FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Wengine tumemsoma Mohamed miaka 20 iliyopita na tunamjua si kupitia mnakasha huu bali kwenye viwanja vingine.
Kama unakumbuka, Nyerere alipostaafu kila gazeti ndani na nje ya nchi, kila mwanasiasa kama Kambona, Fundikira, Katumbo Sanga n.k walitoa maneno makali sana ya kejeli dhidi yake. Hakuwahi kujibu tuhuma hizo kwasababu wakati mwingine ukibishana na Mjinga watu wanaweza wasielewe tofauti. Lakini pia Nyerere hana sababu ya kumjibu mtu kama Mohamed Said, dunia ndiyo inaweza kumjibia kama tuonavyo. Huyu ni moja ya wanasiasa maarufu wa karne wanaojulikana duniani, na ni haki kutojishughulisha na simulizi ziszo na majibu za Mohamed Said.
By the way, Nyerere ndiye mhusika alitakiwa afanye tafiti gani kumjibu Mohamed. Yeye amefanya kazi na Sykes hadi picha ya soksi ndeeeefu anayoongelea mtafiti Kiongozi Sheikh Mohamed kila siku ipo. Anayetakiwa kufanya utafiti ni yule aliyesimuliwa. Nyerere afanye ili iwe nini!!
Hivi inahitaji utafiti kumjibu Mohamed, tunahityaji taa ya kandili mchana maana mwanga uliopo hautoshi.
Ama kweli ukipenda chongo huita kengeza, licha ya wana jamvi kuonyesha udhaifu wa hali ya juu bado kuna watu wanaita masimulizi utafiti, sijui yale ya Dr Koch n.k tutaita nini.
Umeona jinsi tunavyovuta nyuzi zinazo contradict maneno ya mtafiti Sheikh Mohamed. Leo anaongea hili jioni neno lile lile analitolea maelezo tofauti. Mfano anasema AMNUT ilianzishwa kulinda masilahi ya waislam, halafu anasema waislam waliikataa kwasababu itakuwa udini.!!!????
Ahal wangu baru baru, rejea nyuzi uone jinsi Mzee wetu anavyojikanyaga. Hapa si pale gogo vivu, ni JF tunasoma maneno si mistari na tutakuwa naye samba samba ili kuhakikisha kuwa azma yake ya kuleta vurugu nchi haifanikiwi.
Endelea kukata kiu sisi tiulishakata kiu miaka 20 iliyopita kwa version ya english na kiswahili ,kwa makala Nasaha, Annur n.k. na wakti mwingine kumsikiliza mubashar, kama hatukumuelewa miaka 20 it is unlikely tutamwelewa leo.
Tunachojua, hakuna utafiti, ni hadithi za kusikia alizoshadidia na uongo uliopambwa kwa lugha nzuri mashallah. Tunachuja chuya na bahati mbaya mchele unaonekana kidogo sana.
Hatupingi simulizi zake na hutakatai anayosema, tunachokataa ni kile kisichokuwepo, au amekificha na uchochezi usio na shaka wa kutaka kulitumbukiza taifa katika matatizo kwa makusudi kabisa. Tupo naye ili historia isje muacha nje.
Umemwaga pumba hebu zitwange na upepete ubaki mchele. Hivi, kinachokuuma ni nini haswa?
- Kuwa Nyerere si muasisi wa kudai madaraka?
- Kuwa Nyerere hakupokelewa na Abdul Wahid Sykes, Dar Es salaam?
- Kuwa Nyerere hajaishi nyumbani kwa Abdul Wahid Sykes?
- Kuwa Mshume Kiyate hakuwepo?
- Kuwa Mshume Kiyate hakumfadhili Nyerere?
- Kuwa Nyerere alisahau hata wadhifa wa mtu aliyempokea?
- Kuwa anaowataja Mohamed Said hawakuwepo?