleta evidence (researched) kwamba hao watu walihusika katika kuhujumu watu fulani au Taifa?? kama alivyofanya Mohammed kwa nyerere au unataka tusikilize ngojera za mtaani na kukuamini???

Acheni kumshambulia Mohammed kwa Udini wakati huo huo mnashindwa kumshambulia Nyerere kwa udini wapi na wapi?? mnabaki na double standards???
 
Mohamed Said hawezi kubishana na mtu kuhusu TANU kwani Mohamed Said ndiye pekee mwenye asili ya TANU ? Mohamed Said ana jeuri ya kuikataa historia ya wengine kwani hakuna kitabu kimeandikwa kupinga kitabu chake chenye hadithi alizosimuliwa utotoni na wazee wake, lakini hapo hapo kitabu chake anadai kukiandika kupinga historia rasmi kama anavyoiita. Na sasa anatupiga marufuku kuzungumzia historia ya TANU na siasa za Dar es Salaam na yalokuja baada ya uhuru ? Talk of the absurd, kuna ufedhuli kuliko huu wa Mohamed Said - halafu akiitwa mpuuzi anadai katukanwa ! Eti anatoa darsa, darsa my foot ! Mods nawaombeni samahani but JF is where we call a spade a spade and Mohamed Said is a fake anayejaribu kutumia Udini kupandikiza mbegu ya chuki miongoni mwa Watanzania, period.

Conclusion kama hizi ni za watu ambao ni "incompetent" unakimbilia hoja dhaifu ya udini ...

Hizo ngojera za kutishia watu kuwa ni wadini kwa kusema ukweli zimeshapitwa na wakati..as you said call as spade a spade

Wewe ndio mdini mkubwa unatetea udini simply because nyerere aliyefanya udini ni mkristo..

Unaanza kujificha kwenye zana ya uzalendo (my foot) huna uzalendo wowote zaidi ya udini ukrito period!
 
Bob,

Mimi sina cha kuongeza ubarikiwe sana kwa hoja zako makini zilizokwenda shule. Sema jamaa akina invisible walishaondoa kale kadude ka thanks..wanatumia fesibuku ambayo wengine hatumo huko!

I wish kaka MS angekusoma na kukuelewa. Kikubwa ni kwamba ukishajenga hoja sensitive kama hii kwa kofia ya imani zetu ni vigumu sana watu kuafiki hoja zako kwa sababu..rightly or wrongly...wengi tunapoteza objectivity kama MS alivyodhihirisha.

In all, I deeply salute your analysis!

Bravo mkuu!
Huyo ndiyo Mkandara .'ashomile'..! Inasikitisha sana kuona jinsi taasisi nyingi za waislam zilivyokosa watu wa calibre ya Mkandara...!
 
Huyo ndiyo Mkandara .'ashomile'..! Inasikitisha sana kuona jinsi taasisi nyingi za waislam zilivyokosa watu wa calibre ya Mkandara...!

Si aanzishe taasisi yake ya kiislam aendeshe...

Kama ana calibre hajatumia vizuri ataulizwa siku ya mwisho..

Besides sidhani kama wewe ndio utoe sifa na siyo waislamu????
 
Huu mjadala kwangu mzito ila nnajambo ntasema na natoka nje ya mnakasha,Waislam kweli mliumbwa kulalama,matatizo yenu yameletwa na wakristo,basi muwanyonge sana kwani wakristo huyo mungu wao yukoje mbona anawapigania na wanashinda,nanyi muulizeni Allah kulikoni mbona siye wamwisho tu kila mahali,na kama mtaendelea kusema matatizo yenu yameletwa na wakristo sahauni neno maendeleo,wenzenu wanahamia vijijini wakijenga huduma kubwa kubwa za kijamii.
 
Hujaelewa mjadala anza upya kuusoma..

Halafu tofautisha kulalama na kusema ukweli na haki...
 
Huyo ndiyo Mkandara .'ashomile'..! Inasikitisha sana kuona jinsi taasisi nyingi za waislam zilivyokosa watu wa calibre ya Mkandara...!
Hata sasa Mohamed saidi anatumia jina tu la uislam lakini sidhani mtu kama Mohamed said anaweza kukubali au Kuamini kuwa sheikh mkuu wa waislam wa kweli Tanzania anaweza kutoka kwa kina Mkandara au au Kigoma.

........Besides sidhani kama wewe ndio utoe sifa na siyo waislamu????
khe khe khe khe Kumbe kuna sheria kuwa waislam wanatkiwa kutolewa sifa nzuri na waislam tu ?. Na nyie waislam je mnaruhusiwa kuwatolea sifa wasio waislam?
 
Mohamed Said hawezi kubishana na mtu kuhusu TANU kwani Mohamed Said ndiye pekee mwenye asili ya TANU ? Mohamed Said ana jeuri ya kuikataa historia ya wengine kwani hakuna kitabu kimeandikwa kupinga kitabu chake chenye hadithi alizosimuliwa utotoni na wazee wake, lakini hapo hapo kitabu chake anadai kukiandika kupinga historia rasmi kama anavyoiita. Na sasa anatupiga marufuku kuzungumzia historia ya TANU na siasa za Dar es Salaam na yalokuja baada ya uhuru ? Talk of the absurd, kuna ufedhuli kuliko huu wa Mohamed Said - halafu akiitwa mpuuzi anadai katukanwa ! Eti anatoa darsa, darsa my foot ! Mods nawaombeni samahani but JF is where we call a spade a spade and Mohamed Said is a fake anayejaribu kutumia Udini kupandikiza mbegu ya chuki miongoni mwa Watanzania, period.
Siyo hilo tu, Mohamed Said kama historian aliombwa aandike historia ya Watanzania wengine ambao happened to be Christians. Mohamed akakataa akasema hiyo kazi ifanywe na wengine. Lakini wangekuwa ni Waislamu wa Kigoma, Tabora, au Arusha, Mohamed angekubali mara moja
kuifanya kazi hiyo. Mwanahistoria habagui. Lakini mwanahistoria wa kidini hujikita zaidi katika matukio yanayohusu dini yake. Wanaomchukulia Mohamed kama mwanahistoria wanahitaji kujiuliza.
 
Bismillah,

wanajanvi naona mnazunguka saana pasipo kutuliza vichwa vyenu mkamsoma Mohammed Said vizuri anakotokea na kwa nini amekatalia kipande cha ardhi yake kuwa historia..Na muda mrefu nimekuwa najiuliza kama kuna haja ya kupasua jipu hili lakini nadhani umefika muda muafaka nizungumzie kulikoni...Itakuwa hadithi ndefu kidogo naomba uvumilivu wenu..

Nimemsoma sana Mohammed Said na nadhani lengo lake la awali ni historia ya Wazee wake ktk mchango wa Uhuru wa Tanganyika, wazee ambao baada ya Uhuru leo hii wamesahaulika - FORGOTTEN HEROES - ktk historia ya nchi yetu lakini hakutafuta sababu zaidi ya maelezo alosimuliwa na jamaa zao wenyewe, ama misukosuko ilotokea kuwa sababu ya maswali mengi anayojiuliza lakini hukwepa kipande cha matukio kati ya mwaka 1963 hadi kufikia 1967, matukio ambayo yalisababisha na upande huo huo anaoutetea na muhimu sana kuyaelewa toka upande wa pili ili kuhitimisha.

Mohammed Said anazungumzia wazee wake kina Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Yusuf Badi, Dossa Aziz, Sheikh Mohamed Ramia, Bi Tatu biti Mzee, Dharura biti Abdulrahman, na Sheikh Hassan bin Amir ambao kweli wamesahaulika ktk historia ya nchi yetu na wala hakuna kumbukumbu zao ama baadhi yao Kitaifa..Madai haya ni regit na naweza kuelewa wapi Mohammed Said kasimama dhidi ya historia ya Tanganyika iliyopo ana inayonadiwa sana na waandishi wa vitabu na habari..

Nafikiri hadi hapa wengi tunaweza kukubaliana naye na haswa mtu kama Abdulwahid Sykes, Dosa Aziz wakati watu kama Julius Nyerere, John Rupia, Oscar Kambona, Paul Bomani na wengine kibao ni maarufu hata kwa kizazi hiki kipya wanajua mchango wa watu hawa katika Uhuru wa Tanganyika kupitia historia yetu..Katika hili bila kutaja dini zao nakubaliana sana na Mohammed na ndio maana nikauliuza historia ya Cecil Matola na mbona kiongozi huyu kasaulika?..

Kikubwa anachokosolewa Mohammed Said ni pale alipotengua lengo la awali na kulifanya swala hili kuwa la imani ya dini (conclusion yake) na kwamba hawa viongozi wamesahaulika kwa sababu ni Waislaam ama serikali imepotosha mchango wa Waislaam ktk harakati za Uhuru wa Tanganyika hivyo kuifanya hoja nzima ya TAA na TANU kuwa ya kidini zaidi ya chama cha siasa...

Nachomuomba Mohammed Said ni kimoja tu ya kwamba, hata historia ya Zanzibar haiwezi kuwa historia sahihi kama hutazungumzia viongozi waarabu wa Hizbu party. Na mtu yeyote kipenzi wa Hizbu anaweza kuja hapa na kudai haoni sababu kwa nini Karume maarufu kuliko Shamte, akatumia hata race card ya kama tunavyowasoma Wazanzibar wengi wakizungumzia Mapinduzi kama ilikuwa njama ya watu weusi dhidi ya Wazanzibar wenye asili ya Kiarabu na kadhalika..Yote haya yanaweza kuwa na ukweli lakini lengo la mwandishi linapokuwa linalenga kuonyesha dhulma fulani ni muhimu sana kwetu kupima hiyo dhulma inayodaiwa kisha tujenge hoja zinazopinga ama kuhalalisha dhulma hiyo..

Mimi nachoweza kumwambia Mohammed Said, historia ulopewa ya wazee wako kuna mengi umefichwa ama wewe mwenyewe umeamua kuiacha pembeni lakini kati ya kundi kubwa la wazee wako toka mwaka 1964 kufikia mwaka 1967 walikuwa tayari wamejitenga na chama TANU, walikuwa tayari wakitaka kufanya Mapinduzi dhidi ya chama TANU ambacho kiliongozwa na Nyerere walikuwemo waislaam wengi sana viongozi vile ivle, na Waislaam karibu mikoa yote walipingana na dhana ama lengo la hawa wazee wako waliojitenga...Hivyo, unapojitoa ktk chama kumbuka pia unapoteza haki zote ulostahili kupewa na historia yako inakuwa na picha tofauti kama ilivyokuwa kwa kina Mtenvu na Kambona.

Hatuwezi kuwa na historia njema ya Kambona zaidi ya kwamba alitaka kuipindua nchi. Na vile vile hatuwezi kuwa na historia nzuri ya kundi la watu walitaka kuanziusha vurugu nchini kwa kutumia sanduku la Udini ila naweza sana kukubaliana na wewe kwamba kuna viongozi wetu waliokuwa na mchango mkubwa sana ktk harakati za Uhuru wetu wamesahauliwa. Hawa ndio wanatakiwa kuitwa mashujaa na hawa ndio wanatakiwa kuenziwa kwa kila sifa ya Uzalendo na hata kusherehekewa ktk Memorial day!.

Nilichoweza kujifunza mimi kutoka vitabu vya Mohammed Said ni kwamba - Historia ya Tanganyika inapotea na ipo haja na sababu kubwa ya vitabu kama cha John Lliffe - A Modern History of Tanganyika kiwe ktk vitabu vinavyotakiwa kufundishwa mashuleni iwe Primary school au Secondary. Lakini haya maswala ya Udini au kutumia Uarabu kudai haki ya Uzanzibar haiwezi kujenga umoja wa kitaifa bali unabomoa hata imani ndogo ya uzalendo iliyokuwepo..Leo hii ukimwambia Mgazija kwamba Waarabu ndio waasisi wa Uhuru wa Zanzibar na Shamte alikaribishwa tu, sijui kama kutakalika.

Maasalaam!

Bob heshima mbele.....hii ndio tunaita mwendo wa JF.....kumkoma nyani giladi....
 
Mohamed Said;2789448]
Bwana Mkandara,Tubishane kwa mengine si haya ya TANU.Mimi nina asili na chama hiki na nadhani ushaona kuwa najua.Lakini sikuzuii kuamini upendavyo.Ndiyo maana nimeikataa historia rasmi na nimekuja na ya wazee wangu hadi leo hakijaandikwa kitabu kupinga kitabu changu.Zungumzeni mengine lakini si hii TANU na siasa za Dar es Salaam na yalokuja baada ya uhuru.
Mohamed
Mohammed Said, huwezi kuibadilisha historia kwa jinsi utakavyo hata sisi tunajua vile vile. Bibi Titi hahusiki kabisa na maswala nayozungumzia yeye scandal yake iko na kina Michael Kamaliza waliotaka kupindua serikali mwaka 1969, hatuzungumzii haya kwa sababu pamoja na kushindwa uchaguzi mwkaa 1965 she remained party official na muhimu ktk chama hadi tuhuma za mwaka 1969.

Hao wazee wako walitaka kuipindua seriikali na Nyerere alitonywa na Sheikh Kassim bin Jumaa na kuthibitishwa na Tewa Said Tewa hizi ni habari zilizotoka ndani ya EAMWS. Kwa hiyo kama hutaki historia inajionyesha walikamatwa kwa kosa ya kutaka kuipindua serikali. Wewe kama una ushahidi kuonyesha haikuwa kweli utoe hapa kwa sababu mimi najua watu wote ulokamatwa walihusika na walikuwa wanachama wa AMNUT, wengine wamejitoa TANU. Ni sawa na aloyafanya Ghadaffi unaweza yachukua kwa mtazamo wowote ule upendao.

Kulikuwepo na walokamatwa bila hatia? hilo sijui wewe mwenye taarifa hizi twambie watu hao nahawakuhusika kwa vipi?.. maana kutokuwa kiongozi haina maana huungi mkono mapinduzi. Mimi leo hii naunga mkono kabisa kuondolewa kwa CCM na serikali inaweza kuniweka ktk kitabu cheusi kama mpinzani hatari nayetakiwa kushughulikiwa. Being right or wrong itakuwa ktk macho ya mhadithiwa!
Mkuu Mkandara, kwanza nikushukuru umeandika mengi na si rahisi kuyasherehesha yote.
Huko nyuma niliwahi kusema Mohamed anadhani anajua kuliko watu wengine akasema ni tusi. Nashukuru amekuja mwenyewe kudhihiri na kunisafisha kwa tuhuma.

Hayo unayoyasema si kuwa Mohamed hayajui, anayajua sana lakini akiyasema yatakinzana na kile alichokusudia wakati anaandika masimulizi.

Tatizo la Mzee said ni ushahaulifu kila anaposema au kuandika. Huko nyuma amewahi kusema kuwa siasa za TANU zilifanywa misikitini(ushahidi upo). Sasa hivi anasema masheikh walikamatwa kwa kuonewa kwa vile hawakuwa wanafanya siasa.

Huko nyuma amesema kulikuwa na mgogoro ndani ya AMNUT japo haelezi sababu kwa ukamilifu. Hii ilikuwa mwaka 1959 kabla Nyerere hajawa rais, sasa hivi anasema Nyerere ndiye aliyeleta fitna na kuwagawa waislam. Kwamba walikuwa kitu kimoja 1959.

Hilo la mpango wa mapinduzi wa mwaka 1969 analielewa lakini hataki kujibu ila anabaki na hoja yake dhaifu sana, andikeni kupinga. Hicho ulichokieleza ndio ukweli ambao yeye anaujua. Kwa bahati mbaya ukweli huo hauruhusu kuchomeka ukristo na unabadilika kutokuwa ukweli.

Mohamed hataki kujifunza na ameshaamini kuwa yeye ndiye yeye. Sote humu tunasema watu waliopigania nchi hii wapewe heshima katika historia. Mimi niliwahi kujiuliza hakukuwa na akina mama waliompikia Nyerere alipokuwa katika harakati, na mbona hatuwasikii japo kwa kutajwa. Kwahiyo kimsingi tunakubaliana kuwa kuna sehemu zinahitaji kufanyiwa kazi ili kuleta taswira ya historia iliyokuwepo bila kubagua au kuchomeka mbegu za aina yoyote.

Tunapotofautina na Mohamed ni pale ambapo anaamini kuwa uhuru wa nchi hii umeletwa na waislam. Ni kweli kuwa vugu vugu lilichgizwa sana kutoka Dar es Salaam kulikokuwa na waumini wengi wa kiislam. Hii haina maana hakukuwa na harakati kwingine, hapana jitihada zilikuwepo kila kona ya nchi.

Ukisoma maandishi ya Mohamed ni wazi kabisa wazee waliopigania uhuru hawakuupigania kama Uislam bali ni kwa uzalendo wao. Tofauti kati ya Sykes na Takadir ni ushahidi wa kutosha. Uchaguzi wa TAA ni ushahidi wa kutosha kwasababu waliopiga kura wengi ni waislam na walimchagua Nyerere.

Kinachoendelea hapa ni Mohamed kujenga hoja za kuufanya Uislam na kutumia majina ya kiislam si kwa lengo la masimulizi yake bali kujenga chuki. Kama anakubali kuwa Kyaruzi Vedastos, Mtamilwa Clement, Kirlo Japhet, Rupia John, Munanka Bhoke, Mzee Mkaranga n.k walikuwa sehemu ya harakati, ushujaa wa kusema wakristo walikaa pembeni anaupata wapi? Ni ukweli pia si waislam wote waliounga mkono, je hiyo inatosha kusema waislam hawakushiriki uhuru. Na mifano zaidi.

Kibaya zaidi ni pale Mohamed anapowaficha watu ukweli hasa waislam. Anajenga hoja za kuwafanya waislam waamini kuwa tatizo lao ni Nyerere na Wakristo. Anaficha ukweli kuwa ndani ya baraza la wazee wa TANU walikuwepo waislam walioifanya kazi hiyo , ndani ya EAMWS walikuwepo na hawa ni akina Tewa. Lakini ni dhambi kubwa sana kuwataja waislam waliosababisha matatizo kwa wenzao ndiyo maana anatafuta hoja za kumkingia kifua Tewa. Ni hivyo hivyo tunaona kuwa ukoo wa Sykes na akina Mwapachu bado zipo ndani ya chama kwa uimara.

Tunapomuuliza ushiriki wa Mzee Kawawa 'right hand man' wa Nyerere Mohamed anasema 'tuliache kwanza' kwani mjadala wake utayeyusha hoja za masimulizi yake. Double standard ni nyingi sana,lakini hakuna double standard kwa Nyerere na wakristo.!!

Ninachosema hapa ni kuwa kama lipo tatizo basi si lile Mohamed analolijenga, angekwenda mbali zaidi angeupata ukweli.
Lakini kamwe hawezi kuupata ukweli kwasababu tayari ameshajenga ukweli wake anaoamini ni ukweli mtupu na hataki kuwasikiliza wengine kwasababu akitaka kusikilizwa anakwenda Cambridge na New York.
Tutaendelea kuchambua makala zake neno hadi neno
........
 
Wazee wangu hawakujitoa TANU bali walitolewa kwa hila na fitna
Huko nyuma umeeleza mzee mmoja aliyejitoa ili kujikita na shughuli za waislam(uzi ninao nikitakiwa nitauvuta),sasa hili la fitna linatoka wapi? contradiction
Maalim Matar na Shariff Adnan walifungwa jela kwa sababu tu walihusikana msikiti wa Badawiy mjini Dar es Salaam ambako Sheikh Hassan bin Amir, wakatihuo akichukuliwa kuwa ndiyo roho ya waumini wa Tanganyika, alikuwa ikiendeshamadrasa yake kila magharibi pale msikitini
Kwa hiyo umewasafisha kuwa hawana tuhuma. Ni hao hao waliokusimulia, je ulitarajia wakwambie kile usichotaka au wasichotaka tusikie. Hapa unatoa ushahidi usiokuwa nao. Kama harakati za TANU zilifanyika misikitini(kwa mujibu wako) tunawezaje kusema madrasa hazikuwa na harakati kama zile za TANU kwa njia ya mapinduzi!
Huendakile kilichomfanya Nyerere kuwatia kizuizini masheikh na wengine kuhamishwa nikufuata ule msemo wa Biblia usemao, "yule ambae hayuko nasi basi ni dhidiyetu
Neno huenda maana yake huna uhakika kwanini unalijengea dhana ya biblia na Nyerere ikiwa hujui nini hasa kilitokea. Hapa utafiti uko wapi!
Abdulwahid alikufa mwaka 1968 wakati nchiilikuwa imegubikwa na hasama za chinichini kati ya Waislam na Wakristo ambaosasa walikuwa wamehodhi madaraka yote katika serikali
.Tumeona ugomvi wa Nyerere na wenzake, sasa uhasama wa wakristo na waislam unatokea wapi kama si kutaka kujenga hoja isiyojkuwepo. mohamed unaweza kusimama mbeye ya Rais mstaafu Mwinyi, Mzee Kawawa ukasema hayo unayoyasmea kweli."
Sheikh Hassan bin Amir alikuwa kati yaWaislam wachache ambao walithubutu kusimama kidete dhidi ya serikali na kutoamawazo yake kuhusu jinsi serikali ilivyokuwa ikiwakandamiza Waislam
Hapa hujasema walikandamizwaje maana bado tupo katika ugomvi wa Nyerere na wenzake na ni miaka michache tu ya uhuru. Ukandamizwaji katika nini kwa wakati huo.
Abdulwahid alikuwa anajua vyema nguvu ya umoja waWaislam wakati walipokuwa wanapigania uhuru wa Tanganyika. Abdulwahidhalikadhalika alikuwa anafahamu nguvu ya wale waliokuwa nyuma na njama zile zakuwagawa Waislam katika makundi hasimu.Kwahiyo unakiri kuwa waislam waligawanyika katika makundi hasimu
Sasa hapa ni nani wa kulaumiwa? Mohamed, mtafiti makini angewaambia waislam kwanini walikubali kugawanywa, nini sababu yake na si kuwaficha.
Kama Uislamulitumika kuwaondoa wakoloni Uislam hautashindwa kuwatoa wao madarakani. Uislamikiwa itkadi ya kupinga ukoloni sasa ilikuwa ni tishio kwa Ukristo katikaTanzania huru."
Hapa ndipo mzee wetu unapopotoka. Uganda hakukuwa na waislam wengi, je hawakumuondoa mkoloni. Hebu tuambie Sykes alipokuwa anafanya kazi na Nyerere, au akina Rupia, Mtamilwa, Kyaruzi n.k nao walikuwa sehemu ya waislam na kama hawakuwepo huko walikuwa kundi gani liloleta uhuru. Lakini pia unathibitihsa dhana aliyokuwa nayo Nyerere kuwa huenda walipanga mapinduzi kwa maelezo yako. Kwanini nyerere aonekana mbaya wa kuwafunga wakati kauli yako inasema wazi kuwa hilo lingewezekana
 
Mkuu Mkandara, kwanza nikushukuru umeandika mengi na si rahisi kuyasherehesha yote.
Huko nyuma niliwahi kusema Mohamed anadhani anajua kuliko watu wengine akasema ni tusi. Nashukuru amekuja mwenyewe kudhihiri na kunisafisha kwa tuhuma.

Hayo unayoyasema si kuwa Mohamed hayajui, anayajua sana lakini akiyasema yatakinzana na kile alichokusudia wakati anaandika masimulizi.

Tatizo la Mzee said ni ushahaulifu kila anaposema au kuandika. Huko nyuma amewahi kusema kuwa siasa za TANU zilifanywa misikitini(ushahidi upo). Sasa hivi anasema masheikh walikamatwa kwa kuonewa kwa vile hawakuwa wanafanya siasa.

Huko nyuma amesema kulikuwa na mgogoro ndani ya AMNUT japo haelezi sababu kwa ukamilifu. Hii ilikuwa mwaka 1959 kabla Nyerere hajawa rais, sasa hivi anasema Nyerere ndiye aliyeleta fitna na kuwagawa waislam. Kwamba walikuwa kitu kimoja 1959.

Hilo la mpango wa mapinduzi wa mwaka 1969 analielewa lakini hataki kujibu ila anabaki na hoja yake dhaifu sana, andikeni kupinga. Hicho ulichokieleza ndio ukweli ambao yeye anaujua. Kwa bahati mbaya ukweli huo hauruhusu kuchomeka ukristo na unabadilika kutokuwa ukweli.

Mohamed hataki kujifunza na ameshaamini kuwa yeye ndiye yeye. Sote humu tunasema watu waliopigania nchi hii wapewe heshima katika historia. Mimi niliwahi kujiuliza hakukuwa na akina mama waliompikia Nyerere alipokuwa katika harakati, na mbona hatuwasikii japo kwa kutajwa. Kwahiyo kimsingi tunakubaliana kuwa kuna sehemu zinahitaji kufanyiwa kazi ili kuleta taswira ya historia iliyokuwepo bila kubagua au kuchomeka mbegu za aina yoyote.

Tunapotofautina na Mohamed ni pale ambapo anaamini kuwa uhuru wa nchi hii umeletwa na waislam. Ni kweli kuwa vugu vugu lilichgizwa sana kutoka Dar es Salaam kulikokuwa na waumini wengi wa kiislam. Hii haina maana hakukuwa na harakati kwingine, hapana jitihada zilikuwepo kila kona ya nchi.

Ukisoma maandishi ya Mohamed ni wazi kabisa wazee waliopigania uhuru hawakuupigania kama Uislam bali ni kwa uzalendo wao. Tofauti kati ya Sykes na Takadir ni ushahidi wa kutosha. Uchaguzi wa TAA ni ushahidi wa kutosha kwasababu waliopiga kura wengi ni waislam na walimchagua Nyerere.

Kinachoendelea hapa ni Mohamed kujenga hoja za kuufanya Uislam na kutumia majina ya kiislam si kwa lengo la masimulizi yake bali kujenga chuki. Kama anakubali kuwa Kyaruzi Vedastos, Mtamilwa Clement, Kirlo Japhet, Rupia John, Munanka Bhoke, Mzee Mkaranga n.k walikuwa sehemu ya harakati, ushujaa wa kusema wakristo walikaa pembeni anaupata wapi? Ni ukweli pia si waislam wote waliounga mkono, je hiyo inatosha kusema waislam hawakushiriki uhuru. Na mifano zaidi.

Kibaya zaidi ni pale Mohamed anapowaficha watu ukweli hasa waislam. Anajenga hoja za kuwafanya waislam waamini kuwa tatizo lao ni Nyerere na Wakristo. Anaficha ukweli kuwa ndani ya baraza la wazee wa TANU walikuwepo waislam walioifanya kazi hiyo , ndani ya EAMWS walikuwepo na hawa ni akina Tewa. Lakini ni dhambi kubwa sana kuwataja waislam waliosababisha matatizo kwa wenzao ndiyo maana anatafuta hoja za kumkingia kifua Tewa. Ni hivyo hivyo tunaona kuwa ukoo wa Sykes na akina Mwapachu bado zipo ndani ya chama kwa uimara.

Tunapomuuliza ushiriki wa Mzee Kawawa 'right hand man' wa Nyerere Mohamed anasema 'tuliache kwanza' kwani mjadala wake utayeyusha hoja za masimulizi yake. Double standard ni nyingi sana,lakini hakuna double standard kwa Nyerere na wakristo.!!

Ninachosema hapa ni kuwa kama lipo tatizo basi si lile Mohamed analolijenga, angekwenda mbali zaidi angeupata ukweli.
Lakini kamwe hawezi kuupata ukweli kwasababu tayari ameshajenga ukweli wake anaoamini ni ukweli mtupu na hataki kuwasikiliza wengine kwasababu akitaka kusikilizwa anakwenda Cambridge na New York.
Tutaendelea kuchambua makala zake neno hadi neno
........

Nguruvi3,

Umemtaja Sheikh Kassim.

Mimi nina "paper" nzima niliitoa Kenyatta University kuhusu Sheikh Kassim Juma. Nakupa kipande kidogo hapo chini kisha tutaendelea na mengine Insha Allah:
"It was Sheikh Kassimbin Juma's sudden change from being a pawn of Nyerere to becoming a champion ofMuslim rights, to use his own words, "usurped by a political systemestablished by Julius Nyerere," which made his life history worthy of record. Sheikh Kassim who for manyyears was shunned by Muslim intellectuals not taking him seriously seeing himas a lackey, was by this sudden change caused this group to come forward tosupport him. Short of thistransformation Sheikh Kassim's life would not have been remarkable. Historywould have remembered him as a Muslim scholar who sold himself to Nyerere andbetrayed Islam. In order to understand the change in Sheikh Kassim one needs totrace his transformation from the time in 1985 when power changed hands inTanzania. "

Nimekupa hapa juu kidogo kuhusu hali ya siasa ilivyokuwa wakati ule ila kwa ufupi Sheikh Kassim mpaka anafikia kufa alikuwa kajutia nafsi yake na alitaka aondoke duniani Waislam wakimkumbuka kwa hivyo.

Hayo ya AMNUT si kweli. Kuna masheikh waliwekwa kizuizini wala si wana siasa na mifano ni mingi. Maalim Matar kafungwa hakuwa mwanasiasa wala hajui AMNUT ni kitu gani. Maalim Matar yeye alikuwa sufi. Mzee Ali Comorian kafungwa hakuwa mwanasiasa mifano ni mingi sana.

Katajwa Kawawa. Nakuwekea pitio la kitabu chake "Simba wa Vita katika Historia ya Tanzania" kilichoandikwa na Magotti usome kidogo:

"It is strange thatKawawa's book does not have references to his personal papers which are notonly important to Kawawa's life history but to the history of Tanganyika aswell. Magotti did not even interview Kawawa's contemporaries still living likeAlly Sykes and Victor Mkello a fellow trade unionist now on his death bed. This was Magotti's greatest omission. Had hedone that he would have come across Kawawa's other contemporaries and names ofother patriots who Kawawa had worked with in TAGSA like Dr. Wilbard Mwanjisi,Dr. Michael Lugazia, Dr Kyaruzi and others... The story of AliMigeyo is among the sad chapters in the history of Tanganyika's independencestruggle. Migeyo who was a leading voice in the Lake Region was imprisoned bythe colonial government for mobilizing the people against British colonialism.After independence Migeyo was detained by Nyerere's government for his politicalactivities. It would have been very interesting to hear from Kawawa why Nyereretook the decision to imprison a fellow patriot and one of the leading figureswho spearheaded the struggle for Tanganyika's independence. On the same breathit would have been interesting to know how he felt when in 1964 leaders in thetrade union movement, patriots like Victor Mkello, Paul Pamba, Abdallah Mwamba, Hassan Khupe, SalumAbdallah and manyothers who he had worked with during the struggle for independence were detainedand while in detention the government outlawed the trade unions they wereleading and formed a new organisation NUTA lead by handpicked personalitieswithin the TANU echelons...it would have been interesting to read about Kawawa's role in the banning of the EAMWS and formation of BAKWATA...There is an interesting partin which the book portrays Kawawa as a government servant working in the MauMau camps set up by the colonial government to detain Kenyans suspected ofbeing Mau Mau living in Tanganyika. These camps were opened up soon after thedeclaration of emergence in Kenya when Kenyatta and other patriots the famousKapenguria Six - Bildad Kaggia, Jomo Kenyatta, Kun'gu Karumba, Achieng Oneko,Paul Ngei and Fred Kubai were arrested. Among the Mau Mau detainees at HandeniCamp where Kawawa was working were two TANU members although they were Kenyans.These were Dome Okochi Budohi and Patrick Aoko. Budohi's TANU card was no. 6. Budohiand Aoko were arrested in 1955 soon after the formation of TANU. They weredetained at the Central Police Station in Dar es Salaam and interrogated forsix months. The two were kept in chains. Kawawa if propped could have talkedabout these Kenyan patriots who struggled for Tanganyika's independence andabout his experiences with them in the Mau Mau camps and what became of themwhen both Kenya and Tanganyika were liberated from the British...the door is still open for researchers to enterand write about the life history of Rashidi Mfaume Kawawa because his biographyis yet to be written. But I congratulate the author for writing this bookbecause it is from this book that I derived the strength to write the littlethat I know on the times of Mzee Kawawa. Surely Kawawa has beaten all of themin Tanzania he has two books on his life but again his is a tale of two booksand the book that never was."

Nguruvi3,
Nyie mna maneno matupu mimi nina "papers" na vitabu kwa mkono wangu na kwa utafiti wangu.
"Papers" hizi ndiyo zishaandikwa zishatolewa katika makongamano. Vitabu vyangu vipo na ni rejea katika historia ya Tanganyika.

Nini nitahitaji zaidi?

Ndiyo nasema vuteni subira mniache nitoe darsa.
Nina mengi niyajuayo kuhusu historia ya TANU.

Mohamed
 
Siyo hilo tu, Mohamed Said kama historian aliombwa aandike historia ya Watanzania wengine ambao happened to be Christians. Mohamed akakataa akasema hiyo kazi ifanywe na wengine. Lakini wangekuwa ni Waislamu wa Kigoma, Tabora, au Arusha, Mohamed angekubali mara moja
kuifanya kazi hiyo. Mwanahistoria habagui. Lakini mwanahistoria wa kidini hujikita zaidi katika matukio yanayohusu dini yake. Wanaomchukulia Mohamed kama mwanahistoria wanahitaji kujiuliza.

Jasusi,

Nimekusoma.

Mohamed
 
Huko nyuma umeeleza mzee mmoja aliyejitoa ili kujikita na shughuli za waislam(uzi ninao nikitakiwa nitauvuta),sasa hili la fitna linatoka wapi? contradiction Kwa hiyo umewasafisha kuwa hawana tuhuma. Ni hao hao waliokusimulia, je ulitarajia wakwambie kile usichotaka au wasichotaka tusikie. Hapa unatoa ushahidi usiokuwa nao. Kama harakati za TANU zilifanyika misikitini(kwa mujibu wako) tunawezaje kusema madrasa hazikuwa na harakati kama zile za TANU kwa njia ya mapinduzi! [/B]Neno huenda maana yake huna uhakika kwanini unalijengea dhana ya biblia na Nyerere ikiwa hujui nini hasa kilitokea. Hapa utafiti uko wapi! [/COLOR][/SIZE][/FONT].Tumeona ugomvi wa Nyerere na wenzake, sasa uhasama wa wakristo na waislam unatokea wapi kama si kutaka kujenga hoja isiyojkuwepo. mohamed unaweza kusimama mbeye ya Rais mstaafu Mwinyi, Mzee Kawawa ukasema hayo unayoyasmea kweli."[/COLOR][/SIZE][/FONT]Hapa hujasema walikandamizwaje maana bado tupo katika ugomvi wa Nyerere na wenzake na ni miaka michache tu ya uhuru. Ukandamizwaji katika nini kwa wakati huo.
[/SIZE][/COLOR][/FONT]Sasa hapa ni nani wa kulaumiwa? Mohamed, mtafiti makini angewaambia waislam kwanini walikubali kugawanywa, nini sababu yake na si kuwaficha.
Hapa ndipo mzee wetu unapopotoka. Uganda hakukuwa na waislam wengi, je hawakumuondoa mkoloni. Hebu tuambie Sykes alipokuwa anafanya kazi na Nyerere, au akina Rupia, Mtamilwa, Kyaruzi n.k nao walikuwa sehemu ya waislam na kama hawakuwepo huko walikuwa kundi gani liloleta uhuru. Lakini pia unathibitihsa dhana aliyokuwa nayo Nyerere kuwa huenda walipanga mapinduzi kwa maelezo yako. Kwanini nyerere aonekana mbaya wa kuwafunga wakati kauli yako inasema wazi kuwa hilo lingewezekana[/COLOR][/SIZE][/FONT][/FONT]

Nguruvi3,

Subiri hadi mwisho wa darsa utapata majibu yote.

Mohamed
 
Nimesema hivi ukichora mstari kutoka kwa "wazee" wa Mohammed Said na wale waliotaka kuondoka TANU kupitia AMNUT mwaka 1958 na wale waliomkataa Nyerere mara ya kwanza alipotambulishwa kwao early 1950s utakuwakuta kuwa niw atu wale wale. Chuki dhidi ya Ukatoliki wa Nyerere haikuanza 1962 kwenye congress ya Waislamu wote na wala siyo Waislamu wote wa Dar walikuwa na chuki dhidi ya Nyerere. Ndio maana waliowashinda AMNUT mwaka 1958 walikuwa ni Wazee Waislamu wa Tanga.

Ukiniuliza mimi hadi leo huoni akiwataja wazee hawa kwa heshima. Barubaru anawajua sana wazee wa Tanga lakini ni ndio hawa ambao majina yao hayatajwi lakini kiukweli kabisa naweza kuwaita ndio MASHUJAA WA UHURU kwa maana ya kwamba kama wangekubali AMNUT nchi ingegawanyika. NI hawa wazee wa Tanga walioona mbali zaidi kuwa Tanganyika ni moja na wote tuna maslahi ndani yao. Katika kitabu cha Bw. Said anasimulia vizuri sana jinsi Nyerere alivyoonesha ushawishi mkubwa na kuweza kuwazidi siasa kina Mtemvu kwenye ule Mkutano wa Tabora. Mashehe wa Tanga hawatajwi sana japo walikuwa na mchango mkubwa sana.

Ningefurahi kusikia kama Barubaru anaweza kutusaidia kutoka upande huo.

Bw. Said angetaka kuandika historia ya wale "MASHUJAA WALIOSAHAULIWA" kwa kweli angekuja nahistoria tamu sana ya wazee 'wetu'. Asingeangalia dini zao kabisa lakini hilo lingevunja vunja kabisa kile alichotaka kusema ambacho kwa uhakika kabisa hajawahi kupata changamoto ambazo anazipata hapa. Nimeangalia kwenye youtube nyingi anapozungumza mbele ya vijana ambao maskini wa Mungu hawana hili wala lile zaidi ya kuitia na kuonesha kushangazwa. Vijana hawa ambao wengine hawajui kabisa historia ya nchi yetu imetoka wapi lakini wako tayari kuaminishwa histohisa ambayo inapendekezwa kwao kuwa ni historia.

Kwa kutumia 'authority' ya kuwa vitabu vyake vinachapishwa na kusomwa sehemu mbalimbali duniani Bw. Said anawaaminisha wasikilizaji wake kuwa anachosema ni kweli. Kwa sisi wengine tunajua kabisa kuwa vyuo vikuu kama vya Marekani vina vitabu vya kila aina na vyenye dhana mbalimbali si lazima vikubaliane na dhana hizo. Wenyewe wanaita "academic freedom". Ndio maana utakuta vitabu vinavyozungumzia masomo ya ajabu ajabu lakini kwa vile ni vyuo vikuu vinakubalika kwa sababu ndio kufunguana mawazo. Kwa wale vijana wa mitaani ambao wana kiu na kujua historia yao wanajikuta wanakubali masimulizi haya hasa kwa vile jamaa alikuwa ametoa mihadhara kwenye vyuo mbalimbali.

Nina uhakika wa asilimia mia Bw. SAid hawezi kuita mhadhara wa wazi na wasomi wa historia ya Tanzania akaweza kujitetea zaidi ya mbinu hii mpya "na nyie nendeni kaandikeni". Madai yake mengi hawezi kuyatetea, ushahidi wake hawezi kuutetea, na mahitimisho mbalimbali hayana msingi wa kihistoria.

Lengo lililo ni jepesi tu - kupandikiza chuki kwa Waislamu dhidi ya Kanisa na Wakristu. Ni kwa kufanya hivi tu ndio anapata uwezo wa kuzunguka na kuaminisha watu. Lakini Watanzania wakikataa hii chuki - ambayo imepata mashabiki hata wasomi wa hali ya juu na maafisa wa juu katika taasisi zetu mbalimbali - watapoteza nguvu ya sumu hii. Ni sawasawa na simulizi moja la kwenye Star Trek ambapo silaha moja ilikuwa na madhara zaidi kama wale wanaoshambuliwa nayo na wao wanaonesha aggressive behavior. Kwa hasira na kutaka kupigana ndivyo silaha ya adui yao ilivyokuwa inazidi kupata nguvu. Lakini Patrick Stewart (Capt. Jean Luc Picard) anawaambia kina Worf na maofisa wengine "to empty all aggressive thoughts" ndivyo yule adui yao alivyoshindwa kutumia silaha yake. Kwani kila akijaribu kuwaprovoke wapigane naye wao waliweka silaha zao chini na badala yake wakarudisha amani na upendo na kumshinda.

Chuki ya kidini ambayo Bw. Said anajitahidi sana kuipanda kwa mbinu ya upotoshaji wa hali ya juu wahistoria hata hivyo haiwezi kuachiliwa kimya kama wanavyofanya baadhi ya viongozi wetu. Bali inatakiwa ijibiwe kwa nguvu ya hoja ambazo zinasimama zenyewe. Baba wa Taifa aliwahi kusema kuwa "hoja dhaifu hushindwa kwa kuoneshwa kuwa ni hoja dhaifu na huondolewa kwa hoja nzuri zaidi". Hoja ya kuwa Kanisa na WAkristu ndio tatizo la Waislamu nchini inavutia. Inaonesha ina ukweli na kwa namna fulani inakubaliana na hisia za watu. Lakini inaposogezwa karibu kwenye darubini watu wanatambua mara moja kuwa hicho ni kisingizio tu. Na ndipo hapa Watanzania wamekuja pamoja wenye threads hizi zote kupinga hoja za Bw. Said, kuzionesha kuwa ni dhaifu na kuzikosoa pasipo huruma.

Na tuelewane vizuri kabisa. Hoja zinazopingwa siyo historia au sehemu ya historia ambayo Bw. Said anaisimulia. Kutuambia habari za kina Sykes, Plantan, Tambaza na wengine ni sehemu ya historia yetu. Bw. Said yeye anafanya ni historia ya Waislamu wakati kwa kweli kabisa ni urithi wetu sote kwani hawa wote ni wazee 'wetu' tena ni WETU kwa herufi kubwa. Ni sawasawa na Wamarekani ambao mwanzoni waliona kuwa sikukuu ya Martin Luther King Jr. ilikuwa ni sikukuu ya Watu weusi tu. Lakini sasa hivi Wamarekani weupe kwa weusi, wanjano na wa kahawia wote wanamkubali MLK Jr kama shujaa wao. Leo hii watu mbalimbali ambao miaka michache nyuma walionekana ni wa kikundi fulani tu wanaonekana ni wa Taifa zima kwa sababu mchango wao ni mchango wa historia ya Marekani. Ni sawa sawa na Wazungu kule Afrika ya Kusini. Unafikiri Wazungu hawamuenzi Mandela? Well walimfunga gerezani lakini leo hawamuenzi? You bet they do! kwa sababu ni historia yao ni mzee wao na wanaona fahari kuwa naye.

Sasa leo hii Bw. Said anataka kuwafanya mashujaa wa historia yetu kuwa ni mashujaa wa watu wa Dar peke yao. Anajaribu kuwagawa mashujaa wa historia yetu katika makundi ya Waislamu na Wakristu! Ili kiwe nini? Well... soma sentensi ifuatayo vizuri: Nyerere awe shujaa wa Wakristu na Abdulwahid Sykes awe shujaa wa Waislamu! Bahati mbaya hawezi kuwa na Sykes katika kiwango hicho kwa kadiri ya kwamba Nyerere naye bado yupo juu. Said hawezi kusema jema lolote la Nyerere, hawezi kukiri mambo yoyote mazuri ambayo Nyerere aliwafanyia Waislamu, hawezi kuthubutu kukiri kuwa Nyerere alikuwa na unique role (yeye anaseme 'leading role'). Kwake yeye Sykes ndiye muasisi wa Tanganyika na Nyerere alikaribishwa tu. There nothing special about Nyerere. Unfortunately, some of our young politicians as well some educated/miseducated elite wameingia kwenye mtego huu.

Bahati mbaya ni kuwa Watanzania wametambua mtegu huu mwepesi. Tunatambua mchango wa wazee wetu wengi ambao hawajulikani. Nakumbuka niliwahi kuandika nyuma kuwa labda wakati umefika kuwa restore to honor baadhi ya waasisi wa taifa letu. Wote wale ambao walitoa mchango mkubwa kabla ya Uhuru regardless of what happened after independence warudishiwe heshima yao na hadhi yao irudi. Ukiondoa wale ambao labda ambao hawakuweza kabisa kurudishwa katika historia. Na hili haliwezekani isipokuwa.

1. Tuwe wa kweli kwa historia. Tuwataje wote na binafsi kweli kabisa ningependa kweli kuwasikia watu wa familia za kina Aziz, Mwapachu, Sykes wanasema nini kuhusu haya. Kwa ukimya wao wametoa baraka kuwa na wao wanaamini kuwa kweli Nyerere alikuwa na chuki dhidi ya Waislamu.
2. Tusahihishe na kuhoji histohisia inayoendesha na Bw. Said ambayo inapambwa kama historia.
3. Wasomi wetu wajibu changamoto ya Bw. Said ya kuandika historia yetu nzima bila kuiogopa. Ni kweli bado hatujazama sana katika historia yetu inavyopaswa hasa linapokuja kwenye suala la harakati za kupigania uhuru.
4. Binafsi naamini kama kuna kipindi cha historia yetu ambacho kinahitaji kusomwa vizuri ni 1961-1971 (Miaka 10 ya kwanza). Ni kipindi hiki matukio yote muhimu ambayo yameifanya Tanzania ya leo iwe yametokea na ni matukio ambayo yangeweza kujaza juzuu za vitabu. Fikiria
- Uhuru
- Mapinduzi ya Zanzibar
- Muungano
- Kuasi kwa Jeshi
- Uamuzi wa Chama Kimoja
- Azimio la Arusha
- Expulsion of prominent figures from the Party

Haya mambo yote ni ya kihistoria sana na wakati umefika kuanza kuyaangalia na si rahisi kuyaangalia moja moja bali ni mambo ambayo japo labda yanaoverlap yanahitaji kuangalia moja nje ya jingine.
 
Huku mzee nilishaaga kwa kudhani kwamba tumeelewana na MS na mashabiki wake. Lakini nilipochungulia nikaona bandiko lako, kwa kweli ni hitimisho zuri sana, lakini naomba niongezee kitu kidogo ambacho niliona kwenye mjadala huu.

Kwanza kuna dhana mbili ambazo ndizo zinaongoza mjadala mzima na tafakuri ya MS kwenye kuwasilisha mada yake ya "Udini wa wakristu" na ile mada ya pili ya "Uonevu dhidi ya waislamu". Dhana mbili zinazoongoza mada za MS ni "uislamu ni dini bora kuliko nyingine" na " Mfumo bora wa kuendesha nchi ni kwa kutumia mfumo wa Kiislamu"

Dhana hizi mbili ndizo MS anazitumia kujengea hoja zake nyingi. Ndiyo maana alitaka kuonyesha ni kwa kuwa kwao waislamu ndiyo maana Kinjekitile, Chabruma, na Mkwawa walipigana na wakoloni wa Kijerumani.
 
Tusihangaike sana na Maandishi haya ya Mzee Mohamed ambayo yamekuwepo zaidi ya miaka 10 iliyopita na hayakuleta madhara wala kuibadili HISTORIA ya NCHI yetu. Pengine tunayakuza bila sababu. TANZANIA itabaki bila DINI. Hatutagawana vyeo, madaraka, elimu, viwanja, mashamba,...., kwa misingi ya DINI.
 
Hakuna kinachobadilishwa wala kubatilishwa bali inaongezwa yale yalio ondolewa kwa makusudi kabisa kwa nia maalu.

Kumbuka hata mbuyu ulianza kama mchicha. Miaka 50 kazi kwenu kila kitu kipo hadharani.
 
Back
Top Bottom