Nguruvi3,
Umezungumza mengi lakini niko katikati ya darsa ziwezi kulivunja wanafunzi wana "full concentration na mwalimu..."
Nitakujibu moja tu kuhusu mapenzi ya nchi hii.
Wewe (samahani kwa kukunyooshea kidole) na wengine mfano wa wewe hamuwezi kuwa na mapenzi ya nchi hii kupita Said Chamwenyewe aliyeiletea TANU wanachama wake wa mwanzo kutoka Rufiji safari akenda kwa baiskeli wala haombi masurufu na akirudi Dar es Salaam anarudi na hela za kadi alouza anamkabidhi, Idd Faiz Mafongo mweka hazina wa TANU.
Wewe na mfano wa wewe hamuwezi kuwa na mapenzi ya nchi hii kupita Abdulwahid Sykes aliyejitolea kwa hali na mali kuunda TANU na hakuna ajuae marehemu Abdu alitoka kiasi gani kwa TANU katika uhai wake.
Wewe na mfano wako hamuwezi kuwa na mapenzi ya nchi kushinda Dossa Aziz ambae kafa kafilisika, masikini.
Wewe huwezi kuipenda nchi hii kuliko wengi wengi wengi katika wazee wangu ambao wamekufa na kinyongo...nimeshaeleza humu habari za Mshume Kiyate ambae kuna mtu kamkashifu kuwa ni mpeleka kabichi.
Wewe huwezi kuipenda nchi hii kushinda babu yangu Salum Abdallah aliyeweka historia Tanganyika kwa kuongoza mgomo uliodumu siku 82 mwaka 1960...alijitolea kwa mali na hali kuunga mkono harakati za uhuru...akaishia kuwekwa kizuizini...Ali Migeyo...Dharura biti Abdulrahman, Yusuf Ngozi, Tatu biti Mzee, Asha Ngoma, Mama biti Maalim, Yusuf Chembera, Salum Mpunga,Fundi Muhindi, Bilal Rehani Waikela, Sheikh Yusid Badi orodha ni ndefu sana, sana, sana, sana...
Naishia hapa nina darsa linanisubiri Insha Allah.
Mohamed
Brother MS.....hilo hapo juu ni moja ya tatizo kubwa sana ulilonalo...na kwa maana hiyo darsa unalotoa lina tatizo na lake si jema kwa Tanganyika yetu
Unapimaje mapenzi ya mtu kwa nchi yake...Sijui ulimuona/julia wapi Nguruvi3
Nikitu gani hasa kinachokufanya uamini wazee wako walikuwa na mapenzi ya Tanganyika kuliko Watanganyika wengine....
Wengine tukisema Wazee wako ni mamluki na walitaka wao waonekane ni bora zaid ya wengine, wapendelewe wao na familia zao na zaidi kwa kuangalia dini yao......(proved by your statements above)....tutakuwa tunakosea?
Hii ni dharau na matusi makubwa kwa Watanganyika wengine wenye mapenzi ya dhati kwa Tanganyika, na waliipigania vilivyo Tanganyika yetu, iwe kwa senti zao (zisizolingana na za wazee wako wa gerezani), mawazo yao, mazao yao...
Brother MS inabidi ututake radhi siye ambao wazee wetu hawakutokea gerezani, na walitoa "senti/mawazo/nia nk" zao kwenye kupigania uhuru wa Tanganyika...