Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

MM,

Umetoa uchambuzi mzuri pasi kifani.

Sasa cha kustaajabisha ni fitna gani iliingia kati ya Nyerere na watu hawa ikaja hata hataki kuwasikia wakitajwa katika historia ya TANU na wengine akawaweka kizuizini?

Karibu tutafikia kilele cha Tanzania Miaka 50 mashujaa hawa walopigania uhuru wa Tanganyika bega kwa bega na Nyerere wataenziwa?

Mohamed
Hivi ni Nyerere aliyeamrisha hawa mashujaa wasitajwe kwenye historia? Una ushahidi gani kwamba Nyerere hakutaka kuwasikia wakitajwa au ni dhana tu?
 
Mohamed!
Hapo kwenye blue, ni chanzo kimojawapo cha hoja zetu zinazoelekezwa kwako pamoja na wafuasi wako.

Je, wale ambao hawakutajwa katika historia ya TANU, pamoja na waliowekwa kizuizuini, walikuwa waislam tu? This is a one million dollar question.

Ni kwanini kila baya wakitendewa watu kwa ujumla wao, tuanze tena ku-single out Waislam pekee na kuwa wametendewa mabaya kwa sababu ya dini yao?

Mimi na wewe tunatimuliwa vumbi barabarani, wote tunakereka, lakini wewe unaanza kudai kuwa umetimuliwa vumbi kwa sababu ya dini yako eti kwa sababu tu yule aliyetimua vumbi yupo dini moja na mimi. Hii inakuja kweli?

Watoto wetu wanakosa nafasi ya kwenda chuo kikuu, wewe unasema ni kwa sababu ya dini yako, unasahau kuwa hata mimi wa dini tofauti na wewe, mtoto wangu kanyimwa nafasi hiyo hiyo.

Kwenye baadhi ya posts zako umeonesha wazi kuwa kuna watu wanaogopa uislam na ndio sababu ya "kupindisha" historia. Unaonesha kuwa kuna wamakonde walienda Zanzibar kusaidia mapinduzi, yote hiyo ili kuvunja uislam kwa vile uislam unaogopwa...
Hivi hao wamakonde hawakuwa waislam?

Na je hii dhana ya kwamba uislam unaogopwa mnaipata wapi?
Hata hapa jamvini kuna wafuasi wako wanafikiri eti majina ya kiislam yanatutisha.. Ha ha ha.
Uislam una nini mpaka ututishe?

Mbona ni dini tu ambayo hata miaka ya nyuma iliweza kuenea kwa amani tu (ukiondoa Nyakati za Jihad).
Hata hivyo naweza kuelewa kwa nyakati za sasa, kama kuna watu wanaogopa hiyo dini, kwa vile magaidi wengi wamesingizia uislam. Na kama ni suala la ugaidi, hata kuna waislam wanauogopa pia. Lakini nashindwa kuelewa na kuamini kuwa eti kile kipindi cha miaka ya sitini, kuna watu ndani ya Tanganyika waliokuwa wanaogopa uislam na kwa hiyo wakaanza kufuta hayo majina ya waislam kwenye historia. Hii ndugu Mohamed, imegoma ku-register kichwani kwangu.

Ninafikiri kuwa hizi ni hisia ambazo wengi wenu mnazo, kufikiria kuwa tusio waislam tunawaona waislam kama adui zetu ilhali sisi uislam wenu wala hautubugudhi. Ni hisia hizo ndizo ambazo zinawafanya kwa kila jambo msilolipenda, mna-single out waislam tu na kuwa wameonewa kwa sababu ya uislam hata kama jambo hilo limetokea hata kwa wasio waislam.

Au inawezekana mmegundua kuwa tunawapenda kama ndugu zetu sasa mnataka kulazimisha tuwe maadui?
 
Hivi ni Nyerere aliyeamrisha hawa mashujaa wasitajwe kwenye historia? Una ushahidi gani kwamba Nyerere hakutaka kuwasikia wakitajwa au ni dhana tu?

Jasusi,

Hebu soma hii kama inaweza labda kuamsha fikra zako:

"Mwakawa 1950 wakati marehemu Abdulwahid Sykes akiwa katika harakati za uongozi waTAA alikuwa akifanya kazi kama Market Master soko la Kariakoo. Ofisi yakeilikuwa kati ya Mtaa wa Swahili, mbele Mtaa wa Mkunguni na nyuma yake Mtaa waTandamti. Mtaa huu wa Tandamti umebadilishwa jina sasa unajulikana kama MshumeKiyate ingawa wahusika hawajabadili kibao sasa takriban miaka kumi na zaidi kwakuwa wanapinga mabadiliko hayo kwa fikra kuwa kilichopelekea Meya wa Dar esSalaam Kitwana Selemani Kondo kumuenzi Mshume Kiyate ni udini na wala siuzalendo na mchango wa muhusika katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Huendakizazi cha leo na wanasiasa wa sasa hawawajui mashujaa wa nchi yetu na yaliyokuwayakipitika pale Kariakoo ofisini kwa Abdulwahid. Katika ofisi ile alikuwapoMzee Abdallah yeye alikuwa ndiyo mhudumu wa ofisi na alimjua Mwalimu Nyererepale ofisini kwa Abdulwahid na anachokumbuka kwa maskhara ni ile kazi yake yakuchukua kuku pale sokoni akawachinja na kumpelekea Bi Mwamvua biti Masha lakinizaidi akijulikana kama Mama Daisy mke wa Abdulwahid kwa ajili ya chakula chamchana cha Nyerere na wanaharakati wengine hasa Nyerere alipoacha kazi yaualimu na kuja kukaa na Abdulwahid nyumbani kwake Mtaa wa Stanley kwa mudakabla hajenda Musoma.

Pale ndipo ilipokuwa sehemu kuu ya mawasiliano yaTAA. Siku zile akiwa pale nyumbani kwaAbdulwahid akenda ofisini kwake Kariakoo na wakati wa chakula cha mchanaMwalimu Nyerere alikuwa akiongozana na Shariff Attas ambae alikuwa akifanyakazi chini ya Abdulwahid Sykes kama dalali wa soko. Shariff Attas alikuwaakiongozana na Nyerere kwenda nyumbani kwa Abdulwahid kwa ajili ya chakula.

Jambo hili likawafanya Shariff Attas na Mwalimu Nyerere wawe karibu sana nawajuane vizuri. Nyumba ya Abdulwahid Sykes haikuwa mbali sana na soko, ilikuwaMtaa wa Aggrey na Sikukuu nyumba ya kona. Shariff Attas na Mama Daisy ni mmojawa watu wa mwanzo kujuana na Mwalimu Nyerere achilia mbali kuwa walikuja kuwawanachama wa mwanzo wa TANU ilipokuja kuundwa mwaka 1954.

Wakatiulikuwa miaka ya mwanzo 1950 na Abdulwahid Sykes alikuwa keshakutana na JomoKenyatta Nairobi na kufanya mkutano na KAU nia ikiwa ni kuunganisha nguvu zaTAA na KAU yaani juhudi za Watanganyika na Wakenya kupambana na ukoloni. Katikahalmashauri ya TAA walikuwapo Waafrika kutoka Kenya na Nyasaland kama DomeOkochi Budohi na Patrick Aoko kutoka Kenya na Denis Phombeah kutoka Nyasalandwakiendesha harakati bega kwa bega na ndugu zao Watanganyika.

Harakati hizizilipelekea kuwa na mawasiliano ya karibu sana na ya siri kati ya AbdulwahidSykes na Kenyatta kiasi kwamba mwaka 1953 Kenyatta alimwalika kwa mara ya piliAbdulwahid Nairobi katika mkutano mwingine ambao alikuwa aende na Dossa Aziz.Ule mkutano wa kwanza Abdulwahid alisindikizwa mkutanoni na Ahmed Rashad Aliambae baadae alikuja kuwa mtangazaji maarufu wa Radio ya Ukombozi wa Africa(Radio Free Africa) kutoka Cairo.

Kutokana na mkutano huu Rashad akaja fahamiana vizuri sana na Kenyatta.Kipindi hiki harakati dhidi ya ukoloni zilikuwa zimepamba moto Afrika nzima.Abdulwahid na Ally Sykes walikuwa na mawasiliano na Kenneth David Kaunda katibuwa African National Congress pamoja na Asia Socialist Conference Anti-ColonialBureau.

Idara ya Usalama ya kikoloni ikijulikana kama Special Branch walikuwawakifuatilia kwa karibu sana nyendo za ndugu hawa. Mtafiti akipitia nyaraka zaSykes atakutana na shajara za marehemu Abdulwahid baadhi zikiwa zimeandikwa kwahati ya kawaida na nyingine zikiwa katika hati mkato. Inaaminika shajara zakeza hati mkato ndizo zenye taarifa nyingi za harakati zake za kuanzisha TANU nasafari zake nje ya nchi kukutana na wapigania uhuru wengine kama Jomo Kenyatta,Bildad Kaggia, Kung'u Karumba, Achieng Oneko, Fred Kubai na Paul Ngei. Hawawalikuja fahamika kama Kapenguria Six kwa kuwa walifungwa jela kwa tuhuma zaMau Mau sehemu inayojulikana kama Kapenguria.

Bahati mbaya ni kuwa akina Sykeswenyewe hawajaruhusu watafiti kuzisoma shajara za marehemu Abdulwahid ambazosasa takriban zina umri wa zaidi ya miaka hamsini. Nyaraka za siri za serikaliya kikoloni ambazo sasa ziko wazi huko Uingereza baada ya kupita miaka hamsinizinaonyesha kuwa Abdulwahid wakati akiwa Market Master Soko la Kariakoo nyendozake zilikuwa zikifuatiliwa kwa karibu sana na "Special Branch" kiasi cha kuwajalada lake la siri limemtaja kama "mtu hatari."

Wakatiakina Bildad Kaggia na Kenyatta lile kundi la Kapenguria likikamatwa Nairobibaada ya muda Budohi na Aoko nao walitiwa mbaroni Dar es Salaam. Abdulwahid ilibidiakaimu nafasi ya rais baada ya Dr. Kyaruzi kupewa uhamisho kwenda Kingolwirakama adhabu ya kupinga serikali. Kama kuna mtu ana fikra kuwa TAA haikuanzishwakwa ajili ya kudai uhuru wa Tanganyika basi na aeleze hizi harakati za viongoziwake kuweka mikakati ya pamoja na akina Jomo Kenyatta na Kenneth Kaundakatikati ya 1950 na 1953 na kuweka uhusiano na vyombo kama Asia Socialist Anti- Colonial Bureau ilikuwa ya kutafuta nini.

Vilevile aeleze kwa nini serikaliilitoa sekula no. 5 na 6 ikiwaonya Waafrika watumishi wa serikali kuhusukufanya siasa wakiwa watumishi wa Malkia.

Kupitiakwa Abdulwahid Sykes Mwalimu Nyerere akajuana na watu wengine pale sokonimashuhuri mjini kama Mshume Kiyate, Shariff Mbayamtu na wengineo. Mshume Kiyateakampenda Mwalimu Nyerere kama mwanae. Mzee Mshume na Mwalimu Nyerere wotewawili walikuwa wapenzi wa kucheza bao na wakati mwingine Mzee Mshume akichezabao na Mama Maria. Ofisi ya Abdulwahid pale Kariakoo na ofisi ya Hamza MwapachuIlala Wefare Centre ndipo palipokuwa na pilikapilika za ingia toka za wanasiasawa wakati ule kwa nyakati za mchana na ikiingia usiku harakati zilihamia TangaClub iliyokuwa Mtaa wa New Street na Mkunguni.

Uchaguziwa rais wa TAA wa 1953 kati ya Abdulwahid Sykes aliekuwa akitetea kiti chake naJulius Nyerere ulikuwa uchaguzi wa aina yake katika historia ya uhuru waTanganyika. Ulitanguliwa na majadiliano ndani ya Kamati Ndogo ya Siasa ya TAAkueleza umuhimu wa kumweka Nyerere katika kiti badala ya Abdulwahid ambae mudawake wa uongozi ulikuwa unakwisha. Hapa ndipo mwanzo wa matundu na chanzo chamatatizo ya historia ya kudai uhuru wa Tanganyika. Kwa kuwa Nyerere mwenyewehakupata kueleza vipi aliingia TANU inaonekana kama alizuka tu kutoka Musomaakatua Dar es Salaam na kuanzisha TANU. Jambo ambalo haliwezekani.

Ukweli wamambo ni kuwa uchaguzi baina rais wa TAA, Abdulwahid Julius Nyerere, ulifanyikakwenye Ukumbi wa Arnatouglo tarehe 17 Aprili, 1953. Nje ya uongozi wa TAA ambaoulimpendekeza kugombea nafasi hiyo, Nyerere alikuwa mgeni kabisa kwa wotealiokuwa akiwaomba kura zao. Nyerere alikuwa mgeni na alikuwa hana historia yakuongoza mapambano ya umma dhidi ya serikali ya kikoloni. Ukoo wa Sykes ulikuwamaarufu na unatambulikana katika siasa za Dar es Salaam kwa takriban robokarne.

Ushahidi wa haya unapatikana katika nyaraka kati ya ukoo huu na serikaliya kikoloni. Katika kipindi cha miaka zaidi ya ishirini, serikali kwa nyakatitofauti, kati ya mwaka 1929 hadi 1953 ilikuwa na barua za Kleist Sykes na zamwanaye Abdulwahid wakiwa viongozi wa African Association wakichagiza serikalikuhusu madhila tofauti yaliyokuwa yakiwakabili wananchi. Maarufu katika hayo nimigomo ya wafanyakazi kati ya mwaka wa 1938 hadi 1947 na ule mgogoro wa ardhiya Wameru. Uchaguzi ulikuwa kwa kunyoosha mikono.

Denis Phombeah aliyekuwaakifanya kazi Ukumbi wa Arnatouglo ndiye alikuwa msimamizi wa uchaguzi. Phombeah aliwaomba Abdulwahid na Nyerere kutoka nje ya ukumbi ili uchaguziuanze. Wiki nzima kabla ya uchaguzi Phombeah alikuwa akizunguka mji mzima napikipiki yake akimfanyia kampeni Nyerere. Lakini kwa hakika hakukuwa na haja yakufanya hivyo.

Uongozi wa ndani wa TAA wa Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz na JohnRupia ulikuwa tayari umekwishaamua kumpa Nyerere urais wa chama. Uchaguziulikuwa kutimiza utaratibu tu. Baada ya Abdulwahid na Nyerere kuombwa naPhombeah kutoka nje, upigaji kura ulianza.

Nyererealishinda uchaguzi huo dhidi ya Abdulwahid kwa kura chache sana. Huu ulikuwa ndiyo mwanzo wa Nyererekujulikana katika siasa za Tanganyika. Kuanzia siku ile historia ya Tanganyikaikabadilika na siasa za Tanganyika zikachukua sura nyingine kabisa. Siasazilichukua sura nyingine kwa sababu walingia watu katika harakati ambaowaligeuza mwelekeo kudai haki kwa vipaji vya kuhamasisha watu ambavyoTanganyika ilikuwa haijapata kuona. Hapa ndipo unapokutana na Titi Mohamed,Tatu bint Mzee, Said Chamwenyewe, Sheikh Suleiman Takadir, na wengine wengilakini kwa bahati mbaya hawa wote historia imewasahau hawatajwi kabisa.

Nyereremwenyewe kamwe hajazungumzia kuhusu uchaguzi huu au namna alivyokuja kuongozaTAA Dar es Salaam. Kiasi cha karibu sana alichofika kumhusisha Abdulwahid nahistoria yake kilikuwa katika ile hotuba ya mwaka wa 1985 ya kuwaaga wazee Dares Salaam, na kwa bahati mbaya Nyerere alipojaribu kumueleza Abdulwahid,alishindwa kwa kuwa kwa kauli yake alisema hakumbuki cheo alichokuwa akishikaAbdulwahid katika TAA wakati yeye Nyerere alipojiunga na chama mwaka 1952. Hatahivyo gazeti la serikali, "Daily News" lilijaribu kurekebisha historia kwakutaja cheo cha Abdulwahid, ingawa kwa makosa, kwa kusema kuwa Nyererealipojiunga na TAA makao makuu Abdulwahid alikuwa katibu.

Ukweli ni kuwaNyerere alimkuta Abdulwahid akiwa rais wa TAA. Nini sababu ya mparaganyiko huu

KleistSykes baba yao Abdulwahid, Ally na Abbas ameacha kumbukumbu nyingi zinazoelezeasi tu hali ya siasa Tanganyika ilivyokuwa mwanzo wa karne ya ishirini balizinatoa historia kamili ya mji wa Dar es Salaam na watu wake na jinsi yeyemwenyewe alivyoasisi African Association.

Ukipitia nyaraka hizo zinakurudishamiaka mia moja nyuma toka baba yake Kleist, Sykes Mbuwani alipoingia nchiniTanganyika kama mamluki akiwa katika jeshi la Wazulu mia nne wakiongozwa naMjerumani Von Wissman kuja kupigana na Bushiri bin Salim Pangani na ChifuMkwawa huko Kalenga. Nyaraka zinaonyesha maisha ya Kleist katika jeshi laWajerumani katika Vita Kuu ya Kwanza akiwa Aide de Camp (Mpambe) wa Von LettowVorbeck. Nyaraka zinafichua vipi Kleist alikuja kuwa mwanasiasa hodari nakiongozi wa chama cha wafanyakazi katika kipindi cha vita kuu mbili za duniabaada ya kukutana na Dr James Kwegyir Aggrey mwaka 1924 na kumshauri aanzisheumoja wa Waafrika katika Tanganyika.

Kutokanana ushauri huu wa Dr Aggrey mwaka wa 1929 Kleist na baadhi ya rafiki zake wakaribu kama Mzee bin Sudi, ambaye wazazi wake walikuwa Wamanyema kutoka BelgianCongo, Ibrahim Hamis - Mnubi ambaye baba yake alitoka Daffur nchini Sudan, ZibeKidasi, Ali Said Mpima - Mzaramo, Suleiman Majisu, Raikes Kusi, Rawson Watts naCecil Matola - Myao kutoka Masasi walianzisha African Association, Kleist akiwakatibu muasisi. Gavana wa wakati ule Donald Cameroon akawaonya akina Kleistkuwa wasikiingize chama katika siasa.

Mikutano ya mwanzo ya chama hikiilifanyika Mtaa wa Masasi Mission Quarter Dar es Salaam kwenye nyumba ambayoilikuja hapo baadae ikanunuliwa na John Rupia. Mwaka wa 1930 katika juhudi zakuikiimarisha chama, Kleist akawa anasimamia ujenzi wa jengo la makao makuu yaAfrican Association, New Street (sasa Mtaa wa Lumumba) ambalo wananchi walikuwawakijenga ofisi yao hiyo kwa kujitolea nguvu zao wenyewe. Hili ndilo jengoambalo TANU ilikuja kuzaliwa tarehe 7 Julai, 1954.

Historia inamwonyesha Kleist kama Mwafrikaalielimika vizuri kwa viwango vya wakati ule. Kleist akizungumza Kijerumani naKiingereza, akijua kupiga chapa na hati mkato. Kleist alikuwa mwanasiasa wakuheshimika na aliasisi chombo ambacho ndicho kulichokuja kuasisi TANU. Kleistalikuja kuwa mfanyabiashara na akatajirika.

Abdulwahidamepata kueleza kuwa akiwa mtoto mdogo ameshuhudia kwa macho yake ujenzi wajengo la TAA kwa kuwa alikuwa akifuatana na baba yake pale New Street siku zaJumapili ambayo ndiyo ilikuwa siku ya ujenzi kwa wanachama kujitolea.

Kleisthakuishia hapo baada ya kuasisi African Association mwaka 1929 akaasisi "AlJamiatul Islamiyya fi Tanganyika" (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) mwaka 1933akiwa katibu. Vyama hivi viwili vikawa vinafanya kazi kwa pamoja kwa kuwaviongozi hao hao wa TAA ndiyo wakajakuwa viongozi wa "Al Jamiatul Islamiyya" nahuu ndiyo ulikuwa mtindo hadi mwaka wa 1954 TANU ilipoasisiwa. Mweka Hazina wa"Al Jamiatul Islamiyya" ndiye aliyekuwa pia mweka hazina wa TANU na "AlJamiatul Islamiyya" ilitoa fedha katika kuchangia safari ya Nyerere Umoja waMataifa mwaka 1955.

Iddi Faizi Mafongo nandugu yake Iddi Tosiri ndiyo waliompeleka Nyerere Bagamoyo kumtambulisha kwandugu yao Sheikh Mohamed Ramia Khalifa wa Tariqa Kadiriyya. Sheikh Ramia naNyerere wakaja kuwa marafiki wakubwa sana. Iddi Faizi Mafongo ndiye aliyetumwaTanga na TANU kwenda kuchukua fedha kutoka kwa Mwalimu Kihere kuja kukamilishanauli ya Nyerere kwa safari ya Umoja wa Mataifa mwaka wa 1955.

Special Branchwalimkamata njiani Turiani wakamshusha kwenye basi lakini hawakuziona fedhazile na zikafika Dar es Salaam ofisi ya TANU salama.

Inasikitishakuwa Mwalimu Nyerere hakupata kueleza chanzo cha hotuba ile ambayo hivi sasaimo katika moja ya vitabu vyake na kwa hakika hiki ni kisa kirefu sana na chakumvutia mtafiti yeyote. Waraka ulioandikwa na Kamati Ndogo ya Siasa ya TAAmwaka 1950 na ndiyo ulikuja kuwa chanzo cha hotuba ya Mwalimu Nyerere Umoja waMataifa umepotea na haujulikani ulipo.

Jalada lake Tanzania National Archive(TNA) ni tupu na hata "microfilm" ya waraka ule imetoweka. Laiti ungelipatikanamtafiti angeliona sahihi ya marehemu Abdulwahid Sykes, Vedasto Kyaruzi, SheikhHassan bin Amir, Hamza Mwapachu na wajumbe wengine. Mtafiti akitaka kujua vipiAfrican Association iliasisiwa na ni nani wahusika wakuu basi hana budi kusomanyaraka za Kleist Sykes lakini ikiwa atataka kutafiti kuhusu TANU itabidi asomenyaraka pamoja na shajara za Abdulwahid Sykes.

Ikiwa huu ndiyo ukweli wahistoria ya kupigania uhuru wa Tanganyika huu ubishi wa kuwa nani kaasisi TAAumetoka wapi? Halikadhlika unaweza mtu ukahoji kwa nini waliokuja baada ya TAAwaseme kuwa hapa ndipo ilipozaliwa TANU badala ya kusema kuwa hapa ndipoilipozaliwa TAA? Au vipi ikawa muhali kunasibisha familia ya Kleist Sykes nanguvu ya Watanganyika kujikomboa? Kipi kinachoogopwa?

Mara ya kwanza kuchapwahistoria kinzani na historia rasmi ya uhuru wa Tanganyika ilikuwa mwaka wa 1988na mwandishi alikuwa mwandishi wa makala haya. Makala hayo, ‘In Praise of Ancestors' yalichapwa na gazeti Africa Events lililokuwa likichapwaLondon, katika toleo la March/April 1988, (uk. 37-41). Gzeti hili lilikusanywana watu wasijulikana na kutolewa katika mzunguko. Nakala chache sanaziliwafikiwa wasomaji. Kada wa Chama Cha Mapinduzi akiandika kutoka Makao Makuuya CCM Dodoma alitoa vitisho kwa mwandishi katika gazeti hilo hilo toleo la Mei,1988.

Hivikweli Nyerere angeweza kuukana ukweli huu wa historia ya TANU mbele ya watu wakawaida tu na wala si wanasisasa, watu kama Shariff Attas na Mzee Abdallah naakabaki na heshima yake achilia mbali wanasiasa wa wakati ule kama SheikhHassan bin Amir, Hamza Mwapachu, Dr. Kyaruzi na wengineo?

Ama kuenezwa kwa TANU katika majimbo hiyo kaziilifanywa na wengi ambao leo hawatajwi na hata pale Mwalimu Nyerere alipotoamedali 3979 mwaka wa 1985 katika viwanja vya Ikulu kwa Watanzania waliofanyamengi katika nchi hiii ilistaajabisha wengi kuwa hakuna hata mmoja wa waliopigania uhuru aliyepata heshima hiyo. Si Dossa Aziz,wala Abdulwahid Sykes au Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Yusuf Badi, Tatu bintMzee, Mshume Kiyate, Mwinjuma Mwinyikambi, Suleiman Masudi Mnonji, Bi. ShariffaMzee, Sheikh Mohamed Ramia, Zuberi Mtemvu, Ali Mwinyi Tambwe, Hamza Mwapachu,Dr. Kyaruzi, Dr. Michael Lugazia, Ali Migeyo, Suedi Kagasheki, Iddi FaizMafongo, Yusuf Olotu, Yusuf Chembera, Salum Mpunga, Hamisi Taratibu, OmariSuleiman, ohn Rupia, Joseph Kasella Bantu na wengine wengi.

Yusuf Chembera na SalumMpunga ni waasisi wa TANU Lindi 1956 Mpunga ndiyo waliyomfuata Mwalimu NyerereDar es Salaam kuuomba aende Lindi kuhamasisha wananchi kuhusu TANU na ni waowaliomjulisha Nyerere kwa Sheikh Yusuf Badi.

Hakuna katika mashujaa wa uhuru aliekumbukwa kwakupewa medali licha ya kuwa wao walitembea nchi nzima kuieneza TANU pamoja naNyerere.

Walasi kweli kuwa wazalendo hawa hawakumaliza kazi. Abdulwahid na Ally Sykeswalifadhili chama hadi uhuru unapatikana. Inatosha kusema tu Dossa Azizalifadhili chama hadi kufikia kufilisika kabisa na akafa kijijini Mlandiziakiwa masikini kabisa.

Sheikh Hassan bin Amir katika kumbukumbu zake anasemaalijiuzulu siasa baada ya uhuru kupatikana na kuanzisha "Daawat Islamiyya"(Mwito kwa Waislam) ili ashughulikie elimu kwa Waislam na hii ndiyo ikawa kisacha ugomvi baina yake na Nyerere mwishowe Mufti Sheikh Hassan bin Amirakakamatwa kwa amri ya Nyerere na kurejeshwa kwao Zanzibar. Baraza la Wazee waTANU lilikokuwa na wajumbe 170 chini ya uenyekiti wa Iddi Tulio baada yakufukuzwa Sheikh Takadir TANU lilishiriki katika mapambano hadi mwisho nalilikuja kuvunjwa na Nyerere mwaka 1963 kwa sababu ambazo hadi leo hazijaelezwasawasawa.

MwalimuNyerere alitaka historia ya TANU iandikwe na fikra hii ilitokea katika mjadalaulofanyika kati yake Abdulwahid, Mwalimu Kihere na Dossa Aziz. Mwalimu alimpakazi hiyo ya uandishi wa historia ya kudai uhuru wa Tanganyika AbdulwahidNyerere akamteua Dr. Wibert Kleruu awe msaidizi wa Abdulwahid katika kazi ile. Historiaya Sykes Mbuwane na Von Wissman wakati wa enzi wa utawala wa Wajerumani kishahistoria ya Kleist Sykes na Von Lettow Vorbeck wakati wa Wajerumani na kuingiautawala wa Waingereza. Historia ya mwanae Abdulwahid kuanzia Burma hadi kurejeaTanganyika na harakati zake na akina Kenyatta, Japhet Kirilo na Earl Seatonhadi kufikia Kirilo na Seaton kwenda Umoja wa Mataifa na Japhet Kirilo kuhutubiaUmoja wa Maataifa katika Mgogoro wa Ardhi ya Wameru mwaka 1952 ilikuwa mithili ya mchezo mzuri wa senema kutoka Hollywood. Historia hii ni ya kupendeza iliyojaa matokeomengi yaliyoendana na historia ya Afrika baada ya Vita Kuu ya Pili. Akiwakatika kikosi cha askari wa miguu huko Burma historia ilionyesha kuwaAbdulwahid alionyesha fikra za kutaka kuwaunganisha Watanganyika chini ya TANU.Fikra hii aliitoa siku ya mkesha wa Krismas mwaka 1945 akiwa Kalieni Camp Indiapamoja na askari wenzake wakingojea meli kurudi Tanganyika baada ya kwisha vita.Historia iliandikwa lakini haukuchapwa hadi hii leo na wala hakuna ajuayemswada ule uko wapi. Baadaya kupatikana uhuru mwaka 1961 iko siku Mwalimu Nyerere alikwenda ofisi yaTANU. Pale akamkuta Shariff Attas.

Mwalimu alimwuliza Shariff Attas wapiwamekutana kwani sura yake inaonyesha kama wanafahamiana. Shariff Attas kwautulivu akamjibu Nyerere kuwa hawajapata kukutana katika maisha yao. ShariffAttas alikuwa kidogo ameghadhibika akiona kama vile sasa Nyerere kawa rais wanchi kesha wasahau rafiki zake wa zamani na yeye hakuwa tayari kujipendekezakwake akamwambia kwa mkato kuwa hawajuani.

Lakini kubwa zaidi na la kushangazani kuwa Nyerere mwaka 1985 katika hotuba ya kuwaaga wazee wa Dar es Salaamaliokuwanao wakati wa kupigania uhuru alisema kuwa katika vijana waliokuwepowakati ule alikuwa Dossa Aziz na Abdul Sykes lakini hakumbuki Abdulwahidalikuwa na cheo gani katika TAA.

Inasemekanakatika kipindi chake chote alipokuwa madarakani Nyerere hakupata kusikikakuwataja katika hadhira yoyote viongozi wa TAA aliowakuta katika siasa kablayake. Watu kama Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Luciano Tsere, Dr. JosephMutahangalwa, Dr. Michael Lugazia, Dr. Wilbard Mwanjisi na wengineo. Historiaya harakati za uhuru wa Tanganyika inalazimishwa ianze na Nyerere kiasi kwambainapotajwa kuwa Nyerere alichukua uongozi wa TAA mwaka 1953 haitajwi kauchukuauongozi huo kwa nani na katika mazingira gani.

Inawezekana kweli mtu wa kiwangocha akili ya Mwalimu Nyerere akawa na kumbukumbu fupi kiasi cha kusahau kuwaaligombea nafasi ya urais wa TANU na Abdulwahid Sykes?

Siku alipojaribu kumtajaAbdulwahid Sykes ndipo ulimi ukamteleza akasema hakumbuki Abdulwahid Sykesalikuwa na cheo gani katika TAA. Jambo la kusikitisha ni kuwa aliyasema manenohayo mbele ya wazee wa Dar es Salaam ambao yeye asingewajua sama na Abdulwahidna Dossa. Leo hii si tabu kujua picha aloiacha Mwalimu Nyerere kwa wazee wale.Ilikuwa Nyerere kafika safari yake lakini kasahau kituo alichopandia basi.

Kweliinawezekana vipi Nyerere akawa kasahau uchaguzi ambao ndiyo uliomwingiza yeyekatika siasa na uongozi wa Waafrika wa Tanganyika na mwishowe kuupata ubaba wataifa?

Nyerere anaweza kweli kamsahau Shariff Attas dalali wa soko au hata MzeeAbdallah muhudumu wa ofisi ya Abdulwahid lakini vipi Nyerere amsahau rafikiyake Abdulwahid mtu aliempokea Dar es Salaam akaishi nyumbani kwake alipoachakazi, mtu alieshughulika na safari yake ya kwenda Umoja wa Mataifa kwa niaba yaTANU na mtu aliyemwingiza na kumpa uongozi wa TAA na kumkabidhi majalada naofisi ya chama achilia mbali ile kumjulisha kwa wanachama na watu mashuhuri wamjini?

Mwandishiwa makala haya alipoandika kitabu kuhusu maisha ya Abdulwahid Sykes "The Lifeand Times of Abduwahid Sykes the Untold Story of the MuslimStruggle against British Colonialism in Tanganyika" alimlaumu John Illife ambaealiandika sana kuhusu historia ya Tanganyika kwa kutokuwa makini katika utafitiwake kiasi cha kukosa kuzisoma nyaraka za Sykes na hivyo kuandika historiailiyokuwa na ukweli nusu. John Iliffe alipoandika pitio la kitabu katikaCambridge Journal of African History aliandika kwa hasira na kusema kuwaAbduwahid Sykes hakuasisi TANU.

Hata hivyo Jonathan Glassman na James Brenanwanahistoria vijana kutoka Marekani, mahiri katika historia ya Tanganyikawamesema kuwa si rahisi kwa mtafiti yeyote kupuuza kitabu hicho kwani kimekujana mengi mapya ambayo hayakuwa yanafahamika kwa wengi.

Kwa kumalizia ningependakusema kuwa isidhaniwe kuwa kwa kuwapuuza wazalendo wengine na kubadilishahistoria ndipo ilipo njia ya kumjenga Nyerere.

Kwa kufanya hivyo hawamjengibali wanambomoa vibaya sana hasa ikiwa sasa Mwalimu Nyerere yuko katikamchakato wa kuwa "mwenye heri" kuelekea kuwa "mtakatifu" kamili. Uongo naudanganyifu si sifa ya utakatifu. Itapendeza ikiwa tutamuenzi Mwalimu kwa yaleanayostahili na yapo mengi sana."
 
Mohamed!
Hapo kwenye blue, ni chanzo kimojawapo cha hoja zetu zinazoelekezwa kwako pamoja na wafuasi wako.
Je, wale ambao hawakutajwa katika historia ya TANU, pamoja na waliowekwa kizuizuini, walikuwa waislam tu? This is a one million dollar question.
Ni kwanini kila baya wakitendewa watu kwa ujumla wao, tuanze tena ku-single out Waislam pekee na kuwa wametendewa mabaya kwa sababu ya dini yao?
Mimi na wewe tunatimuliwa vumbi barabarani, wote tunakereka, lakini wewe unaanza kudai kuwa umetimuliwa vumbi kwa sababu ya dini yako eti kwa sababu tu yule aliyetimua vumbi yupo dini moja na mimi. Hii inakuja kweli????
Watoto wetu wanakosa nafasi ya kwenda chuo kikuu, wewe unasema ni kwa sababu ya dini yako, unasahau kuwa hata mimi wa dini tofauti na wewe, mtoto wangu kanyimwa nafasi hiyo hiyo.

Kwenye baadhi ya posts zako umeonesha wazi kuwa kuna watu wanaogopa uislam na ndio sababu ya "kupindisha" historia. Unaonesha kuwa kuna wamakonde walienda Zanzibar kusaidia mapinduzi, yote hiyo ili kuvunja uislam kwa vile uislam unaogopwa...
Hivi hao wamakonde hawakuwa waislam?
Na je hii dhana ya kwamba uislam unaogopwa mnaipata wapi?
Hata hapa jamvini kuna wafuasi wako wanafikiri eti majina ya kiislam yanatutisha.. Ha ha ha.
Uislam una nini mpaka ututishe? Mbona ni dini tu ambayo hata miaka ya nyuma iliweza kuenea kwa amani tu (ukiondoa Nyakati za Jihad).
Hata hivyo naweza kuelewa kwa nyakati za sasa, kama kuna watu wanaogopa hiyo dini, kwa vile magaidi wengi wamesingizia uislam. Na kama ni suala la ugaidi, hata kuna waislam wanauogopa pia. Lakini nashindwa kuelewa na kuamini kuwa eti kile kipindi cha miaka ya sitini, kuna watu ndani ya Tanganyika waliokuwa wanaogopa uislam na kwa hiyo wakaanza kufuta hayo majina ya waislam kwenye historia. Hii ndugu Mohamed, imegoma ku-register kichwani kwangu.
Ninafikiri kuwa hizi ni hisia ambazo wengi wenu mnazo, kufikiria kuwa tusio waislam tunawaona waislam kama adui zetu ilhali sisi uislam wenu wala hautubugudhi. Ni hisia hizo ndizo ambazo zinawafanya kwa kila jambo msilolipenda, mna-single out waislam tu na kuwa wameonewa kwa sababu ya uislam hata kama jambo hilo limetokea hata kwa wasio waislam. Au inawezekana mmegundua kuwa tunawapenda kama ndugu zetu sasa mnataka kulazimisha tuwe maadui?

Usifanye haraka na huenda hujui.

Nanren,

Sisi tayari ni maadui.
Angalia walikotoka Waislam na hulka zao na sasa wako katika hali gani.

Labda hujasikia kwa kuwa vyombo vya habari vimegomea kuandika yaliyotokea Diamond Jubilee Hall ktarehe 16 Oktoba 2011katika majumujisho ya Waislam kuhusu
mfumokristo.

Waislam wamekuwa wakifanya mikutano ya wazi kutahadharisha kuhusu mfumokristo. Wametembea nchi nzima kwa takriban miezi 9.

DVD zinapatikana misikitini tafuta uangalie ndipo utajua ukweli.

Tafuta habari hizo kisha tujadili.

Kimepitika nini hadi Waislam wamefika hali hiyo? Huu ni muhtasari tu kwa kuwa nahisi si mada iliyopo mezani. Nchi yetu ipo katika tatizo kubwa sana.

Mohamed

PS: Kuna uzi nimeuweka leo jkuhusu hisia za Waislam usome kichwa kikiwa kikmefunguka na nakusihi ndugu yangu wala usidhani ni maskhara huo ndiyo ukweli wenyewe.
 
Nimefuatilia mjadala tokea mwanzo na kuna mengi nimejifunza.La muhimu kuliko yote ni kuwa kwenye mapambano dhidi ya ukoloni kuleta uhuru kulikuwa na makundi mawili yanayosukumwa na dhamira tofauti kuleta uhuru.

Kuna kundi lilikuwa linapigania uhuru likisukumwa na imani ya dini na jingine likisukumwa na uzalendo wa kitaifa.Kinara wa kundi la pili alijua athari za kutumbukiza dini kwaajili ya siasa.Hata kama uhuru ungepatikana kwa njia ya umoja wa kiislamu bado taifa letu lisingekuwa na utulivu huu uliopo.Mwalimu alijua njia pekee ya kuwa na taifa moja hata baada ya uhuru ni kupingana na wale wote ambao walikuwa na dhamira ya kidini.

Kwa bahati mbaya wengi wao ndiyo wazee wa Mohamed Said na genes zao zaendelezwa na mjukuu wao.Ulazwe pema peponi mwl J.K Nyerere kwa kupigania taifa moja la Tanganyika huru.Wale wote ambao wanasukumwa na udini na wenye dhamira ya kutusambaratisha waislamu na wakristo tusioane, tusisalimiane, tusishirikiane kwenye misiba/ harusi, tusipande gari moja...washindwe na wasifikie lengo lao.
 
Mohamed!
Hapo kwenye blue, ni chanzo kimojawapo cha hoja zetu zinazoelekezwa kwako pamoja na wafuasi wako.
Je, wale ambao hawakutajwa katika historia ya TANU, pamoja na waliowekwa kizuizuini, walikuwa waislam tu? This is a one million dollar question.
Ni kwanini kila baya wakitendewa watu kwa ujumla wao, tuanze tena ku-single out Waislam pekee na kuwa wametendewa mabaya kwa sababu ya dini yao?
Mimi na wewe tunatimuliwa vumbi barabarani, wote tunakereka, lakini wewe unaanza kudai kuwa umetimuliwa vumbi kwa sababu ya dini yako eti kwa sababu tu yule aliyetimua vumbi yupo dini moja na mimi. Hii inakuja kweli????
Watoto wetu wanakosa nafasi ya kwenda chuo kikuu, wewe unasema ni kwa sababu ya dini yako, unasahau kuwa hata mimi wa dini tofauti na wewe, mtoto wangu kanyimwa nafasi hiyo hiyo.

Kwenye baadhi ya posts zako umeonesha wazi kuwa kuna watu wanaogopa uislam na ndio sababu ya "kupindisha" historia. Unaonesha kuwa kuna wamakonde walienda Zanzibar kusaidia mapinduzi, yote hiyo ili kuvunja uislam kwa vile uislam unaogopwa...
Hivi hao wamakonde hawakuwa waislam?
Na je hii dhana ya kwamba uislam unaogopwa mnaipata wapi?
Hata hapa jamvini kuna wafuasi wako wanafikiri eti majina ya kiislam yanatutisha.. Ha ha ha.
Uislam una nini mpaka ututishe? Mbona ni dini tu ambayo hata miaka ya nyuma iliweza kuenea kwa amani tu (ukiondoa Nyakati za Jihad).
Hata hivyo naweza kuelewa kwa nyakati za sasa, kama kuna watu wanaogopa hiyo dini, kwa vile magaidi wengi wamesingizia uislam. Na kama ni suala la ugaidi, hata kuna waislam wanauogopa pia. Lakini nashindwa kuelewa na kuamini kuwa eti kile kipindi cha miaka ya sitini, kuna watu ndani ya Tanganyika waliokuwa wanaogopa uislam na kwa hiyo wakaanza kufuta hayo majina ya waislam kwenye historia. Hii ndugu Mohamed, imegoma ku-register kichwani kwangu.
Ninafikiri kuwa hizi ni hisia ambazo wengi wenu mnazo, kufikiria kuwa tusio waislam tunawaona waislam kama adui zetu ilhali sisi uislam wenu wala hautubugudhi. Ni hisia hizo ndizo ambazo zinawafanya kwa kila jambo msilolipenda, mna-single out waislam tu na kuwa wameonewa kwa sababu ya uislam hata kama jambo hilo limetokea hata kwa wasio waislam. Au inawezekana mmegundua kuwa tunawapenda kama ndugu zetu sasa mnataka kulazimisha tuwe maadui?

Paranoia !!
 
Inasemekanakatika kipindi chake chote alipokuwa madarakani Nyerere hakupata kusikikakuwataja katika hadhira yoyote viongozi wa TAA aliowakuta katika siasa kablayake.
Mohammed.

Kwa nukuu hiyo inaonyesha kuwa hii ni "hearsay," kitu ambacho hakina ushahidi. Mtafiti unapaswa kufanya kazi ya ziada kuondoa dhana ya hearsay. Ndio maana tunasema una agenda.
 
Na kama kumbukumbu zangu ni sahihi, aliyekuwa rais mwaka 1988 alikuwa Ali Hassan Mwinyi. Kwa hiyo kama gazeti la Africa Events lilikusanywa lisisambazwe basi hii ilifanyika chini ya rais Mwinyi, Muislamu mwenzenu.
 
Usifanye haraka na huenda hujui.

Nanren,

Sisi tayari ni maadui.
Angalia walikotoka Waislam na hulka zao na sasa wako katika hali gani.

Labda hujasikia kwa kuwa vyombo vya habari vimegomea kuandika yaliyotokea
Diamond Jubilee Hall ktarehe 16 Oktoba 2011katika majumujisho ya Waislam kuhusu
mfumokristo.

Waislam wamekuwa wakifanya mikutano ya wazi kutahadharisha kuhusu mfumokristo.
Wametembea nchi nzima kwa takriban miezi 9.

DVD zinapatikana misikitini tafuta uangalie ndipo utajua ukweli.

Tafuta habari hizo kisha tujadili.

Kimepitika nini hadi Waislam wamefika hali hiyo?

Huu ni muhtasari tu kwa kuwa nahisi si mada iliyopo mezani.

Nchi yetu ipo katika tatizo kubwa sana.

Mohamed

PS: Kuna uzi nimeuweka leo jkuhusu hisia za Waislam usome kichwa kikiwa kikmefunguka na nakusihi ndugu yangu wala usidhani ni maskhara huo ndiyo ukweli wenyewe.

MS

Asante mkuu MS kwa kunitahadharisha kuhusu huu uadui kati yenu waislam na tusio waislam. Nafikiri kambi yako imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutengeneza/kueneza uadui huu kwa kisingizio cha kuandika historia iliyosahauliwa.
Ugumu ninaopata ni jinsi ya kutofautisha waislam wanaonichukulia mimi kama adui yao, na waislam wanaoniona mimi ni ndugu yao.

Ila pia nakupa tahadhari na wewe.
Vurugu zikitokea, yeyote anaweza kuathirika- Haijalishi yeye ni Milosevic, Savimbi, Sadam au Gadaffi. Yeyote aweza kuathirika na vurugu. Wewe kwa ushawishi ulionao, unaweza kabisa kuwaambia vijana wako waache kutufikiria sisi kama maadui.

Kwa sisi tunaotanguliza utaifa na undugu kwanza, tupo tayari kukosa mengine yote, lakini tutapigania Taifa letu libaki na amani yetu.
 
Aneudhulumiwa hatahadharishwi.
Siku zote mwenye kupewa nasaa ni dhalim yule mwenye kudhulumu.

Unamtahadharisha nini yule anaedhulumiwa. Kuwa aikubali hali yake kwa kuchelea vurugu?

Usifanye haraka wala usidhani mimi napepea vurugu. Nakuomba sana tuliza akili na sikiza kilio cha Waislam wa nchi hii nini wananung'unikia.

Ukishafanya hivyo utakuwa uko pazuri kufanya mnakasha na mimi. Wala hilo si suala la kuandika historia yetu kwa kuwa waliokuwa na uwezo wa kuiandika wameipuuza.

Hili haliwezi kuleta vurugu katika nchi. Si hii historia nimeandika na leo Waislam wameichukuwa kuwa ndiyo historia
yao rasmi?

Nani kanyanyua jiwe?

Mohamed
 
Na kama kumbukumbu zangu ni sahihi, aliyekuwa rais mwaka 1988 alikuwa Ali Hassan Mwinyi. Kwa hiyo kama gazeti la Africa Events lilikusanywa lisisambazwe basi hii ilifanyika chini ya rais Mwinyi, Muislamu mwenzenu.

Jasusi,

Rais Mwinyi.
Hapana nina paper "The Christian Lobyy in Tanzania."

Iko siku tutamzungumza. Mambo si mepesi hivyo.

Unajua kazi ya utafiti unajua mengi mengine mazuri, mengine mabaya
na mengine yanachekesha.

Mwinyi anahitaji uzi wake wa pekee na nakuhakikishieni mtafurahi Insha Allah. Nkuonjesheni hii kidogo:

Through research and many years of observations it isnow possible to know a little how the unseen hand of the Church functions. Itworks like a secret society and yet it is not one at least from outside.

Itworks in a two prong fashion. It has agents in all important institutions ofthe civil society who co-ordinates their activities when the need arise formingwhat could be identified as the Christian lobby. This is a multi-denominationpower house..."

Hawa ndiyo walikuwa watendaji wa Rais Ali Hassan Mwinyi. Nadhani jibu umelipata.

Mohamed
 
Kama mtu atakuja na kukataa haya,alafu nakudai yeye anaijua Historia harisi ya Nchii hii ,ati sijui kwasababu yeye kazaliwa sijui mwaka gani..... lazima atakuwa na matatizo.

Hiyo "harisi" una maanisha bokoboko lako? Au una maanisha mlinzi wako? Kama ni hayo uliomaanisha sidhani kama humu JF utampata atakaeongelea hayo labda Barubaru akusaidie. Unanchekesha!
 
Mohammed Said,
Kwanza Asalaam aleikum, amani iwe juu yako mkuu wangu.
Leo nimepania kuwaeleza ukweli hasa nyie Waislaam wa Tanzania na hakika namwomba Mwenyezi Mungu awape subra na muda wa kutafakari ktk imani zenu. Nakuomba sana nisome kwa makini kisha uchukue mkondo wenye mafundisho mema ya dini yetu badala ya kutumia watu kama ndio dini na Uislaam..

Nimewahi kuandika huko nyuma ya kwamba - ISLAAM ni dini siyokuwa na WATU na WAKRISTU ni WATU wasiokuwa na DINI. Maelezo hyaya yaliwatatiza wengi na wengine wakaja na tafsiri zao lakini maneno haya ni muhimu sana kwa Msomaji yeyote anayetaka kuelewa maana na leo nitawambia.

ISLAAM NI DINI ISYOKUWA NA WATU:-

Ni muhimu sana kuelewa kwamba Islaam ni dini inayosimama peke yake, islaam ni way of life yaani hata kama watu wote hawaikubali bado dini hii itasimama kutokana na kwamba sio kitu kilichotengenezwa na binadamu. Hivyo ni sisi watu tunaoingia ktk Uislaam na kufuata mafundisho na maisha yake kuitwa waislaam kama vile Tanzania ni ardhi na nchi ambao hata kama haina watu bado itabakia kuwa Tanzania.. Nasi tunaodai kuwa Watanzania kuna process inafanyika ili tuwe Watanzania...Hata wale waliozaliwa nje ndani ya Utanzania hawawezi kujiita Watanzania ikiwa hawana Uraia wa Tanzania..

Islaam ni dini iliyokuwepo hata kabla ya Mtume Muhammad, hili wengi hawalifahamu kwa sababu wamefundishwa kuamini hivyo. Na kaa utafuatilia historia ya msikiti (kanisa, sinagogi ) wa Bait ul Muqaddas ulojengwa na Daud pbuh (David) na ulikuwa sehemu ya kuabudu kwa mitume wote waliofuata hadi Nabii Issa pbuh(Yesu) ambaye alikataza biashara za uchuuzi zisifanyike ndani ya msikiti huu naye alikuwa akisalia msikiti huu..

Na hata historia ya Muhammad inatueleza kwamba aliweza kuuzungumzia msikiti huu jinsi ulivyojengwa hata kabla hajauona wala kufika pale na maswahaba (wafuasi) wake walishangazwa..Na kwa nini walishangazwa?.... kwa sababu hawa walishafika na kufanya ibada zao na wanaujua msikiti huo ulikuwaje pia walijua kuna mtume atakuja baada ya Yesu, naye Muhammad aliwahakikishia kuwa ndiye analiyekusudiwa!. Hii yote inakuonyesha wazi kwamba Uislaam ulikuwepo hata kabla ya Muhammad. Hivyo, kwa mtu anayekebehi Islaam kama dini, huwaumiza wengi wenye kufahamu maana lakini mtu hawezi kuwa ndiye kitambulisho cha Uislaam. Sisi wote na wale waliotutanguliwa tutakufa na kuuacha Uislaam kama dini. Kuna menig ya kueleza lakini nitakomea hapo na kwenda sehemu ya pili.

WAKRISTU NI WATU WASIOKUWA NA DINI

Katika hili nitajaribu sana kuwa makini kwa sababu nazungumzia imani ya watu wengine. I know nachukua risk kubwa sana, lakini itanibidi nielezee maana ya maneno haya.
Historia ua Ukristu inatuleza wazi kwamba, WATU, (kina Paul, Peter na wengineo) waliokuwa wafuasi wa mafundisho ya Issa (Yesu) walikusanya vitabu na kuunda Biblia moja kama chombo mwongozo wa Wakristu..Kwa hili naomba Wakristu mnisamehe tena, lakini yanibidi kutolea mfano huu..Makanisa ya kikristu ni sawa na kuundwa kwa chama, yaani kundi la watu wamekaa na kuitafakari itikadi fulani kama mwongozo wao wakaunda umoja wao wa na watu waliojiunga na chama hicho wakaitwa Wakristu wa kanisa fulani ili kufuata mafundisho yake. Hivyo, imani ya Wakristu inatokana na mafundisho ya Biblia ambayo ni kama constitution na yeyote asiyekubaliana nayo sii mwanachama.. Hivyo ni watu walioanzisha makanisa ya dini na ndio maana nikasema wakristu ni watu wasiokuwa na dini.

Kwa nini nimeandika haya!... nimeandika haya kwa sababu nataka wewe na waislaam wengine wote mfahamu ya kwamba huwezi kutumia majina ya watu ktk kuutangaza Uislaam... Hawa wote kina Sykes, Dosa na wengine wote walifanya waliyoyafanya kwa Uzalendo wa Utaifa wao kama Watanzania na sio kwa sababu ya Uislaam wao. Na siku zote nachukia sana watu wanapotumia Uislaam ktk kujenga hoja zao kwa sababu Islaam ni dini imesimama peke yake you either in or out na unachoweza wewe kupigania na ukapongezwa ni pale Islaam (way fo life) inapopigwa vita. Wote mitume toka David hadi Yesu na Muhammad walipigania Uislaam kwa sababu Islaam sio uanachama au wa kuzaliwa bali ni UTU wa binadamu.
 
Inasemekanakatika kipindi chake chote alipokuwa madarakani Nyerere hakupata kusikikakuwataja katika hadhira yoyote viongozi wa TAA aliowakuta katika siasa kablayake.
Mohammed,
Kwa nukuu hiyo inaonyesha kuwa hii ni "hearsay," kitu ambacho hakina ushahidi. Mtafiti unapaswa kufanya kazi ya ziada kuondoa dhana ya hearsay. Ndio maana tunasema una agenda.

Jasusi,

Mie unadhani nina neno? Ikiwa hiyo ndiyo tafsiri yako sawa. Kwangu mimi ni kuwa ujumbe nimeufikisha kukubalika hilo ni jambo ambalo sina madaraka nalo.

Wala siwezi kusumbuana na mtu kwa hilo.

Mohamed
 
Mohammed Said,
Kwanza Asalaam aleikum, amani iwe juu yako mkuu wangu.
Leo nimepania kuwaeleza ukweli hasa nyie Waislaam wa Tanzania na hakika namwomba Mwenyezi Mungu awape subra na muda wa kutafakari ktk imani zenu. Nakuomba sana nisome kwa makini kisha uchukue mkondo wenye mafundisho mema ya dini yetu badala ya kutumia watu kama ndio dini na Uislaam..

Nimewahi kuandika huko nyuma ya kwamba - ISLAAM ni dini siyokuwa na WATU na WAKRISTU ni WATU wasiokuwa na DINI. Maelezo hyaya yaliwatatiza wengi na wengine wakaja na tafsiri zao lakini maneno haya ni muhimu sana kwa Msomaji yeyote anayetaka kuelewa maana na leo nitawambia.

ISLAAM NI DINI ISYOKUWA NA WATU:-

Ni muhimu sana kuelewa kwamba Islaam ni dini inayosimama peke yake, islaam ni way of life yaani hata kama watu wote hawaikubali bado dini hii itasimama kutokana na kwamba sio kitu kilichotengenezwa na binadamu. Hivyo ni sisi watu tunaoingia ktk Uislaam na kufuata mafundisho na maisha yake kuitwa waislaam kama vile Tanzania ni ardhi na nchi ambao hata kama haina watu bado itabakia kuwa Tanzania.. Nasi tunaodai kuwa Watanzania kuna process inafanyika ili tuwe Watanzania...Hata wale waliozaliwa nje ndani ya Utanzania hawawezi kujiita Watanzania ikiwa hawana Uraia wa Tanzania..

Islaam ni dini iliyokuwepo hata kabla ya Mtume Muhammad, hili wengi hawalifahamu kwa sababu wamefundishwa kuamini hivyo. Na kaa utafuatilia historia ya msikiti wa Bait ul Muqaddas ulojengwa na Daud pbuh (David) na ulikuwa sehemu ya kuabudu kwa mitume wote waliofuata hadi Nabii Issa (Yesu) ambaye alikataza biashara za uchuuzi zisifanyike ndani ya msikiti huu..

Na hata historia ya Muhammad inatueleza kwamba aliweza kuuzungumzia msikiti huu jinsi ulivyojengwa hata kabla hajauona wala kufikia pale na maswahaba (wafuasi wake walishangazwa..Na kwa nini walishangaa kwa sababu hawa walishafika na kufanya ibada zao na wanaujua msikiti huo ulikuwaje pia walijua kuna mtume atakuja naye Muhammad aliwahakikishia kuwa ndiyenaliyekusudiwa. Hii yote inakuonyesha wazi kwamba Uislaam ulikuwepo hata kabla ya Muhammad. Hivyo, kwa mtu anayekebehi Islaam kama dini, huwaumiza wengi wenye kufahamu maana lakini mtu hawezi kuwa ndiye kitambulisho cha Uislaam. Sisi wote na wale waliotutanguliwa tutakufa na kuuacha Uislaam kama dini. Kuna menig ya kueleza lakini nitakomea hapo na kwenda sehemu ya pili.

WAKRISTU NI WATU WASIOKUWA NA DINI

Katika hili nitajaribu sana kuwa makini kwa sababu nazungumzia imani ya watu wengine. I know nachukua risk kubwa sana, lakini itanibidi nielezee maana ya maneno haya.
Historia ua Ukristu inatuleza wazi kwamba, WATU, (kina Paul, Peter na wengineo) waliokuwa wafuasi wa mafundisho ya Issa (Yesu) walikusanya vitabu na kuunda Biblia moja kama chombo mwongozo wa Wakristu..Kwa hili naomba Wakristu mnisamehe tena, lakini yanibidi kutolea mfano huu..Makanisa ya kikristu ni sawa na kuundwa kwa chama, yaani kundi la watu wamekaa na kuitafakari itikadi fulani kama mwongozo wao wakaunda umoja wao wa na watu waliojiunga na chama hicho wakaitwa Wakristu wa kanisa fulani ili kufuata mafundisho yake. Hivyo, imani ya Wakristu inatokana na mafundisho ya Biblia ambayo ni kama constitution na yeyote asiyekubaliana nayo sii mwanachama.. Hivyo ni watu walioanzisha makanisa ya dini na ndio maana nikasema wakristu ni watu wasiokuwa na dini.

Kwa nini nimeandika haya!... nimeandika haya kwa sababu nataka wewe na waislaam wengine wote mfahamu ya kwamba huwezi kutumia majina ya watu ktk kuutangaza Uislaam... Hawa wote kina Sykes, Dosa na wengine wote walifanya waliyoyafanya kwa Uzalendo wa Utaifa wao kama Watanzania na sio kwa sababu ya Uislaam wao. Na siku zote nachukia sana watu wanapotumia Uislaam ktk kujenga hoja zao kwa sababu Islaam ni dini imesimama peke yake you either in or out na unachoweza wewe kupigania na ukapongezwa ni pale Islaam (way fo life) inapopigwa vita. Wote mitume toka David hadi Yesu na Muhammad walipigania Uislaam kwa sababu Islaam sio uanachama au wa kuzaliwa bali ni UTU wa binadamu.

Mkandara,

Hakuna Muislam anaeweza kuthubutu kutangaza Uislam kwa jina la mtu. Sijafanya hivyo na wala siwezi kuthubutu.

Nilichofanya mimi nimeandika historia ya wazee wangu ambayo ilikuwa imesahaulika.

Hicho ndicho nilichofanya. Na nimekwenda mbele zaidi na kusema silazimishi mtu kuiamini kwa kuwa historia rasmi iko na wazee wangu hawamo sina ugomvi na yeyote.

Nimefanya hivyo kwa kugundua kuwa kuna wengi historia ile inawachoma roho hawataki kuamini kuwa hayo niliyosema ni kweli.

Ila nitafahamisha moja ya mafunzo ya Uislam. Allah anawaasa Waislam "wasidhulumu na wasikubali kudhulumiwa."

Mohamed
 
Nimefuatilia mjadala tokea mwanzo na kuna mengi nimejifunza.La muhimu kuliko yote ni kuwa kwenye mapambano dhidi ya ukoloni kuleta uhuru kulikuwa na makundi mawili yanayosukumwa na dhamira tofauti kuleta uhuru.Kuna kundi lilikuwa linapigania uhuru likisukumwa na imani ya dini na jingine likisukumwa na uzalendo wa kitaifa.Kinara wa kundi la pili alijua athari za kutumbukiza dini kwaajili ya siasa.Hata kama uhuru ungepatikana kwa njia ya umoja wa kiislamu bado taifa letu lisingekuwa na utulivu huu uliopo.Mwalimu alijua njia pekee ya kuwa na taifa moja hata baada ya uhuru ni kupingana na wale wote ambao walikuwa na dhamira ya kidini.Kwa bahati mbaya wengi wao ndiyo wazee wa Mohamed Said na genes zao zaendelezwa na mjukuu wao.Ulazwe pema peponi mwl J.K Nyerere kwa kupigania taifa moja la Tanganyika huru.Wale wote ambao wanasukumwa na udini na wenye dhamira ya kutusambaratisha waislamu na wakristo tusioane,tusisalimiane,tusishirikiane kwenye misiba/harusi,tusipande gari moja...washindwe na wasifikie lengo lao.

Mnyakatari soma hii hapo chini:

Catholics form 76% of all members of Parliament the remaining 24% seatsare divided between Christians of other dominations and Muslims. Muslims controla mere 6% of the seats.

Most areas which are underdeveloped in Tanzania mainland are areas with Muslim majority like Kigoma,Tabora, Kilwa, Mtwara, Lindi etc. These areas are now re-examining themselvesand are gradually turning into local factions of radical Muslim politicsreminiscence of the era of nationalist politics of the 1950s.

This could be asource of civil unrest in the very near future. Signs of this have begun toshow in the recurrent violent conflicts between Muslims and the government. Tanzaniahas experienced the Buzuruga Muslim-SungusunguConflict (1983), Pork Riots (1993) and Mwembechai Upheaval (1998). For moreinformation See Hamza Mustafa Njozi, MwembechaiKillings and Political Future of Tanzania, Globalink Communications Ottawa,2000. (The book is banned by the government). In all these conflicts, Muslimblood has been shed. In between these conflicts Muslims have sent severalpetitions to the government requesting it to look into these problems but allof them have been ignored.

As a result of this Muslims from all regions ofTanzania met in Dar es Salaam at Masjid Tungi in 1990 and issued the TungiDeclaration which among other things stated that Muslim should prepare todefend their rights by all means even if it means by force of arms.

The late Prof. Haroub Othman after reading Sheikh Ali Muhsins book Conflict and Harmony in Zanzibar and thewriters book The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 1968 The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialismin Tanganyika, Minerva Press, London 1998 andhaving come across hitherto unknown information on Nyerere was devastatedbecause he was a great admirer of Nyerere as a patriot and a nationalist.

Thetwo books had painted him differently. Prof. Haroub confronted Nyerere and toldhim that the allegations in those two works have tarnished his image and headvised him to respond to them. Nyerere never did. Christian lecturers at Dares Salaam University are discouraging students from making references to thosetwo books.

Dr. Harith Ghassanys book KwaheriUkoloni Kwaheri Uhuru, has also come up with more information on Nyererehitherto unknown in the Zanzibar Revolution and the bloodbath which followed.

Tumefikaje katika hali hii kuwa fursa zote zimehodhiwa na Wakatoliki? Nadhani una habari ya mfumokristo na harakati za Waislam kupambananao. Haitasidia kujifanya hatuna tatizo. Lipo tatizo kubwa sana sasa hivi.
 
Mkandara,

Hakuna Muislam anaeweza kuthubutu kutangaza Uislam kwa jina la mtu. Sijafanya
hivyo na wala siwezi kuthubutu.

Nilichofanya mimi nimeandika historia ya wazee wangu ambayo ilikuwa imesahaulika.

Hicho ndicho nilichofanya. Na nimekwenda mbele zaidi na kusema silazimishi mtu
kuiamini kwa kuwa historia rasmi iko na wazee wangu hawamo sina ugomvi na yeyote.

Nimefanya hivyo kwa kugundua kuwa kuna wengi historia ile inawachoma roho hawataki
kuamini kuwa hayo niliyosema ni kweli.

Ila nitafahamisha moja ya mafunzo ya Uislam. Allah anawaasa Waislam "wasidhulumu na
wasikubali kudhulumiwa."

Mohamed
Sawa labda nikuulize wewe kwa nini Historia ya Marekani inaanzia kwa George Washington wakati kuna watu wengine waliomtangulia?.. Kwa nini marais wote waliopita na waliopo hawazungumzii Freemasons kama ndiko chimbuko la Mapinduzi na Uhuru wa Amerika..Hawawazungumzii kina Lawrence na William Fairfax au niseme familia nzima ya Fairfax. Kwa nini kila nchi inaaza historia yake na mtu alowaletea Uhuru wao badala ya mwanzo wa harakati?..Kwa nini usichukue muda mrefu kuandika habari za kina Mkwawa, Mirambo, Mangi Sina na wengineo ambao pia waliwatangulia viongozi hawa wa kisiasa maanake unataka kuzungumzia historia. Cecil Matola sii ndiye alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa TAA mbona humzungumzii yeye?

Kama wewe unataka kuiandika upya historia ya Tanzania fanya hivyo na siii kuitumia dini ktk mabandiko yako mengi tu nimekuwa nikikusoma ukielekeza chuki zako kwa Nyerere ambaye sioni sababu yake kutaja jina la Sykes au Matola inaweza kujenga kitu. Yes, Usilaam unakataza kudhulumu wala kudhulumiwa, lakini unachofanya wewe hapa unataka kumdhulumu Nyerere aonekane mtu mbaya sana, wakati wewe unalilia kutodhulumiwa kwa kina Sykes, hivyo unapotosha Uislaam -- Do the right thing brother!
 
Faiza usidhani kumkalia kooni afisa elimu wa mkoa ilikuwa kazi nyepesi hadi useme nilikuwa treated tofauti na wewe. Baada ya kubaini kwamba nilikuwa nimefaulu, mzazi wangu hakukubali kamwe kusikiliza story na uzingatie miaka hiyo nafasi za sekondari zilikuwa chache sana. Nakumbuka wilaya yetu ilikuwa inapata nafasi 106 tu za sekondari, hatukuwa na sekondari ya kutwa wilayani kwetu, tulipigania nafasi hizo chache katika shule za bweni zilizokuwa nje ya wilaya yetu na zile nafasi za shule za kitaifa kama moshi tech, ilboru, ihungo, tabora boys & girls, msalato n.k

Katika kupigania haki yangu ya kusoma, baba yangu alifunga safari toka Tabora alipokuwa akilitumikia taifa- JWTZ, hadi kwa afisa elimu wa mkoa wa Mara, akiwa amepiga kombati mwanzo mwisho!! Afisa elimu hakuwa na namna nyingine zaidi ya kunipeleka shule. Ni bahati mbaya kwamba wazazi wako hawakukomaa, kwahiyo utaona kwamba si suala la kuwa muislamu bali haki yangu ilitaka kuporwa na mzazi wangu akasimama imara kuipigania.

Katika hili Nyerere hahusiki hata kidogo, kwani hata tangu tuanze kutumia namba kwenye mitihani mambo yamebadilika? kama Nyerere ndo alikuwa akitumia u superpower wake kuwadhulmu waislamu, hata baada ya yeye kung'atuka mbona mnadai dhulma bado ipo??

Hongera sana kwa kuwa wazazi wako waliweza kumkalia kooni afisa elimu kwa kumvalia kombati mpaka ukapewa nafasi kati ya chache zilizokuwepo. Hayo wazazi wangu hawakuweza na ni kweli kabisa hawakukomaa kama wazazi wako ikapelekea nikanyimwa haki yangu, niliyoitolea jasho usiku na mchana, labda wazazi wa Elizabeth nae walienda kikomando kama wazazi wako?

Isitoshe hadithi yako inaonesha kuwa rushwa ilianza kuota mizizi wakati huo. Nakupa pongezi sana kwa kuwa na wazazi majasiri na walioweka kukusimamia mpaka kwa kuvaa full kombat kudai haki yako. Hiyo inaonesha jinsi ya udhalim uliokuwepo wakati huo, wale tusio na wazazi wavaa kombat na tuliofaulu vizuri sana tena sana, hatukupata haki yetu. Jee, ni mimi au wazazi wangu wa kulaumiwa kwa kukosa ukakamavu wa kudai haki yangu ya msingi? Utawala wa namna hiyo ya kupatiwa "haki" unafaa sana na inabidi tuupongeze sana na mtawala alietufikisha hapo inafaa tumpe utakatifu kwa shangwe.

Kwa sasa, haya ya shule tumeshaona yakishughulikiwa, si unajuwa minimum education ya sasa ni ipi?
 
Hiyo "harisi" una maanisha bokoboko lako? Au una maanisha mlinzi wako? Kama ni hayo uliomaanisha sidhani kama humu JF utampata atakaeongelea hayp labda Barubaru akusaidie.
Unanchekesha!

Embu acha hayo mambo yako,kama ni kosa la kimaandishi halina maana yoyote kwako wewe kuongeza "vikolombwezo" acha watu wajifunze kutoka kwa Mzee MS,hayo yakwako fungulia uzi wake.
 
Back
Top Bottom