WC,
Inaelekea husemi kweli. Ungesoma kitabu changu ungekutana na "Muslim symbols" nyingi ndani lau kama TANU ilifuata "a nationalist secularist ideology." Soma hii:
"Kwa ajili ya wasiwasi huu, viongozi waTANU wa Tanga walimuomba Nyerere wawe pamoja ili ifanywe tawaswil waombe msaadawa Allah awape ushindi dhidi yaa vitimbi vya Waingereza. Maili tatu kutoka Tanga kipo kijiji chaMnyanjani ambako kulikuwako na tawi la TANU lililokuwa na nguvu sanalikiongozwa na Mmaka Omari kama mwenyekiti na Akida Boramimi bin Dai akiwakatibu. Mmaka alikuwa kijana aliyekuwa akiendesha mgahawa pale kijijini naAkida bin Dai alikuwa mwashi. Akida aliongoza tawi la vijana wa TANU ambalobaadae lilikuja kujulikana kama Tanga Volunteer Corps (TVC). TVC ilikuwasawasawa na Bantu Group, ambayo wakati huo ilikuwa imekwishaanzishwa huko Dares Salaam na Tabora. Vikundi hivi mbali na kufanya shughuli za propaganda nakuhamasisha wananchi halikadhalika viliifanyia TANU ujasusi. Nyerere naKissenge walichukuliwa hadi Mnyanjani na tawaswil ikasomwa. Waliohudhuriakisomo hicho walikuwa Abdallah RashidSembe, Sheikh Dhikr bin Said, Mzee Zonga, Hemed Anzwan, Salehe Kibwanaaliyekuwa mshairi maarufu, Akida Boramimi bin Dai na Mmaka Omari.Aliyechaguliwa kusoma Quran Tukufu alikuwa mjomba wa Mwalimu Kihere, Sheikh AliKombora."
Nakuongeza na hii nyingine:
"Lakini matukio mawili ya kumbukumbu kubwayalikuwa katika safari ya pili ya Nyerere alipozuru tena Jimbo la Kusini.Kumbukumbu ya kwanza ilikuwa tawaswil aliyosomewa Nyerere na Sheikh Yusuf Badimwenyewe pamoja na Waislam aliowachagua yeye sheikh mwenyewe maalum kwa haflahiyo, pamoja na waliochaguliwa na masheikh wengine.[1] Kumbukumbu ya pili ni ilekaramu iliyoandaliwa kwa heshima yaNyerere na Mussa Athumani Lukundu, kiongozi wa Dockworkersí Union. Hii ilikuwaheshima kubwa aliyoonyeshwa Nyerere, ilikuwa kilele cha upendo na heshima kwaMuislamu yoyote anaweza kumfanyia asiyekuwa Muislamu.Siku ya ukumbusho mkubwa sana mjini Lindiilikuwa siku ya uhuru, tarehe 9 Desemba, 1961. Sheikh Badi, bingwa wa mashairi,aliombwa na TANU kuandika hotuba ya uhuru itakayotolewa na Yusuf Chembera mbeleya DC akiwa kama mwakilishi wa utawala wa Kiingereza uliokuwa ukingíoka. Hotubahiyo ya Sheikh Badi na iliandikwa kwa Kiarabu na Chembera. Akiwa mtoto mdogoChembera alipelekwa kwa Sheikh Yusuf Badi na baba yake kwenda kusoma elimu yadini na aliendelea kuwapo hapo chuoni kwa Sheikh Badi hadi alipohitimu. SheikhBadi hakuona kama ipo hotuba yoyote iliyoandikwa na mwanadamu iliyostahikihafla kama ile ya siku ya kujikomboa kutoka minyororo ya ukoloni. Sheikh Badialimsomea mwanafunzi wake Chembera, dua ya kunut ambayo husomwa na Waislamkatika kila sala ya alfajir. Usiku wa manane wa tarehe 9 Desemba, 1961 ulikuwausiku adhim sana kwa wote wawili, mwalimu na mwanafunzi wake, pale watuwalipokusanyika katika ule uwanja wa gofu na kumsikiliza Chembera akisoma kunutkupokea uhuru wa Tanganyika. Lakini mara tu baada ya uhuru Wakristo walianzakuuchimba ule waliouona kuwa uongozi wa Waislam katika TANU kwa kisingizio kuwauongozi ule haukuwa na elimu. Suleiman Masudi Mnonji alikamatwa na kutiwakizuizini kwa amri ya Nyerere chini ya Preventive Detention Act ya mwaka 1962kwa kile kilichoitwa ëkuchanganya dini na siasaí na Waislam wengine waanzilishiwa harakati za kudai uhuru walitupwa nje ya uongozi."
Na hii ya kuhitimisha:"Katika mikutano ya TANU katika zile sikuza mwanzo, kabla Nyerere au Bibi Titi kuhutubia umma, Sheikh Suleiman Takadiralikuwa akisimama na kuomba dua. Kwa kawaida alikuwa akisoma ghaibu SuratFatihah, sura ya kwanza katika Qurían Tukufu: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi waRehema, Mwenye Kurehemu. Kila sifa njema ni milki yake Mwenyezi Mungu, Mola waUlimwengu wote. Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu. Mfalme wa siku ya Hukumu.Wewe tu ndiyo tunayekuabudu na wewe tu ndiyo tunakuomba msaada. Tuongoze katikanjia iliyonyooka, njia ambayo umewaongoza wale uliowaneemesha, si ya waleuliowaghadhibikia wala ya wale waliopotea."Hii ni dua ambayo kwa kawaida husomwa naWaislam kabla ya kuanza jambo lolote la kheri. Wakati Sheikh Takadir akisomadua hii watu walikuwa wima mikono yao juu wakimshukuru Allah. Baada ya hapoNyerere au Bibi Titi, kutegemea na ujumbe maalum uliotaka kutolewa katika sikuhiyo, alikuwa akisimama na kuhutubia.
Mohamed