Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Yawezekana kwako nondo anazomwaga Mohamed zikawa si mchezo kama unavyodai lakini aache kudanganya Watanzania kuwa anaandika historia ya harakati za uhuru za Tanganyika. Hatungekuwa na ugomvi naye kama angekiri kuwa historia anayoiandika ni ya wazee wake wa Dar es Salaam na hasa eneo la Gerezani na katu si ya Tanganyika kama anavyodai.
Kati ya hao wazee wote anaowataja pamoja na kukoleza chumvi nyingi hakuna hata moja aliyeongoza chama cha siasa kilichopigania uhuru na kama walishiririki katika harakati za kudai haki za msingi na kupinga uonevu basi wako wengi tena waliotoa changamoto kubwa kuliko za kwao lakini hawatajwi inapofika kudai uhuhru kupitia chama cha siasa.
Chama cha TAA hakikua peke yake katika harakati hizi na tumejaribu kuorodhesha watu, vyama na vikundi mbalimbali vilivyowapa wakoloni changamoto nyingi tu kupitia kilichoitwa petitions kwa serikali ya kikoloni. Anapotaja wazee wake tena wa Dar es Salaam na kudai anaandika historia baada ya kufanya utafiti nchini Tanganyika anasema uwongo.
Mathalani mwulizeni kama anaijua iliyoitwa Meru Citizen Union na wapiganaji wake kama Munya Lengoroi, Gamaliel Sablak na kama amewahi kuwasikia kwa nini hawatajwi. Jibu jepesi linalopatikana ni kuwa hawa kwanza si wazee wake, pili hawakuzaliwa wala kuishi Gerezani na tatu si Waislaam. Udini ndio unamsukuma zaidi Mohamed Said katika maandishi yake karibu yote.
Mag3,
Kwa hakika najua habari za Meru Citizens Union. Nilizisoma katika Nyaraka za Sykes na habari za akina Sablak nimezieleza katika kitabu. hebu soma hii hapa chini. Nilifika hadi kwa Mzee Kirilo USA River wakati nafanya utafiti lakini bahati mbaya alikuwa kasafiri kenda Nairobi. Aliyenipeleka na Abdulwahid Ally Sykes ambae walikuwa wakifahamiana vyema.
"Baadaya Dr Kyaruzi kuhamishiwa Nzega nafasi ya rais ikawa wazi. Abdulwahid Sykesakakaimu nafasi hiyo na kuwa katibu na kaimu rais wa TAA. Katika uchaguzi wa mwakawa 1952, uliofanyika Arnautoglo Hall akiwa na umri wa miaka 28 Abdulwahidalichaguliwa kuwa rais wa chama cha TAA. Wakati ule mgogoro wa ardhi ya Wameru ulikuwaumekwishaanza lakini bado haujalipuka kuwa suala lililowahusu Watanganyikawote. Umoja wa Mataifa ulipotuma ujumbe wake wa pili kuzuru Tanganyika mwaka wa1950, Wameru waliwasilisha rasmi malalamiko yao kwa ujumbe huo. Abdulwahidaliwaomba wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria washirikiane na TAA katikakutatua baadhi ya matatizo yanayokabili jamii ya Waafrika. Abdulwahidalifadhaishwa na wajumbe Waafrika katika Baraza la Kutunga Sheria palewaliposhindwa kuipinga Wilson Report ambayo ilipendekeza kuondolewa kwawananchi wa Meru kutoka kwenye ardhi yao. Katika barua aliyoiandikia MeruCitizenís Union, Abdulwahid, kwa niaba ya makao makuu ya TAA, aliwahakikishiawatu wa Meru kuwa tatizo lao llilikuwa tatizo la Watanganyika wote. Abdulwahidaliamua kutumia mgogoro wa ardhi ya Wameru kuwaunganisha Watanganyika wotedhidi ya serikali ya kikoloni. Barua hizi kati ya Abdulwahid na viongozi waMeru Citizens's Union, Kirilo na Sablak walizoandikiana kati ya Septemba naDesemba 1952 zinatoa picha halisi ya jinsi hali ya siasa ilivyokuwa Tanganyika.(Barua hizi zinapatikana katika katika Nyaraka za Kirilo Tanzania NationalArchives (TNA), Dar es Salaam). Uamuziwa serikali juu ya mapendekezo ya TAA kwa Constitutional Development Committeeulikuwa bado umo akilini mwake. Alitambua kwamba uamuzi wa Gavana ulikuwa nimpango wa muda mrefu wa kuwadhalilisha Waafrika katika utumwa wa daima.Abdulwahid sasa akiwa na ghera kubwa alianza kufanya kazi ya kuwahamasisha watuwa Tanganyika chini ya vuguvugu la kuunganisha umma dhidi ya utawala waWaingereza. Abdulwahid aliwasiliana na Earle Seaton mjini Moshi kutaka ushauriwa kisheria juu ya tatizo la Meru. Seaton alikuja Dar es Salaam na kukutana naAbdulwahid na uongozi wa TAA. Ilikubaliwa na pande zote mbili kuwa makao makuuya TAA, Meru Citizenís Union ikiongozwa na Japhet Kirilo na Seaton lazimawaunganishe shughuli zao katika kesi hiyo na kwa pamoja watume rufaa yao kwenyeBaraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa huko New York. Kwa sasa uongozi wa chamacha TAA ulitambua kwamba nusura yao ilitegemea uwezo wao wa kudhibiti nakushawishi matukio na maamuzi ndani ya Baraza la Kutunga Sheria. Ili kuweza kufanya hayo shinikizo lilitakiwakuwekwa katika Baraza la Udhamini huko New York, nchini Amerika na siyo katikaOfisi ya Makoloni pale London Uiengereza. Katikamatawi ya TAA yaliyokuwa na nguvu sana Tanganyika mojawapo lilikuwa tawi laTabora. Tawi la chama cha TAA la Tabora lilichukua changamoto la Mgogoro waArdhi ya Wameru kwa ghera kubwa na kwa kupitia juhudi za Saadani Abdu Kandoro yeyealilibeba tatizo lile kama jukumu lake binafsi. Kandoro aliitisha mkutano wamatawi ya TAA ya Mwanza, Kigoma na Tabora kujadili suala hilo. Mwanzailiwakilishwa na Bhoke Munanka, Mzee Mkama Mlaji na Mohamed Kihaka Kitenge;kutoka Kigoma mjumbe aliyekuja alikuwa Jumanne Mawimbi na Tabora iliwakilishwana Sheikh Kinana, Kandoro na George Magembe kama rais wa TAA tawi laTabora. Mkutano wa Tabora uliahidimshikamano wa pamoja na watu wa Meru katika mapambano dhidi ya walowezi. Mgogorowa ardhi ya Meru ni wa pekee katika historia ya Tanganyika. Ilikuwa kupitiakatika mgogoro huo ndiyo Mtanganyika, Japhet Kirilo, akifuatana na Earle Seatonkama mkalimani na mshauri wa sheria wa TAA, kwa mara ya kwanza alizungumzambele ya Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa huko New York, na kuonyeshaudhalimu wa ukoloni. Waingerezawalikataa kumpa Kirilo pasi ya kusafiria kwenda Amerika na ikabidi Abdulwahidna uongozi wa TAA uingilie kati na mwishowe serikali ikatoa pasi. November, 1952 Kirilo alizungumza mbele yaKamati ya Nne ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York. Watu wa Tanganyikasasa walikuwa wanayachukua mapambano yao toka mipaka yao hadi kwenye kumbi zaUmoja wa Mataifa, mjini New York kutafuta haki. Lakini Kirilo alirudi mikonomitupu. Rufaa ya mgogoro wa ardhi ya Wameru ilitupiliwa mbali. Kiriloaliuhakikishia Umoja wa Mataifa kuwa watu wake kamwe hawatachukua silahakuikomboa ardhi yao kama Wakikuyu wa Kenya walivyojaribu kufanya. Kwa kwelihapakuwa na sababu ya kutoa kauli hii, kwa kuwa uhakikisho wa kutokuwepomapambano uliwafanya walowezi washushe pumzi na kujiona wako salama. Tangumwanzo wa mgogoro wazalendo nchini Kenya kama Fred Kubai na Kung'u Karumbawalikuwa wakitoa ushauri kwa Meru Citizenís Union kwa kuwa wao walikuwa naujuzi zaidi wa matatizo ya walowezi kuliko watu wa Tanganyika. Kwa mtazamo wajuu juu mtu anaweza kudhani kuwa TAA ilikuwa akipata kipigo kutoka sehemu zoteilipojaribu kujipenyeza. Kushindwa huku si kwa sababu TAA ilikuwa ina viongozidhaifu au ilikuwa haiuingwi mkono na umma. TAA ilikuwa haifanikiwi katika madaiyake kwa sababu serikali ya kikoloni ilikuwa imeamua kutosikiliza lolote kuhusumatatizo ya Waafrika. Matokeo ya hali hii iliifanya TAA Iamue kuwa njiailiyobakia ya Tanganyika kujitoa katika makucha ya Waingereza ni kuuandaa ummawa Tanganyika chini ya chama cha siasa. Maratu baada ya Kirilo kurejea kutoka New York, mpango wa kuanzisha chama cha siasacha kushirikisha umma wote ulianza kiongozi wa mpago huu alikuwa Abdulwahid Sykes na ile kamati ya siasandani ya TAA. Uongozi wa TAA Makao Makuuulianza kampeni ya nchi nzima kuueleza umma matokeo ya safari ya Kirilo Umojawa Mataifa kuhusu mgogoro wa ardhi ya Wameru na vilevile kuchangisha fedha zakupeleka msafara mwingine Umoja wa Mataifa kuueleza umoja huo kuwa Tanganyikailikuwa chini ya udhamini na Watanganyika walikuwa sasa na haki ya kudai uhuruwao. Kamati ya TAA ya watu watatu iliyowajumuisha Kandoro, Kirilo na AbbasSykes iliundwa kwa ajili hiyo. Ally Sykes akiwa mweka hazina msaidizi wa TAAchini ya John Rupia aliombwa ampelekee Kirilo hawala ya posta Usa River kamanauli ya kumwezesha kusafiri hadi Dodoma kujiunga na ile kamati ya watu watatu.Kulikuwa hakuna huduma ya fedha katika posta ya Usa River na fedha zile zilikaahapo kwa muda bila ya kuchukuliwa hadi hapo zilipopelekwa posta ya Arusha mjiniambako Kirilo alizichukua. Kuanziatarehe 26 Septemba, 1953 kwa takriban mwezi mmoja ile kamati ilitembelea nakuhutubia mikutano ya hadhara, ikikusanya fedha Dodoma, Mwanza, Bukoba,Ukerewe, Tarime, Musoma na Shinyanga. Rais wa chama cha TAA, kanda ya ziwa,Paul Bomani aliipokea ile kamati ya watu watatu na kuhutubia mikutano pamojanao katika jimbo lote. Bomani aliwaambia wanachama wa TAA na wananchi wotemjini Mwanza kuhusu umuhimu wa kuchanga fedha kwa kwa kusudio hilo. TAA iliunda sekretarieti ya kudumu katika ofisi ya NewStreet kushughulikia kazi za kila siku za chama.KIjana mmoja aliyejulikana kamaAlexander Tobias aliajiriwa kama mfanyakazi wa kwanza wa TAA. Kwa bahati mbayasana Alexander Tobias aliisaliti TAA kwaWaingereza."
Mohamed