Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Kwa mtu makini, Hata Nyerere mwenyewe alikipata kitabu chako (kwani kilitoka zaidi ya miaka miwili kabla kufariki kwake, na ninavyomjua Nyerere alivyokuwa msomi wa vitabu laazima atakuwa amekisoma) Lakini hakuthubutu kuandika kupinga maandiko hayo.Kwani aljua ni lazima atulie na kufanya utafiti kidogo kabla kujibu au alikubaliana na kilichomo ndanimwe.
Unaamini vipi kuwa alikisoma? Au kwa vile alikuwa msomi basi kila kitabu kilichompitia unadhani alikisoma? Haujui msomi anachagua kipi kitamsaidia na kipi hakina tija kwake. Halafu unaditiki kusema kuwa "hakuthubutu" kuandika kupinga kilichoandikwa! Nitajie kuna vitabu vingapi alivyoandika Mwalimu kiasi cha kuamini kuwa hata cha Mohamed Said asingechelea kukiandikia?
Nafikiri inakupasa wakti mwingine ufikirie nje ya box.
Usichukulie maneno ya wanasiasa kuwa Tz ni nchi ya amani na utulivu wakti watu ni waoga na wanafiki ingawa kiukweli kuna dhulma kubwa na unyanyasaji wa hali ya juu.
Kumbuka usitegemee kupanda mchicha ukavuna maharage.
Na kila wakti tunasema penye dhulma na pasipo na haki basi hakuna amani wala upendo bali kuna uwoga. Hiyo ndio Tz.
Soma mnakasha vizuri utagundua hilo. Kinachovunwa sasa na zile mbegu zilizopandwa tokea mlipopata uhuro miaka 50 iliyopita. sasa kazi kwenu kwani kuna mwimbaji mmoja wa Raggae akiitwa Robert Nesta Marley (maarufu kama Bob Marley) alimba katika one of his song
You can fool some people sometime But you can't fool all the people all the time.
Cha ajabu kipi Tanzania kuwa na dhulma. Unataka kutuambia kuwa huko uliko hakuna dhulma? Huko wananchi wako huru kukemea dhulma na udhalimu wanaotendewa na watawala wao? Tunachokataa ni kudai kuwa Tanzania kuna institutionalised dhulma dhidi ya kikundi fulani inayotokana na mtazamo wa kidini. Dhulma ipo lakini si hiyo mnaotaka kutuaminisha.
Na hayo maneno unayodai ni ya Bob Marley, yalisemwa kwanza na Abraham Lincoln.
Skillionare,
Umesema maneno ya busara kabisa.
Sisi Waislam kwa umoja wetu tumepita nchi nzima kuwaelimisha Waislam hatari inayokabili nchi yetu kutokana na mfumokristo.
Tunaisubiri serikali itupe jibu.
Mohamed
Hapa ndipo ulipojivua gamba. Mnawafahamisha ili iwaje? Na hiyo hatari ni ipi?
Katika moja ya nchi za nje nilipangiwa mnakasha mimi bila ya kujua kumbe wale host wa ule mnakasha ni "staunch Catholics" hili ni kundi la wasomi na mabingwa katika historia ya Tanzania. Mnakasha jioni baada ya L 'Asr. Mimi hili na lile sina wala siwajui kama hawa ni Catholics mie nimewachukulia kuwa ni "scholars" wa African history."
Ala! Sikujua hili. Kuwa mkatoliki hawezi kuwa scholar wa historia ya kiafrika hata kama nae ni muafrika. Kumbe ndio maana Nyerere anawaudhi! Anayeweza kuzungumza ukweli kuhusu historia yetu ni muislamu peke yake!
Nimeanza na Mnazi Mmoja Sheikh Suleiman Takadir kapanda jukwaa anapiga fatha inasomwa surat fatha kisha dua na watu wote wamesimama mikono wamenyanyua wanaitikia "Amin."
Kisha Nyerere anatambulishwa na kuombwa kuhutubia...
Wazungu kimya...ukumbi utadhani umemwagiwa maji...nawaambia hizo ndizo "Muslim symbols" katika kupigania uhuru wa Tanganyika na zipo nyingi.
Na alipoenda unyakyusani, wakina Mwakangale waliposalimia jamii kwa kusema "ugonile" nayo ni Nyakyusa symbols katika kupigania uhuru wa Tanganyika?
Unataka kweli kutuaminisha kuwa katika jopo la unaowaita wasomi (ambalo lina utata maana sifa hiyo uliishawanyang'anya na kuwabakizia ya ukatoliki) walishangaa kusikia kuwa katika sehemu iliyojaa waislamu, dua ikatangulia kusomwa? Bila shaka waliduwaa kukuona unachukua kitu kama hicho kuwa ni ishara wa pivotal role ambayo uislamu ulibeba katika kupigania uhuru wa nchi yetu.
Abdu anamjulisha kwa mdogo wake Ally, kwa mama yake Bi Mluguru,Bi Mluguru na Bi Mugaya mama yake Nyerere wanakuwa mashoga wakubwa, Abdu anampeleka Nyerere kwa Dossa, Rupia...Abdu anamfikisha Nyerere kwenye madras ya Sheikh Hassan bin Amir Mtaa wa Udoe, Idd Faiz na nduguye Idd Tosiri wanamchukua ndani ya basi la Bagamoyo hadi kwa Sheikh Mohamed Ramia...wanamwakikishia kuwa wapo pamoja nae kwa kheri na shari.
Hawa ni sehemu ya watu aliokutana nao. Hao ndio uliowaona lakini kuna wakina John (Rupia),Joseph Kasella Bantu, Patrick Kunambi, Joseph Kimalando, Kirilo Japhet. Unasahau mchango mkubwa alioutoa Oscar Kambona, ambaye alikuwa Katibu wa kwanza wa kudumu ambae mshahara wake ulitokana na ada za wanachama aliowaingiza TANU. Unapuuzia mchango wa wakina Munanka na Bomani. Mnadai kuwa ndugu zenu walisahauliwa, mbona wakina Kambona tulifikia hatua ya kuwaimbia nyimbo za kuwatukana wakati wa mchakamchaka? Wakati wote huo ndugu zenu wakiachiwa kufanya biashara na kujilimbikizia utajiri katika nchi ambapo wengine hata kufuga kuku ilikuwa nongwa! Huyo Oscar alikuwa Muislamu? Huyo Kasella Bantu alikuwa muislamu?
Leo hii mnazunguka mkilaani mnachokiita mfumo kristo wakati nchi yenu toka ipate uhuru imekuwa ikibebwa na nchi za Nordic ambako asilimia 90 ya watu wake ni wakristu! Mnalalamika kuwa kodi zenu zinafaidia makanisa wakati mkisahau kuwa mnatulaumu kwa kuhodhi ajira na utajiri ambayo inatufanya kuwa wachangiaji wakubwa wa kodi katika nchi hii, kwa hiyo ni kodi ya wamisheni ndiyo tunayoizungumzia hapa!
Ndipo sasa nikatiwa katika ma "journals" na nikatiwa katika mradi wa Dictionary of African Biographies (DAB), Oxford University Press New York wakishirikiana na Harvard. Hii ni kwa sababu nilikuja na kitu kipya katika duru za kisomi.
Hapa una exaggerate tena. Mradi wa DAB uliokuwa chini ya W.E.B. Du Bois Institu ulikuwa na dhamira wa kukusanya maandiko mengi iwezekanavyo inayohusu waafrika, na "article" ilikuwa mojawapo na si kwa sababu uliandika kitu kipya katika duru ya usomi. Hauwezi kuandika historia ya ujerumani bila kugusa Mein Kampf. Kwa kufanya hivi hakutamaanisha kuwa unakubaliana na vyote vilivyoandikwa mle !
Hivi kweli tumefika mahali pa kudai kuenziwa kwa sababu Mwalimu aliwahi kulala kwenu, au mama yake alikuwa shoga na mama yenu, au mjomba wenu alimpakiza kwenye baiskeli n.k. Wengi tu walifanya yote hayo na zaidi na fadhila waliyopewa ni nchi yao kupata uhuru. Kwa wengi wao, hiyo ilikuwa thawabu tosha!
Amandla.....
