Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Kama vile wewe utaandikiaje TANU isiyo na Julius Nyerere, John Rupia, Oscar Kambona, Joseph Kasella Bantu, Kirilo Japhet, Bhoke Munanka, Paul Bomani,Patrick Kunambi, Pombeah, Mwakangale, Zacharia Madilla, James Malashi, Dominikus Misano, Stanley Kaseko na wengine wengi kama hao! Hao uliowataja walikuwa waislamu, na pengine baadhi yao walitanguliza dini yao kwanza lakini wengi wao walikuwa watanganyika walioungana na watanganyika wenzao wakristu, wahindu na wasio na dini kupigania uhuru wa nchi yao. Wanstahili heshima na kuenziwa si kwa sababu ya dini zao au kabila zao bali utaifa wao.
Oscar Kambona alikuwa Katibu wa kwanza aliyefanya kazi Full time na kulipwa mshahara kutokana na makusanyo ya ada za wanachama. Zuberi Mtemvu alikuwa part time kama walivyokuwa viongozi wengi wa mwanzo, pamoja na Mwalimu.
Amandla......
Fundi Mchundo,
Tusivutane kwa hili la Zuberi Mtemvu mimi kanihadithia mwenyewe kuwa yeye aliacha kazi Community Development Department kwa kushauriwa na Nyerere ili ashike nafasi ya ukatibu. Hata hivyo inawezekana pia kuwa pakawa na kugongana kwa kumbukumbu kama tujuavyo TANU wenyewe walipoandika historia yao mengi waliyaacha. Hebu soma hii:
"TANU ilinufaika sana kwa siasa za wastaniza Nyerere, umakini wake na kipaji chake cha kuzungumza. Vilevile harakati kwa ujumla zilinufaika kwa ujasiri waMtemvu na Ally. Wao walitenda mambo kwa ujasiri zaidi. Hawakushughulishwa sana na nadharia katikamaamuzi yao ya siasa. Ilikuwa katika kipindi hiki cha kuijengea TANU misingiimara ya uongozi ndipo Nyerere alimshauri Mtemvu aache kazi serikalini ajiriwena TANU. Mtemvu alikubali ushauri ule na akaacha kazi. Mtemvu akawa katibu wakwanza wa TANU. Mtemvu na Mhando walijukanakama ëwakomunistií na serikali, lakini wao wenyewe hawakuhughulishwa na jinahilo. Hivi ndivyo ilivyokuwa Zuberi Mwinshehe Manga Mtemvu alivyokuja kuwammoja wa viongozi wa juu katika TANU. Tutaona hapo baadaye kisa cha Mtemvukutupana mkono na Nyerere na TANU. Katika siku za mwanzonafasi ya katibu mwenezi ilikuwa ikishikwa na viongozi mbali mbali baina yaMtemvu Denis Phombeah, Oscar Kambona, Iddi Faizi Mafongo na Stephen Mhando.Mtemvu akiwa katibu mwenezi alikuwa na kazi ngumu ya kuwashawishi na kuwashirikishawatu kujiunga na kusajili matawi ya TANU."
Kuna wazalendo umewataja ambao nami nakubaliana na wewe kabisa kuwa historia ya TANU haiwezi kukamilika bila ya kuwataja.
Mimi kama wewe ningependa sana mchango wao ukaelezwa ili waadhimishwe na nimeshauri na kutoa changamoto hapa ukumbini lakini naona hili jambo watu hawana uwezonalo.
Publisher mmoja baada ya kusoma kitabu changu aliniomba niandike short biographies za watu kama Bhoke Munanka, Chief Patrick Kunambi nk. nk. lakini mimi nilimshauri atafute mwandishi mwengine.
Hatujachelewa kazi hii ni muhimu na lazima Insha Allah ifanyike.
Sasa hili la dini. Sisi watu wa pwani Uislam umo hadi katika utamaduni wetu na kwa kuwa TANU iliasisiwa na Waislam hili halikuweza kuepukika.
Ndiyo maana mikutano ya mwanzo ilikuwa ikianza kwa kupigwa "fatha." TANU ikikwama kwenye jambo wanafanya "tawasul" na wakati mwingine wanafunga "saum."
Ndiyo maana Sheikh Hassan bin Amir akiuza kadi za TANU msikitini.
Ndiyo maana Baraza la Wazee wa TANU lilitawaliwa na Waislam.
Huu ndiyo ukweli wa historia ya TANU na ndiyo maana kitabu changu kikavutia wengi kwa kuwa ilikuja na kitu kipya ambacho kilikuwa hakifahamiki kwa wengi.
Nimeweka uzi hapa kuwa katika kongamano moja nilipewa onyo kabla kuwa nisiutukuze Uislam na mie nilopoanza "presentation" yangu nilifungua na "Surat Fatha" nikawaambia Wazungu wale kuwa hii ndiyo dua iliyokuwa ikisomwa kabla ya mikutano ya TANU Mnazi Mmoja kisha Nyerere ndiyo anakaribishwa na Sheikh Suleiman Takadir.
Nakumbuka swali moja waliloniuliza ni kuwa Wakristo walikuwa wapi wakati huo?
Jibu langu nalikumbuka hadi leo: "you find out it will make very interesting topic for reaserch..."
Mohamed