Barubaru
JF-Expert Member
- Apr 6, 2009
- 7,161
- 2,324
Mkandara,
Maneno mazuri.
Nami nakuwekea maneno yangu hapa chini:
Wazee wangu hawakujitoa TANU bali walitolewa kwa hila na fitna. Hawa wafuatao ni baadhi ya wazee wangu walowekwa kizuizini: Abdillah Schneider Plantan, SheikhAbdulkarim Abdulwahid, Maalim Popo Saleh, Suleiman Masudi Mnonji, Ali Migeyo,Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Shariff Hussein Badawiy, Shariff Mwinyibaba,Shariff Adnan, Bilali Rehani Waikela, Sheikh Jumanne Bias, Maalim Matar,Abdalah Mwamba, Sheikh Hashim Haji Abdallah, Sheikh Nurdin Hussein, SalumAbdallah Popo, Sheikh Mzee Ali Comoriam, Sheikh Al Amin Maftah, Rajab Kiguu chaMbuzi na wengine wengi. Lakini ukweli ulikuwa kwamba si wote katika walewaliokamatwa na kuwekwa kizuizini walijihusisha na siasa. Baadhi yao walikamatwakwa sababu tu walikuwa wakishirikiana na wale waliodhaniwa ni wapinzani waNyerere. Maalim Matar na Shariff Adnan walifungwa jela kwa sababu tu walihusikana msikiti wa Badawiy mjini Dar es Salaam ambako Sheikh Hassan bin Amir, wakatihuo akichukuliwa kuwa ndiyo roho ya waumini wa Tanganyika, alikuwa ikiendeshamadrasa yake kila magharibi pale msikitini. Shariff Hussein na nduguyeMwinyibaba walihamishiwa Kenya, walikotoka si kwa sababu walikuwawamejishughulisha katika harakati za kuipinga serikali, ila lakini kwa sababuwalikuwa waangalizi wa msikiti wa Badawiy. Sheikh Mzee Ali Comorian alitiwa kizuizini kwa sababu kila mara alikuwaakifuatana na Sheikh Hassan bin Amir kama vile alikuwa kivuli cha sheikh. Huendakile kilichomfanya Nyerere kuwatia kizuizini masheikh na wengine kuhamishwa nikufuata ule msemo wa Biblia usemao, "yule ambae hayuko nasi basi ni dhidiyetu."Jinsi siasa na za Tanzaniazilivyobadilika na jinsi Nyerere alivyoanza kuonyesha uadui dhidi ya Waislamkulimsikitisha sana Abdulwahid. Alishindwa kuelewa uhasama huu ulikuwa unatokawapi. Alihisi kuwa anahusika na yale yaliyokuwa yanawapata Waislam. Mawazo hayayalimzonga kama jinamizi. Kwa ufahamu wake alikuwa anadhani matatizo yote yaudini walikuwa wameyashinda toka miaka ya 1950. Mwaka 1953 Abdulwahid akiwaMuislam na akiungwa mkono na Al Jamiatul Islamiyya aligombea kiti cha urais waTAA na Nyerere, Mkatoliki. Abdulwahid alishindwa uchaguzi ule. Waislamhawakuuchukulia uchaguzi ule kama uchaguzi kati ya Muislam na Mkristo. Kilichotazamwani uwezo wa wagombea. Nyerere alikuwa amemzidi Abdulwahid na kwa ajili hiialichaguliwa kuiongza TAA. Abdulwahid alikumbuka ugomvi wa Sheikh SuleimanTakadir wakati ule Mwenyekiti wa Baraza La Wazee wa TANU. Sheikh Takadiraliwaonya Waislam wachukue tahadhari kwani Nyerere atakuja kuwapendeleaWakristo wenzake pale atakaposhika madaraka. Kama walivyofanya Waislam wengi,Abdulwahid alimuunga mkono Nyerere na kumpinga Sheikh Takadir. Wakati uleAbdulwahid aliamini kama Waislam wengi walivyoamini kuwa Sheikh Takadir alikuwaanataka kuleta siasa za kibaguzi ambazo alikuwa anaziegemeza katika dini.Abdulwahid aliona udini aliokuwa anataka kuuleta Sheikh Takadir lilikuwa jamboambalo litailetea hatari Tanganyika.Abdulwahid alikufa mwaka 1968 wakati nchiilikuwa imegubikwa na hasama za chinichini kati ya Waislam na Wakristo ambaosasa walikuwa wamehodhi madaraka yote katika serikali. Umoja wa kitaifa, mojaya maadili ambayo yeye aliyapigania katika maisha yake yote katika siasaulikuwa unahatarishwa. Halikadhalika umoja wa Waislam ulikuwa unaelekeakuvunjika. Kulikuwepo na kuwekwa kizuizini kwa masheikh chini ya PreventiveDentation Act of 1962. Baadhi ya masheikh waliotiwa gerezani walikuwa watu waliomuunga yeye mwenyewe mkono wakatianaunda TANU. Baadhi yao aliwashawishi kumuunga mkono Nyerere na TANU katikakile kipindi kigumu cha harakati za kudai uhuru. Mwanakamati wa Kamati Ndogo yaSiasa ya TAA, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, kiongozi wa ngazi ya juu kabisa kwaWaislam alikuwa amekamatwa na kuondolewa nchini na kurudishwa kwao Zanzibar kwaamri ya Nyerere.[1]Sababu iliyotolewa ya kukamatwa kwa Sheikh Hassan bin Amir ilikuwa alikuwaati "akipanga njama ya kupinduaserikali."Sheikh Hassan bin Amir alikuwa kati yaWaislam wachache ambao walithubutu kusimama kidete dhidi ya serikali na kutoamawazo yake kuhusu jinsi serikali ilivyokuwa ikiwakandamiza Waislam. Kablahajafa Abdulwahid alikuwa akifikiwa na habari kuwa kulikuwa na kampeniiliyokuwa ikiendeshwa kwa makini sana naWakristo ndani ya chama kuufuta Uislam ndani ya TANU. [1]Abdulwahid alikuwa anafahamu matokeo yakuvunjika kwa umoja wa Waislam. Yeye alikuwa anajua vyema nguvu ya umoja waWaislam wakati walipokuwa wanapigania uhuru wa Tanganyika. Abdulwahidhalikadhalika alikuwa anafahamu nguvu ya wale waliokuwa nyuma na njama zile zakuwagawa Waislam katika makundi hasimu. Vilevile alikuwa anatambua hofu na watuwote waliokuwa nyuma ya njama zile. Alifahamu kuwa wale aliowapokea na kuwatiakatika harakati za kudai uhuru sasa walikua na hofu na Uislam. Kama Uislamulitumika kuwaondoa wakoloni Uislam hautashindwa kuwatoa wao madarakani. Uislamikiwa itkadi ya kupinga ukoloni sasa ilikuwa ni tishio kwa Ukristo katikaTanzania huru."
Mohamed
Inna Lillahi wainna ilaihi rajihunnah