Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Yawezekana kwako nondo anazomwaga Mohamed zikawa si mchezo kama unavyodai lakini aache kudanganya Watanzania kuwa anaandika historia ya harakati za uhuru za Tanganyika. Hatungekuwa na ugomvi naye kama angekiri kuwa historia anayoiandika ni ya wazee wake wa Dar es Salaam na hasa eneo la Gerezani na katu si ya Tanganyika kama anavyodai.

Kati ya hao wazee wote anaowataja pamoja na kukoleza chumvi nyingi hakuna hata moja aliyeongoza chama cha siasa kilichopigania uhuru na kama walishiririki katika harakati za kudai haki za msingi na kupinga uonevu basi wako wengi tena waliotoa changamoto kubwa kuliko za kwao lakini hawatajwi inapofika kudai uhuhru kupitia chama cha siasa.

Chama cha TAA hakikua peke yake katika harakati hizi na tumejaribu kuorodhesha watu, vyama na vikundi mbalimbali vilivyowapa wakoloni changamoto nyingi tu kupitia kilichoitwa petitions kwa serikali ya kikoloni. Anapotaja wazee wake tena wa Dar es Salaam na kudai anaandika historia baada ya kufanya utafiti nchini Tanganyika anasema uwongo.

Mathalani mwulizeni kama anaijua iliyoitwa Meru Citizen Union na wapiganaji wake kama Munya Lengoroi, Gamaliel Sablak na kama amewahi kuwasikia kwa nini hawatajwi. Jibu jepesi linalopatikana ni kuwa hawa kwanza si wazee wake, pili hawakuzaliwa wala kuishi Gerezani na tatu si Waislaam. Udini ndio unamsukuma zaidi Mohamed Said katika maandishi yake karibu yote.

Mag3,

Kwa hakika najua habari za Meru Citizens Union. Nilizisoma katika Nyaraka za Sykes na habari za akina Sablak nimezieleza katika kitabu. hebu soma hii hapa chini. Nilifika hadi kwa Mzee Kirilo USA River wakati nafanya utafiti lakini bahati mbaya alikuwa kasafiri kenda Nairobi. Aliyenipeleka na Abdulwahid Ally Sykes ambae walikuwa wakifahamiana vyema.

"Baadaya Dr Kyaruzi kuhamishiwa Nzega nafasi ya rais ikawa wazi. Abdulwahid Sykesakakaimu nafasi hiyo na kuwa katibu na kaimu rais wa TAA. Katika uchaguzi wa mwakawa 1952, uliofanyika Arnautoglo Hall akiwa na umri wa miaka 28 Abdulwahidalichaguliwa kuwa rais wa chama cha TAA. Wakati ule mgogoro wa ardhi ya Wameru ulikuwaumekwishaanza lakini bado haujalipuka kuwa suala lililowahusu Watanganyikawote. Umoja wa Mataifa ulipotuma ujumbe wake wa pili kuzuru Tanganyika mwaka wa1950, Wameru waliwasilisha rasmi malalamiko yao kwa ujumbe huo. Abdulwahidaliwaomba wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria washirikiane na TAA katikakutatua baadhi ya matatizo yanayokabili jamii ya Waafrika. Abdulwahidalifadhaishwa na wajumbe Waafrika katika Baraza la Kutunga Sheria palewaliposhindwa kuipinga Wilson Report ambayo ilipendekeza kuondolewa kwawananchi wa Meru kutoka kwenye ardhi yao. Katika barua aliyoiandikia MeruCitizenís Union, Abdulwahid, kwa niaba ya makao makuu ya TAA, aliwahakikishiawatu wa Meru kuwa tatizo lao llilikuwa tatizo la Watanganyika wote. Abdulwahidaliamua kutumia mgogoro wa ardhi ya Wameru kuwaunganisha Watanganyika wotedhidi ya serikali ya kikoloni. Barua hizi kati ya Abdulwahid na viongozi waMeru Citizens's Union, Kirilo na Sablak walizoandikiana kati ya Septemba naDesemba 1952 zinatoa picha halisi ya jinsi hali ya siasa ilivyokuwa Tanganyika.(Barua hizi zinapatikana katika katika Nyaraka za Kirilo Tanzania NationalArchives (TNA), Dar es Salaam). Uamuziwa serikali juu ya mapendekezo ya TAA kwa Constitutional Development Committeeulikuwa bado umo akilini mwake. Alitambua kwamba uamuzi wa Gavana ulikuwa nimpango wa muda mrefu wa kuwadhalilisha Waafrika katika utumwa wa daima.Abdulwahid sasa akiwa na ghera kubwa alianza kufanya kazi ya kuwahamasisha watuwa Tanganyika chini ya vuguvugu la kuunganisha umma dhidi ya utawala waWaingereza. Abdulwahid aliwasiliana na Earle Seaton mjini Moshi kutaka ushauriwa kisheria juu ya tatizo la Meru. Seaton alikuja Dar es Salaam na kukutana naAbdulwahid na uongozi wa TAA. Ilikubaliwa na pande zote mbili kuwa makao makuuya TAA, Meru Citizenís Union ikiongozwa na Japhet Kirilo na Seaton lazimawaunganishe shughuli zao katika kesi hiyo na kwa pamoja watume rufaa yao kwenyeBaraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa huko New York. Kwa sasa uongozi wa chamacha TAA ulitambua kwamba nusura yao ilitegemea uwezo wao wa kudhibiti nakushawishi matukio na maamuzi ndani ya Baraza la Kutunga Sheria. Ili kuweza kufanya hayo shinikizo lilitakiwakuwekwa katika Baraza la Udhamini huko New York, nchini Amerika na siyo katikaOfisi ya Makoloni pale London Uiengereza. Katikamatawi ya TAA yaliyokuwa na nguvu sana Tanganyika mojawapo lilikuwa tawi laTabora. Tawi la chama cha TAA la Tabora lilichukua changamoto la Mgogoro waArdhi ya Wameru kwa ghera kubwa na kwa kupitia juhudi za Saadani Abdu Kandoro yeyealilibeba tatizo lile kama jukumu lake binafsi. Kandoro aliitisha mkutano wamatawi ya TAA ya Mwanza, Kigoma na Tabora kujadili suala hilo. Mwanzailiwakilishwa na Bhoke Munanka, Mzee Mkama Mlaji na Mohamed Kihaka Kitenge;kutoka Kigoma mjumbe aliyekuja alikuwa Jumanne Mawimbi na Tabora iliwakilishwana Sheikh Kinana, Kandoro na George Magembe kama rais wa TAA tawi laTabora. Mkutano wa Tabora uliahidimshikamano wa pamoja na watu wa Meru katika mapambano dhidi ya walowezi. Mgogorowa ardhi ya Meru ni wa pekee katika historia ya Tanganyika. Ilikuwa kupitiakatika mgogoro huo ndiyo Mtanganyika, Japhet Kirilo, akifuatana na Earle Seatonkama mkalimani na mshauri wa sheria wa TAA, kwa mara ya kwanza alizungumzambele ya Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa huko New York, na kuonyeshaudhalimu wa ukoloni. Waingerezawalikataa kumpa Kirilo pasi ya kusafiria kwenda Amerika na ikabidi Abdulwahidna uongozi wa TAA uingilie kati na mwishowe serikali ikatoa pasi. November, 1952 Kirilo alizungumza mbele yaKamati ya Nne ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York. Watu wa Tanganyikasasa walikuwa wanayachukua mapambano yao toka mipaka yao hadi kwenye kumbi zaUmoja wa Mataifa, mjini New York kutafuta haki. Lakini Kirilo alirudi mikonomitupu. Rufaa ya mgogoro wa ardhi ya Wameru ilitupiliwa mbali. Kiriloaliuhakikishia Umoja wa Mataifa kuwa watu wake kamwe hawatachukua silahakuikomboa ardhi yao kama Wakikuyu wa Kenya walivyojaribu kufanya. Kwa kwelihapakuwa na sababu ya kutoa kauli hii, kwa kuwa uhakikisho wa kutokuwepomapambano uliwafanya walowezi washushe pumzi na kujiona wako salama. Tangumwanzo wa mgogoro wazalendo nchini Kenya kama Fred Kubai na Kung'u Karumbawalikuwa wakitoa ushauri kwa Meru Citizenís Union kwa kuwa wao walikuwa naujuzi zaidi wa matatizo ya walowezi kuliko watu wa Tanganyika. Kwa mtazamo wajuu juu mtu anaweza kudhani kuwa TAA ilikuwa akipata kipigo kutoka sehemu zoteilipojaribu kujipenyeza. Kushindwa huku si kwa sababu TAA ilikuwa ina viongozidhaifu au ilikuwa haiuingwi mkono na umma. TAA ilikuwa haifanikiwi katika madaiyake kwa sababu serikali ya kikoloni ilikuwa imeamua kutosikiliza lolote kuhusumatatizo ya Waafrika. Matokeo ya hali hii iliifanya TAA Iamue kuwa njiailiyobakia ya Tanganyika kujitoa katika makucha ya Waingereza ni kuuandaa ummawa Tanganyika chini ya chama cha siasa. Maratu baada ya Kirilo kurejea kutoka New York, mpango wa kuanzisha chama cha siasacha kushirikisha umma wote ulianza kiongozi wa mpago huu alikuwa Abdulwahid Sykes na ile kamati ya siasandani ya TAA. Uongozi wa TAA Makao Makuuulianza kampeni ya nchi nzima kuueleza umma matokeo ya safari ya Kirilo Umojawa Mataifa kuhusu mgogoro wa ardhi ya Wameru na vilevile kuchangisha fedha zakupeleka msafara mwingine Umoja wa Mataifa kuueleza umoja huo kuwa Tanganyikailikuwa chini ya udhamini na Watanganyika walikuwa sasa na haki ya kudai uhuruwao. Kamati ya TAA ya watu watatu iliyowajumuisha Kandoro, Kirilo na AbbasSykes iliundwa kwa ajili hiyo. Ally Sykes akiwa mweka hazina msaidizi wa TAAchini ya John Rupia aliombwa ampelekee Kirilo hawala ya posta Usa River kamanauli ya kumwezesha kusafiri hadi Dodoma kujiunga na ile kamati ya watu watatu.Kulikuwa hakuna huduma ya fedha katika posta ya Usa River na fedha zile zilikaahapo kwa muda bila ya kuchukuliwa hadi hapo zilipopelekwa posta ya Arusha mjiniambako Kirilo alizichukua. Kuanziatarehe 26 Septemba, 1953 kwa takriban mwezi mmoja ile kamati ilitembelea nakuhutubia mikutano ya hadhara, ikikusanya fedha Dodoma, Mwanza, Bukoba,Ukerewe, Tarime, Musoma na Shinyanga. Rais wa chama cha TAA, kanda ya ziwa,Paul Bomani aliipokea ile kamati ya watu watatu na kuhutubia mikutano pamojanao katika jimbo lote. Bomani aliwaambia wanachama wa TAA na wananchi wotemjini Mwanza kuhusu umuhimu wa kuchanga fedha kwa kwa kusudio hilo. TAA iliunda sekretarieti ya kudumu katika ofisi ya NewStreet kushughulikia kazi za kila siku za chama.KIjana mmoja aliyejulikana kamaAlexander Tobias aliajiriwa kama mfanyakazi wa kwanza wa TAA. Kwa bahati mbayasana Alexander Tobias aliisaliti TAA kwaWaingereza."

Mohamed


 
Shehe Said naomba uyarejee hayo maswali mawili kuhusu Aga Khan na Tanganyika/Tanzania maana yanahusiana nakundwa kwa EAMWS.
 

Mwisho nakushauri huko usoni usitumie neno "muongo" sema "hasemi kweli" kauli
zako zitaonekana za kiungwana.

Huenda hufahamu lakini ukimwita mtu "muongo" unamfedhehesha ni neno zito.

Mohamed
Ni kweli, lakini nimejibu post kama ilivyochangiwa na FaizaFox. Ndiye aliyetumia neno muongo bila kukemewa nikajua ni la kawaida.
 
[TABLE="width: 100%, align: left"]
[TR]
[TD="class: kaziBody"]By ALVAR MWAKYUSA, 20th October 2011 DAILY NEWS

The two leaders showered praise on the varsity for producing professionals who have played significant leadership roles in their countries.

They made the remarks when addressing delegates in Dar es Salaam on Thursday at the climax of the 50th anniversary of the university.

"I acknowledge the role played by UDSM in training key personnel for other countries in the East African region. A number of experts and graduates from this university have been recognized regionally and internationally," Mr Kikwete said.

His remarks were supported by President Museveni who mentioned some high-ranking people from his country, including himself, as graduates of the renowned university 'Hill'.

Mr Museveni mentioned former East African Community (EAC) Secretary General, Mr Amanya Mushenga, Uganda's Chief Justice Mr Benjamin Odoki as well as his wife who is also the Minister for Karamoja Affairs, Ms Janet Museveni.

"On the list of great people who studied here at the Hill, is Dr John Garang, the late Vice-President of Sudan," he noted.

Mr Museveni said most veteran lawyers in his country were trained at UDSM.


The Ugandan leader also spoke highly of Father of the Nation Mwalimu Julius Nyerere, for establishing a higher learning institution at a time when the region needed educated people.

Mr Museveni, who has been collecting funds in his country for the construction of a students' centre at UDSM, pledged to hand over the contribution to the varsity's authorities.


Meanwhile, the Father of the Nation, the late Mwalimu Nyerere, was among six people who were recognized for their contribution in setting up the university.

Others are Prof Robert Pratt, who was the first Principal of the then University College Dar es Salaam, Chief George Kunambi, who played a crucial role in locating the current site of UDSM.

Others are Justice Julie Manning (Rtd), the first and lone female student at inception, Dr Wilbard Chagula, the first indigenous Principal and Prof Arthur Weston who was the Dean of Law at the inception.

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: kaziBody"][TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TD] My take: Rais Kikwete na Museveni wanasema kuwa UDSM imesaidia kutoa wahaitimu katika ukanda wa Afrika mashariki. Ninahakika aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kenya bw. Kivuitu naye pia ni mhitimu wa hapo.Watu wanaposema kuna nafasi za upendeleo ili kuminya waislam, mbona 'trend' inaonekana kuvuka mipaka?

Lakini kilichonisukuma zaidi kuleta hii habari ni hiyo kauli ya kwamba aliye locate eneo la ujenzi ni George Kunambi kwa mujibu wa UDSM
Mohamed Said anasema ni (Sykes au Dossa sikumbuki vema) aliye muonyesha mwalimu eneo hilo akimpeleka Pugu. Hapa pia historia inatakiwa kurekebishwa! ili tujue ukweli

Ufafanuzi mzee Said.

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Ni kweli, lakini nimejibu post kama ilivyochangiwa na FaizaFox. Ndiye aliyetumia neno muongo bila kukemewa nikajua ni la kawaida.

Ukisoma vizuri utakuta FaizaFoxy alitumia neno muongo kumjibu aliyelisema neno hilo. Usitake kupindisha maneno, yatakushinda.
 
Nilidhani tunaandikia wino. Haya maneno ya nani, Bibie?
maana mwenzako kaandika kuhusu TANU lakini hakuandika walioianzisha yeye kamtaja Nyerere tu kama vile ni mali ya Nyerere na si chama halafu karukia ANC kamtaj

Sasa hapo umeelewa nini? ni wazi kabisa hayo maneno "kaandika kuhusu TANU lakini hakuandika kuhusu walioianzisha" au na hilo ni tatizo kwako kulielewa?

"He/she wrote about TANU but he/she did not write about those who founded it..." maana naona kiswahili kinakupa taabu kuelewa.
 
Kitu kimoja nilicho na hakika nacho kwa asilimia 100% ni kwamba wale wote wenye mapenzi ya kweli kwa taifa letu la Tanzania wanasita sana kuchangia hii hoja inayofinyangwafinyangwa na huyu anayejiita Mohamed Said. Bila kumung'unya maneno nayaita madai ya Mohamed Said la kutoa elimu ya historia ya kweli ni porojo hatari iliyojaa uchochezi ambayo lengo lake hasa ni kuleta uhasama wa kidini miongoni mwa wananchi. Sijui anachotegemea kufaidika nacho kwa kupanda hii mbegu ya hatari ambayo nina hakika mtu kama Mohamed Said anajua fika madhara yake.

Mohamed Said ni kama kipofu ambaye baada ya kusimuliwa na wazee kwamba tembo ni mnyama mkubwa kuliko wanyama wengi anapata nafasi ya kumpapasa tembo. Kwa bahati mbaya anaupapasa mguu wa tembo na si mwili wote halafu katika imani yake anadai anao uwezo wa kutoa somo kuhusu umbo la mnyama tembo na ushuhuda wake, kuwa tembo ni kama gogo la mti mkubwa, ndio ukweli na anayesema tofauti hajui kitu. Watu wote wanaolalamikiwa na Mohamed Said kuwa walisahauliwa, wengi wao walikuwa wakazi wa Dar es Salaam eneo la Gerezani.
Mkuu Mag3, heshima kwako.
Huyu Mohammed Said ana pepo la chuki.
Watu wa aina yake fuatilia sana , wamesoma sana, lakini hawajui kitu kinaitwa maendeleo, kazi kukaa vibarazani, kunywa kahawa na kucheza bao.
Ana lalama sana juu ya uhuru wa Tanganyika utafikiri sie tulikombolewa na mababu zake tu , tena waislamu na si wengine.
Zaidi ya kulalalama hakuna mawazo ya ziada.
Ni kawaida yao watu wa itikadi yake, lakini mpango huu lazima unaasisiwa mahali na Mohammed Said ni mdomo wa jipu tu!
 
Mkuu Mag3, heshima kwako.
Huyu Mohammed Said ana pepo la chuki.
Watu wa aina yake fuatilia sana , wamesoma sana, lakini hawajui kitu kinaitwa maendeleo, kazi kukaa vibarazani, kunywa kahawa na kucheza bao.
Ana lalama sana juu ya uhuru wa Tanganyika utafikiri sie tulikombolewa na mababu zake tu , tena waislamu na si wengine.
Zaidi ya kulalalama hakuna mawazo ya ziada.
Ni kawaida yao watu wa itikadi yake, lakini mpango huu lazima unaasisiwa mahali na Mohammed Said ni mdomo wa jipu tu!

Kama huna hoja kaa pembeni, wengine tunapata elimu hapa...

Niliwahi kuzungumza na Mzee Martin Shikuku wa Kenya, akanieleza mambo mengi kuhusu Tanzania mpaka nikajishangaa kama kweli ninaifahamu nchi yangu na yatokanayo, habari hizi ni muhimu sana kwa wapendao ufahamu.
 
Kama huna hoja kaa pembeni, wengine tunapata elimu hapa...

Niliwahi kuzungumza na Mzee Martin Shikuku wa Kenya, akanieleza mambo mengi kuhusu Tanzania mpaka nikajishangaa kama kweli ninaifahamu nchi yangu na yatokanayo, habari hizi ni muhimu sana kwa wapendao ufahamu.

Butola,
Inawezekana Marti Shikuku anaifahamu historia ya harakati za uhuru wa Tanganyika kuliko wazalendo wa Tanganyika waliopigania uhuru wao!?

Na yeye ni miongoni mwa wakenya waliokuwa nchini Tanganyika wakati wa harakati za kudai uhuru? Kama ndiyo, alikuwa na role gani?
 
Kama huna hoja kaa pembeni, wengine tunapata elimu hapa...

Niliwahi kuzungumza na Mzee Martin Shikuku wa Kenya, akanieleza mambo mengi kuhusu Tanzania mpaka nikajishangaa kama kweli ninaifahamu nchi yangu na yatokanayo, habari hizi ni muhimu sana kwa wapendao ufahamu.
Tatizo wengi wenu ni watoto, pumba na mapuya yote mnameza wala hamchuji.
Wengine historia mnayosikia ikihadithiwa tuliishi.
 
Hii thread is one of my best have JF in recent years. INAFUNDISHA NA INATOA CHANGAMOTO. Nimejifunza na naendelea kujifunza sana kwa Mag3, Nguruvi, na muungwana Mohamed.

Ushauri wangu, kwa wananchi wenzangu, kamwe hatuwezi kuwa na mijadala endelevu kama hatutavua imani ya dini zetu. Kinachotukwamisha ni hiki. Tujitahidi sana kuheshimiana na tutafute suluhisho la matatizo yetu kama taifa. Umeme ukikosekana anayeathirika ni Hamisi, Said, Mwajuma, Peter, Selina nk. Tujitahidi sana kuepuka hizi emotions za udini. Siku zote nilisema kuna watu walicheza karata ya udini kwa maslahi binafsi lakini kwa uhakika walifungulia pandora`s box maana hawataweza kuuzima. In anycase it is by fate that we are a nation. Kwamba iko Siku TANZANIA inaweza kuwa nchi ya kiislam wote tukavaa kanzu. Never. Forget. Kwamba iko siku wote wataimba mapambio kanisani ya kilokole. Never. Forget it. Kikubwa tujifunze kuthaminiana na ku-celebrate tofauti zetu. Tutafute suluhisho la matatizo ya taifa letu. Kwa yeyote yule anayetaka historia imkumbuke hajachelewa bado. Tanzania kama taifa bado tunachangamoto nyingi sana. Toa mchango wako. WANANCHI tutauuona na tutakuenzi.

Swali kubwa kwetu naomba lisiwe nani alipigania uhuru. Bali tujiulize, kwa nini tulipigania uhuru? na tulipoupata tuliufanyia nini huo uhuru? je huo uhuru umetuletea nini? Mjadala kama huu ni mzuri usipokuwa na sentiments za kidini na kiimani.

Naamini kabisa taifa letu liko katika critical period na ni wasomi kama sisi wenye jukumu la kutafuta majibu ya matatizo yetu kwa kutumia elimu yetu kuliko kujenga chuki na na uhasama. Its unfortunate hizi chuki wengi wetu tunazijenga kwa maslahi binafsi. Sioni logic iko wapi ukafanye PhD Cambridge au kwingineko..halafu uje kuhubiri hapa watu wasome madrasa au mambo ya dini tuu. Its really a tragic. And this goes way far to show how the lites manipulates the poor for their own ends.

Ushauri wangu: tuwekeze katika elimu na mambo mengineyo yanayojenga ustawi wa binadamu. Yes, Iamni ni jambo muhimu sana, lakini tujitahidi kadri tuwezavyo kuwaachia wananchi/waumini wenyewe waamue ni jinsi gani ya kuabudu. Hii ya kujifanya kwamba we know what is good for entire 'we' si jambo la busara. Na ndo maana muungwana mmoja kasema hapo juu..nenda huko ulaya na America..watoto wa hao hao masultani na wafalme wanaolinda msikiti wa Mecca wanasoma top schools za ulimwengu wa leo..Harvard, Oxford, Yale, Princeton, Imperial, LSE, nk...na ndo kesho wanaenda kuwatawala wananchi wao....jamani imani ni muhimu lakini we shouldnt collectivise it. Kila mtu apewe uhuru wa kuwa yeye.

Watanzania tuamke, matatizo tuliyonayo ni mengi mno, dini inabidi liwe swala la mwisho kutufarakanisha.
 
Tatizo wengi wenu ni watoto, pumba na mapuya yote mnameza wala hamchuji.
Wengine historia mnayosikia ikihadithiwa tuliishi.

Ikifika wakati mtu akaona hana haja ya kujifunza/kusikia/kufanya tena vitu vipya then hana sababu tena ya kuendelea kuishi..

By the way,nategemea kupata vitu mlivyoviishi kwa hoja mkuu wangu sana Majoja, hii ndio elimu ninayoihitaji hapa hasa kutoka kwenu.
 
--------
Sasa hapo umeelewa nini? ni wazi kabisa hayo maneno "kaandika kuhusu TANU lakini hakuandika kuhusu walioianzisha" au na hilo ni tatizo kwako kulielewa?

"He/she wrote about TANU but he/she did not write about those who founded it..." maana naona kiswahili ----n-akupa taabu kuele-

[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TD]FF nimekuwekea hapa maana kunakohusika nime-pata shida niwie radhi.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]"Salum Matimbwa anaingia katika historia ya ukombozi wa Tanganyika si tu kama mwanachama wa awali waliojiunga na TANU kabla ya 1958 bali kama mmoja wa wazalendo waliochanga fedha kuanzisha Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Fikrra ya kuanzisha Chuo Kikuu inasemekana ilianza na Nyerere akiwa na Dossa. Ilkuwa kawaida ya Dossa baada ya mikutano ya TANU pale Mnazi Mmoja kumchukua Nyerere na gari lake kumrudisha Pugu. Njia ya zamani kwenda Pugu ilikuwa inapita hapo kilipo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Sasa ilikuwa kiza kimeingia na walitaka kutoka nje ya gari kuangalia mandhari ya Dar es Salaam maana kutokea pale mji ulikuwa unapendeza sana kwa taa zilizokuwa zikiwaka barabarani. Nyerere alimwambia Dossa, "Dossa tukipata uhuru wetu hapa lazima tujenge Chuo Kikuu."Hili wazo lilifanyiwa kazi na wananchi wakahamasishwa kuchangia ujenzi wa Chuo hicho. Fedha zilichangwa na Chuo kikajengwa pale New Street kwenye kiwanja cha John Rupia alichokitoa kuwapa TANU. Hapo ndipo kilipoanza Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. (Chuo hiki sasa ni Chuo Cha Watu Wazima).Abdallah Salum alikuwa mmoja wa wachangiaji wa chuo hicho na mwanae Salum Matimbwa hadi leo amehifadhi stakabadhi ya malipo y ash. 50.00 stakabadhi ambayo ina saini ya Bhoke Munanka."

Mohamed

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Butola,
Inawezekana Marti Shikuku anaifahamu historia ya harakati za uhuru wa Tanganyika kuliko wazalendo wa Tanganyika waliopigania uhuru wao!?

Na yeye ni miongoni mwa wakenya waliokuwa nchini Tanganyika wakati wa harakati za kudai uhuru? Kama ndiyo, alikuwa na role gani?

Sidhani kama nimesema hivyo.

Ila itoshe tu kusema nchi hii kama zilivyo nchi zingine ina historia pana na ina mengi sana yasiyo wazi kwa wengi, kwa sie tunaopenda kujifunza ni afya kwetu kupata vingi iwezekanavyo.
 
Unanchekesha, huko Scotland hujui wanachovaa?

Mag3 ndio jina lako? Unanchekesha, jibu na mengine, mbona umerukia hilo tu? Kama hujibizani na Mohamed Said utafikia kumtukana kuwa ni "mpuuzi" na kumuita "muongo"? Unasema hujibishani na MS...

Ikiwa mtu kaongea na Ali Sykes ana kwa ana na Ali Sykes ndio alioisaini kadi ya TANU ya Nyerere hivi kweli unataka kutuambia hiyo sio "direct source"? Unanchekesha!

Uandishi wako huwa unanchekesha, "mulitiple contradictions". Hebu tazama nilipoweka nyekundu. Punguza jazba, ukitaka raha ya mjadala uliza moja moja ujibiwe, na unaposema "si kweli" inapaswa uuweke...

Na hao wote waliomzunguka hawajui fashion, aijuwae fashion mwenye kaptura tu? Unanchekesha

Endeleeni kutupa elimu maana kuna mengi tunayojifunza hapa ila pia punguzeni "Kumchekesha" huyu bibi maana anaharibu radha ya majadiliano hapa kwa kupost jinsi "anavyochekeshwa-chekeshwa"
 
Endeleeni kutupa elimu maana kuna mengi tunayojifunza hapa ila pia punguzeni "Kumchekesha" huyu bibi maana anaharibu radha ya majadiliano hapa kwa kupost jinsi "anavyochekeshwa-chekeshwa"

Kwenye nyekundu ungeandika "ladha". Unanchekesha.
 
Back
Top Bottom